Friday, October 12, 2018

YESU NI MUNGU

YESU NI MUNGU
No automatic alt text available.
Naanza na aya ambayo inatumiwa sana na Waislam kupinga Uungu wa Yesu. "MUNGU WETU NI MMOJA"

Kumbukumbu la Torati Mlango 6: 4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 

SASA TUANZE KUZISOMA AYA KWA UMAKINI, JE, YESU NI BWANA? MAANA KATIKA KUMBUKUMBU LA TORATI INATUFUNDISHA KUWA "BWANA NDIYE MMOJA NA BWANI NDIYE MUNGU, BASI YESU LAZIMA NA YEYE AWE NA HIZO SIFA ZA KIPEKEE"

Yohana Mlango 13:13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.

Wanafunzi wa Yesu walimuita "BWANA" kama ambayo Kumbukumbu la Torati inavyo sema. YESU AKASEMA WAMENENA VYEMA NA NDIVYO ALIVYO.

Je, Yesu ni Bwana Mungu?

Endelea kusoma:

Yohana Mlango 20: 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!

Tomaso anasadiki na kukiri kuwa Yesu ni "BWANA" na "MUNGU"

Je, Yesu alikataa kuitwa hivyo?

Yohana Mlango 20: 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.

Yesu anamjibu kuwa "WEWE TOMASO UNASADIKI KWA KUWA UMENIONA" Kumbe Yesu hakukataa kuitwa Mungu bali thibitisha yeye ni Mungu na ni Bwana.

Endelea kusoma aya:

Yohana Mlango 10: 33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.

Wayahudi walio ishi na Yesu walisadiki kuwa "YESU ALIJIFANYA MUNGU. Kumbe basi Yesu alithibitisha yeye ni Mungu wakati alipo kuwa hapa hapa duniani.

Endelea kusoma aya:

Yohana Mlango 5: 18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,

Kumbe moja ya sababu ya Wayahudi kutaka kumuua Yesu ni vile Yesu alimuita Mungu BABA YAKE na zaidi ya hapo Yesu alijifanya SAWA NA MUNGU.

Biblia ipo kamili na haina shaka ndani yake. Leo tumejifunza kuwa Yesu ni Mungu. Haya yalithibitishwa na Yesu mwenyewe pamoja na Wayahudi walio taka kumuua kwa kwasababu Yesu alimuita Mungu Baba yake na Kujifanya sawa na Mungu. Zaidi ya hapo, hata wanafunzi wake walimuita Bwana na Mungu.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. TITO 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW