Wednesday, February 22, 2017

JE, MAJINI, MASHETANI, MAPEPO NA MAHAYAWANI YOTE YAMEUMBWA NA ALLAH?

Image may contain: ocean, sky and text
1. Kwanini Allah alimuumba Shetani?
2. Kwanini Allah aliumba Majini machafu?
3. Kwanini Allah aliumba Mapepo?
4. Kwanini Allah aliumba Mahayawani?
MAJIBU YA MASWALI HAYO MANNE HAPO JUU UTAYAPATA KWENYE KAZI ZA MAJINI.
MTUME MUHAMMAD AKUTANA NA MAJINI USKU
Allah S.W.T. ametuhakikishia wazi kuwa ujumbe aliopewa Mtume S.A.W. ulikuwa kwa Wanadamu na Majini na Mashetani pia. Na katika Qurani na Hadithi za Mtume S.A.W. kuna dalili zilizo wazi zinazoyakinisha kuwa Mtume S.A.W. alikuwa akikutana nao na kuwafundisha dini. Na hata wakati mwingine Majini walikuwa wakitoa majibu mazuri zaidi kuliko Binadamu kwenye masuala ya dini. Na mfano ni wakati waliposomewa Suratir Rahmaan. Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na iliyotolewa na Ttirmidhi kasema, “Wakati ambapo Mtume S.A.W. alipowasomea Majini Suratir Rahmaan, “
لَقَدْ قَرَأْتُهَا ‘‘يعني سُورَةَ الرَّحْمَنِ’’ عَلَى الْجِنِّ …، فَكَانُوا أَحْسَنَ مَرْدُودًا مِنْكُمْ ، كُنْتُ كُلَّمَا أَتَيْتُ عَلَى قَوْلِهِ ]فَبِأَيِّ آلاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ[ قَالُوا: لا بِشَيْءٍ مِنْ نِعَمِكَ رَبَّنَا نُكَذِّبُ ، فَلَكَ الحمد
Maana yake, “Hakika nimewasomea Majini (yaani Suratir Rahmaan)…wamejibu vizuri zaidi kuliko nyinyi. Kila nilipofikia kauli Yake (Mwenyezi Mungu S.W.T.) “Fabiayyi A-alaai Rabikumaa Tukadhibaan.) Maana yake, “Basi ipi katika neema za Mola wenu ambayo mnayoikanusha kuwa si kweli?” (Basi Majini) walijibu “Laa bishaay Min Niamika Rabbana Nukadhibu, Falakal Hamdu.”
Maana yake, “Hakuna neema yoyote katika neema Zako Mola wetu tunayoikadhibisha, bali tunashukuru.” Na Mtume S.A.W. alipowasomea Wanadamu hawakujibu chochote, akawaambia, “Ndugu zenu wa Ki-Jini wamejibu jawabu nzuri waliposikia haya.” Na dalili nyingine kuwa Mtume S.AW. pia alikuwa ametumwa kwao ni kisa cha baadhi ya Majini ambao baada ya kuisikiliza Qurani waliiamini na wakarejea kwao na kuanza kuwaita wenzao kwenye dini ya Kiislamu.
KUTOKANA NA BIBLIA
Majini au Mapepo au Mashetani (Malaika walio asi) ni viumbe ambavyo havionekani kwa macho, ni viumbe kama Malaika isipokuwa Majini na Mapepo yalifukuzwa Mbinguni pamoja na Shetani baada ya kuasi, na yalitupwa duniani yakisubiri siku ya mwisho ya hukumu. Hivyo Majini, Mashetani, Mapepo ni tokeo la kuasi kwa malaika. Ni sawa na kusema JAMBAZI ni tokeo au sifa ya mtu mwizi wa kutumia nguvu.

Biblia haisemi kuwa Mungu aliumba MAJINI, MASHETANI AU MAPEPO, maana Mungu wa Biblia hakuumba dhambi au ubaya au chuki au Ushetani au aina yeyote ile ya dhambi.
Shetani na Majini, wanajua kabisa kuwa Jehanum ya moto ipo kwa ajili yao, ndiyo maana wanafanya kila mbinu wasiingie peke yao huko Jehanum, Shetani ni mwongo, laghai anawatumia sana wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota kupandikiza majini, kuiba nyota yako ya mafanikio, kuchukua watu misukule nk.
KUNA AINA NYINGI ZA MAJINI, BAADHI YAO NA KAZI ZAO NI HIZI HAPA:-
1) Murafari – hili ni jini linalozuia mafanikio ya kupata fedha, mafanikio ya elimu nk.
2) Latifu – hili jini linaloleta ufukara, mateso, hata ukipata pesa matumizi yake yanakuwa ni hovyo
3) Jahari – Jini anayetumiwa kuiba mali na kuzuia biashara kustawi
4) Hasinani – jini hili ni la fujo, ulevi wa pombe, bangi na dawa za kulevya
5) Jube – jini hili linasababisha utasa
6) Subiani – jini la ajali, linasababisha wanawake kutokupata siku zao, na kunyonya damu za akina mama siku zao za hedhi ambapo wanapata maumivu makali sana.
7) Sumil – jini hili huangamiza mimba changa
8) Waidadat – jini hili husababisha wanaume kuvaa hereni kusuka nywele na kutoga masikio.
9) Alibadiri – jini la kifo, likikupata kifo hutokea wakati wowote.
10) Anzura – Linawazuia vijana wa kike na kiume kuolewa/kuoa
11) Maimuna – linawakamata wanaume wenye ndoa zao hadi ndoa inavunjika
12) Makata – linasababisha vifo vya mfululizo kwenye familia
13) Faziur – jini la maandishi. Unaletewa barua ukiisoma tayari umelikwaa
14)Subha – jini hili linasababisha mtu kuwa na kiburi sana na kujiinua.
15) Maulan – jini linalofanya watu kuwa kichaa, au mtu ananuka wakati wowote
16) Al-maul – jini hili linamfanya mtu kuwa ombaomba
17) Zuhura au Zohari – Jini la fujo
18) Araba – Jini hili linafanya mtu apende sana ubani
19) Farkh – jini hili linatumwa hasa kwa wakristo kuangalia kama ana kinga (Wokovu)
20) Baradi – jini hili likikupata basi ndoa yako ni lazima itavunjika.
21) Shamsu – jini hili huvaa umbile la binadamu kwa sura yoyote.(sasa hivi mitaani majini haya yapo mengi sana)
22) Abuni – jini wa hasira
23) Kaimu – jini la kutambua nyota za watu
24) Tajuruni – jini la utajiri wa kichawi – ni lazima utoe kafara ya mwanao, mkeo au kufanya tendo la ndoa na mama yako mzazi
25) Al-taliki – jini hili linapoteza watu katika mazingira ya kutatanisha
26) Naluju – linasimamia lugha
27) Janatusi – linatumwa alfajiri kabla ya adhana kuleta usingizi kwa Wakristo wasifanye sala
28) Riyaron – jini hili linamfanya mtu afanye kila kazi peke yake
29) Zaitun – Jini hili linasababisha wasichana kuwa na maringo
30) Ruyati – jini linalosimamia ndoto mbaya
31) Al-rahabu – jini linalosababisha hitilafu ya umeme
32) Hadharaji – jini hili linafanya kazi ya kukata kichwa cha mtu ili wapate damu
33) Anazihaji – jini hili ndilo linachukua roho yako ukifa kwenye dhambi
34) Nghruk – linasababisha maafa
35)Munkara – jini la makaburini
36) Takadhuru – jini linaloleta mali za masharti.
37) Rabindi – jini la Waislamu pekee yao ili wafanye fujo.
38) Balishebe – jini la magonjwa yasiyopona
39) Sajiduri – jini linalokusaidia kupata pesa, kisha zinapotea kwa haraka
40) Rumiran – linasimamia uwongo
41) Lairlihabi – linasimamia hofu, kutojiamini na kukata tamaa
42) Rohani – jini la mateso na fujo
43) Betrah – jini hili linasimamia mapambo, kwa mwanamke huwa anajipamba isivyo kawaida, halikadhalika mwanaume
44)Hanshari – linatumiwa sana na waarabu kulinda maduka yao
45) Walihuni – linazunguka nyumba likilinda biashara
46) Kurasih – jini la kupoteza fahamu
47) Tarik – huondoa amani nyumbani, kazini. Linafanya watu wasielewane
48) Atha – mungu wa kiarabu wa kuabudu sanamu
49) Munakir – linapoteza watu kimiujiza
50) Malik – jini la kumiliki biashara
51) Ghatabu – jini la kulainisha macho wa wanawake. Wanakuwa wanarembua
52) Khatuh – jini la uchawi wa kuchukua kucha, nywele na nguo za ndani
53) Fanken – jini hili linasimamia mtu kuzunguza kiswahili cha pwani
54) Zamzam – jini la marashi na kusimamia mikataba ya imani. Mkristo anaposilimishwa basi hutupiwa jini hili kupofushwa akili yake.
55) Mukitala – linatumwa kuangalia kinga za watu
56) Laufili – jini la uvivu
57) Al-khah – linakula damu iliyoganda
58 Abasaa – jini la hasira wivu na jeuri
59) Aherumi – jini la homa za mara kwa mara
60) Muba – jini la maradhi ya kuambikiza
61) Kamariram – jini hili linatoa kinga kwa majambazi
62) Zubiran – jini la uongo na uzushi
63) Abadi – Jini la wizi, umalaya na ujambazi
64) Muzamili- jini la matambiko ya kiarabu
65) Ruhadi – jini la wizi, umalaya na umasikini
66 Usuran – jini la wizi, umalaya, ujambazi na umaskini
67)Tubuyali – jini hili linamfanya mtu kuiba vitu vya ndani ya nyumba. Haibi nje ya nyumba
68) Zirach – jini la wizi, umalaya, ujambazi na umaskini
69) Ashuran – jini la utasa na maradhi ya akina mama
Kinga ya majini haya ni nyepesi ni KUOKOKA na kusimama katika neno la Mungu. Kama unayo dalili yoyote iliyosababishwa na Majini hayo hapo juu na umeokoka, taja jina la hilo jini, ni lazima litaitika, kisha liwashie moto wa Roho Mtakatifu. Tumia Damu na Jina la Yesu kuyavunja vunja
Marko 16:17-18 inasema, "ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina Langu watatoa pepo...." Kila Mkristo anao uwezo wa kuwatoa pepo! Sio swala la kwamba "una nguvu" kiasi gani au jinsi gani upo "kiroho" ; cha muhimu ni kuwa Yesu Amekupa mamlaka Yake; unatembea katika jina Lake.
Kama hujaokoka usiyarushie mawe au moto yatakuumiza. Muone kiongozi yeyote wa Kanisa akuongoze sala ya toba, kisha anza kuwasha moto, hakika yatakimbia na kuacha biashara, kazi, ndoa, na watoto wako huru.
Leo basi, tumejifunza aina za Majini na jinsi ya kuyaharibu kwa Jina la Yesu alie hai.
Max Shimba Ministries

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW