Sunday, February 26, 2017

ALLAH ANAKIRI KUWA YEYE ANA USO

Image may contain: text
1) Allah anasema: "Popote mtapogeukia kuna Uso wa Mwenyezi Mungu". Sura 2, Aya 115.
Kwenye hiyo aya hapo juu, Allah amesha wajibu wanao bisha kuwa Allah hana uso. Je, kuwa na uso si sifa ya binadamu?
2) Allah anasema: "كل شيء هالك إلا وجهه" (Kila kitu kitaangamia isipokuwa Uso wake (Allah)." Sura 28 Aya 88.
Ndugu zanguni, Allah anaendelea kukiri kuwa yeye ana uso kama viumbe.
Sasa, kwanini Waislam wanasema kuwa Allah hana wakufanana naye?
HUU NI MSIBA,

ALLAH ANAVAA NGUO KAMA VIUMBE

Image may contain: one or more people and text
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA NDUGU ZANGUNI.
الكبرياء ردائي والعظمة إزاري
Allah anasema katika Hadithi hii Qudsi "Ukuu ndio vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini".
Sasa kama Allah anavaa nguo inamana kuwa Allah ana mwili kama viumbe?
Msiba huu ni mkubwa sana ndugu wasomaji.
Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema: "….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia juu yake. Na mja huwa anaendelea kujikurubisha kwangu kwa nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka nampenda: "فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به، وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله) (التي يمشي بها" Basi nikimpenda nakuwa (Mimi ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea."
Hapo Allah kesha kiri kuwa yeye ana masikio, mikono na macho.

QURAN YATHIBITISHA KUWA, YESU NI ZAIDI YA MUHAMMAD

Image may contain: one or more people, people sitting, meme and text
KINACHOMFANYA YESU ASIWE SAWA NA MUHAMMADI, NI HII AYA YA QURAN 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
فاطر (22) Faatir
Wala hawalingani walio hai na maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
Hapo 👆 Tunaambiwa hawalingani walio hai na Maiti,
YESU YEYE YUPO HAI 👇
Ufunuo 1:17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
MUHAMMADI KAFA 👇
( قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ )
الطور (31) At-Tur
Sema: ngojeni na mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongojea (sifi mimi peke yangu, nanyi mtakufa vilevile)
YESU YEYE AMEWEZA KUWASIKILIZISHA SAUTI WALIO MAKABURINI 👇
Yohana 11:38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
MUHAMMAD YEYE AMEAMBIWA KUWA HAWEZI KUWASIKILIZISHA SAUTI WALIOMO MAKABURINI 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
35:22
............. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.

Wednesday, February 22, 2017

NENO LAKO NI TAA YA MIGUU YANGU

Image may contain: text
UWEZA ULIO KATIKA NENO LA MUNGU
Neno ni nini?
Neno ni matamshi yenye maana yanayotoka kwenye kinywa cha mtu, au kitu !
Kibiblia Neno ni yale mambo yaliyojaza moyo wa mtu , Biblia inasema “Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake , hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoka yaliyo maovu; kwa kuwa mtu hunena yale yaujazayo moyo wake” Luka 6:45 Amplified Bible moyo umeandikwa kama (storehouse)
Neno la Mungu ni nini?
Neno la Mungu ni yale maneno yanayotoka kwa Mungu, na ni makusudio ya somo hili kujifunza uweza ulio katika neno la Mungu ili yamkini tupate kujua msaada tutakao upata kwenye neno hilo! Mungu anaongea sana kupita unavyofikilia lakkini unawezaje kulipokea neno na kulitumia hapo ndo wengi wanaposhindwa.
Uwezo wa NENO kukuongoza katika njia sahihi.
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” Zaburi 119:105,
Neno linatuonyesha tunapoelekea, linatuongoza kutenda kwa usahihi kama vile nchi bila katiba inapotea, ndivyo mtu anayemwamini Yesu kutokuwa na neno la Mungu moyoni mwake! lazima atapotea! Mungu akamwambia Joshua “kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku…ndipo utakapoifanikisha njia yako…” Joshua 1:8. Ni kwa kufuata Neno la Mungu ndipo mtu anaweza ifanikisha njia yake!
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

JE, MAJINI, MASHETANI, MAPEPO NA MAHAYAWANI YOTE YAMEUMBWA NA ALLAH?

Image may contain: ocean, sky and text
1. Kwanini Allah alimuumba Shetani?
2. Kwanini Allah aliumba Majini machafu?
3. Kwanini Allah aliumba Mapepo?
4. Kwanini Allah aliumba Mahayawani?
MAJIBU YA MASWALI HAYO MANNE HAPO JUU UTAYAPATA KWENYE KAZI ZA MAJINI.
MTUME MUHAMMAD AKUTANA NA MAJINI USKU
Allah S.W.T. ametuhakikishia wazi kuwa ujumbe aliopewa Mtume S.A.W. ulikuwa kwa Wanadamu na Majini na Mashetani pia. Na katika Qurani na Hadithi za Mtume S.A.W. kuna dalili zilizo wazi zinazoyakinisha kuwa Mtume S.A.W. alikuwa akikutana nao na kuwafundisha dini. Na hata wakati mwingine Majini walikuwa wakitoa majibu mazuri zaidi kuliko Binadamu kwenye masuala ya dini. Na mfano ni wakati waliposomewa Suratir Rahmaan. Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na iliyotolewa na Ttirmidhi kasema, “Wakati ambapo Mtume S.A.W. alipowasomea Majini Suratir Rahmaan, “
لَقَدْ قَرَأْتُهَا ‘‘يعني سُورَةَ الرَّحْمَنِ’’ عَلَى الْجِنِّ …، فَكَانُوا أَحْسَنَ مَرْدُودًا مِنْكُمْ ، كُنْتُ كُلَّمَا أَتَيْتُ عَلَى قَوْلِهِ ]فَبِأَيِّ آلاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ[ قَالُوا: لا بِشَيْءٍ مِنْ نِعَمِكَ رَبَّنَا نُكَذِّبُ ، فَلَكَ الحمد
Maana yake, “Hakika nimewasomea Majini (yaani Suratir Rahmaan)…wamejibu vizuri zaidi kuliko nyinyi. Kila nilipofikia kauli Yake (Mwenyezi Mungu S.W.T.) “Fabiayyi A-alaai Rabikumaa Tukadhibaan.) Maana yake, “Basi ipi katika neema za Mola wenu ambayo mnayoikanusha kuwa si kweli?” (Basi Majini) walijibu “Laa bishaay Min Niamika Rabbana Nukadhibu, Falakal Hamdu.”
Maana yake, “Hakuna neema yoyote katika neema Zako Mola wetu tunayoikadhibisha, bali tunashukuru.” Na Mtume S.A.W. alipowasomea Wanadamu hawakujibu chochote, akawaambia, “Ndugu zenu wa Ki-Jini wamejibu jawabu nzuri waliposikia haya.” Na dalili nyingine kuwa Mtume S.AW. pia alikuwa ametumwa kwao ni kisa cha baadhi ya Majini ambao baada ya kuisikiliza Qurani waliiamini na wakarejea kwao na kuanza kuwaita wenzao kwenye dini ya Kiislamu.
KUTOKANA NA BIBLIA
Majini au Mapepo au Mashetani (Malaika walio asi) ni viumbe ambavyo havionekani kwa macho, ni viumbe kama Malaika isipokuwa Majini na Mapepo yalifukuzwa Mbinguni pamoja na Shetani baada ya kuasi, na yalitupwa duniani yakisubiri siku ya mwisho ya hukumu. Hivyo Majini, Mashetani, Mapepo ni tokeo la kuasi kwa malaika. Ni sawa na kusema JAMBAZI ni tokeo au sifa ya mtu mwizi wa kutumia nguvu.

KWA JINA LA YESU MTATOA PEPO

Image may contain: one or more people and text
Marko 16:17-18 inasema, "ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina Langu watatoa pepo...."
Kila Mkristo anao uwezo wa kuwatoa pepo! Sio swala la kwamba "una nguvu" kiasi gani au jinsi gani upo "kiroho" ; cha muhimu ni kuwa Yesu Amekupa mamlaka Yake; unatembea katika jina Lake.
Shetani hana haki ya kuendesha mambo katika maisha yako, au nyumbani mwako au katika maisha ya wale uwapendao. Tumia mamlaka yako katika Kristo dhidi yake.
Matendo 16:16-18 Ikawa tulipo kuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye juu, wenye kuwahubiria Njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo Akakasirika, akageuka akamwambia yule pepo, nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Unaweza kuwatoa pepo siku yoyote, muda wowote na mahala popote, kwa kutumia jina la Yesu tu.
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

KANISANI JUMAPILI YA FEBRUARY 19, 2017 NA RAIS OBAMA, WASHINGTON DC.

Image may contain: 7 people, people standing and wedding

Its great to see the OBAMA Family in church. You know its a good idea to serve GOD after serving in the highest office on Earth

Max Shimba Ministries 

HATIMAE SHETAN KWA KINYWA CHAKE AKIRI KUWA YESU NI MUNGU

Image may contain: text
AKIRI KUWA YESU NDIYE ATAKAE MHUKUMU SIKU YA MWISHO/KIYAMA:
Ndugu msomaji,
Unapoona mada hii inajirudia katika mandiko tofauti, tofauti, ikithibitisha mamlaka kuu na nguvu za Yesu kuanzia mbinguni, duniani na hadi chini ya aridhi;
Nikwamba INAKUJENGEA IMANI WEWE USIYE AMINI UUNGU, UKUU, NA MAMLAKA YA YESU.
Kwahiyo shetani yeye anaitumia fulsa hiyo ya kuivunja imani hiyo ya Yesu kwa kusema "Yesu ni mtu tu kama nyinyi sichohote silolote" NAKUIVUNJA IMANI YA WATU WAKIFIKILI YESU SILOLOTE,
Tuanze na Qur'an Al-Hijr 34 ( ALLAH ) akasema basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! 35 na hakika juu yako ipo laana mpaka siku ya malipo, 36 akasema (Iblisi) mola wangu mlezi! NIPE MHULA MPAKA WATAKAPO FUFULIWA. 37: (ALLAH) akasema HAKIKA WEWE NI KATIKA WALIO PEWA MHULA. 38 MPAKA SIKU YA WAKATI MAALUMU.
Katika mstari wa 36 shetani anaomba apewe MHULA MPAKA WATAKAPO FUFULIWA.
JE NINANI HUYO AMBAE SHETANI ANASEMA ATAFUFUA?
Yohana 11:25 YESU akamwambia, MIMI NDIMI HUO UFUFUO NA UZIMA, yeye aniaminiye Mimi HAJAPO KUFA ATAKUA ANAISHI:
Kumbe shetani anamfahamu fika Yesu na ndio maana anamuomba atakapo kujakufufua wafu siku ya mwisho ndipo nae ahukumiwe.
Katika mstari wa 37-38 tunaona Allah kwa kinywa chake anamwambia shetani kwamba AMEPEWA MHULA MPAKA WAKATI MAALUMU.
ALLAH #HAKUMWAMBIA SHETANI KWAMBA NIMEKUPA MHULA, LA HASHA,
BALI ALIMWAMBIA #UMEPEWA MHULA.
JE MUNGU ALIYE MPA MHULA SHETANI ANAITWA NANI?
KWASABABU ALIYE PEWA MHULA NI SHETANI, NA SHETANI ANAMJUA ALIYE MPA MHULA, SHETANI MWENYEWE ANATHIBITISHA KWA KINYWA CHAKE:
UTHIBITISHO WA AYA:

KUNYWA MAJI YA UZIMA

Image may contain: text
Njoo Kwake Kristo Yesu
“Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.” (Ufunuo Wa Yohana 22:17)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

HABARI NJEMA

Image may contain: text
Injili, ambayo inamaanisha, “Habari Njema,” ni kwamba Mungu ametuandalia njia ya kumrudia huku akiadhibu dhambi zetu. Njia hiyo ni kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6)
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Warumi 5:8)
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.” (Waefeso 2:8)
“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” (Wakorintho Wa Pili 5:21)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

TRENDING NOW