Wednesday, June 17, 2015

JE, IBADA ZA WAFU NI ZA KIBIBLIA?


Ukweli hakuna Andiko lolote lenye pumzi ya Mungu mahali popote linasomeka kuwakumbuka marehemu, iwe kwa dakika moja au kwa dakika mbili. Lakini lipo Andiko linasomeka, "wafu hawana Ijara tena katika nchi ya walio hai". Kwa hiyo kwa mujibu wa andiko hilo, hata misa za wafu HAZIRUHUSIWI, ikimaanisha arobaini za marehemu wote hazina nafasi ndani ya Neno la Mungu.

WAFU/MFU NI NANI?
Utangulizi:-Neno wafu ndani ya Biblia limetumika likiwa na Maana zaidi ya moja, Linaweza kutumika kama

i.                   Ni hali ya Roho kutengana na mwili yaani Kifo cha mwili.(Luka 8:55, Muhubiri 9:5)

ii.                 Ni hali ya Mtu kutengana na Mungu au kuvunja uhusiano mwema na Mungu (Kutenda dhambi) yaani Kifo cha Kiroho (Ayubu 21:25)

Kifo cha kiroho. Kuna aina tatu ya wafu katika eneo hili ambayo mtu anaweza kufa kiroho lakini bado anaendelea kuwa hai kimwili. Huyu anaweza akatubu na kufufuka katika wafu akawa hai tena .Pia mtu anaweza kufa kiroho na kimwili maana yake Roho imekufa na mwili umekufa hana nafasi ya kutubu tena. (Ufunuo 20:5). Kifo hiki ni kibaya zaidi na kinatisha. Ambacho Bwana Yesu alisema msiwaogope wawezao kuuwa mwili bali Mungu mwenye uwezo wa kuuwa mwili na Roho, (Soma Matayo 10:28). Kifo cha tatu ni Mtu kufa kimwili lakini bado anaendelea kuishi Kiroho. Hapa Yesu alisema mtu akiniamini mimi na kutimiza neno langu ataishi hata kama akifa.


MAOMBI KWA AJILI YA WAFU 

Viongozi wengi hufundisha kwamba hakuna kuokoka duniani na hao hao mtu akifa wanamwombea kwamba alazwe pema peponi kana kwamba kuna wokovu baada ya kufa. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu.(Waebrania 9:27).

Kanisa au Mchungaji au Padri, au Mtume haliwezi kuomba mfu kupumzika kwa amani pema peponi, Ndugu zangu wakati wa wokovu ni sasa hivyo baada ya kufa ni hukumu (Waebrania 9:27). Watakie kupumzika kwa amani wafu ila tambua kwamba huwezi kuwabadilishia makao yao ya milele, kama ni mbinguni ni mbinguni tu na kama ni motoni ni motoni tu.

Kuombea wafu huwafanya wenye dhambi kuendelea kutenda dhambi wakiamini kwamba baada ya kufa kanisa litaomba ili wao waingie mbinguni. Ndugu nakuambia tena WOKOVU NI SASA. Katika Luka 16:26…Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'' Biblia inatuonyesha watu waliokufa  wengine wako pema peponi na wengine wako kuzimu,’’  ’’ MUNGU humpokea mwenye dhambi ambaye hutubu kwa woyo na kujitakasa kwa msingi wa imani peke yake katika damu ya YESU KRISTO. Hivyo humpa uzima wa milele. 2 WaKorintho 6:2’’(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)‘’ Wakati wa wokovu ni sasa Wakati wa kuokolewa/kuokoka ni sasa Wakati huu ndio unatakiwa kuokolewa sio baada ya kufa.

Ndugu zanguni, ningependa kuwakumbusha kuwa, wakati wa Wokovu ni sasa na sio utakapo kufa. Mafundisho ya kuombea wafu hayapo kwenye Biblia na hatuoni Yesu akiombea wafu bali akifufua wafu. (Yohana 11:43-44; Luka 7:11 -15; Marko 5:35).

Mungu awabariki sana


Max Shimba Ministries Org.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW