BINTI AITWAYE THERESIA AMBAYE ALIKUWA ANATUMIKISHWA NA SHETANI AELEZEA JINSI ALIVYOSHIRIKI KATIKA KUIZAMISHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER KWA NJIA ZA KISHETANI.
Theresia ni binti aishiye Jijini Tanga na Mama yake mzazi, na siku hii ambayo alifunguliwa kutoka kuzimu kwa shetani alikuwa amekuja kwenye Mkutano wa Injili uliokuwa umeandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima Jijini Tanga na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Na baada ya Mchungaji Josephat Gwajima kuanza kuwaombea maelfu ya watu ambao walikuwa mkutanoni wengi walifunguliwa, na waliokuwa katika vifungo vya shetani, na msukuleni walifunguliwa na kurejeshwa katika hali zao za kawaida.
![]() |
| Mchungaji Kiongzoi Josephat Gwajima akiwa na Binti Theresia pamoja na Mama mzazi wa binti Theresia |
![]() |
| Theresia akiwa tayari kuanza kuelezea habari nzima.. |
ALIFIKAJE KUZIMU
Siku moja nilikuwa nimetumwa dukani na mama yangu mkubwa, wakati navuka barabara ghafula nikakutana na mtu ana kila kiungo katika mwili wale kikiwa kimoja kimoja , akajitambulisha kwa jina la Lucifer akanipa mkono ila nikakataa, akauchukua mkono wangu kwa nguvu akanikumbatia, nikajikuta chini ya bahari. Akaja mwenyewe nikaogopa sana akaniambia nimekuchagua kwa sababu nimekuchagua hata kabla hujazaliwa. Kwa sababu una akili sana.
![]() |
| Theresia akiwa anaelezea ushuhuda wa yale aliyaona katika ulimwengu wa kishetani. |
Akaniambia nilipozaliwa aliniwinda sana ila alishindwa kunichukua kwa sababu bibi yangu alikuwa ananiombea sana . Lucifer akaniambia anataka niwe mke wa mtoto wake. Tukafunga ndoa na baada ya miezi 6 baba yake akaniambia anaweza kunipa nguvu nyingi sana lakini anataka nimtumikie yeye. Baada ya miaka 6 akanipeleka shemu Fulani ndani ya bahari ya pacific lakini ni chini sana, sehemu hiyo ni mji kama ilivyo miji ya huku.
Tukaingia sehemu Fulani tukamkuta dragon ambae alianza kuongea na Lucifer, nikafunga macho na nikajisikia kujawa na nguvu sana, akaniambia amenipa nguvu na mamlaka ya kumiliki na kutawala fahamu za wanadamu.
![]() |
| Mama mzazi wa Theresia alianza kulia kwa uchungu sana baada ya kunza kusikia habari hizi za kutisha ambazo mwanae wa kuzaa ameyapitia. |
Siku moja niliamka asubuhi nikiwa na njaa sana kwa sababu usiku wake sikula chakula, Lucifer akaniambia kuna meli inaitwa Mv spice nikaenda na baadhi ya watu tukatega nyaya za kopa, ile meli ikawa inakuja tukatega pale maji yanapogawanyikia ili watu waseme ni mkondo wa maji, kuna maneno nikayasema halafu nikasimama pembeni, ile meli ikaanza kuzama mpaka kwenye kina cha chini kabisa cha bahari ambacho nilitaka mimi, kisha tukaunganisha mabomba mpaka kule pacific na tukapata damu nyingi sana. Mimi nilikuwa nahitaji kunywa damu kiasi cha tani 5000 kwa siku ili niwze kutena kazi kwa nguvu nyingi.
![]() |
| Theresia akiendelea kuelezea huku mama mzazi akiwa anaendela kusikiliza kwa umakini wakiwa na Mchungai Josephat Gwajima |
Pia kazi yetu nyingine ilikuwa kuwafanya watu wanaompenda Mungu waache kabisa na kuanza kuwaza vitu vilivyo tofauti kabisa na mapenzi ya Mungu, na waliuwa wakiifanya kazi hii kwa ku-control akili na fikra za wanadamu, yani utawala mkubwa wa shetani ni kuzishika na kuzikamata fikra za wanadamu ili watende mambo ya kumchukiza Mungu na kujiondolea neema ya Mungu, na walikuwa na uwezo wa kumfanya binadamu atende jambo lolote baya iwe kuuwa,kulewa kutokwenda kanisani.
ULITOKAJE HUKO?











