Thursday, June 18, 2015

SAA YA WOKOVU NI SASA!

NINI MAANA YA KUOKOKA?

KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani.Ambavyo jamii yetu maneno haya tunayatumia sana,

NINI MAANA YA WOKOVU?  

Watu wengi neno hili wamelitafsiri vile wa pendavyo au waonavyo  sasa Swali hili acha lijibiwe na maandiko matakatifu, na maneno haya yasibadilishwe kwamba ni wakati gani wa kuokoka kitendo kikishamalizika cha kukiri kifuatacho ni uwokovu kwa mjibu wa neno, fuatilia hapa chini,
Kwasababu ukimkiri Yesu  Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)

Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)

 

Lini unatakiwa ufanye uamuzi huu muhimu?

Hebu MUNGU na aseme nawe kupitia maneno yake ambayo ni amina na kweli anasema:
Warumi 13:11 
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini

2Wakorintho 6:2 
"Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa"

Biblia inaonya kuwa "tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa" yaani wakati huu unaposoma hapa ndio wakati wako wa kutubu na kumgeukia Mungu kwa njia ya kristo kama bado haujafanya hivyo kwani huu ni uamuzi ambao kila mwanadamu lazima aufanye.Mungu ana kalenda yenye miaka mingi lakini kwenye swala la kuukiri wokovu wa kristo wakati ni sasa..Ninakuomba umpe kristo maisha yako,ili hata kama ukifa muda wowote akupokee na uishi naye milele.

WOKOVU SIO DINI

MAANA HALISI YA WOKOVU
Wokovu ni mpango wa Mungu mwenyewe wakumtafuta na kumkomboa Mwanadamu.

Baada ya Adam na Hawa wanadamu wa kwanza kutenda dhambi na kuvunja uhusiano wa Mungu na Mwanadamu , bado Mungu aliendelea kumpenda mwanadamu na kutafuta ni kwa namna gani na kwa njia ipi ya kurudisha uhusiano wake na mwanadamu aliyemuumba.

“kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele, Yohana 3:16”


“Kila mtu amwaminiye” hii ina maana kwamba wokovu ni kwa wale tu watakao mwamini mwana pekee wa Mungu ambaye ni Yesu Kristo na ambao hawajamwamini hawajaokolewa hivyo wamepotea na hawana uzima wa milele. Wokovu ni njia pekee aliyoichagua Mungu ili   kurudisha uhusiano wake na Mwanadamu kwa Kumwamini Yesu Kristo.

Usidanganyike wala mtu yeyote asikudanganye Wokovu unatoka kwa Mungu mwenyewe kwa njia ya Kristo Yesu. “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho yangu ndani yenu na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda, Ezekiel 36:25-27”

“Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao , Nao watakuwa watu wangu, kwa sababu nitawasamehe maovu yao na dhambi zao sitazikumbuka tena, Waebrania 8:10,12”   “Naye atazaa Mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao, Mathayo 1:21” Hivyo mtu aliyepokea wokovu halisi wa Mungu hatendi dhambi yoyote kwani anaongozwa na Mungu mwenyewe kwa njia ya Roho Mtakatifu na amri za Mungu kwake sio nzito (Yohana 14:26). Anaishi maisha ya utakatifu, yanayompendeza Mungu  ( Zaburi 16:3)

MAANA HALISI YA DINI

Dini ni mpango wa wanadamu wenyewe wa kumtafuta Mungu. Na Mungu ameukataa mpango huu Kwani haufikii viwango anavyohitaji. “mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzuia tamaa za mwili, Wakolosai 2:23”
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami, nao huniabudu bure, wakifundisha maf- undisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Mathayo 15:8-9”

Hivyo dini haiwezi kumusaidia mtu kushinda dhambi kwani anakua hana msaada wowote wa Mungu atajitahidi kujizuia kwa ukali lakini atashindwa. Na kwa mtu anayeshiklia dini kwake amri za Mungu ni nzito.Mtu yey- ote anaweza kuanzisha dini na kupata wafuasi wengi laki- ni sio wokovu kwani unatoka kwa Mungu mwenyewe.

WOKOVU NI HAPA DUNIANI

Usikubali uongo wowote wokovu ni hapa duniani na      baada ya kufa ni hukumu na hukumu hii itategemea uliishije hapa duniani.” Na Kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, baada ya kufa hukumu, Waebrania 9:27”

“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo Watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale waliofanya mabaya kwa ufufuo wa hukumu Yohana 5:28-29

Kwa hiyo maisha yetu ya hapa duniani ndiyo yatakayoamua hukumu yetu itakavyokuwa.
Mungu amezibitisha mwenyewe kuwa kuna Watakatifu Duniani.”Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, Nao ndio nliopendezwa nao, Zaburi 16:3”
Kataa uongo wowote tunaokoka hapa duniani na tunaishi Maisha ya utakatifu yanayompendeza Mungu.

SALA YA TOBA

Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.

Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.

Kwa hiyo kama unataka kuokoka - tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.

Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.

Baada ya kuokoka

Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:

1.Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4.Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5.Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)

Ukipenda unaweza kuniandikia kwa anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia: maxshimbaministries@gmail.com.

Mungu akubariki sana

Max Shimba Ministries Org.


No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW