Friday, May 6, 2016

WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI?

(SEHEMU YA KWANZA)
Ndugu msomaji,
Leo tunaanza na mada hii kubwa ambayo inauliza na kuwaomba Waislam watuletee uthibitisho wa Muhamamd akisilimu na kuwa Muislam.
Tunaposoma kitabu cha maisha ya Muhammad S.A.W. kilichoandikwa na aliyekuwa kadhi mkuu wa Kenya na Zanzibar Sheikh Farsy ukurasa wa 5 kuna maneno haya…
Pale pale alfajiri alipokwisha kuzaliwa mtume alikwenda kuitwa babu yake kuja kumwona mjukuu wake. Babu huyu alifurahi sama na akamfunika maguo mjukuu wake, akajikongoja naye mpaka kwenye Al-ka’ba akafungua mlango akaingia ndani, akasimama, akamwombea dua kwa mashairi mazuri ya kiarabu aliyoyatunga mwenyewe wakati ule ule, kisha akarejea naye na jua bado halikuchomoza.
Hapa tunaona Babu yake Muhammad akimchukua mjukuu wake Ndani ya alkaaba alfajiri kwenda kumfanyia ibada, kumkabidhi kwa Mola wake, kutia wakfu.
Lakini je Kuna nini Hapa cha kuzingatia?
(1) imani ya Abdul muttalib ilikuwa hii.
Katika kitabu " Acha Biblia Iseme" kilichoandikwa na mwanachuoni maarufu wa kiislamu aitwae Ali muhsin Barwani ukurasa wa 153 tunasoma maneno haya; “hapakutokea mwarabu ambaye alipewa jina hilo(Muhammad) na babu yake tangu kuzaliwa kwake, na huyo babu hakuwa Mkristo bali alikuwa akifuata mila za kishirikina.” Na wala hakujua taurati wala injili." mwisho wa Nukuu
Ushahidi wa wazi unaothibitisha kuwa babu yake Muhammad Abdul muttalib pamoja na kuomba miungu haswa mungu Hubaal sanamu kuu ndani ya alkaaba; vilevile aliomba dua kwa Allah; Mungu atakayerithiwa baadaye na mjukuu wake katika uislamu; ushahidi tunaupata tunaposoma utangulizi wa suratul al-fyl ulio katika juzuu ya ukurada wa 946 Qurani iliyotafsiriwa kwa kiswahili chapa ya nane tunasoma maneno hayo. “chifu mkuu wa makka zama hizo alikuwa Abdul muttalib, alikwenda al ka’ba pamoja na baadhi ya machifu wa kikuraish na akilishika komeo la chuma la mlango wa al-ka’ba, akamwambia Allah (S.W.0 kuilinda nyumba yake pamoja na wahudumu wake. Zama hizo kulikuwa na masanamu 360 ndani na kando ya Al- ka’ba.”
Ndugu zetu kiuanadamu waislamu Wanadai kwa mujibu wa Quran 30:30 sote tunapozaliwa tunazaliwa Hali tukiwa waislamu ila wazazi wetu uja na kutuondoa kwa uislamu Ima kwa Mfano kubatiswa na kadhalika. Hivyo na Hapa tunaona Mtoto huyu alipozaliwa mwanzo alipewa Jina na babu yake aliyekuwa mshirikina Kisha babu huyu Zamani za kabla ya uislamu alijikokota na mjukuu wake hadi alkaaba na alfajiri Ile kumtoa wakfu.

WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI?


(SEHEMU YA PILI)
Ndugu Waislam,
Asanteni kwa majibu yenu katika Sehemu ya Kwanza ya Huu Mjadala Mzito ambao mpka sasa bado hamjatoa majibu kuthibitisha lini Muhamamd alisimu, badala ya Waislam kutoonyesha wapi Muhammad Kawa mwislamu kwa hoja hii na hii wenzetu wanabaki tu kwenye Hali ya kujaribu kujibu Yale niliyokuwa naelezea pasina mwanzo kutupa somo kuonyesha wazi mwezetu huyu Hana hoja. Pili Waislam wanadai tu kuwa kwa mujibu wa Qurani 30:30 Muhammad atakuwa kazaliwa muislamu na hili pia linazua balaa kama tutakavyoona , na ndio maana nikaanza kwa kutuonyesha kuwa Babu yake ambaye alikuwa mshirikina tena alikufa katika hiyo Hali ya ujahiliwa aliwahi kumpeleka mjukuu wake Ndani ya alkaaba wakati huo ikiwa na miungu 360 ya kikafiri wakati wa swala ya alfajiri akamtia wakfu kwa dua ila kumwandaa kwa siku za usoni. Kupanga pia kafiri huyu mshirikina ndiye aliyemchagulia mjukuu wake jina sio kama jina la Yohana au Ishmael au Yesu yaliyoletwa na Malaika. Jina ili ndilo alilotumia hata baada ya kujibashiria utume.
Lakini pia tunapo soma kwenye sura ya 93: kuna maneno haya; "Naapa kwa mchana! 2. Na kwa usiku unapo tanda! 3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. 4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. 5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. 6 Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa? 8 Akakukuta mhitaji akakutosheleza? 9. Basi yatima usimwonee! ZINGATIA MANENO HAYA :::::: NA AKAKUKUTA UMEPOTEA AKAKUONGOA!!!
Hapa kwa mwenye kutaka kufahamu Kuna mazingatio. Neno ambalo mabingwa wa tafsiri ya Qurani wamelifasiri kupotea njia ni neno "Dhaallan" kwenye Aya ya saba. Tazama the noble Quran pia hivi ndivyo walifasiri kina Ibn Kathir, Jalalayneen
Pili katika Surah ya 42:52 tunasoma "Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka."
Zingatia kauli hii ULIKUWA HUJUI KITABU WALA IMANI na ndio maana allah akasema akimwambia muhammad ulikuwa umepotea njia!!!!
MASWALI:

ALLAH WA WAISLAM SIO YEHOVA - MUNGU ALIYE UMBA KILA KITU


Ndugu msomaji,
Leo tutajifunza tofauti kati ya Allah wa Waislam na YEHOVA MUNGU ALIYE UMBA KILA KITU.
QURAN 92 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..
Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu? Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa katika aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah hakuumba.
Qr. 15 au surat Hijr 30-39,
Basi Malaika wote pamoja walimsujududia, Isipokuwa Ibilisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu. (Mwenyezi Mungu) akasema: ewe Ibilisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?
Akasema: Hiwi mimi nimsujudiemtu uliyemuumba kwa udongo unaotoa sauti! Unaotokana na matope yenye sura.
Mwenyezi Mungu akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! Na hakika juu yako ipo laana mpaka siku ya malipo.
Akasema (Ibilisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula, mpaka siku maalum.
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapo duniani na nitawapoteza wote.
Qr. 51 au Surat Adh-Dhaariyat 56 (sur aya upepo),
Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu
Kumbe Allah ni Mola Mlezi wa Shetani. Sasa kuna haja gani ya kumfuata Allah anaye mlea Shetani?
Kumbe malezi ya Allah kwa Shetani ndio yaliyo mfanya Shetani awe mbaya namna hii.
Kumbe Shetani kafundishwa ushetwain na mlezi wake Allah.
Nilipo endelea kuisoma Biblia Takatifu ambayo imekamilika, Mungu alimwabia Musa katika Kutoka 6:2, 3Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. https://www.wordproject.org/bibles/sw/02/6.htm#0
ALLAH NI MDOGO KINYUME NA YEHOVA MUMGU MKUU
Qr.92 au surat Al-Layl 1-3,
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Naapa kwa usiku unapofunika! Na mchana unapodhihiri! Na kwa aliyeumba dume na jike! Kuapa kwa Mungu kuhusu viumbe

MUHAMMAD AWANYANG'ANYA MALI MASWAHIBA WAKE


Ndugu msomaji,
Kama ulikuwa haujui, basi leo utafahamu kuwa, Muhammad alikuwa anatabia mbaya sana ya kunyang'amya Maswahiba wake mali.
Quran Surat Al Anfaal aya 1. Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini. http://www.quranitukufu.net/008.html#8:1
Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiswahili
Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ewe Nabii! Waambie: Hizo ngawira ni za Mwenyezi Mungu kwanza na Mtume wake. Basi wacheni kukhitalifiana kwa ajili ya hayo. Na uwe mtindo wenu ni kumkhofu Mwenyezi Mungu na kumt'ii. Na tengenezeni yaliyo baina yenu, na mfanye mapenzi na uadilifu ndio makhusiano baina yenu. Kwani hakika hizi ndizo sifa za watu wa Imani.
Ndugu msomaji, baada ya kuisoma aya iliyo teremshwa huko Madina, Muhammad anasema kuwa MALI WALIYO ITEKA YEYE NA MASWAHIBA YAKE, ni za kwake yeye na Allah.
Sasa, kama mali iliyotekwa vitani itagaiwaje kwa Allah ambaye Muhammad hakuwai muona?
Kwanini Muhammad alizikwapua mali zote na kuwanyima Maswahiba wake?
Ipo wapi aya ambayo Muhammad anamgawia Allah sehemu yake ya mali walizo ziteka kwenye vita?
Hakika Muhammad alikuwa mroho wa mali na alitumia ujanja ujanja katika kutengeneza dini yake ya Uislam.
MUHAMMAD ANASEMA KUWA MALI NI YA KWAKE NA ALLAH, HIVI TOKEA LINI ALLAH ANASHIDA NA AU HITAJI MALI YA MATEKA NA KUWAACHA MASWAHIBA WA MUHAMMAD MIKONO MITUPU?
Eti Muhammad anawaaambia Maswahiba wake kuwa, wao washike sala tu, lakini kwenye mali, ni zakwake yeye na Allah. Hakika huu ni wizi wa wazi wazi ambao Muhammad alikuwa anaufanya kwa Maswhiba wake.
Poleni sana Waislam kwa kumfuata huyu jamaa aliye kuwa anawaingiza Maswahiba wake Mjini.
In His Service
Max Shimba Ministries Org

MUHAMMAD APASULIWA NA KUTOLEWA SHETANI


Huu ni msiba mkubwa sana kwa Waislam.
Katika vitabu vya hadithi na vya siira yaani Maisha ya Muhammad, tunasoma: Mtume Muhammad alipasuliwa (akatolewa fungu la shetani) mara nne. Mara ya kwanza, Muhammad akiwa katika umri wa miaka mitatu. Mara ya pili, akiwa katika umri wa miaka kumi. Mara ya tatu, akiwa katika umri wa miaka arobaini. Mara ya nne pale alipoandaliwa kupelekwa Israa, akiwa katika umri wa miaka arobaini na tatu.
Naomba kunukuu
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik kuwa "Mtume s.a.w alikuwa akicheza pamoja na watoto, mara akafikiwa na Malaika Jibril (a.s) ndipo alipomchukua na akamtupa chini, kisha akapasua kwenye moyo wake, mara akautoa moyo, tena akatoa humo pande la damu akasema: Hili ni fungu la shetani (nimelitoa) kutoka kwako! kisha akaukosha (moyo wake) katika chombo cha dhahabu chenye maji ya Zamzam, kisha akaufunga na akaurejesha mahali pake.
Swali la kujiuliza, hili fungu la Shetani liliingiaje kwenye moyo wa Muhammad?
Swali la pili: Hivi tokea lini Shetani anatoka kwa kuoshwa kwa maji?
Taz: Sahih Muslim J.l Uk. 147 713.
Ujumbe tunaoupata kutokana na hadith hii ni: Malaika Jibril alimfanyia upasuaji Mtume ili atoe fungu la shetani lilikuamo ndani ya moyo wa Muhammad.
Kwa hiyo, kabla ya upasuaji huu, Mtume Muhammad alikuwa na shetani ndani yake, lakini cha ajabu Anasema Abu Huraira: amesema Mtume kuwa: "Kila mwanadamu anapozaliwa, shetani huingia katika mbavu zake kwa vidole vyake, isipokuwa Isa bin Mariam, alikwenda kumwingia, lakini akakuta pazia."..... Sasa mbona basi msije kwa Yesu amabaye hakuwai guswa na Shetani tokea kuzaliwa kwake?
Kwanini Muhammad aliingiwa na Shetani?
Natanguliza pole kwa Waislam ambao wao wanamsafisha Shetani na maji kama vile Shetani anamwili au ni uchafu fulani.
Hakika hakuna Allah sio Mungu bali ni kiumbe cha ajabu ajabu kinacho sema kuwa, eti Shetani anasafishwa na maji ya Zamzam.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
May 6, 2016

MAMA YAKE NA MUHAMMAD ALIKUFA KAFIRI


Bi Amina mamake na Muhammad kafa kafiri. tunasoma
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((اسْتَأْذَنْتُ رَبِّي أَنْ أَسْتَغْفِرَ لأُمِّي فَلَمْ يَأْذَنْ لِي ، وَاسْتَأْذَنْتُهُ أَنْ أَزُورَ قَبْرَهَا فَأَذِنَ لِي )) مسلم 
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Niliomba ruhusa kutoka kwa Allaah kumuombea msamaha mamangu, lakini Hakunipa ruhusa. Nikamuomba idhini nilizuru kaburi lake (mamangu), Naye Akanipatia ruhusa)) [Muslim]

Inaelezwa katika Kitabu cha ‘Awn al-Ma’abuud:
“Kauli yake (Muhammad) ((lakini Hakunipa ruhusa)) ina maana kuwa (mama yake) alikuwa kafiri na hairuhusiwi kumuombea maghfirah kafiri.”

Huu ni msiba mwengine kwa Waislam. Wazazi wake Muhammad wote wamekufa na dhambu kubwa kubwa na huku wakiwa MAKAFIRI.

Hivi huyu Allah mbaona aliwachukiwa sana wazazi wa Muhammad?
Je, unafahamu kuwa baba yake Muhammad na yeye alikufa akiwa KAFIRI na yupoe Jehannam?
Hakika kuna mamb ya ajabu ajabu kwenye uislamu.

LAKINI HATUSOMI KUWA MAMA YAKE YESU ALIKUFA NA DHAMBI.
Mungu awabariki sana.

Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,

For Max Shimba Ministries Org,

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

May 6, 2016

Tuesday, May 3, 2016

ALLAH WA WAISLAM SIO YEHOVA - MUNGU ALIYE UMBA KILA KITU


Ndugu msomaji,

Leo tutajifunza tofauti kati ya Allah wa Waislam na YEHOVA MUNGU ALIYE UMBA KILA KITU.

Qr. 15 au surat Hijr 30-39,
Basi Malaika wote pamoja walimsujududia, Isipokuwa Ibilisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu. (Mwenyezi Mungu) akasema: ewe Ibilisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?

Akasema: Hiwi mimi nimsujudiemtu uliyemuumba kwa udongo unaotoa sauti! Unaotokana na matope yenye sura.

Mwenyezi Mungu akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! Na hakika juu yako ipo laana mpaka siku ya malipo.
Akasema (Ibilisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa.

(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula, mpaka siku maalum.

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapo duniani na nitawapoteza wote.
Qr. 51 au Surat Adh-Dhaariyat 56 (sur aya upepo),
Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu

ALLAH NI MDOGO KINYUME NA YEHOVA MUMGU MKUU

Qr.92 au surat Al-Layl 1-3,
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Naapa kwa usiku unapofunika! Na mchana unapodhihiri! Na kwa aliyeumba dume na jike! Kuapa kwa Mungu kuhusu viumbe

Qr. 91 au surat Ash-Shams 1-7 (sura ya Jua)
Naapa kwa jua na kwa mwangaza wake. Na kwa mwezi unapoliandama. Na kwa mchana unapolidhihirisha. Na kwa usiku unapolifunika. Na kwa mbingu na kwa Aliyezijenga. Na kwa ardhi na Aliyeitandaza. Na kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza.

Qr. 92 au surat Al-Layl 1-3 (Usiku),
Naapa kwa usiku ufunikapo (kila kitu). Na kwa mchana uangazapo. Na kwa aliyeumba kiume na kike.

Hapa tunaona Allah Mungu anayeabudiwa na Waislamu anaapa kwa mbingu na kwa aliyezinjenga, kwa ardhi na aliyeitandaza. Je, huyo mtandazi wa ardhi na mjengaji wa mbingu ni nani? Qurani inaendelea kuhadithia hivi…

Qr. 45 au surat AL- Jathiyah 22 (kiyama/ kupiga magoti), Na mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki…
Qr. 44 au surat Ad-Dukhan 7-8 (sura ya moshi)

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, ikiwa mnayo yakini (basi yakinisheni haya) Hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye anahuisha na kufisha. Mola wetu na ni mola wa wazee wenu (wote) wa mwanzo (na mola wa kila kitu)

Hapa tunaona kuwa Allah kupitia Qurani anasema kuwa mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi na tena anasema hakuna aabudiwaye ila yeye.

Mjengaji wa mbingu na mtandazaji wa ardhi anajieleza hivi ……
Isaya 44:24

BWANA, mkombozi wako yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi, “Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote, nizitandaye mbingu peke yangu, niienezaye nchi. Ni nani aliye pamoja nami?”
Mungu wetu Yehova anasema mimi ninafanya vitu vyote.
(Soma Isaya 45:6-7, 11-12, Yeremia 27:5) Bila shaka Yehova ndiye muumbaji wa vitu vyote
JE Mungu Yehova aliapia vitu alivyoviumba kama Allah?

Isaya 45:22-23
Niangalieni MIMI mkaokolewe, Enyi ncha zote za dunia. Maana MIMI ni Mungu hapana mwingine. Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba, mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.

Waebrania 6:13-16
Kwa maana Mungu alipompa Ibrahimu ahadi, Kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake. Akisema “Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza, Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo kwa kuyathibitisha.

Hapa tunaona Mungu wetu Yehova haapi kwa mtu wala vitu alivyoviumba kama Allah anavyoapa, bali Yehova anasema “Naapa kwa nafsi yangu”.Waweza pia kusoma jinsi Yehova alivyoapa kwa nafsi yake katika aya hizi;
Isaya 14:24 na Mwanzo 22:16

Hapa anayeapa ni Allah,
Hivi mtu anayeapa kwa mwingine anakuwa Mungu au mwanadamu?

Je, nani aliyeumba hapo?
Maana Allah anaapa katika aliyeumba, na kuumba ni moja kati ya sifa zake Yehova Mungu kumbe Allah hakuumba chohote!


ALLAH NI MUONGO!

Tukiyachunguza maandiko matukufu ya kiislamu yaani Quran na maandiko matakatifu yaani Biblia tutawapata hao wanaume wawili kuwa na utofauti wa mbali sana.

Tukianza na Quran hizi hapa kweli za wazi kabisa:
Allah wa quran anamkana na kumkataa Yesu Kristo kama si mwana wa Mungu yaani Yehova,
Qr. 19 au surat Maryam 35
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanau, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
Qr. 112 au suratAl-Ikhlas 1-4 (sur aya utakaso)
Sema: Yeye ni Mwenyenzi Mungu mmoja (tu) Mwenyenzi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea) Hakuzaa wala hakuzaliwa Wala hana anayefanana naye hata mmoja.
Kadiri ya aya hii Allah asema kuwa mungu hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana mfano wa mtu au watu Yehova anasema hivi kuhusu mtu au watu……

Kila wanapoingizwa watu wajinga katika wavu wa huyo Mpinga-Kristoanayeitwa kwa jina ALLAH haya ndiyo maneno ya kukiri kumwabudu na kumtumikia:

Kwa kiarabu:
Ashihadu Allah ilaha inla ilah
Washihadu ana Muhamad rasuruhlah
Kwa kiswahili:
Nashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah,
Na nashuhudia kwamba Muhammad (amani na rehema ziwe juu yake) nimtumishi wake na mjumbe

Biblia inasemaje ?
1Yohane 2:22-26,
Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. Kila amkanayeMwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.

Na hii ndiyo ahadi aliyoyuahidia, yaani, uzima wa milele.
Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.

Wakolosai 1:13-15,
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana,mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

Yohane 3:16-17,
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoaMwanawe pekee, ili kila mtu amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Kwa maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.


Bila shaka Biblia Takatifu inamweka wazi ALLAH wa kila muislamu kama mwongo na Anti-Kristo ambaye waislamu wanamwita Dadjal bila ya wengi wao kujuwa kama ndiye wanaomwabudu

Sunday, May 1, 2016

KWANINI ALLAH HAWEZI KUWA NA MWANA BILA YA MKE?



Ndugu msomaji,
Leo nitawaeleza kwa kutumia aya kwanini Allah wa Waislam hana uwezo wa kuwa na Mwana bila ya kufanya tendo la ndoa, nikimaanisha kuwa na mke.
Hebu kwanza tuanze kusoma aya yake kutoka Surat AL An A'am iliyo teremk Makka:
Surat Al An A'am ayat 101. Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.
Allah anaye dai kuumba kila kitu na kudai kuwa ni mjuzi wa kila kitu anatutaarifu katika Surat Al An A'am kuwa hawezi kuwa na mwana bila ya kufanya tendo la ndao kwa Mkewe Allat. Huu ni msiba mkubwa sana, maana iweje Mungu mwenye uwezo wa kufanya atakalo sasa anashindwa kuwa na mwana mpaka afanye tendo la ndoa?
Kama kweli Allah aliumba kila kitu, mbona Miti inaweza kuongezeka bila ya tendo la ndoa? http://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK9980/
Mbona Seli zako zinazaana au ongezeka bila ya kuwa na Seli Jike na Seli Dume. Wote tunafahamu hii "Mitosis" na stages zake Nne ambazo ni "Prophase" "Metaphase" "Anaphase" na "Telophase". Sasa Allah yeye anadai ndie aliye umba Seli za zetu tena zinazaliana bila ya kuwa an Seli Dume na Seli Jike, lakini cha kushangaza, Allah yeye hawezi kuwa na Mwana bila ya Mke, je, tunawezaje muamini huyu Allah mwenye udhaifu namna hii? https://ghr.nlm.nih.gov/primer/howgeneswork/cellsdivide
Sasa, tumsome Maryamu, je aliweza kuwa na Mwana bila ya kuwa na Mume?
Maajabu ya dunia, Maryamu anauwezo wa kuwa na Mwana bila ya Mume, lakini Allah hana uwezo wa kuwa na Mwana bila ya Mke. Hakika haya ni maajabu makubwa sana, ingawa Allah atadai eti alimpa yeye huo uwezo.
Kama ni kweli, je , kwanini Allah alishindwa kujipa huo uwezo yeye mwenyewe na aweze kuwa na Mwana bila ya tendo la ndoa?
Hebu tuanze kwa kusoma Surat I'mran iliyo teremka Madina:
Surat I’mran 45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
Surat Im'mran 47. Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa. http://www.quranitukufu.net/003.html
Maryam anamuuliza Allah, iweje niweze kuwa na Mwana bila ya Mume, Allah anadai kuwa, eti Mwenyezi Mungu hufanya apendalo, kwa kuliambia jambo, kuwa na LIKAWA. Sasa, kama huu uwezo wote ni wa Allah, kwanini anashindw akuutumia kwake yeye mwenyewe na kusema kuwa na Isa Akawa bila ya kuwa na Mama wala Baba?
Hakika Allah ni dhaif na kamwe hakuumba kitu chechote kile. Uthibitisho ni huu hapa, Quran 92 1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..
Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu? Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa kwa aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah hakuumba.
Kumbe ndio maana Allah alikiri kuwa, yeye hawezi kuwa na Mwana bila ya kuwa na Mke. Waswahili wanasema kuwa njia ya mwongo ni fupi. Leo tumesha mgundua Allah anaye apa kwa Aliye umba kiume na kike.
Kama Allah ndie aliye umba kila kitu,
1. Kwanini hawezi kuwa na Mwana bila ya Mke?
2. Kwanini Maryamu aliweza kuwa na Mwana bila Ya Mume?
3. Kwanini Allah anashindwa kutumia uwezo wake anao dai kumpa Maryamu aliye weza kuwa na Mwana bila ya Mume, kwa kupata Mwana bila ya MKE?
Hapa kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu huyu Allah ambaye anaonyesha udhaifu mkubwa sana baada ya kushindwa kupata Mwana bila ya Mme.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
May 1, 2016

Saturday, April 30, 2016

MAJINA YA MUNGU WA BIBLIA


MSIFU MUNGU KWA MAJINA YAKE.
Majina ya Mungu, hueleza sifa za Mungu, Tabia za Mungu au Matendo ya Mungu. Mfano; Wayahudi wanamwita Mungu El‐Shaddai. Ni neno lenye majina mawili ndani yake. ‘El’ maana yake Mungu, na ‘Shaddai’ lenye maana itokanayo na neno ‘Shad’ yaani Titi (Ziwa) la mama anyonyeshaye.
Kutokana na ukweli kwamba, titi/ziwa la mama anyonyeshaye, linampa mtoto mchanga kila kitu anchohitaji. Maziwa ya mama yake, humpa mtoto kila kitu mtoto anachohitaji. Ndani ya maziwa kuna vitamini, protini, wanga, mafuta, madini, maji, na kila kitu mtoto anachohitaji. Maziwa ya mama, yanamtosheleza mtoto kwa kila kitu. Hivyo, Waisraeli wanapomwita Mungu El‐Shaddai, wanamaanisha kuwa, kama ziwa linavyo mtosheleza mtoto, vivyo hivyo, Mungu ni ‘Mtoshelezi’ kwetu. Halleluyah!
Hivyo, kila jina la Mungu, linabeba aidha Sifa yake au Tabia yake au Matendo yake. Ndio maana Mfalme Daudi anasema
“Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu … Mpeni Bwana utukufu kwa jina lake. Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.” (Zab 29:1‐ 2) Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni Jina lake, kwakuwa lapendeza.(Zaburi 135:3).
Na Bwana Yesu alitufundisha kuanza sala namna hii;
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako tukutuzwe, hakafu Ufalme
wako uje hapa duniani.
Kwahiyo, unaweza pia kumsifu Bwana kwa majina yake. Majina ya Mungu, hueleza aidha sifa za Mungu au tabia za Mungu au Matendo makuu ya Mungu. Yafuatayo hapa chini, ni baadhi ya majina ya Mungu kwa lugha ya Kiebrania, yatakayokusaidia kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu.
MAJINA YA MUNGU NA UKUU WAKE.
MUNGU akubariki sana na msingi wa somo letu uko katika Zaburi 83:18 inayosema ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.''
1: JEHOVAH ADONAI =MUNGU Mwenye Enzi Yote (Mwanzo 15:2-8 )
2: JEHOVAH EL – SHADAI =MUNGU Ututoshalezae MUNGU Mwenyenzi (Mwanzo 17:1)
3: JEHOAH EL-OHEENU =BWANA MUNGU Wetu (Zaburi 99:5,8,9)
4: JEHOVAH EL- GIBBOR= MUNGU Mwenye Nguvu ( Isaya 9:6-9)
5: JEHOVAH EL-OLAM =MUNGU wa Milele (Mwanzo 21:23)
6: JEHOVAH EL-OHEEKA= BWANA MUNGU Wako (Kutoka 20:2,5,7)
7: JEHOVAH EL-ELYON= MUNGU Aliye Juu Sana (Mwanzo 14:18)
8: JEHOVAH EL-OHIM =Muumbaji wa Milele (Mwanzo 1:1)
9: JEHOVAH SABAOTH =BWANA wa Majeshi (1 Samweli 1:3)
10: JEHOVAH TSIDKEMU= BWANA ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)
11: JEHOVAH RAPHA= MUNGU Nikuponyae (Mwanzo 15:26)
12: JEHOVAH MEKADDISHKEM =BWANA Niwatakasae (Kutoka 31:13)
13: JEHOVAH ROHI =BWANA Mchungaji Wangu( Zaburi 23:1)
14: JEHOVAH JIREH= MUNGU Atupaye /Atoaye (Mwanzo 22:14)
15: JEHOVAH HOSEENU= BWANA Aliyetuumba (Zaburi 95:6)
16: JEHOVAH NISSI= BWANA ni Bendera(Beramu) yangu (Kutoka 17:15)
17: JEHOVAH SHALOM =BWANA ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24)
18: JEHOVAH SHAMMAH= BWANA Yupo Hapa (Ezekiel 48:35).
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka yaani hujampokea BWANA YESU awe ni BWANA na MWOKOZI wa maisha yako ndugu hakikisha unampokea leo maana wokovu ni sasa.
Namna za kumshukuru, kumsifu, na kumwabudu Mungu wetu.
Kwahiyo, katika maisha yetu sisi, kama waumini, tunatakiwa kumpa Mungu wetu ibada, (kumshukuru, kumsifu na kumwabudu) kwasababu ya mambo yote hayo niliyoyataja. Tunatakiwa kumtukuza Mungu kwasababu ya sifa zake,
na kwasababu ya tabia zake, na matendo yake na fadhili zake na ahadi zake kwetu.
Sasa basi, hapa chini, nimekuwekea njia kuu tatu ambazo unaweza kumsifu na kumtukuza Mungu kwazo. Utengapo muda wa kwenda mbele za Mungu, unaweza kutuia njiia kuu zifuatazo; Kumtukuza Mungu kwa,
1. Kumwimbia nyimbo za kumsifu na kuwabudu
2. Kumweleza au kusimulia kwa maneno
3. Kumtolea Mungu sadaka na dhabihu
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 30, 2016

ALLAH SIO JINA LA MUNGU (SEHEMU YA PILI)


Ndugu msomaji,
Katika mada iliyo pita, tumethibitisha kuwa Mungu wa kwenye Biblia ana jina/majina na Allah wa kwenye Quran naye ana majina 99 kama ilivyo shahidiwa kwenye vitabu vyake angalia link hii:http://www.islamicity.com/mosque/99names.htm .
ZAIDI YA HAPO, NIMETHIBITISHA KUWA ALLAH SIO JINA BALI NI WADHIFA TU KAMA ILIVYO "RAIS" "MFALME" nk. Hayo maneno "Rais", "Mfalme" sio majina bali hao wenye huo wadhifa wanayo majina yao na ndio maana huwa tunasema Rais "fulani" kasema hivi au Mfalme fulani kasema hivi na vile, Lazima tuweke jina la huyo Rais au Mfalme katika maelezo yako.
Kwenye hii mada tunaendelea kumuuliza Allah mswali na kuwauliza Waislam maswali kuhusu huyu Allah mwenye jina lisilo tambulika na au halipo kwenye Taurat, Zaburi, na Injili.
SASA TUANZE MADA YETU:
Waislam hupenda kuanza kusema maneno haya katika hotuba zao: Nukuu: "KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU"
Hayo maneno yanatuambia kuwa "Mwenyezi Mungu" anaye tamkwa na Waislam ana Jina, kama sio "majina".
Swali la kwanza: Kwa ndugu zetu Waislam ni hili hapa. "Mnaweza tuambia hilo jina la Mwenye Mungu ambaye ni mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu ni lipi" Tafadhali tujibuni kwa kutumia aya.
Swali la pili kwa Waislam:
Kama "Allah" ni jina la Mwenyezi Mungu wa Waislam, tunaomba mtupe aya kutoka Quran yenu ambayo Mwenyezi Mungu ambaye ni mwingi wa rehema na mwenye kurehemu anasema kuwa "ALLAH" ni jina langu.
Ndugu Waislam, hakuna haja ya kuchukia wala kutuletea lugha chafu kama ilivyo utamaduni wenu baada ya kusoma maswali yetu mawili ya kwanza ambayo yameenda shule. Kitu cha muhimu ni nyie Waislam mtuletee aya ili tufahamu JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEM ambaye mnamtaka kila mnapo anza khutbah zenu Msikitini.
LAKINI KILA NINAPO ISOMA BIBLIA, MUNGU WA KWENYE BIBLIA ANAJITAMBULISHA KWA MAJINA YAKE KITU AMBACHO NI TOFAUTI NA ALLAH WA KWENYE QURAN AMBAYE MPAKA HII LEO HATUJUI JINA LAKE NI NANI.
Kutoka 3: 13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini? 14Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.
Nilipo endelea kuisoma Biblia Takatifu ambayo imekamilika, Mungu alimwabia Musa katika Kutoka 6:2, 3Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. https://www.wordproject.org/bibles/sw/02/6.htm#0
Ndugu msomaji, hata wewe ambaye ni binadamu unalo jina au majina, lakini kitu cha kushangaza Allah ambaye mwenye Majina 99 tofauti kabisa na Mungu wa Musa na Ibrahim na Daudi na Yesu, yeye ameweka "aina za nomino" na kudai hayo ni majina yake. Huu ni msiba mkubwa sana kwa Waislam.
Kusoma juu ya majina tofauti tofauti ya Mungu kunaweza kutusaidia katika kutambua jinsi Mungu alivyo. Baadhi ya Majina yenyewe ni kama yafuatayo:
Elohim – Mwenye nguvu, mtakatifu (Mwanzo 1:1)
Adonai – Bwana, ikiashiria uhusiano wa mtumishi na bwana wake (Kutoka 4: 10, 13)
El Elyon – Aliyetukuka, mwenye nguvu kupita wote (Mwanzo 14:20)
El Roi – Mwenye nguvu kupita wote na aonaye (Mwanzo 16:13)
El Shaddai – Mwenyezi Mungu (Mwanzo 17: 1)
El Olam – Mungu wa milele (Isaya 40:28)
Yahweh – BWANA “NDIMI”, yenye maana ya Mungu wa milele adumuye kwa uwezo wake mwenyewe (Kutoka 3:13, 14).
Unaona raha iliyo katika Ukristo? Mungu wetu anajitambulisha kwa Majina yake ambayo yanaamanisha na au yatatufundihsa jinsi Mungu alivyo.
Sasa nategemea kuwa umeanza kuelewa kuwa Allah sio jina la Mungu bali ni kitu kingine kabisa na wala hana Uhusiano wowote ule na Mwenyezi Mungu ambaye ni Yehova, Mimi Niko Ambaye Niko wa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 30, 2016

Jesus demonstrated He is God

 

TRENDING NOW