Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima 23.9.2012
UTANGULIZI:
Huu ni mwendelezo wa somo la Nyota na Maisha mtu aliyonayo. Mathayo 2:1; Kama tulivyoona tangu mwanzo kuwa nyota ni kipawa, uweza, hatma au hali ya mtu ya baadaye. Tukaona nyota ya Yesu ilionekana kabla Yesu hajazaliwa na mamajusi wa mashariki walimwona kama Mfalme.
MAANA YA NYOTA:
Kama tulivyooa sehemu ya kwanza kuwa nyota ni kiashiria cha rohoni, kinachoonesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu au hatma ya mtu. Viashiria hivi ndivyo vinavyoitwa nyota.
NYOTA KATIKA BIBLIA:
Hesabu 24:14-17 Baraki alikuwa mfalme, na alipoona kuwa wanaisrael wanakuja ili kushambulia ufalme wake, akamtafuta Balaam amtabirie. Hayo ni maneno ya Balaamu aliyoona, Hivyo Balaamu alipoangalia taifa la Israel akaona nyota, kimsingi nyota ya mtu inaonyesha jinsi mtu atakavyokuwa baadaye. Hivyo balaamu aliweza kumuona Yesu tangu mwanzo na ndio maana mamajusi wa mashariki nao pia walimwona Yesu kama nyota.
Nyota yaweza kuonyesha kusudi la maisha ya mtu, na ndio maana ingawa Suleimani alizaliwa na mke wa Huria ambaye Daudi alimuua mumewe ili ampate lakini kwasababu nyota ya kujenga hekalu ilikuwa juu yake (yaani Suleimani), Mungu alimchagua kujenga Hekalu. Daudi alikuwa na watoto wengine wengi, lakini aliyechaguliwa kujenga ni Suleimani kwasababu ndio mwenye nyota ya kujenga yaani tangu anazaliwa
Isaya 47:8-12; Hapa biblia inataja neno “wajuao Falaki”, hii ni elimu inayohusu mambo ya nyota ambayo wachawi husoma. Katika Mathayo 2:1- Biblia inataja mamajusi, wao ni wasomaji wa nyota ambao waliiona nyota ya Yesu kabla ya Yesu hajazaliwa. Nyota ya Yesu iliwafanya mamajusi kumfuata kutoka mbali, na wakati huohuo Herode alifadhaika. Kumbe nyota ya mtu ikionekana watu wanaweza kuifuata na kukuletea unalohitaji. Watu wengi wapo katika vifungo mbalimbali kwasababu nyota zao zimefunikwa.
MAMBO 15 AMBAYO UTAYAONA KAMA NYOTA YA MTU HAIPO:
· Umahiri na utendaji kazi wa mtu hauonekani; kama mtu hana nyota ule umahiri wa wake na utendaji kazi hauwezi kuonekana. Hata ajitahidi kufanya kazi kwa bidii umahiri hawezi kuonekana.
· Hawezi kuwa mbunifu katika maisha; nyota huleta ubunifu sasa kama haipo basi ubunifu wa mtu hautaonekana. Mtu huyo atakuwa anashindwa kubuni kitu cha kufanya ili kupata mafanikipo katika maisha.
· Hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi; nyota huleta ufanisi katika kazi, mtu akikosa nyota basi ule ufanisi wake hauwezi kuonekana, mtu huyo atakosa ufanisi katika kazi zake.

















