
Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni - Sehemu ya 1
Allah alitokea wapi?
Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?
Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?
Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?
Asili Ya Allah
Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.
Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.
Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani. Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.
Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.










