Friday, September 2, 2016

YESU ANAWEZAJE KUWA MUNGU NA MWANADAMU KWA WAKATI MMOJA?


Ni nini maana ya muungano wa kimwili na Uungu?
Hili ni swali linalo ulizwa mara nyingi sana, ni kivipi Mungu awe binadamu na au Kivipi Mungu awe na nafsi mbili, "TWO NATURES" God and Man?
Muungano wa Uungu na mwili ni neno linalotumika kuelezea jinsi Mungu Mwana, Yesu Kristo, alichukua asili ya mwanadamu, lakini alibakia kikamilifu Mungu kwa wakati mmoja. Kila mara Yesu alikuwa Mungu (Yohana 8:58,10:30), lakini katika utatu Yesu akawa binadamu (Yohana 1:14). Ile hali ya kuongezea hali asili ya mwanadamu kwa asili ya Uungu wa Yesu, Mungu-mwanadamu. Huu ndio muungano wa Uungu na kimwili. Muungano wa Uungu na mwili Yesu Kristo, mtu mmoja, Mungu kamili na mwanadamu kamili.
Asili mbili za Yesu, ubinadamu na Uungu, ni namna isiyoweza kutenganishwa. Yesu milele atabaki kuwa Mungu-mwanadamu, Mungu kamili na binadamu, asili mbili tofauti katika mtu mmoja. Ubinadamu wa Yesu na utukufu wake aucha changanyika, lakini umeunganishwa pamoja bila kupoteza utambulisho tofauti. Wakati mwingine Yesu alihudumu katika hali ya upungufu ya mwanadamu (Yohana 4:6, 19:28) na mara nyingine katika nguvu ya uungu wake (Yohana 11:43, Mathayo 14:18-21). Katika hali zote mbili, matendo ya Yesu yalitokana na Nafsi yake moja. Yesu alikuwa na asili mbili, lakini nafsi moja tu.
Mafundisho ya muungano wa Uungu na mwili ni jaribio la kueleza jinsi Yesu anaweza kuwa Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. ingawa hatimaye ni ngumu, mafundisho ambayo sisi hatuna uwezo kamili wa kuyaelewa. Ni vigumu kwetu kuelewa kikamilifu jinsi Mungu anavyofanya kazi. Sisi, kama binadamu na akili finyu,tusitarajie kuelewa kabisa Mungu asiye na mwisho. Yesu ni Mwana wa Mungu kwa sababu yeye alikuwa wa mimba ya Roho Mtakatifu (Luka 1:35). Lakini hiyo haimaanishi kuwa Yesu haikuwepo kabla ya kuumbwa kwa tumbo. Yesu umekuwepo (Yohana 8:58, 10:30). Wakati Yesu alichukuliwa mimba wakati huo akawa, akawa binadamu mbali na kuwa Mungu (Yohana 1:1, 14).
Yesu ni Mungu na mwanadamu. Yesu daima amekuwa Mungu, lakini hakuwa mwanadamu hadi pale alikuwa mimba katika tumboni mwa Maria. Yesu alikuwa binadamu ili ajihusishe nasi katika mapambano yetu (Waebrania 2:17) muhimu zaidi, ili aweze kufa juu ya msalaba alipe adhabu ya dhambi zetu (Wafilipi 2:5-11). Kwa muhtasari, muungano wa mwili na Uungu watufundisha kwamba Yesu ni binadamu kamili na Mungu kikamilifu, kwamba hakuna mchanganyiko au kupungukiwa na aidha ile asili, na kwamba yeye ni yule yule Mtu moja mmoja, milele.
Shukrani ziwaendee na kwa ruhusa ya:
1. Huduma ya Maswali "Got Questions"
2. King James Version
3. Max Shimba Ministries Org

YESU KRISTO AMEUMBA MBINGU, MALAIKA, DUNIA, WATU NA WALIMWENGU WOTE


KUMBE YESU NI MUNGU.
KUMBE MUHAMMAD ATAHUKUMIWA NA YESU.
YESU NI MUUMBAJI.
Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 ) “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesuaitwa Neno la Mungu (UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(YOHANA 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote. Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.
Biblia Takatifu inatuambia kwamba:
“...tuliumbwa katika Kristo Yesu...” (Waefeso 2:10)
Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa sisi wanadamu wote pamoja na viumbe vyote ni kazi ya mikono ya Yesu. Yesu ameumba vitu vyote; tendo la mtu kuukana Uungu wa Yesu ni jambo la kumkosea heshima Mungu aliyekuumba. Ndio maana Yesu aliwaambia Wayahudi kwamba: “...ninyi mwanivunjia heshima Yangu...” (Yohana 8:49).
Tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha YOHANA sura ya kwanza, tunaona pameandikwa:
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:1,3,14)
Huyo “Neno” anayetajwa hapo ndiye Yesu Kristo. Mwandishi wa kitabu hicho cha YOHANA ametumia usemi wa: “...Neno alikuwako kwa Mungu...” akiwa anawafahamisha hususani Wayahudi waliokuwa wanajua kuwa YEHOVA ndiye Mungu wao. Kwa hiyo Yohana anasema “...Neno alikuako kwa Mungu...” kwa maana ya kwamba; huyu “...Yesu alikuwako kwa YEHOVA...” ambaye wao Wayahudi walimtambua kuwa ndiye Mungu wao.
Pia zaidi tunaona Yohana anafafanua kwa kusema kuwa; huyu “...Yesu alikuwa Mungu...” Ufafanuzi zaidi tunauona katika YOHANA 1:14 ambapo Yohana amefafanua kwa kusema; “...Yesu alifanyika mwili; akakaa kwetu...” Biblia Takatifu inamtaja kwa wazi kabisa kuwa Yesu ni Mungu na ameumba vitu vyote “...Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika...” (Yohana 1:3).

YESU KRISTO NDIE ATAKAYE WAHUKUMU WAISLAM WOTE PAMOJA NA MUHAMMAD MTUME WA ALLAH


Yesu Kristo Ndiye anayekuja kuuhukumu ulimwengu wote siku ya kiyama
Jambo hili si mzaha wala uzushi bali ni kweli; Yesu Kristo anakuja kuhukumu ulimwengu wote. Yesu Kristo ametutamkia kwa kiywa Chake kwa kusema kwamba;
“Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.” (Yohana 5:22,23)
Katika hukumu siku ya kiyama hatutegemei kumwona YEHOVA akija kuhukumu ulimwengu, bali, Yesu Kristo ndiye ajaye kuhukumu ulimwengu. Hii itakuwa hivyo ili WATU WOTE WAMHESHIMU Yesu sawa sawa na jinsi ambavyo wanamheshimu YEHOVA. Hapo ndipo viumbe vyote watathibitisha kuwa Yesu ni Mungu. Biblia Takatifu inasema kwamba:
“...kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA...” (Wafilipi 2:10,11)
Hakika Yesu ni Mungu. Najua hapa huwachanganya baadhi ya watu hata wanaweza kuhoji;
Je! Wapo Miungu wangapi? Kwa maana tunasikia habari za Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu? Inawezekanaje tuseme Yupo Mungu mmoja wakati hapo tunaona wapo watatu?
Ni kweli Utatu Mtakatifu wa Mungu umekuwa mgumu sana kueleweka kwa watu wengi kutokana na mafundisho dhaifu waliyoyapokea kutoka kwa viongozi wao wa madhehebu yao na imani zao. Je! Utatu Mtakatifu wa Mungu ni uzushi uliotungwa na wanadamu kwa lengo la kupotosha watu au Biblia Takatifu inatuthibitishia wazi wazi kuhusu Utatu Mtakatifu wa Mungu? Hebu twende katika neno la Mungu tuone jinsi lisemavyo.
Biblia Takatifu inatuambia kwamba:

YESU KRISTO HAJAUMBWA BALI ALIKUWEPO MILELE YOTE

Ndugu msomaji,
Ni kweli kabisa kwamba Yesu alikuwepo tangu milele yote kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile. Bwana Yesu kwa kauli ya kinywa chake mwenyewe anasema kwamba:
“Na sasa, Baba, unitukuze Mimi pamoja Nawe, kwa utukufu ule Mimi niliokuwa nao pamoja Nawe kabla ya ulimwengu kuwako.” (Yohana 17:5)
Neno “UTUKUFU” maana yake ni heshima, uweza, uzuri, umaarufu, nguvu, sifa na mamlaka. Mambo hayo yote Yesu alikuwa nayo kabla hata ulimwengu haujaumbwa. Yesu Kristo alikuwapo hata kabla ya kuzaliwa na Mariamu; jambo hili pia Yesu Kristo kwa kinywa Chake Yeye mwenyewe ametuthibitishia alipokuwa akiwaambia Wayahudi kwamba:
“Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?
Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini Mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima Yangu. Wala mimi siutafuti utukufu Wangu; Yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele. Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akuilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si situ; anitukuzaye ni Baba Yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

JE, MUHAMMAD AMETABIRIWA KWENYE BIBLIA? (SEHEMU YA KWANZA)


Waislamu wanashikilia kwamba Muhammad alitabiriwa kwenye Biblia. Andiko lao kuu wanalotumia kutetea hoja hii ni Kumbukumbu la Torati 18:18. Andiko hilo linasema:
Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Haya ni maneno ambayo aliambiwa Musa na Yehova.
Mmojawapo wa watu ambao walijaribu sana kuonyesha kuwa andiko hili lilimhusu Muhammad, alikuwa ni mwanaharakati wa Kiislamu, marehemu Ahmed Deedat wa Afrika Kusini.
Unaposoma au kusikiliza sababu wanazotoa ili kuthibitisha madai yao hayo, kwa kweli ni sababu zenye nguvu sana (kwa mtu ambaye haelewi Biblia); ingawaje hazina uzito hata chembe ukijua Biblia inasema nini katika ujumla wake na ni nini makusudi na malengo ya Mungu kwa uzao mzima wa Adamu.
Siku moja Ahmed Deedat alimkaba mchungaji mmoja kwa maswali kuhusu mstari huu wa Kumbukumbu 18:18 kiasi kwamba, kwa maneno yake, Deedat anasema kuwa mchungaji yule alikosa cha kusema.
Deedat alimpomsomea mstari huo, alimwuliza, “Unabii huu unamhusu nani?”
“Unamhusu Yesu,” mchungaji alijibu.
“Unajua,” alisema Deedat, “Maneno ya msingi kabisa kwenye unabii huu ni ‘mfano wako’. Sasa, ni kwa vipi Yesu ni mfano wa Musa?”
“Musa alikuwa Myahudi na Yesu alikuwa Myahudi. Pili, Musa alikuwa nabii na Yesu alikuwa nabii,” alijibu mchungaji.
Deedat anaendelea kusema, “Kama hizi ndizo sababu mbili pekee zinazotuwezesha kumtambua mhusika wa unabii huu wa Kumbukumbu 18:18, basi unabii huu unaweza kumhusu yeyote kati ya wafuatao baada ya Musa: Sulemani, Isaya, Ezekieli, Danieli, Hosea, Yoeli, Malaki, Yohana Mbatizaji, n.k. maana hawa wote nao walikuwa Wayahudi na pia manabii. Kwa nini basi useme kuwa unabii huu unamhusu Yesu na si hawa wengine?”
Deedat anasema kuwa mchungaji yule alikosa cha kusema. Kisha Deedat akasema, “Mimi nadhani Yesu ndio hafanani kabisa na Musa.”
Zifuatazo sasa ndizo sababu ambazo Deedat na watoa hoja wa Kiislamu juu ya suala hili wanazozitoa ili kutetea hoja hii:

ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA (UTHIBITISHO WA NANE)


Kuna tofauti kubwa sana kati ya Isa wa Quran na Yesu wa Biblia. Quran inakiri kuwa Isa wake si chochote bali ni mtume tu .
ISA WA QURAN SI CHOCHOTE ILA NI MTUME TU
1.Qurani inasimulia kuhusu Isa bin Maryamu hivi.
Qurani 5;75 Suratul Al Maidah (Meza)
Masihi bin Maryamu “si chochote ila mtume (tu).” (Na) bila shaka mitume wengi wamepita kabla yake (Hawajaona?) na mamake ni mwanamke mkweli (na) wote wawili walikuwa wakila chakula (na kwenda choo. Basi waungu gani wanaokula na kwenda choo?) Tazama jinsi tunavyo wabainishia aya, kisha tazama jinsi wanavyogeuzwa (kuacha haki).
Hapa tunaona Quran inasimulia kuwa masihi Isa si chochote ila mtume tu. Huu ndio mtego ambao Allah anautumia kwa Waislam, eti Isa ni Yesu na Yesu si chochote bali ni mtume tu. Ili kujua kama Allah anasema ukweli, lazima tulinganishe na maneno ya Biblia ambayo ndio yana mamlaka zaidi ya Quran na yalisemwa miaka 632 kabla ya Quran kuandikwa.
YESU ANAMAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI
Biblia inatuambia katika Injili kutokana na Matayo kuwa:
Mathayo 28:18
Yesu akaja kwao akasema nao akawambia, “nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Yesu kwa mdomo wake anakiri kuwa Mamlaka yote ya Mbinguni na duniani amepewa yeye na haya madai ni kinyume kabisa na madai ya Allah ambayo yanasema kuwa eti Yesu si chochote kile bali ni Nabii tu. Kumbuka Yesu alisema haya maneno takribani ya miaka 632 kabla ya Allah kuja na kudai kuwa Yesu si chochote kile. Sasa, Allah alikuwa wapi miaka yote hii 632 ? Kwanini Allah asinge sema haya madai kwenye Injir na akasubiri miaka 632 baadae? Hakika Isa wa Quran sio Yesu wa Biblia.
Malaika Gabrieli naye anashuhudia kuwa, Yesu ni Mkuu na Mwana aliye juu.

KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS? (SEHEMU YA TANO)




Mwalimu Chaka
Injili ya Barnaba ni ushuhuda pinzani dhidi ya Qur'an:
Tayari nimekwisha onyesha jinsi Kitambu hiki kilivyo na mafundisho yaliyo kinyume na Biblia Takatifu.. Yafuatayo ni baadhi ya maandiko yaliyomo katika Injili hii ya Uzushi ya Barnaba ambayo, kwa kweli pia, yanakwenda kinyume na kile kilichomo ndani ya Qur'an: Pamoja na hayo Bado Waislamu wengi Maamuma, wanashabikia kitabu hiki japo baadhi ya wasomi kama vile Sheikhy Shabir Ally wamekiri wazi kuwa Injili hii ni uzushi wa miaka ya karne ya kumi na saba. Ebu tutizame baadhi ya Aya za injili hii tukilinganisha na yaliyomo ndani ya Qurani
1. Yusufu akaenda kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, na mke
wake ambaye alikuwa na
mimba ... kuandikishwa kutokana na amri ya Kaisari. Alipo fika
Bethlehemu,
hakupata nafasi ya kupumzika kwa sababu mji ulikuwa mdogo
na wageni walikuwa wengi. Alikwenda nje ya mji mahali
ambapo wachungaji hukaa.
Wakati Yusufu alikuwa angali huko, siku za Mariamu za
kujifungua mwanawe zikatimia. Bikira alikuwa kuzungukwa na
mwanga mkali sana, NA ALIJIFUNGUA MTOTO WAKE BILA
UCHUNGU WALA MAUMIVU YOYOTE YA KUZALIWA KWA
MTOTO
( Surah 3:5-10).
Ujumbe wa Qur'an unathibitisha kwamba Mariamu alijifungua mwanawe kwa njia ya uchungu wa uzazi-kama mwanamke yoyote yule. Qur’ani inasema,

IMAM WA MSIKITI ABAKA MVULANA WA MIAKA TISA (9)


Imam Mohammad Rizvan wa kutoka kijiji cha Foundarynagar ameshitakiwa kwa kumbaka mvulana wa miaka 9 (Jina lake limehifadhiwa) amesha shitakiwa na Polisi wa Agra.
Msemaji wa Polisi bwana Shatrunja Signh anasema kuwa Mohammad ameshatikiwa kwa kutumia kifungu cha IPC Section 377 (unnatural offence) na POSCO,"
Mohammad ambaye anafahamika na familia ya mbakwaji, alikuwa namfudisha Quran na lugha ya Kiarabu.

NINI MAANA YA KUUMBWA KWA MFANO WA MUNGU?

Mungu ni Roho. Je wewe ni nani?
Katika somo hili la uumbaji wa binadamu, nitajibu hoja na maswali mbali mbali ambayo yanaulizwa zaidi na waumini wa dini ya Kiislam katika Mihadhara mbalimbali ya kidini, kupitia wahadhiri wao wa Dini, Waislamu wamekuwa wakipinga kuwa Mungu hana Mfano kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Mwanzo Sura ya Kwanza na aya ya 26.
Ndugu msomaji, nakusihi ufuatilie somo hili kwa makini ili ujue ukweli kuhusu kuumbwa kwa Binadamu kwa Mfano wa Mungu na nini maana yake:
Katika siku ya mwisho ya uumbaji, Mungu alisema, "Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu" (Mwanzo 1:26). Mungu alimuumba Mtu kutoka vumbi na akampa uhai kwa kumpulizia pumzi yake mwenyewe (Mwanzo 2:07). Binadamu ni kiumbe cha kipekee ambacho Mungu alikiumba na baada ya kukiumba, akatumia pumzi yake kukipa uhai, zaidi ya hapo, binadamu ni kiumbe pekee chenye Mwili, Roho na Nafsi.
Kuwa "mfano" wa Mungu maana yake, katika suala rahisi ni kwamba sisi hatufanani na Mungu katika maana ya mwili na sura na/au mwonekano wetu, bali sisi tunafanana na Mungu katika Roho. Maandiko yanasema kwamba "Mungu ni roho" (Yohana 4:24). Binadamu tuna Mwili, Roho, na Nafsi. Unaweza kuniuliza, ni kivipi ninaweza kuthibitisha hayo? Ngoja nikupe mfano mdogo. Mtu anapo kufa, huwa tunasema hivi: Huu ni Mwili wa Marehemu “Fulani”. Kwanini tunauita “MWILI WA MAREHEMU”…Fulani? Kwa kifupi ni kwamba, Yule ambaye alikuwa anaishi katika huo MWILI amesha ondoka na/au toka katika huo MWILI na kwenda sehemu nyingine. Kumbe basi Binadamu si Mwili, bali kuna zaidi ya MWILI.
Biblia inasema kuwa, Mungu alipo pulizia pumzi ya uhai ule udongo ambao aliuumba, huo udongo ukafanyika na ukawa kiumbe chenye uhai. Kumbe basi, kilicho fanya huo udongo kuwa kiumbe chenye uhai ni ile pumzi ambayo Mungu alipulizia ule udongo alio ufanya katika umbo la mtu. Hiyo pumzi ndio Roho ya Binadamu. Hiyo Roho ndio mfano halisi wa Mungu.

KUMBE MALAIKA WANA AKILI KULIKO ALLAH WA ISLAM!


Malaika Watabiri Mwenendo wa Binadamu kabla ya kuumbwa. Allah atumia hila kuficha udhaifu wake.
Katika somo letu la leo, tutajifunza kuwa Malaika wa Allah wana Akili na ufahamu wa mambo ya baadae kuliko Allah wa Islam.
Quran Surah 2:
30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. ***
KATIKA AYA YA 30. Tunasoma kuwa Malaika wanampa darsah Allah, jinsi gani Mtu atakuwa kabla ya uumbaji wake. Malaika wameonyesha upeo mkubwa kwa kufahamu maisha ya baada ya Adam/binadamu kabla ya hata kuumbwa.
31. Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. ***
Kwenye aya 31 hapo juu, tunasoma kuwa Allah anamfundisha kwa siri Adam ili aweze kuwazima mdomo Malaika. Kitendo cha Allah kumfudisha Adam ili kushindana na Malaika haikuwa haki kwani Malaika walimpa changamoto Allah, Je, Allah ni mwenye ufahamu wa yote?
32. Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima. ***
Je, Allah alipo tumia udanganyifu na uongo ili kujitetea mwenyewe dhidi ya mashtaka kwa Adamu kama yalivyo letwa na Malaika (mashtaka ambayo aligeuka kuwa ni sahihi) ni sahihi?
33. Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha? ***

TRENDING NOW