- Je, madai ya kuwa Quran imekalika na ipo
waziwazi ni ya kweli?
- Allah ateremsha aya na kudai kuwa, Quran
haijakamilika na haipo waziwazi.
- Allah asema kuwa aya zingine ndani ya Quran
hakuna ajua maana yake isipokuwa Allah.
Ndugu wasomaji;
Leo tutaangalia utata ulio
jaa ndani ya Quran ambayo wanadhuoni wengi hudai kuwa imenyooka, huku Allah
akiwapinga na kuteremsha aya ambayo inasema kuwa Quran haijanyooka na haipo
waziwazi.
Kwanza tuanze kwa
kuangalia aya ambayo inasema kuwa Quran ipo wazi na aya zake zimepambanuliwa ni
uongofu kwa walio ongoka.
Surat HUD (11:1). Alif
Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha zikapambanuliwa,
kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari
Surat Al Anaam (6:114).
Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni
Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba
kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka.
Surat An nah’k (16:89). Na (waonye)
siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo
tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia
Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara
kwa WaislamuSurah tulizo ziweka hapo juu, zinasema na kudai kuwa Quran imepambanuliwa na ni kitabu kilizo elezwa waziwazi. Ikimaanisha kuwa, unapoisoma Quran, hautapata maswali au kusoma utata katika aya zilizo teremshwa na Allah.


