Swali la 1: Kwa nini mnaliamini Agano la Kale?
Jibu: Maandiko na elimukale (archaeology) vinaonyesha kuwa hakuna mabadiliko makubwa kwenye nakala za sasa kwa sababu angalau tano:
1. Mungu aliahidi kulinda neno lake katika Isaya 55:10-11; 59:21; 1 Petro 1:24-25, Mathayo 24:35. Hatima ya yote tunapaswa kuamini kuwa ama Mungu anaaminika au haaminiki. Lakini kama Muislam anaamini kuwa Mungu hakulinda neno lake katika Agano la Kale, na kwamba hakulinda neno lake katika Agano Jipya, ni kwa nini abadilishe na kulinda neno lake kwenye Kurani?
2. Yesu na Agano Jipya limethibitisha maandiko ya Agano la Kale katika Mathayo 19:4; 22:32,37; 39; 23:35; Marko 10:3-6; Luka 2:23-24; 4:4; 11:51; 20:37; 24:27,44
3. Ushahidi wa Elimukale: Kwenye Septuagint, Torati ilitafsiriwa kwenye Kiyunani/Kigiriki karibu mwaka 400 K.K. Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) yaliandikwa kuanzia karibu mwaka 100 K.K hadi baada ya Kristo, na tunaweza kuyalinganisha na Biblia zetu za leo. Tafsiri za Kiaremi (Aramaic Targums) zilitolewa karibu na muda Yesu alipokuwepo duniani. Maandiko toka Bahari ya Chumvi yana vipande karibu 95,000 kutoka kwenye nyaraka 867 zilizoandikwa kwa mkono za Agano la Kale na maandiko mengine. Karibu 1/3 ya nyaraka zilizoandikwa kwa mkono za Hati toka Bahari ya Chumvi ni nyaraka za Agano la Kale kwa mujibu wa NIV Study Bible uk.1432. Elimukale inaonyesha kuwa Biblia ambayo Yesu aliijua ilikuwa imehifadhiwa. Nahal Hever ni pango karibu na Engedi, ambalo lina kipande kilichoandikwa kati ya mwaka 50 K.K. na 50 B.K. cha Manabii Wadogo katika lugha ya Kiyunani. Huko Masada, kulikuwa na nakala ya kitabu cha Yoshua iliyoandikwa mwaka 169-93 K.K. Mafunjo ya Nash (Nash Papyrus), yaliyoandikwa mwaka 150 K.K., yana amri kumi. Hati ya wadi Muraba’at ya Manabii Wadogo iliandikwa karibu mwaka 132 B.K.
4. Waandishi wa kanisa la awali, kuanzia kama mwaka 97/98 B.K, walilitumia Agano la Kale mara nyingi sana.
Angalia kwa orodha ya angalau waandishi 15 wakristo hadi mwaka 258 B.K waliotumia Agano la Kale.
5. Waandishi wa Kiyahudi, ingawa walikuwa maadui wa ukristo, walilihifadhi Agano la Kale lile lile lililomo kwenye Biblia za kiprotestant za leo. Kipekee, waandishi wa kiyahudi Philo na Josephus walitumia Agano la Kale mara nyingi sana.
Kwa muhtasari, Mungu ni Mwenye enzi, ajuaye yote, na asiye na uzembe wa aina yoyote ile. Tunaweza kuamini kuwa ameweka muelekeo sahihi kwa wote wanaotafuta kumfuata kokote anakowaongoza.
Swali la 2: Je tunaweza kuliamini Agano Jipya?
Jibu: Ndiyo, kuna sababu tano zinazofanana na zile zilizotangulia, kuanzia na tumaini kuwa Mungu hataruhusu watoto wake wadanganywe kabisa, hadi kwenye ushahidi mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa mkono.
1. Mungu ameahidi kulinda neno lake katika Isaya 55:10-11; 59:21; 1 Petro 1:24-25, Mathayo 24:35. Tunaweza kumwamini Mungu.
2. Nyaraka za zamani zaidi zilizoandikwa kwa mkono zilizolindwa ni pamoja na:
100 B.K. uk.6 (kipande cha Luka)
117-138 B.K. John Rylands (Yohana 18:31-33,37-38)
100-150 B.K. Chester Beatty II (uk.45)
125-175 B.K. - Bodmer II (uk.66)
125-175 B.K. uk.104 (kipande cha Mathayo)
Zaidi ya nyaraka 30 zilizoandikwa kwa mkono zilizoandikwa kabla ya mwaka 300 B.K.





