Nusrat Aman alikuwa ni mwanaharakati wa kiislamu wa kundi la Ahmadiah kule Pakistani. Siku moja aliamua kuingia kanisani ili akamwulize mchungaji ni kwa nini hasa hataki kuwa mwislamu ilhali unabii wote umeshatimizwa ndani ya Muhammad? Nusrat aliishia kupata aibu, hasira na hatimaye wokovu …!
Je, ilikuwaje? Endelea kusoma ushuhuda wake wenye kichwa kisemacho "Kwa nini niliamua kuwa Mkristo?" ambao unafungua macho na mioyo kwa kuwa ni watu wengi walio katika kundi alimokuwa Nasrat hapo zamani.
*****************
Kwa nini niliamua kuwa Mkristo?
Na Nusrat Aman
Nilizaliwa katika familia halisi wa Kiislamu nchini Pakistani mwaka 1958. Nilisoma katika shule ya kimishenari ya Kiislamu na chuo kilichosimamiwa na Ahmadiah Movement in Islam, Pakistani. Wakati wa masomo yangu katika shule ya kimisionari na chuo cha Kiislamu vyenye mwamko mkubwa sana kuhusu Uislamu, nilijenga shauku kubwa ya kujifunza dini ya Kiislamu. Kwa hiyo, nilijiunga na Ahmadiah Movement, kundi ambalo lilitangazwa na Serikali ya Pakistani mwaka 1974 kuwa ni dini ya kizushi isiyo Kiislamu.
Mimi nilikuja kujua neno, "Kristo au Masihi" kwa mara ya kwanza katika maandiko ya Ahmadiah Movement yanayopinga Ukristo. Mwasisi wa harakati za Ahmadiah, Mirza Ghulam Ahmad alidai kuwa yeye ndiye "Masih Maud" (yaani Masihi aliyeahidiwa). Mimi nilikuwa na furaha sana na shauku ya kuhubiri mafundisho ya Ahmadiah Movement ambayo yalikuwa ni mapya na ya kuvutia sana kwangu. Nilikuwa nakumbuka aya zote kwenye Biblia zinazoongelea kuhusu ujio wa pili wa Kristo katika Biblia na Quran lakini bila kuwa na ufahamu wa kina kuhusiana na aya hizo.
Kosa nililofanya, likaniokoa



