Yesu Kristo Ndiye anayekuja kuuhukumu ulimwengu wote siku ya kiyama
Jambo hili si mzaha wala uzushi bali ni kweli; Yesu Kristo anakuja kuhukumu ulimwengu wote. Yesu Kristo ametutamkia kwa kiywa Chake kwa kusema kwamba;
“Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.” (Yohana 5:22,23)
Katika hukumu siku ya kiyama hatutegemei kumwona YEHOVA akija kuhukumu ulimwengu, bali, Yesu Kristo ndiye ajaye kuhukumu ulimwengu. Hii itakuwa hivyo ili WATU WOTE WAMHESHIMU Yesu sawa sawa na jinsi ambavyo wanamheshimu YEHOVA. Hapo ndipo viumbe vyote watathibitisha kuwa Yesu ni Mungu. Biblia Takatifu inasema kwamba:
“...kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA...” (Wafilipi 2:10,11)
Hakika Yesu ni Mungu. Najua hapa huwachanganya baadhi ya watu hata wanaweza kuhoji;
Je! Wapo Miungu wangapi? Kwa maana tunasikia habari za Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu? Inawezekanaje tuseme Yupo Mungu mmoja wakati hapo tunaona wapo watatu?
Ni kweli Utatu Mtakatifu wa Mungu umekuwa mgumu sana kueleweka kwa watu wengi kutokana na mafundisho dhaifu waliyoyapokea kutoka kwa viongozi wao wa madhehebu yao na imani zao. Je! Utatu Mtakatifu wa Mungu ni uzushi uliotungwa na wanadamu kwa lengo la kupotosha watu au Biblia Takatifu inatuthibitishia wazi wazi kuhusu Utatu Mtakatifu wa Mungu? Hebu twende katika neno la Mungu tuone jinsi lisemavyo.
Biblia Takatifu inatuambia kwamba:
“Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni: Baba, Neno, na Roho Mtakatifu; na watatu hawa ni umoja.” (1 Yohana 5:8 / 1 John 5:7)
Andiko hilo katika Biblia ya New King James Version inasema “...these three are one.” (1 John 5:7) kwa maana ya kwamba “...WATATU HAWA NI MMOJA.” Hebu tujiulize; je! Huo umoja wao unaowafanya watatu hao (YEHOVA, Yesu, na Roho Mtakatifu) hata wote wawe MMOJA ni upi?
Umoja wao upo katika Uungu
u. Wote watatu wanaungana kuwa Mungu mmoja kwa maana ya kwamba uumbaji wa vitu vyote umefanywa kwa pamoja na hawa watatu (yaani; YEHOVA, Yesu, pamoja na Roho Mtakatifu).
u. Wote watatu wanaungana kuwa Mungu mmoja kwa maana ya kwamba uumbaji wa vitu vyote umefanywa kwa pamoja na hawa watatu (yaani; YEHOVA, Yesu, pamoja na Roho Mtakatifu).
Tukirejea katika uumbaji; Neno la Mungu linasema kwamba:
“Mungu akasema, Na Tumfanye mtu kwa mfano Wetu, kwa sura Yetu...” (Mwanzo 1:26)
Pindi niliposoma andiko hilo kwa umakini nilijiuliza; Mbona Mungu hakusema;
"...Nimfanye mtu kwa mfano Wangu, kwa sura Yangu..."? Kwa nini Mungu ametumia maneno "...kwa mfano WETU, kwa sura YETU..."? Maneno hayo "...WETU..." na "...YETU..." yanadhihirisha hapo kuna zaidi ya mmoja. Je, ni nani mwingine aliye muumba mwanadamu zaidi ya Mungu?
Wakati nikiwa ninajiuliza maswali mengi, ndipo Roho Mtakatifu akanifundisha kwamba neno "Mungu" ni cheo, na sifa zake ndizo tulizojifunza hapo awali. Mungu hufanya kazi katika ushirika ambao katika Umoja huo ndipo aliumba vitu vyote.
Yesu anakupenda, mpe maisha yako sasa ili akuokoe. Ni jambo la imani tu, ukiamini ndani ya roho yako na kumkiri Yesu kwa dhati kwa kinywa chako; hakika hapo hapo unakuwa umeokoka.
Kumpokea Yesu maishani mwako maana yake ni kukiri kwamba Yesu ni Bwana, Yesu ni Mungu, pamoja na KUKIRI kwamba Yesu pekee ndiye uzima wa milele wala hakuna kiumbe ye yote yule awezaye kuokoa isipokuwa Yesu pekee ambaye ni Mungu wetu.
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya roho yako kuwa Bwana na Mwokozi wako; Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya roho yako kuwa Bwana na Mwokozi wako; Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.
Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalumu wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Wokovu ni kwa ajili ya uponyaji wako ili uwe na uzima wa milele; kamwe usimtazame huyo aliye pembeni mwako kwamba akisikia umeokoka atachukia; wala usiisikilize hiyo sauti ikwambiayo ndani ya akili zako kwamba "subiri" Hiyo ni sauti itokayo kwa yule mwovu Shetani ambaye anataka wewe ufe katika dhambi zako. Fahamu kwamba uzima wako wa milele unauandaa sasa; pia Biblia inasema hakuna neema baada ya kifo; kwa maana imeandikwa:
“Na kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.” (Waebrania 9:27)
Mtu akifa kinachofuata ni hukumu. Asije akatokea mtu akakudanganya kwamba yapo maombi yanayoweza kuwaombea wafu nao wakasamehewa dhambi zao (mwulize mtu huyo akwambiae hivyo; mwambie akuonyeshe andiko ndani ya Biblia Takatifu linalosema unaweza kumwombea mfu.) Huo ni uongo tena utokao kwa Shetani. Neno la Mungu linasema kwamba:
“Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.” (Marko 12:27)
Nakushauri usiiache neema hii ya wokovu iliyopo mbele yako sasa ikipite. Wakati huu ni wa thamani sana kwako kwa maana huijui kesho wala badae ikoje. Tafakari kwa kina kati yako wewe na Mungu ni nani anahitaji msaada wa mwenzake. Tubu sasa. Sikulazimishi ila fanya sawa na kile Mungu anachoshuhudia ndani ya roho yako. Fahamu kuwa;
haiwezekani kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya wewe kuokoka.
Kama unataka kuokoka sasa hivi; Tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa kutamka kwa kinywa chako sala ifuatayo: (ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu yote. Ninatubu kwa dhati ya kweli kutoka rohoni mwangu. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho Wako – Uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Nakuomba unifanye niwe vile utakavyo mimi niwe. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina."
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zote zimesamehewa kabisa. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.
No comments:
Post a Comment