Pamoja na mengine yote Yesu aliyoyasema juu yake mwenyewe, wanafunzi wake waliamini u mungu wake pia. Waliamini kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi jambo ambalo Mungu pekee ndiye mwenye uwezo nalo kwa kuwa ni Mungu anayechukizwa na dhambi (Matendo 5:31; Wakolosai 3:13; na kuendelea. Zaburi 130:4; Yeremia 31:34). Pamoja na haya Yesu ndiye atakayekuja, “kuhukumu wafu na walio hai” (Timotheo wa pili 4:1). Tomaso akamlilia Yesu Akisema, “Bwana wangu na Mungu wangu!” (Yohana 20:28). Paulo anamwita Yesu, “ Mungu Mkuu na Mwokozi” (Tito 2:13), na anaelezea ya kuwa Yesu, “alikuwa katika hali ya Mungu” (Wafilipi 2:5-8). Mwandishi wa kitabu cha waebrania asema juu ya Yesu kuwa, “ Kiti chako cha enzi wewe Mungu, kitadumu milele na milele” (Waebrania 1:8). Yohana aeleza kuwa, “Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwako kwa Mungu, naye neno (Yesu) alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Mifano ya aya zinazofundisha juu ya u Mungu wa Yesu ni mingi (pia Ufunuo wa Yohana 1:17; 2:8; 22:13; Wakorintho wa kwanza 10:4; Petro wa kwanza 2:6-8; Zaburi 18:2; 95:1; Petro wa kwanza 5:4; Waebrania 13:20), kila mojawapo ya aya hizi inatosha kukujulisha ya kwamba wanafunzi wa Yesu walimwamini kuwa Yesu alikuwa Mungu.
Yesu pia apatiwa adhama ambazo zina Yahweh pekee (Jina maalum la Mungu) katika agano la kale. Adhama ya “Mkombozi” (Zaburi 130:7; Hosea 13:14) inatumika juu ya Yesu katika agano jipya. (Tito 2:13; Ufunuo wa Yohana 5:9). Yesu anaitwa Immanueli (“Mungu pamoja nasi” katika mathayo 1). Katika Zakaria 12:10, ni Yahweh anayesema, “watanitazama mimi waliyenipasua.” Lakini agano jipya haya yanatumika kwa kusulibiwa kwake Yesu (Yohana 19:37; ufunuo wa Yohana 1:7). Kama ni Yahweh mwenye kupasuliwa na mwenye kutazamwa, na Yesu ndiye aliyepasuliwa na kutazamwa basi Yahweh ni Yesu. Paulo anatafsiri Isaya 45:22-23 kama yale ya Yesu katika wafilipi 2:10-11. Pia Jina la Yesu linatumika pamoja na la Yahweh katika sala, “Neema na amani kutoka kwa Mungu baba na Bwana wetu Yesu kristo iwe kwenu” (Wagalatia 1:3; Waefeso 1:2). Hili lingekuwa kufuru kama Yesu hangekuwa Mungu. Jina la Yesu linapatikana tena na la Yahweh katika amrisho la ubatizo Yesu aliposema, “kwa Jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19; pia tazama wakorintho wa pili 13:14.
Matendo ambayo yanaweza kufanywa na Mungu Pekee yanaonyeshwa yakifanywa na Yesu. Licha ya kuwa alifufua wafu (Yohana 5:21; 11:38-44), na kusamehe dhambi (Matendo 5:31; 13 38), aliumba ulimwengu (Yohana 1:2; Wakolosai 1: 16-17)! Jambo hili linatia msisitizo wakati tunapochukulia ya kwamba Yahweh aliumba akiwa peke yake. (Isaya 44:24). Hata hivyo, Yesu ana sifa sawa na Mungu, kama Umilele (Yohana 8:58), kuwa kila mahali (Mathayo 18:20, 28:20), kufahamu yote (Mathayo 16:21), muweza yote (Yohana 11:38-44).