
Tangia Agano la Kale, kila aina ya kafara iliyofanyika Damu ilitumika. Ndiyo maana hata sasa, wachawi na waganga wa kienyeji wakitaka kufanya kazi zao za uharibifu huhitaji damu, aidha ya wanyama kama kondoo, mbuzi, kuku n.k.
Damu inanena / au ina uwezo wa kuongea. WAEBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.]
Yesu Kristo alimwaga damu yake kwa ajili ya ukombozi wetu – tumekombolewa na damu ya Yesu. (Waefeso 1:7; Wakol.1:20; 1 Petro 1:19; Ufunuo 5:19; Waebrania 9:12).
TABIA ZA DAMU
Damu ina uhai ndani yake. WALAWI 17:11….[Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.]….
MWANZO 9:4… [Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. 5 Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.]… Hii ina maanisha kwamba, kwa kuwa uhai u ndani ya damu, ndiyo maana wanasayansi wameshindwa kutengeneza damu, la sivyo wangeweza kutengeneza uhai pia.
Damu ina Sauti.
Damu inanena / au ina uwezo wa kuongea. WAEBRANIA 12:24…[na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.]
















