Sunday, April 10, 2016

JE, MUHAMMAD AU JIBRIL NI ROHO YA KWELI/ROHO MTAKATIFU?



Leo nitawajibu Waislam wote duniani kwa kutumia Biblia Takatifu kuwa Muhammad hakuwa Roho ya Kweli kama alivyo ahidiwa na Yesu Kristo ambaye ni Bwana na Mwokozi wetu.
Mara nyingi Waislam wanauliza, "Roho ya Kweli ni nani ambaye Yesu alimuhadi katika Yohana 16 aya ya 12 mpaka 14.
Nimekuwa nikiwauliza Waislam, hivi wao wanafikiri huyu Roho wa Kweli ni nani? Na wakanijibu kuwa huyo Roho wa Kweli ni Malaika Jibril.
Yohana 16:13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Zaidi ya hapo, Waislam wengi wanadai kuwa, Yesu alikuwa anamtabiri Muhammad, na wakati huo huo, wengine wanasema kuwa alikuwa anatabiriwa Jibril. KINYUME CHAKE, kama ilivyo shahidiwa katika Yohana 16 aya 13, Yesu alikuwa anamzungumzia Roho Mtakatifu. Tunafahamu hili kwasababu Yesu anamzungunzia Roho ambaye atawaongoza Wanafunzi wake kuanzia wakati huo na sio miaka mamia baadae.
Ukiisoma Biblia kwa makini kuanzia Yohana 16 aya ya 5 mpaka 15 utagundua hapo hapo kuwa Waislam wote pamoja na Allah wao ni waongo.
Lakini, kuna njia nyingi tunaweza kuzitumia kufahamu kama Waislam wako sahihi katika ufafanuzi wao kwa kuangalia na au soma kila wakati Yesu alipo sema "ROHO" katika Injili hiyo hiyo ya Yohana na tuone kama kweli alikuwa anamtabiri Muhammad wa Waislam katika aya mojawapo.
UTHIBITISHO WA KWANZA:
Yohana 1 aya ya 32 inasema: Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake "YESU".
Wote tunafahamu kuwa Muhammad hakuwa Mtakatifu na vile vile hakuwa anapaa kama ndege na alikuja miaka 600 baada ya Kristo, hivyo basi, ni dhahiri kuwa Roho Mtakatifu sio Muhammad ambaye alikuja miaka 600 baadae. Yohana hakuwai mwona Muhammad.
UTHIBITISHO WA PILI:
Yohana 1:33, [ Yohana Mbatizaji anaendelea kusema] "Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu."
Yohana anaweka kiuwazi zaidi aya hiyo hapo juu kuwa Yesu ndie atakaye kuwa anabatiza kwa Roho Mtakatifu.
Kwa kifupi Yesu atamtuma ROHO ambaye ni Mwenye Nguvu ya Mungu na ni Mungu.
Je, Muhammad ni huyo Roho? HAPANA KABISA, kwasababu Yesu aliwabatiza Wanafunzi wake na zaidi ya hapo, wafuasi wake walibatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. Mda mchache baada ya Yesu kupaa kwenda kwa Baba yake Mbinguni, hivyo basi, na narudia tena, hii ilifanyika Miaka mia sita 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa. Wanafunzi wa Yesu hawakubatizwa kwa kupitia Muhammad wala Waislam hawabatizi au batizwa.
UTHIBITISHO WA TATU:

KAMA YESU ALIKUWA NI MUNGU, JE ALIKUWA ANAMWOMBA NANI?



Swali la Yesu ni Mungu na nani alikuwa anamwomba, huwa linaleta utatanishi mkubwa sana na kama usipo kuwa makini, unaweza kuanza kuuliza maswali katika imani yako ya Ukristo. Katika mijadala mbali mbali ya kidini, wanadhuoni wa Kiislam na hata Mashahidi wa Yehova huwa wanauliza:- Yesu alipo kuwa katika Bustani ya Gethemane, alikuwa anamwomba nani? Tena zaidi ya hapo, wanauliza, tokea lini Mungu akaomba msaada? Hakika maswali haya yanahitaji majibu thabit tena yenye aya za Biblia.
Ili umwuelewe Yesu kama Mungu duniani akiomba kwa Baba yake mbinguni , tunahitaji kutambua kwamba Mungu Baba na Yesu “Mwana” walikuwa na uhusiano wa milele kabla ya Yesu kuuchukua mwili wa mwanadamu. Zaidi ya hapo, itakupasa uelewe kuwa, Yesu alipo kuwa duniani alikuwa na asilia mbili, yaani Yesu alikuwa Mungu na wakati huo huo alikuwa Binadamu (Rejea katika Kijarida cha “Asilia mbili za Yesu Kristo”). Tafadhali soma Yohana 5:19-27, hasa mstari wa 23 ambapo Yesu anafundisha kwamba Baba alimtuma Mwana (pia tazama Yohana 15:10.
Katika Isaya 9:6 inatuambia kwamba Mwana alipeanwa na mtoto alizaliwa. Yesu alikuwa daima sehemu ya utatu, pamoja na Roho Mtakatifu. Utatu ulikuwa kila mara, kama, Mungu Baba , Mungu Mwana, na Mungu Roho, si miungu mitatu, lakini Mungu ni mmoja anajidhihirisha kama watu watatu. Yesu alifundisha kwamba Yeye na Baba yake ni kitu kimoja (Yohana 10:30), kumaanisha kwamba Yeye na Baba yake ni wa kiini kimoja na asili moja. Baba, Mwana na Roho ni watu watatu walio na ushirikiano sawa wakiwepo kama Mungu. Hawa watatu walikuwa, na wataendelea kuwa na uhusiano wa milele. Hawa watatu walikuwepo kabla ya mwanzo kuwepo na wataendelea kuwepo milele na milele yote.
Wakati Yesu, mwenye asili mbili kwa wakati mmoja, yaani Mungu na Binadamu, (Isaya 9:6) aliuchukua ule mwili wa mwanadamu usio na dhambi Yeye pia alichukua namna ya mtumwa, kupeana utukufu wake wa mbinguni (Wafilipi 2:5-11). Yesu Kama “Mwanadamu”, alikua na kujifunza utiifu (Waebrania 5:8) kwa Baba yake hasa wakati wa kujaribiwa na Shetani, alishitakiwa uongo na wanadamu, kukataliwa na watu wake, na hatimaye alisulubiwa. Kuomba kwa Baba yake mbinguni kulikuwa kwa kumwomba nguvu (Yohana 11:41-42) na hekima (Marko 1:35, 6:46), HAYO YOTE ALIFANYA KAMA MWANADAMU. Kuomba kwake kulionyesha utegemezi wake kwa Baba yake katika ubinadamu wake ili atekeleze mpango wa ukombozi wa Baba yake, kama ilivyoshuhudiwa katika Yohana 17. Kuomba kwake kulionyesha kwamba Yeye hatimaye alijisalimisha kwa mapenzi ya Baba yake, ambayo ilikuwa ni pomoja na kwenda msalabani kulipa adhabu (kifo) kwa kuvunja kwetu sheria Mungu (Mathayo 26:31-46). Bila shaka, Alifufuka katika mwili kutoka kaburini, akishinda msamaha na uzima wa milele kwa wale ambao watatubu dhambi zao na kumwamini kama Mwokozi.

KAZI YA MIKATABA YA DAMU NA KAFARA


Ndugu msomaji,
Ningependa tujikumbushe kuhusu "mikataba ya damu na kafara' ambayo watu wengi wanafanya bila ya kuelewa madhara yake katika maisha yetu/yako/yao.
KWANINI WATU WANATOA KAFARA:
Ukiangalia habari ya Nuhu baada ya kutoka kwenye safina Nuhu alimtolea Mungu sadaka na ile harufu ilipofika kwa Mungu; akasema hatailaani nchi tena kumbe ile harufu ina maana sana kwenye ulimwengu wa roho; vivyo hivyo wanapo mtolea shetani kafara wanalenga kumpa ile harufu na ile harufu inamfanya shetani awa tekelezee wanayohitaji. Mtu anamtoa mwanawe ili kuwapa kafara mashetani, wamtekelezee anacho hitaji kama utajiri n.k.
Mambo ya Walawi 2:12 “Vitu hivyo mtavisongeza kwa Bwana kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.” Utajiuliza hii harufu na sadaka; hapa ni kafara inayotolewa kwa mashetani.Mambo ya Walawi 3:15, 16, Hesabu 5:17, Sadaka ya vinywaji hii ni baadhi ya mila hapa kwetu ni pale mtu anakunywa pombe alafu anawapulizia watu, hii ndio inaitwa sadaka ya vinywaji inayotolewa. Sasa hii inapotolewa kwa mashetani kwenye ulimwengu wa roho wanakuja mahali pale. Hesabu 15:10; 17:24; 18:7
KUWA MAKINI NA KAFARA ZILIZOTOLEWA KWA MASHETANI:
Kumbe shetani anaweza kutolewa kafaraza aina mbalimbali inaweza kuwa ya vinywaji, uji, nafaka, harufu, watoto au watu wazima; na ni muhimu kuwa makini sana na kuhudhuria sherehe ambazo si za ki Mungu kwasababu waweza kujikuta unashiriki kwenye sadaka hiyo. Kuna watu ambao matatizo yao yamewaanza baada ya kushiriki chakula cha kafara jambo hili biblia imekataza kwasababu ya madhara yake.
Ufunuo 5:8; 8:3 hapa biblia inataja sadaka ya harufu, na ndio maana ukienda kwenye maduka mengi utakuta wameweka vitu vinaitwa ubani; Hii ni sadaka au kafala ya kuteketezwa kwa majini, Isaya 43:23; Yeremia 6:20; 17:26, Ubani na Udi ni sadaka ya kuteketezwa, kimsingi; ile harufu ndiyo inayoifanya iitwe sadaka ya kuteketezwa, kwahiyo mtu unayemuona anachoma ubani ni anakuwa anatoa kafara ya ubani. Nehemia 13:9.. sadaka za unga na sadaka za ubani. Kimsingi watu tuliookolewa hatutoi sadaka za ubani kwasababu biblia inasema maombi ya watakatifu ndio sadaka ya harufu kwa Mungu. (Yohana 19:39)
Kumbe unapoona mahali au duka ukakuta wanachoma udi kimsingi ni kwamba wanaita Mashetani ambayo yanawasaidia kuleta wateja. Na ndio maana maduka mengi yana kuwa na vitu hivi ambavyo ni kafara au sadaka ya harufu; ili majini yaite wateja. Na ndio maana watu wengi wenye majini wanapenda ubani kwasababu kile ndio chakula chao.
NGUVU YA KAFARA:
Unaweza ukajiuliza kafara inafanyaje kazi; kimsingi; sadaka au kafara ya vinywaji, damu au vyote tulivyoona ni chakula cha mashetani. Na kimsingi mashetani yapo katika ngazi mbalimbali kuanzia majoka mpaka kwenye majini majini madogo; kwahiyo wachawi au washirikina huita mashetani kulingana na ukubwa wa kafara kama ikitolewa kafara ya kuku anakuja shetani wa ngazi ndogo. Na ikitolewa kafara kubwa kama ya mtu inaliita shetani la ngazi ya juu sana. Hivyo kama mtu hajaokoka ni rahisi kutolewa kafara kwasababu anakuwa hana ulinzi wa Mungu.
TABIA ZA DAMU KATIKA BIBLIA:
Mwanzo 4:10; Adamu alikuwa na watoto wawili mmoja aliitwa Kaini na mwingine Habili; Kaini alipomuua Habili; Mungu akamwambia Kaini, Damu ya ndugu yako inanililia. Kumbe damu yaweza kulia na inaweza kuongea pia.
Kumbukumbu 12:23 Mungu anasema kuwa “…damu ni uhai”. Kumbe damu ina uhai; kwa namna hiyo kuna tabia kadhaa za damu:
i) Damu ina sauti
ii) Damu yaweza kulia
iii) Damu inaleta laana
Na ndio maana Mungu amekataza kula au kunywa damu, hii ni kwasababu hizi tatu Kumbukumbu7:27; Walawi 17:10,12
DAMU INA SAUTI (INANENA):
Damu iliyomwagika chini inaweza kunena mema au yaweza kunena mabaya,damu inenayo mema ni ya Yesu peke yake, Waebrania 12:24 inasema, “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.” Kumbe kuna damu inayonena mema (damu ya Yesu Kristo) na pia kuna damu inayonena mabaya (damu ya wanyama,ndege hata watu)
Damu yaweza kuongea mabaya juu ya mtu; damu ikimwagwa hunena na ndio maana hata nchi yaweza kuingia kwenye matatizo kwasababu ya damu inenayo iliyomwagika.
Mambo ya Walawi 19:26 “Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.” Mungu amekataza kula nyama pamoja na damu kwasababu damu ni uhai, na ina sauti. Na ukiangalia katika biblia kila mahali ambapo damu imekatazwa na uchawi pia umetajwa. Kwa maana hiyo tunajifunza kuwa uchawi upo na unaushirikiano wa karibu na matumizi ya damu.
MAFUNDO YA KICHAWI:
Ukisoma Ayubu 15:26 “Humshambulia na shingo ngumu, Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;” mafundo yapo na wachawi ndio wanayo yafunga. Wachawi wanaweza kuloga katika kufunga mafundo, hivi ni vifungo vya kichawi ambavyo hutumia kudumisha maisha ya watu. Kumbukumbu 18:11 “wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.” Kuna mafundo ya aina mbalimbali mojawapo ni mafundo ya maamuzi; yaani mtu anashindwa kuwa na maamuzi, na ndio maana watu wengi wanashindwa kupiga hatua kwenye maisha kwasababu wamefungwa katika maamuzi.
Wachawi pia hutumia mafundo haya kufunga matumbo ya kina mama ili wasipate watoto; na ndio maana ya maandiko yale yanayosema “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Mathayo 18:18. Kwenye ulimwengu wa mwili mtu anaweza akaonekana anaumwa au ana matatizo lakini katika ulimwengu wa roho anakuwa amefungwa. Luka 13:16 huyu mwanamke alionekana amepooza kumbe shetani alikuwa amemfunga.
DAMU INAVYOTENDA KAZI:
Sasa kwa kujua kuwa kila damu iliyomwagwa inauwezo wa kusema, wachawi hutumia tabia hiyo ya damu kufunga maisha ya watu. kwahiyo wanachofanya wachawi au waganga ni kuchukua mnyama na kumchinja yule mnyama na kuinuizia inene tatizo lako. Kimsingi; hii damu iliyomwagwa ndiyo inayoitwa madhabahu ya tatizo lako. Na ndio maana waganga wa kienyeji huagiza kuku, mbuzi au ng’ombe ile ni kwa ajili ya kumwaga damu ili inene mabaya juu ya mtu.
Damu inapomwagwa inatoa sauti; yaani katika ulimwengu wa roho ni sauti kubwa ili mtu akae katika tatizo; kinachotokea pale damu inaponena mashetani husikia rohoni na kwa njia hiyo mashetani yanapata mlango wa kuingia kwenye maisha ya mtu. Hivyo mashetani huja ili kutekeleza sauti ya ile damu inayonena. Kwa njia hiyo shetani amefunga maisha ya watu na kifungo kinakuwa kikubwa kulingana na wingi wa damu iliyomwagwa
DAMU INAYOTOKANA NA KUCHANJWA CHALE:
Biblia iko wazi sana kuhusu kuchanja chale kwenye miili ya watu. Mambo ya Walawi 19:28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.” Mambo ya Walawi 21:25; Yeremia 48:37 Yaani; mtu huyu sio kwamba imemwagwa damu ya mnyama kwa ajili yake bali anakuwa amechanjwa mwenyewe kwenye mwili na ameitoa damu yake mwenyewe. Kimsingi; mganga anapokuwa anachanja chale huwa ananena maneno ambayo huwezi kuyaelewa. Yale maneno ndio sauti ya ile damu iliyo mwagwa.
Utajiuliza kwanini Mungu anakataza watu kupigwa chale; kimsingi damu inayomwagika ni uhai wako, kwa lugha rahisi ni kwamba unapochanjwa chale unakuwa umeacha uhai wako kwa mganga wa kienyeji. Hivyo mganga anaweza kukuona na kukufuatilia kirahisi, hivyo akiamua kukufanya urudi kwake anaweza kukurudisha kirahisi kwasababu uhai wako umeuacha kwake.
DAMU YA YESU KRISTO:
Unaweza ukajifunza kwanini Yesu alipokuja duniani asingekufa kwa kuumwa au njia nyingine ambayo haimwagi damu, Siri kuu ya kuja Yesu duniani ni kwa ajili yetu sisi tufunguliwe na kutoka kwenye vifungo kwa damu ya Yesu ambayo yenyewe hunena mema daima.
Yaani Mungu alipoaamua kumkomboa mwanadamu ikamlazimu kuvaa mwili ili aje kuukomboa ulimwengu. Na ndio maana aliitwa Immanuel yaani Mungu pamoja nasi, naye alipokuja duniani akaenda msalabani ili atengeneze madhabahu yake kwa njia ya kumwaga damu. Na nguvu ya damu ya Yesu ni kuwa hakutenda dhambi hivyo damu yake ina nguvu dhidi ya madhabahu zote za giza.
Wakati wao wanaitia damu za mafahari na mbuzi sisi tunanena damu ya Yesu, inayonena mema. Kwa kutumia damu ya Yesu twaweza kunyamazisha damu nyingine za giza.
BOMOA MADHABAHU:
Katika jina lenye Nguvu la Yesu Kristo ninaharibu kila madhabahu za kishetani kwa Jina La Yesu. Ninabomoa madhabahu zinazoleta vifungo kwenye maisha yangu katika Jina La Yesu. Madhabahu za magonjwa, mikosi na laana ninazibomoa na kuzisambaratisha katika Jina la Yesu. Ninateketeza madhabahu zote katika Jina La Yesu.
Nyamazisha damu yoyote iliyomwagwa inayonena mabaya kwa ajiliya maisha yako:
Nanyamazisha damu zote zinazonena mabaya juu yangu katika Jina la Yesu, Nanyamazisha damu ya mbuzi na damu zote za wanyama kwa Damu ya Mwanakondoo. Ninaamuru damu yoyote inayonena mabaya juu yangu inyameze Kwa Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa Damu ya Yesu inanena mema nami kwa Damu hiyo ninanyamazisha kila damu za mashetani na damu ya Yesu inene mema kuanzia sasa.
Sasa baada ya kusoma hili jarida, ni uamuzi wako kutumia damu ya Yesu au ya Kafara za Wachawi na waganga wa kienyeji. Nakushauri uchague Damu ya Yesu ambaye inazungumza.nena mambo mema kwa ajili yako.
Katika huduma Yake,
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 10, 2016

Friday, April 8, 2016

KWANINI ALLAH NA MUHAMMAD WANAMCHUKIA ISA BIN MARYAM?

Ndugu msomaji,

Labda hukuwai jiuliza jambo hili, KWANINI ALLAH ALISEMA ISA BIN MARYAM SI CHOCHOTE? 

KWANINI ALLAH HAKUWAI SEMA KWA MANABII WENGINE KUWA WAO SI CHOCHOTE, BALI ALIMDHIHAKI KWA CHUKI MBAYA ISA BIN MARYAM?

Hebu tusome kwanza aya kutoka Suratul Al Maidah:

Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyo wabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa. http://www.quranitukufu.net/005.html

Eti, Isa Bin Maryam si chochote na anageuzwa. Hivi kuna aya gani zingine kwenye Quran zinaita mitume wengine si chochote na wanageuzwa?

Hivi kwanini Allah na Muhammad wanamchukia Isa Bin Maryam namna hii? Huyu Isa bin Maryam aliwafanya nini Allah na Muhammad kiasi cha kusema eti "WAMEKWISHA PITA MITUME KABLA YAKE". Kwani Isa Bin Maryam alikuwa anashindana na Allah na mtume wake Muhammad, mpaka kusema eti wamekwisha pita mitume kabla yake? Nani hajui hilo kuwa kulikuwa na mitume kabla ya Isa bin Maryam? Mbona Allah hakusema maneno haya machafu na ya dhihaka kwa Muhammad?

Eti, Isa na Mama yake walikuwa wanakula chakula!! Hivi wapi Isa na Mama yake walisema hawali chakula? Allah mbona unaonyesha kupaniki namna hii?

Angalia jinsi Allah anavyo endeleza chuki zake kwa Isa Bin Maryam, MARA ASEMA KAZALIWA CHINI YA MTENDE, MARA ASEME ISA KAUBWA KWA KUSEMA KUWA NA ISA AKAWA.

UTATA WA KWANZA: ISA KAZALIWA CHINI YA MTENDE
Tofauti ya kuzaliwa Isa ni hii
- Isa alizaliwa katika shina la mtende, Qr, 19:23 Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! http://www.quranitukufu.net/019.html

Umesoma mwenyewe kuwa Isa anazaliwa chini ya Mtende. SASA ONA MAAJABU YA ALLAH HAPA CHINI.

UTATA WA PILI: ISA BIN MARYAM KAUMBWA
Qr. 3 au surat Imran 59
“Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa” http://www.quranitukufu.net/003.html

Ngugu msomaji, Isa bin Maryam haijulikani alikujaje maana Allah anaweka UTATA mkubwa sana. Mara asema kazaliwa na Maryam, mara asema kaumbwa kwa kusema kuwa na Isa akawa, hivi Isa Bin Maryam alimkosea nini Allah mpaka afanywe namna hii? Allah, kwanini unamchukia Isa Bin Maryam namna hii?

Allah anaendelea kusema kuwa eti, Isa atakapo kuja tena ataoa na kuzaa watoto. Hii nayo ni chuki kubwa kubwa kutoka kwa Allah.

Soma:
ISA BIN MARYAM ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO
Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159 na Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 wanadai kwamba Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija.

Hivi kwanini Allah anapenda kulazimisha mambo? Kama Isa Bin Maryam alitaka kuwa na Mke, si angeoa alipo kuja mara ya kwanza? Lakini Allah na Muhammad wanatuambia uongo eti Isa anakuja Kuoa, hivi, kwani kuoa ni lazima?

Ndugu msomaji, nategemea unaziona chuki kubwa kubwa za Allah kwa Isa Bin Maryam, ETI ISA BIN MARYAM SI CHOCHOTE, kama vile Isa Bin Maryam alikuwa anajigamba kwa Allah kuwa yeye ni zaidi? Hivi Allah kwanini unamchukia Isa bin Maryam?

Labda kwasababu Isa bin Maryam aliumba ndege kutoka UDONGO na Muhammad hakuwai fanya muujiza hata chembe moja.

Labda kwasababu Isa bin Maryam alizaliwa bila ya Baba na Allah hana uwezo wala ubavu wa kuwa na Mwana bila ya MKEWE Allat.

Zipo sababu nyingi tunaweza zitumia kama ushahidi wa Allah na Muhammad kumuonea WIVU Isa Bin Maryam.

Swali kwa Allah na Waislam: Kwanini Allah alisema " Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume"? Kwani Allah alifikiria Isa ni nani? Allah si anadai alimuumba yeye, mbona inaonekana kama vile Allah anajibizana na mtu? Allah, hivi Isa Bin Maryam ni nani kwako? Maana inaonekana kuwa umepaniki na humjui Isa Bin Maryam.

HIVI KWANI ISA BIN MARYAM ALIJIITA NANI? Mpaka uanze kutoa maneno makali na dhihaka namna hii ambayo hukuwai sema kwa Mtume mwengine?

Eti, Isa Bin Maryam si chochote, hivi, Isa bin Maryam alisema yeye ni nani mpaka uanze kujihami namna hii NA KUSEMA "ISA SI CHOCHOTE"?

Eti, Isa na Mama yake wanakula chakula: Kwani ISA NA MAMA YAKE walisema hawali chakula?

Allah, kwanini unamchukia Isa Bin Maryam namna hii?

Sina la ziada zaidi ya kuwaonea huruma Waislam wanao fuata Allah na marehemu Muhammad wenye chuki kubwa kubwa tena kwa viumbe anavyo wana dai kuwa vimeumbwa na Allah.

Poleni sana Waislam kwa msiba huu.

Katika huduma Yake,

Mungu awabariki sana.

Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,

For Max Shimba Ministries Org,

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

April 8, 2016

Thursday, April 7, 2016

KWANINI ALLAH ANAWACHUKIA WAKRISTO NA WAYAHUDI?



Ndugu msomaji,
Leo ningependa tujifunze kuhusu chuki iliyo ndani ya Allah na dini yake ya Uislam kwa Wakristo na Wayahudi. Wengi wenu huwa mnadai na au fikiria kuwa Mungu wa Biblia aliye jaa upendo ni huyo huyo wa kwenye Quran ya Jibril. La hasha.
Allah ambaye ndie mungu wa Waislam yeye amejaa chuki na anawataka na kuwaamrisha Waislam wote kuifanya chuki iliyo ndani ya Quran. Maana Quran ni kama Katika kwa Waislam.
Hebu anza moja kwa moja kusoma chuki za Allah:
ALLAH ANAWAAMBIA WAISLAM WOTE KUWA: NI MARUFUKU KUWA MARAFIKI NA WAKRISTO:
Surat Al Maida 51. Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.http://www.quranitukufu.net/005.html
SASA, kama Allah ni Yehovah wa Biblia, mbona hatusomi Mungu wa Biblia akisema muwachukie watu ambao sio wa imani yenu?
SOMA Luka 6:35 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
35 Bali, wapendeni adui zenu, watendeeni mema. Wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo mtapata zawadi kubwa nanyi mtakuwa wana wa Mungu Aliye Juu. Yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na watu waovu.
MUNGU WA BIBLIA ANSEMA Wapendini adui zenu, ni tofauti kabisa na Allah anaye sema WACHUKIENI WAKRISTO NA WAYAHUDI. Allah wa Quran sio Mungu wa Biblia.
ALLAH ANASEMA KUWA, WAISLAM HAWARUHUSIWI KUWAPENDA WAKRISTO HATA KAMA NI BABA ZAO AU MAMA ZAO AU NDUGU ZAO:
Suratul Al Mujaadalah 22. Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa. http://www.quranitukufu.net/058.html
HIVI, kweli bado unaamini kuwa Allah ni Mungu wa kwenye Biblia? Mbona sifa zake zote ni za SHETANI aliye semwa kwenye Biblia?
ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA WAISLAM WASIWAFANYE WAKRISTO NA WAYAHUDI KUWA MARAFIKI ZAO.
Surat An Nisaai 144. Enyi mlio amini! Msiwafanye Wakristo na Mayahudi kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu? http://www.quranitukufu.net/004.html
Allah anaendelea kuonyesha sifa za Shetani. Leo anasema na kuwaamrisha Waislam kuwa, WASIWE NA URAFIKI NA WAKRISTO. Hivi Mungu gani huyu anaye penda kuchonganisha watu? Hii tabia ya chuki ni ya nani kama si SHETANI?
Hebu tumsome YESU WA KWENYE BIBLIA ANASEMA NINI?
‘Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. MWIVI HAJI ILA AIBE NA KUCHINJA NA KUHARIBU; MIMI NALIKUJA ILI WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. ‪#‎YOHANA‬ 10:7-15
ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA WAISLAM NI MARUFUKU KUWA NA UMOJA NA WASIO WAISLAM
Surat Al Imran 118. Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.
Allah anaendelea kupanda chuki kubwa kubwa kwa Waislam, sasa anasema kuwa Waislam wasiwe na wasiri na watu ambao sio Waislam, hata kama huyo mtu ni Baba yao, mama yao nk. Hii chuki inapatika kwa SHETANI na sio Mungu wa kwenye Biblia.
ALLAH ATEREMSHA YA NA KUSEMA KUWA WAKRISTO NI MAADUI ZA WAISLAM.
Surat An Nisaai 101. Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.
ALLAH AWAAMRISHA WAISLAM KUWAKATAA WAKRISTO
Surat Al Mumtahinah 4 ...............Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake.
ALLAH AWAAMRISHA WAISLAM KUPIGANA NA KUWAUWA WAKRISTO.
Surat Tawba 123. Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mngu
Mwana wa Mungu siku zote Shetani kazi yake ni kuiba, kuua na kuharibu. Ndiyo kazi yake. Hajawahi kubadilika. Toka afukuzwe mbinguni hiyo ndo imekuwa kazi yake hapa duniani. Na Bwana Yesu amelisema hilo bila kumung’unya maneno. Bwana Yesu dhamira yake ni kutupa uzima tele.
Adui siku zote amekuwa ni muuaji tu. Kila sehemu anakopita yeye ni mharibifu. Huwa inafika mahala najiitisha kikao na kujiuliza sisi wanadamu tuna matatizo gani. Kwa nini kufanya urafiki na Shetani na kukubali kuwa mtumwa wake? Unapokubali kuwa mtenda dhambi maanake umekubali kufanya urafiki na Shetani maishani mwako.
Mwana wa Mungu Bwana Yesu anasema yeye amekuja ili wanadamu WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE.
Ikiwa adui amepora chochote ndani yako, ameua chochote ndani yako, amefanya uharibifu wowote ndani yako, ndani ya ndoa yako, au ndani ya familia yako, ndani ya kazi yako, ndani ya biashara yako, katika ukoo wako, kwa watoto wako, kwa wazazi wako, basi nakutangazia BWANA YESU ALIKUJA ILI UWE NA UZIMA, KISHA UWE NAO TELE. Ni ombi langu Bwana akupe uzima tele katika kila eneo adui alifanya uharibifu. Kama ilikuwa kwenye ndoa, kwenye biashara, kwenye kazi, kwenye kuutafuta uso wa Mungu. katika kupata watoto, kupata mume, kupata mke n.k Bwana akupe hitaji lako.
Shetani yuko chini ya miguu yako mpendwa, simama kurudisha chochote adui alikuwa amefanya uharibifu dhidi yako na usikubali kushindwa na Shetani. Yesu aliyemo ndani yako ni mkuu kuliko Shetani. Anataka akupe uzima tena uzima tele.
Barikiwa sana.
Yamkini unataka kuokoka? Basi wasiliana nasi tukusaidie
kuchukua uamuzi mwema wenye busara maishani mwako.
Yesu anakupenda.
Katika huduma Yake,
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 7, 2016

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA KWANZA)


Ndugu msomaji,
Mwezi huu nitaweka mada kadhaa zitakazo fundisha kuwa, Isa wa Quran na Yesu wa Biblia ni wawili na tofauti:
MAANA YA JINA ISA
Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe. Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?
JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?
JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.
Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.
Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
Leo tumejifunza kwa kifupi tu kuwa, Jina la ISA lenye maana ya Wekundu unao zidiana na weupe ni TOFAUTI KABISA NA Jina la Yesu lenye maana ya MWOKOZI katika Biblia. Zaidi ya hapo, tafsir ya Jina la Yesu kwa Kiarabu ni Yasu na sio Isa kama ambavyo Waislam wanadai katika vitabu vyao.
Mungu awabariki sana na tuendele kujifunza Neno lake bila ya kuchoka.
Katika huduma Yake,
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 7, 2016

JE YESU WA WAKRISTO NDIYE YULE ISA WA WAISLAM?

Ndugu msomaji,
Mara kwa mara, unaweza kuwasikia Waislamu wakisema kuwa Isa a.s. kama anavyotajwa ndani ya Qur’an tukufu, ndiye Yesu Kristo wa Nazareti, kama anavyotajwa ndani ya Biblia Takatifu.
Wanafanya hivyo kwa kulinganisha baadhi ya aya zilizomo ndani ya Biblia Takatifu, na zile zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa mfano, wanasema kwa mujibu wa Biblia mama yake Yesu Kristo anaitwa Mariamu. Wanasoma katika Injili ya Marko 6:3-4“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose na Yuda na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” .
Wanafananisha aya hiyo na ile iliyomo ndani ya Qur’an katika Suratul Al-Maidah, 5:75 “ Masih bin Maryam si chochote ila ni mtume tu……”,
Hoja nyingine wanayoitumia ni kusema kwamba eti jina Isa ni katika lugha ya Kiarabu. Jambo hilo siyo kweli. Kwa sababu katika lugha ya Kiarabu, Yesu anaitwa Yasu’a siyo Isa. Na ikumbukwe kuwa Biblia ndicho kitabu kilichotangulia kuwepo duniani miaka ipatayo 1500 kabla ya Qur’an.
Hoja yetu kwa Waislamu ni hii nani aliyebadilisha jina Yasu’a kuwa Isa?. Jina Yasu’a linashabihiana zaidi na Jina Yehoshua ambalo hilo ni katika lugha ya Kiebrania, na katika Kiyunani lugha iliyotumika kuandika Agano Jipya anaitwa Iesous (tamka Yesu) tafsiri ya maneno hayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mwokozi.
Tunasoma hayo katika Math 1:21-23 “ Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa Nabii akisema Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.”
Hoja yetu Je Isa a.s naye ni Mwokozi na Imanueli kama alivyo Yesu Kristo?
Jambo jingine tunalopaswa kulizingatia tunapoangalia tofauti zao ni kuhusu mama zao. Mama yake Yesu Kristo ni Mariam anayetoka katika ukoo wa Yuda. Tunasoma hayo katika kitabu cha Mwanzo 49:10 “ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii”.
Unabii huu umetimia kwa Yesu Kristo.Tunasoma hayo katika Waebrania 7:14 “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani”
Lakini tusomapo habari za Isa, yeye mama yake anatoka ukoo wa Imrani. Ambaye ni baba yao Haruni, Miriamu na Musa.
Tunayasoma hayo katika Suratul Al-Maryam 19:28 “Ewe dada yake Haruni. Baba yako hakuwa mtu mbaya. Wala mama yako hakuwa hasharati”.
fafanuzi unaoifafanua aya hii ya 19:28 uliyomo ndani ya Qur’an, tafsiri ya King Fahd uk. 405, unasomeka hivi “ This Harun (Aaron) is not the brother of Musa (Moses), but he was another pious man at the time of Maryam (Mary)”
Tafsiri “Huyu Harun siyo ndugu yake Musa, bali alikuwa ni mtu mwingine tu mcha Mungu, aliyeishi wakati wa kipindi cha Maryam”
Kwa mujibu wa Biblia, Haruni ni mtoto wa mzee Amran na mama yao anaitwa Yekobedi na kwao wamezaliwa watoto watatu Haruni, Miriam na mdogo wao Musa. Tunasoma hayo katika kitabu cha Hesabu 26:59 “Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi binti wa Lawi ,ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amram Haruni,na Musa,na Miriamu umbu lao”
Tofauti nyingine ni kuumbwa kwao: ISSA KAUMBWA. Qur’an Suratul Imran, 3:59 “ Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa”
Lakini tusomapo kumhusu YESU, YEYE HAKUUMBWA BALI NI NENO LA MUNGU.
Yoh 1 : 1,14 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu……..Naye Neno alifanyika mwili akakaa kwetu…….”
Mika 5:2 “ Bali wewe, Bethlehem Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”
Yoh: 8:58 “ Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahim asijakuwako, mimi niko”.
Zaidi ya hayo Biblia inatujulisha kuwa yeye ndiye Muumbaji mwenyewe
Yoh 1:3 “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”
Kol 1:16-17 “ Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana ; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake”
2) (A) ISSA A.S : BAADA YA KUONDOKA KWAKE, (KAMA WAISLAMU WANAVYOAMINI), HAJAWAHI KUTOKEA KWA NAMNA YOYOTE ILE.
(B) YESU KRISTO: BAADA YA KUONDOKA KWAKE ALIMTOKEA PAUL (SAUL).
Mdo 9:4 “ Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema , Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe”
3) (A) ISSA A.S: ALITABIRI KUJA KWA MUHAMMAD Quran Suratul As Saff , 61:6
“Na (wakumbushe) aliposema (Nabii) Isa bin Maryamu (kuwaambia mayahudi) enyi wana wa Israili! mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu. Nisadikishaye yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati. Na kutoa habari njema ya mtume atakayewajia nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad(Muhammad). Na maana ya majina mawili yote haya ni moja. Maana yake Mwenye kushukuriwa kwa maneno yake mazuri na vitendo vyake vizuri na kila chake kwani vyake vyote ni vizuri).Lakini alipowajia kwa hoja zilizowazi walisema: “ Huu ni udanganyifu uliyo dhahiri”.
(B)YESU KRISTO ALIMTUMA ROHO MTAKATIFU KATIKA SIKU YA PENTEKOSTE.
Yoh: 14:26 “.Lakini huyo Msaidizi,huyo Roho Mtakatifu,ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,atawafundisha yote,na kuwakumbusha yote niliyowaambia”. Katka Kiyunani anaitwa “Paracletos” yaani msaidizi au mfariji
Yoh 15:26 “ Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia”
Yoh 16:7 “Lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke,kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu”.
4) (A) ISSA A.S : JINA LAKE HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI
Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……”
(B) YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU. Mdo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
Baadhi ya aya ndani ya Qur’an zinaeleza kuwa Isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu Batromayo.
Aya zingine zinasema Isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao?
Yesu alimfufua Lazaro.
Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu?

POSA SABA (7) ZA MUHAMMAD ZILIZO KATALIWA

1. Kwanini baadhi ya wanawake walikataa posa za Muhammad?
2. Kwanini muhammad aliendelea kuomba/toa posa na huku zikikataliwa?
Ndugu msomaji,
Leo nitakua ushahid kadhaa kuonyesha jinsi Muhammad alivyo penda wanawake lakini wengine walikataa posa zake na kuto jali utume wake alio pewa na Mkewe.
Muhammad alimwomba amuoe Ghaziyyah kwa sababu ya uzuri wake, lakini alikataliwa. Tabari anadai kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu lakini hatoi ushahidi. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136. Hakuna ushahidi kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu na kwamba Muhammad hakuwa makini kwa kutokumwadhibu, au kwamba hakuwa mwaminifu na Muhammad alimwadhibu.
Layla aligusa bega la Muhammad tokea nyuma na kumuomba amuoe. Muhammad alikubali. Ndugu za Layla walisema, "Ni jambo baya kiasi gani ulilolifanya! Wewe u mwanamke anayejiheshimu, lakini Nabii ni mpenda wanawake. Tafuta kujitengua toka kwake." Layla alikwenda kwa Nabii na kumuomba aikane ndoa hiyo na aliafikianana na hilo [ombi]." al-Tabari juzuu ya 9 uk.139.
Kutoka al-Tabari juzuu ya 9 uk.140-141, Muhammad alimposa lakini aliishia kutokumuoa:
1) Umm Hani’ bin Abi Talib [Hind] kwa sababu alikuwa na mtoto.
2) Duba’ah binti ‘Amir lakini alikuwa mzee sana.
3) Inaripotiwa kuwa alimposa Saffiyah binti Bashshamah, mateka. Alitakiwa achague mmoja kati ya Muhammad na mume wake, na alimchagua mume wake.
4) Umm Habib bint al-‘Abbas lakini kwa kuwa al-‘Abbas alikuwa kaka wa kulelewa pamoja naye kwa hiyo isingeruhusiwa kisheria kwa hiyo Muhammad aliamua kujiondoa.
5) Jamrah binti Al-Harith. Baba yake alida isivyo sahihi kuwa alikuwa anasumbuliwa na kitu Fulani. Aliporudi, alikuta ameisha kumbwa na ukoma.
Haielezwi kwa kauri moja endapo Umm Hani’ alikuwa muislam kabla au baada ya Muhammad kumwomba amuoe. al-Tabari juzuu ya 39 uk.197 na rejeo chini ya ukurasa 857 uk.197.
Ndugu msomaji ambaye ni mfuasi wa dini ya Uislam, je, unaweza tumabia kwanini posa 7 za Muhammad zilikataliwa?
Max Shimba Ministries Org.

JE, YESU ALITUMWA KWA ISRAELI PEKE YAKE (MATHAYO 15:26)?



Ndugu msomaji,
Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi), ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.
Imeandikwa:
Akajibu akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).
Mungu ni Mungu wa utaratibu na ratiba kamili. Ndiyo maana hakuumba kila mtu kwa mara moja. Alianza na mtu mmoja tu, kisha wengine wote tukatokea kwa huyo mtu. Vivyo hivyo, alianza kwa kujifunua kwa taifa moja tu duniani kote. Kisha kutokea hapo ndipo wokovu unasambaa kwenye mataifa yote. Ni ukweli ulio wazi kwamba, ukiacha Israeli, jamii zote zilizobakia duniani, kwa asili zilikuwa zikiabudu miungu (yaani mashetani). Ni Israeli peke yao ndio ambao kwa asili walianza na Mungu wa kweli.
Ndiyo maana Bwana Yesu alipoongea na mwanamke Msamaria pale kisimani alimwambia hivi:
Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. (Yohana 2:22).
Wokovu unatoka kwa Wayahudi kwa sababu hakuna taifa jingine lolote duniani ambalo lilimjua Mungu wa kweli – yote yalikuwa na dini za kipagani – iwe ni wazungu, Waafrika, Wahindi, Waarabu, n.k. Huo ndio ukweli.
Kusema kwamba Yesu hakuja kwa ajili ya mataifa yote hakuna tofauti na kusema kuwa, kwa vile Mungu alimuumba Adamu na Hawa peke yake, basi Yeye si wa familia yangu maana hakuniumba na mimi kama alivyomuumba Adamu.
Yesu aliongea na wanafunzi wake siku moja na akawaambia kuwa:
Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanzia tangu Yerusalemu. (Luka 24:46-47).
Je, unaona kwamba Injili inatakiwa kuanzia Yerusalemu? Na je, unaona pia kwamba anasema kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake? Je, mataifa yote ni Israeli peke yake?
Mwanamke Mkananayo alikuja wakati usio wake. Huo ulikuwa ni wakati wa kuhubiri Injili kwa Israeli kwanza ndipo iende ulimwenguni kote.
Ufuatao ni ushahidi zaidi wa maneno ya Bwana Yesu mwenyewe kuthibitisha kwamba alitumwa kwa mataifa yote ulimwenguni na kwamba Yeye ndiye Masihi wa Mungu, yaani aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu wote.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. (Matendo 1:8).
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19).
Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. (Yohana 3:17).
Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. (Yohana 12:47).
Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. (Yohana 10:15-16).
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. (Mat 24:14).
Nihitimishe kwa kurejea tena mambo machache niliyoyasema. Mungu amekuwa na kawaida ya kuanza jambo na mtu mmoja.
Aliumba mwanadamu mmoja, kisha tukatokea humo wote.
Alijifunua kwa taifa moja, kisha tukamjua wote.
Alianza na Mwana mmoja (Yesu), kisha tunazaliwa wote kwa imani katika huyo.
Vivyo hivyo, alileta wokovu kwa taifa moja la Israeli, kisha unasambaa kote – ndiyo maana anasema na mwanamke Msamaria pale kisimani – “Wokovu watoka kwa Wayahudi.” (Yohana 4:22).
Hali hii ya kuanza na mtu au sehemu moja, ni ushahidi kuwa wale wote wanaojifariji kwa maneno eti “dini mbalimbali ni njia tofauti ambazo zote zinaishia kwa Mungu”, wanajidanganya na kupoteza muda wao na uzima wao wa milele! “Wokovu watoka kwa Wayahudi” – yaani KWA YESU PEKEE!
Sasa, kwa kuwa muda wa kusambaa kwa wokovu huo ulikuwa haujatimia (maana Mungu anakwenda kwa ratiba ya majira na nyakati), ndiyo maana akamwambia yule mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi) kuwa hakutumwa ila kwa Israeli.
Lakini utimilifu wa majira ulipofika, yaani alipokufa na kufufuka, tunaona akiwaagiza sasa mitume wake waende ulimwenguni kote.
Na Biblia inasema wazi: Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. (Waefeso 2:11-16).
Tafakari
Hoji mambo
Jiulize
Chukua hatua
By permission NIV, NKJV, Waislam kwa Yesu, James John, Tanzania Bible Society.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 6, 2016

UISLAM HAUKUTOKA KWA MUNGU

MA-IMAMU, MASHEHE, NA USTAADH HAWAKUTAJWA KWENYE QURAN
ALLAH ASHINDWA KUTUONYESHA SIFA ZA VIONGOZI WAKE KWENYE QURAN
Ndugu msomaji,
Tukisema kuwa Uislam ni bandia, ndugu zetu wanakuja na madai kuwa tunasema uongo na maneno mengi yasio na hata ushahid wa aya.
Leo ningependa kuwauliza Waislam.
1. Wapi katika Quran Allah kasema Uislam uwe na Ma-Imamu, Mashehe na Maustaadhi?
2. Tupeni sifa za Imamu kwa kutumia aya za Quran.
3. Tupeni sifa za Mashehe kwa kutumia aya za Quran.
4. Tupeni sifa za Ustaadh kwa kutumia aya za Quran.
Ningependa ndugu Waislam watupe aya moja kwa moja. Mimi leo hii sina muda wa ngonjera zisizo na aya. Watuletee aya. Mimi nataka kusilimu.
Mkishindwa tuletea aya basi sisi tutaiamini vipi dini yenu ambayo haina mwongozo kutoka kwa Allah wenu?
Kama Adam alikuwa Nabii, basi kutakuwa na aya inayo onyesha Adam akipewa huo unabii, lakini nilipo wauliza Waislam, walishindwa nijibu na kunitukania Yesu wangu bila ya sababu yeyote ile.
Nilipo waomba wanionyeshe, kama Adam aliingia Msikitini, waislam waliendelea kutokwa mapovu kama vile mimi ndie nilisema kuwa Adam alikuwa Muislam.
Basi leo sitawauliza kuhusu Adam, bali leo nataka mnipe aya zinazosema muwe na Ma Imam, Sheikh, na Ustaadh.
Waislam wanasema eti hii aya kwenye Surat Al Baqara inazungumzia Imam: 124. Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. Link:http://www.quranitukufu.net/002.html
Hapo kwenye hiyo aya hakuna cha Imamu wala Shehe zaidi ya Allah kudai anampa uongozi Ibrahimu.
Mkishindwa kutuletea aya kutoka Quran zinaso sema kuwa muwe na hao viongozi wenu wa dini, basi ifahamike kuwa Uislam ni dini ya bandia na kujitungia wenyewe.
Lakini tunapo soma Biblia iliyo kamilika tunapewa aya kuhusu viongozi wa Kanisa. Ngoja niweka aya chache ili kusaidia mada:
SIFA ZA WAANGALIZI WA KANISA KATIKA BIBLIA
Bwana alikuwa wazi sana katika neno lake kuhusu jinsi Yeye anataka kanisa lake duniani kwa lipangwe na kusimamiwa. Kwanza, Kristo ni kichwa cha kanisa na mamlaka yake makuu (Waefeso 1:22; 4:15, Wakolosai 1:18). Pili, kanisa lenyewe linafaa kujitawala, liko huru kutoka mamlaka yoyote ya nje au udhibiti, na haki ya kujitawala na uhuru kutokana na kuingiliwa na uongozi wowote wa watu binafsi au mashirika (Tito 1:5). Tatu, kanisa linastahili kutawaliwa na viongozi wa kiroho likiwa na ofisi mbili kuu - wazee na mashemasi.
MA-ASKOFU NA WACHUNGAJI KATIKA BIBLIA
1 Timotheo 3: 1 Hili ni neno kweli, kwamba mtu akitamani
kazi ya askofu, atamani kazi nzuri. 2Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi,
anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. 3Asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. 4Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. 5(Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?) 6Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya Shetani.
7Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.
MASHEMASI KATIKA BIBLIA
Sifa Za Mashemasi 8Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu
wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali. 9Inawapasa kushikamana sana na ile siri ya imani kwa
dhamiri safi. 10Ni lazima wapimwe kwanza, kisha kama hakuna neno dhidi yao, basi na waruhusiwe kuhudumu kama mashemasi.
11Vivyo hivyo wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasiozungumza maneno ya kuwadhuru wengine, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo. 12Shemasi awe mume wa mke mmoja na inampasa aweze kusimamia watoto wake na
watu wa nyumbani mwake vema. 13Wale ambao wamehudumu vema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Kristo Yesu.
USHAHID ZAIDI: Tito (1:1-4), Tito (1:5—3:11) na Tito (2:11-15)
Ndugu msomaji, nimethibitisha kwa aya kuwa Wakristo wao hawajajitungia vitu bali kuna aya zinazo ongoza jinsi ya kupata hawa viongozi, lakini kwenye Quran na Uislam, hatuoni aya yeyote ile inasema kuwa Waislam wawe na Maimam au Shehe au Ustaadhi na wawe watu wa aina gani.
Mimi leo ningependa Waislamu watuambie, kwanini wana Imamu, Shehe Ustaadh kwenye dini yao/ Hakika Uislam ni dini iliyo jaa shaka na MSIBA mkubwa sana kwa Muhammad.
1. Kumbe "Ma Imam" ni vyeo vya bandia.
2. Kumbe "Ma Shekh" ni vyeo vya bandia.
3. Kumbe "Ma Ustaadh" ni vyeo vya bandia.

Nawakaribisha Waislam waje kwenye Ukristo wenye viongozi walio barikiwa na Mungu na kutajwa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Ministries Org.

Neuroplasticity, Spiritual Formation, and Holistic Redemption in Christ

Neuroplasticity, Spiritual Formation, and Holistic Redemption in Christ By Dr. Maxwell Shimba, Shimba Theological Institute Introduction ...

TRENDING NOW