Agano ni nini?
Agano ni mapatano baina ya mtu na mtu ama baina ya pande mbili na ambalo linawafunga wote wawili . Agano huwa linaambatana na kanuni za Agano ambazo hazipaswi kuvunjwa na zinapaswa kushikwa kama kanuni ambazo zinaunda agano. Mifano ya Agano ni Agano baina ya Mungu na Nuhu [Mwanzo 9:9-17], Agano baina ya Mungu na Abrahamu [Mwanzo 17:1-21], Agano Baina ya Ibrahimu na Abimeleki [Mwanzo 21:27-32,], Agano baina ya Isaka na Abimeleki [Mwanzo 26:26-33], Agano baina ya Yakobo na Labani [Mwanzo 31:43-54].
Agano Jipya ni sehemu ya pili ya Biblia ya Kikristo, ikifuata Agano la Kale: Agano Jipya limefichika katika lile la Kale, na Agano la Kale limedhihirika katika lile Jipya.
Linakusanya vitabu ambavyo Wakristo wote wanaviheshimu kama vitakatifu na vilivyoandikwa baada ya ujio wa Yesu Kristo hadi mwisho wa wakati wa mitume wake.
Vitabu vyake 27 vinaleta habari zake, za mitume wake na za mwanzo wa Kanisa lake.
Agano la Pili ni Agano ambalo Mungu alifanya na watu wake kwa njia ya Yesu Kristo. Kuhusu Agano hili Unabii wa Biblia unasema kwamba Yesu angefanya Agano na watu wengi kwa Mda wa Juma moja. Biblia yasema hivi “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu. [Daniel 9:27]. Yesu alipokufa pale msalabani mwaka 31AD[Nusu Juma ya unabii wa Daniel] Msalaba wa Kristo uliondoa Agano la kwanza na Sadaka zake za kuteketezwa na makafara yake yote na mifumo yote ya Patakatifu pa kidunia, Ukuhani wa kidunia, na sikukuu zote ambazo zilikuwa ni vivuli vinavyomwakilisha Kristo; na kulisimamisha Agano la pili, Na Kristo mwenyewe akawa Mjumbe wa Agano jipya na Damu yake mwenyewe ikawa damu ya utakaso ya Agano jipya. Mwaka 34 AD kulingana na Unabii wa Daniel[Nusu ya pili ya juma la unabii wa Daniel], Wana wa Israeli walitia Muhuri wa uasi wao, kwa Kumpiga Stefano mawe na kuliudhi kanisa. Ndipo mitume wakaachana na Wayahudi na kuzambaza injili kwa watu wa mataifa.
Kuhusu Agano Jipya Biblia yasema hivi: “Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. [Waebr8:6]. Katika Agano jipya Watu wa Mungu wakatakaswa kwa damu ya Yesu mwenyewe. Biblia yasema hivi: “wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. [Waebr9:12-15].
Agano jipya ndiyo jibu katika uasi wetu. Imeandikwa Yeremia 31:33 "Basi agano hili ndilonitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile asema Bwana nitatia sheria yangu ndani yao na katika ioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao nao watakua watu wangu."
Agano jipya laja kwa njia ya Yesu Kristo. Imeandikwa, Luka 22:20 "Kikombo nadho vivyo hivyo baada ya kula akisema; kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu."
Agano jipya yamaanisha twaweza kwende mbele za Mungu bila mpatanishi kupitia kwake Yesu Kristo. Imeandikwa, Waebrania 7:22 "Basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi."
Kuna ondoleo la dhambi katika agano jipya. Imeandikwa, Waebrania 9:14-15 "Basi si zaidi damu ya Yesu Kristo, ambaye kwa roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kua sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? na kwa sababu hi ni mjumbe wa agano jipya ili mauti ikisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya liyokuwa chini ya agano la kwanza hao waliyo itwa waipokee ahadi ya uridhi wa milele."
Agano la Kale dhidi ya Agano Jipya – kuna tofauti gani?
JHuku Biblia ikiwa ni kitabu kimoja, kuna tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa njia nyingi, zinakamilishana. Agano la Kale ni la msingi, na Agano Jipya lajijenga kwa huo msingi na ufunuo zaidi kutoka kwa Mungu. Agano la Kale laanzisha kanuni ambazo zinaonekana kuonyesha ukweli wa Agano Jipya. Agano la Kale lina unabii mwingi ambao unatimia katika Agano Jipya. Agano la kale linatoa historia ya watu ; Lengo la Agano Jipya ni juu ya Mtu . Agano la Kale linaonyesha ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi (kwa kiza cha neema yake) na Agano Jipya linaonyesha neema ya Mungu kwa ajili ya wenye dhambi (kwa kiza cha ghadhabu yake).
Agano la Kale linatabiria Masihi (ona Isaya 53), na Agano Jipya linamdhihirisha masih kuwa yupo ( Yohana 4:25-26). Agano la Kale lakumbukumbu utoaji wa Sheria ya Mungu, na Agano Jipya laonyesha jinsi Yesu Masiya alivyotimiza sheria (Mathayo 5:17, Waebrania 10:9). Katika Agano la Kale, adhabu ya Mungu hasa ni kwa watu wake wateule, Wayahudi; katika Agano Jipya, adhabu ya Mungu hasa ni kwa kanisa lake (Mathayo 16:18). Baraka za kimwili zilizo ahidiwa katika Agano la Kale (Kumbukumbu 29:9) linatoa njia ya baraka za kiroho chini ya Mkataba ya Agano Jipya (Waefeso 1:3).
Unabii wa Agano la Kale kuhusiana na kuja kwa Kristo, ingawa ni wa kina, una kiasi fulani cha utata ambao umerekebishwa katika Agano Jipya. Kwa mfano, Nabii Isaya alisema ya kifo cha Masihi (Isaya 53) na kuanzishwa kwa ufalme wa Masihi (Isaya 26) huku hakuna dalili ya mwenendo wa matukio mawili - hakuna mwanga kwamba mateso na ujenzi wa ufalme utatenganishwa na milenia. Katika Agano Jipya, inakuwa wazi kuwa Masiya ako na ujio aina mbili : katika ule wa kwanza aliteseka na akafa (na kufufuka tena), na katika wa pili Yeye ataimarisha ufalme wake.
Kwa sababu ya ufunuo wa Mungu katika maandiko ni endelefu, Agano Jipya huleta katika lengo kali la kanuni kwamba walikuwa kuletwa katika Agano la Kale. Kitabu cha Waebrania kinaeleza jinsi Yesu kweli ni Kuhani Mkuu na jinsi kafara yake moja kuu ni nafasi ya sadaka zote za awali, ambayo ilikuwa kivuli cha yatakayo kuja. Pasaka ya Agano la Kale (Ezra 6:20) inakuwa Mwana-kondoo wa Mungu katika Agano Jipya (Yohana 1:29). Agano la Kale inatupa sheria. Agano Jipya linafafanua kwamba sheria ilikuwa na maana ya kuonyesha watu mahitaji yao ya wokovu na haikukusudiwa kuwa njia ya wokovu (Warumi 3:19).
Agano la Kale liliona Adamu amepotelewa na peponi na Agano Jipya linaonyesha jinsi peponi inapatikana kupitia Adamu wa pili (Kristo). Agano la Kale lasema kwamba mwanadamu alikuwa ametengwa na Mungu kwa njia ya dhambi (Mwanzo 3), na Agano Jipya linasema kuwa mwanadamu anaweza kurejeshwa katika uhusiano wake na Mungu (Warumi 3-6). Agano la Kale lilitabiri maisha Masihi. Injili imerekodi maisha ya Yesu, na Nyaraka hutafsiri maisha yake na jinsi sisi huitikia yote ambayo amefanya.
Kwa muhtasari, Agano la Kale huweka msingi wa kuja kwa Masihi ambaye atatoa nafsi yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (1 Yohana 2:2). Agano Jipya limenakili kumbukumbu ya huduma ya Yesu Kristo na kisha inaonekana kutizama nyuma juu ya kile alichofanya na jinsi sisi tunastahili kuhitikia. Agano zote mbili zatangaza huyo Mungu mtakatifu, na wa huruma, na hakia ambaye Analaani dhambi bali atamani kuwaokoa wenye dhambi kwa njia ya sadaka ya upatanisho. Katika Maagano yote mawili, Mungu hujifunua kwetu na inatuonyesha jinsi sisi tunastahili kuja kwake kwa njia ya imani (Mwanzo 15:6; Waefeso 2:8).
Katika agano la kale watu wasaki kufanya nini?
Imeandikwa Kutoka 24:3 "Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya Bwana na hukumbu zake zote watu wote wakajibu kwa sauti moja wakasema maneno yote aliyoyanena Bwana Mungu tutayatenda.
Mungu ameagiza kufanya nini katika agano jipya?
Imeandikwa, Waebrania 8:10 "Maana hili ndilo agano nitakalo agana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile asema Bwana nitawapa sheria zangu katika nia zao na katika mioyo yao nitaziandika nani nitakuwa Mungu kwao."
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
No comments:
Post a Comment