Monday, March 18, 2019

MUUJIZA WA BWANA YESU NDANI YA MSIKITI

Huu ni ushuhuda wa dada mmoja wa kutoka Indonesia ambaye, japokuwa zamani alikuwa Mwislamu (na sasa ni Mkristo), Bwana Yesu alimwokoa kimiujiza yeye pamoja na watu wengine kutoka kwenye janga na mauti ya sunami na tetemeko ambavyo vilisababisha vifo vya mamia kwa mamia ya watu
Je, ni nini kilisababisha hadi Bwana Yesu akaingilia kati wakati ule ambapo kifo kilikuwa hakikwepeki?
Fuatilia ushuhuda huu wa kushangaza, ambao kwa maneno yake mwenyewe, dada huyu anasimulia kile kilichotokea, hadi kufikia mahali ambapo yeye na watu hao wakamwamini Bwana Yesu bila hata mahubiri ya moja kwa moja ya Injili. Bwana alihubiri mwenyewe:
Usiku uliotangulia janga lile la sunami na tetemeko, dada huyu aliota ndoto ambayo ilimpa mawazo mengi sana lakini hakujua ina maana gani. Katika ndoto ile, alijiona kuwa anajenga nyumba yake mwenyewe. Kuta tayari zilishasimama lakini kulikuwa hakuna paa; ambalo kwa kawaida huwa ni ishara ya ulinzi. Na nje ya nyumba kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamezunguka nyumba hiyo.
Kulipokucha, dada huyu aliamka na kuendelea na kazi za kawaida za nyumbani. Alikuwa akisafisha vyombo. Ghafla kulitokea tetemeko. Anasema kuwa, “Nilimweleza mume wangu asubuhi ile wakati wa tetemeko kuwa, labda hii ni ishara kuwa watu wengi watakufa. Niliota jambo hili usiku wa leo.
Anaendelea kusema, “Kisha dakika moja baadaye, tetemeko liliisha. Kwa hiyo tulitoka nje. Tutoke nje! Tutoke nje! Halafu maji ya bahari ambayo yalionekana yana kimo kirefu kama urefu wa minazi miwili yalikuwa yakija kuelekea ufukweni.
“‘Tutaenda wapi sasa? Tutaenda wapi sasa?’ kila mmoja aliniuliza. Nikachanganyikiwa kabisa! Nikasema, ‘Ile ni nyumba ya Mungu! Ile ni nyumba ya Mungu!” (yaani msikiti).
“Sote twendeni humo. Nilianza kuomba. Nilijisahau kuwa mimi ni Mwislamu. Nilianza kuomba kama Wakristo wanavyoomba. Nilisema, ‘Bwana Mungu, tulinde kwa wakati huu. Usituharibu Bwana. Usiwe na hasira nasi, Ee Mungu. Tusamehe. Tusamehe dhambi zetu. Bwana Yesu, usiniache.
“Kila mmoja wetu alikuwa akirukaruka, akisema, ‘Bwana Yesu! Bwana Yesu! Ghafla, maji yaliyokuwa yakija, yalikomea kama meta moja hivi kutokea tulikokuwa.”
ya kuona hivyo, dada huyu anaendelea kusema, “Sote tulikuwa tukilia, ‘Asante Bwana Yesu. Kila mmoja aliamini kuwa Bwana Yesu alituokoa wakati ule. Hakuna mwingine wa kumgeukia ila Yeye tu.”
Yanayofuata ni maelezo ya msimuliaji, Dr. Randy Richards, ambaye alikuwa mmoja wa watoa misaada wa kujitolea (Tsunami Relief Volunteer) kwenye eneo hilo:
“Mara maji ya bahari yalipokoma, walienda sehemu zenye mwinuko wa juu, kwenye milima. Na baadaye waliporudi, kila upande kuzunguka msikiti, kulijaa miili ya watu waliouawa na maji ya bahari.
“Akasema,” (yaani yule dada), ‘Hapo ndipo nilipotambua maana kamili ya ile ndoto yangu.’
“Nyumba ilikuwa haijakamilika. Haikuwa na paa. Haikuwa na ulinzi. Hawakuwa na Yesu. Na kama ilivyokuwa kwenye siku za Nuhu, kila mtu aliangamia. Kwa hiyo, watu wote hawa ambao walikuwa wamezunguka nyumba ambayo ilikuwa haijakamilika, waliangamia.
Randy anaendelea kusema, “Yesu aliamua kuwaokoa watu wale kwa ajili ya ushuhuda. Sijui anakusudia nini, lakini hakika ameyabadilisha kabisa maisha ya watu wale; na ushuhuda uko pale.”
INGIA HAPA NA ANGALIA VIDEO YA USHUHUDA https://www.youtube.com/watch?v=1yU87JMtzEo
Yanayofuata ni maneno yangu blogger:
Ndugu unayesoma ushuhuda huu, sijui wewe umo kwenye nyumba ya namna gani? Je, ni nyumba yenye paa au ni nyumba isiyo na paa?
Hebu sikia maneno ya Bwana Yesu mwenyewe:
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. (Mathayo 7:24-27).
Njoo kwa Yesu leo ili upone. Nje ya Yesu, hakika yake, kuna mauti, upotevu na uangamivu pekee. Hakuna uzima isipokuwa kwa Yesu peke yake!

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW