Monday, April 17, 2017

JE, MELKIZEDEKI NA YESU NI MTU MMOJA? (SEHEMU YA KWANZA)


Nini maana ya Kuhani?
Neno “Kuhani” katika Agano Jipya lina maana mtoto wa mfalme au mtumishi. Na makuhani wote kwenye maandiko ni lazima wawe na madhabahu na ni lazima watoe sadaka. Na hakuna mtu kwenye maandiko alikuwa na uwezo wa kutoa sadaka kwa ajili ya watu mbele ya Mungu.
Tofauti ya Nabii na Kuhani ni ipi?
Kazi ya manabii ni kutumikia Mungu kwa ajili ya watu. Lakini kazi ya Kuhani ni kutumikia Watu mbele ya Mungu.
Jina Melkizedeki limeonekana katika Biblia mara kumi (Mwanzo 14:18, Zaburi 110:4, Kitabu cha Waebrania - 5:6, 5:10, 6:20, 7:1, 7:10, 7:11, 7:15, 7:17).
Melkizedeki, ambaye jina lake linamaanisha "Mfalme wa haki," alikuwa mfalme wa Salemu (Yerusalemu) na kuhani mkuu zaidi wa Mungu (Mwanzo 14: 18-20; Zaburi 110: 4, Waebrania 5: 6-11, 6: 20-7: 28). Melkizedeki huonekana ghafla na kupotea katika kitabu cha Mwanzo ni ajabu kwa kiasi fulani. Melkizedeki na Ibrahimu walikutana kwanza baada ya Ibrahimu kushindwa kwa Kedorlaoma na washirika wake watatu. Melkizedeki iliwasilisha mkate na mvinyo kwa Ibrahimu na watu wake walokuwa wamechoka, kwa kuonyesha urafiki. Yeye alitawaza baraka kwa Ibrahimu kwa jina la El Elyon ("Mungu aliye juu zaidi") na kumsifu Mungu kwa kumpa Abraham ushindi katika vita (Mwanzo 14: 18-20).
Tunaona sifa mbili za Melkizedeki, kwanza mfalme na pili ni kuhani wa Mungu aliye juu. Salem ndiyo eneo ambalo mfalme huyu alitawala kulingana na mstari huu. Salem ina maana ya amani. Kwa hiyo Melkizedeki alikuwa mtawala wa sehemu yenye jina lenye tafsiri ya amani. Akiwa kama kuhani, anambariki Ibrahimu na anapokea zaka za Ibrahimu (mst 19-20).
Hatuwezi kusoma kuhusu Ukuhani wa Yesu mpaka kitabu cha Waebrania katika Agano Jipya. Na hapa mwandishi anamtukuza yeye kama Kuhani Mkuu wa pekee na wa milele. Yeye tu ni Kuhani Mkuu wetu na hakuna mwingine. Amekwisha mwaga damu yake kwa ajili yetu na damu yake inafaa milele.
Waebrania 6:20 inasema, "alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki." Tamko kwa mfano kwa kawaida laweza kuonyesha urithi wa kuhani wanaoshikilia ofisi. Hakuna waliotajwa kamwe, hata hivyo, katika kipindi cha muda mrefu kutoka Melkizedeki hadi kwa Kristo, kihoja kinachoweza kusuruhishwa kwa kuchukulia kwamba Melkizedeki na Kristo kweli ni mtu mmoja. Hivyo "mfano wa" umekabidhiwa ndani yake na kwake pekee milele.
Waebrania 7: 3 inasema kuwa ”hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu; huyo adumu kuhani milele.”Swali ni iwapo mwandishi wa waebrania anamaanisha hii halisi au kitamathali.
Kama maelezo katika Waebrania ni halisi, basi ni vigumu kweli kuona jinsi itakavyotekelezwa kamili kwa mtu yeyote ila Bwana Yesu Kristo. Hakuna mfalme wa duniani "atakayebakia kuwa kuhani milele, "na hakuna binadamu wa kawaida“ ambaye hana baba wala mama.” Kama Mwanzo 14 inaelezea kuhusu imani ya kumufahamu Mungu, basi Mungu Mwana alikuja kumpa Ibrahimu baraka zake (Mwanzo 14: 17-19),akionekana kama Mfalme wa Haki (Ufunuo 19: 11,16), Mfalme wa Amani (Isaya 9: 6), na mpatanishi kati ya Mungu na binadamu (1 Timotheo 2: 5).
Ibraham alimpokeza Melkizedeki na zaka ( fungu la kumi) ya vitu vyote alivyokuwa amesanya. Kwa kitendo hiki Ibraham alionyesha kuwa alitambua Melkizedeki kama kuhani ambaye nafasi yake ya kiroho ilikuwa juu kuliko yake.
Katika Zaburi 110, zaburi ya kimasihi iliyoandikwa na Daudi (Mathayo 22:43), Melkizedeki ametolewa kama aina nyingine ya Kristo. Mada hii imerudiwa katika kitabu cha Waebrania, ambapo Melkizedeki na Kristo wote wamechukuliwa kuwa wafalme wa haki na amani.Kwa kudondoa Melkizedeki na ukuhani wake wa kipekee kama aina, mwandishi anaonyesha kwamba ukuhani mpya wa Kristo ni bora kuliko mpangilio wa zamani wa Walawi na ukuhani wa Haruni (Waebrania 7: 1-10).
Baadhi hupendekeza kwamba Melkizedeki alikuwa amepata mwili ulionekana kama Yesu Kristo, au Kristofani . Hii ni nadharia inayowezekana, ikikumbukwa kwamba Ibrahimu alikuwa amepata ziara kama hizo hapo awali. Chukulia Mwanzo 17 ambapo Ibrahimu alimwona na kuongea na Bwana (El Shaddai) katika umbo la mtu.
Kama maelezo ya Melkizedeki ni mfano, basi maelezo ya kutokuwa na nasaba/kisasi, hakuna mwanzo au mwisho, na huduma isiyo na mwisho ni tu kauli inayotia mkazo asili ya kiajabu ya mtu ambaye alikutana na Ibrahimu. Katika kesi hii, kimya katika maelezo ya Mwanzo kuhusu maelezo haya yana kusudi yanahudumu bora kwa kuunganisha Melkizedeki na Kristo.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Saturday, April 15, 2017

NI MANENO GANI YALIANDIKWA KWENYE ANWANI JUU YA KICHWA CHA YESU PALE MSALABANI?


Image may contain: text
Kwenye Mathayo 27:37; Marko 15:26; Luka 23:38 na Yohana 19:19, ni maneno gani hasa yaliyoandikwa kwenye anwani juu ya kichwa cha Yesu?
Kwanza tuangalie mambo matano yanayohusiana na jibu, na kisha majibu mawili.
1. Kwanza kabisa hapakuwa na ujumbe mmoja, lakini kulikuwa na jumbe tatu, kama Yohana 19:29 inavyosema, anwani iliandikwa Kiaramu, Kilatini na Kigiriki.
2. Hivi ndivyo waandishi wa injili wanavyo ripoti:
Mathayo 27:37 inasema, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."
Marko 15:26, "Mfalme wa Wayahudi."
Luka 23:38, "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi."
Yohana 19:19, "Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi."
3. Waandishi wa kale walikuwa na kawaida ya kufafanua maneno badala ya kunukuu. Ripoti Tulizo nazo hapa ni sahihi, lakini hazina maelezo ya kina. Hivyo, kwa mfano, kama mwandishi mmoja alisema "Huyu ndiye Yesu, Mfalme wa Wayahudi", na mwingine alisema "Mfalme wa Wayahudi", wote wanaweza kuwa wanaripoti maneno yale yale. Mwandishi wa kwanza anaripoti maneno zaidi kuliko yule wa pili.
4. Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, anaripoti kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwanza kwa lugha ya Kiebrania (au Kiaramu?) na kisha ikatafsiriwa kwenye Kigiriki. Waandishi wengine waliandiki Kigiriki. Hivyo, kuna tafsiri kati ya maneno yaliyosemwa na yale yaliyoandikwa na waandishi wa Injili.
5. Bila kujali tofauti zilizopo kati ya anwani hizi tatu, Marko anaelekea kuripoti maneno yaliyopo kwa waandishi wote watatu.
Jibu la Kwanza: Jumbe hizi tatu kwenye lugha tatu tofauti zimeripotiwa kwenye Mathayo, Luka, na Yohana. Marko anaripoti maneno yaliyomo kwa waandishi wote watatu. Pilato huenda hakujua Kiaramu kwa hiyo ujumbe ungeweza kuandikwa kwa Kilatini, na kutafsriwa kwenye Kigiriki na Kiaramu ili kila mtu aweze kuusoma.
Jibu la Pili: Kwa kuwa waandishi wa injili waliripoti maneno yaliyokuwa yametafsiriwa, na mambo kama "Hii ni" yalitokea mara kwa mara kwenye tafsiri, tuna uhakika na ujumbe wa anwani, lakini hatuna uhakika na maneno halisi. Hata hivyo, kitu muhimu hapa ni ujumbe, siyo maneno halisi.
HAKIKA YESU NI MFALME WA WAFALME.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UFUFUO WA YESU KRISTO


HOSANA: YESU AMEFUFUKA
UFUFUO WA YESU KRISTO
Ufufuo wa Yesu uliwatia moyo sana wanafunzi wake. Hakuwa mfu kama maadui zake walivyoamini. Yesu alikuwa hai akiwa kiumbe wa roho mwenye nguvu ambaye hakuna mwanadamu angeweza kumdhuru. Ufufuo wake ulithibitisha kwamba alikuwa Mwana wa Mungu na Mungu, na kujua jambo hilo kuliwatia moyo wanafunzi wake, wakawa na shangwe kubwa badala ya huzuni. Na pia wakawa na ujasiri badala ya hofu. Ufufuo wa Yesu ulikuwa muhimu sana katika kutimizwa kwa kusudi la Mungu na ulikuwa msingi wa habari njema waliyohubiri kwa ujasiri kotekote.
Mitume walijua kwamba ufufuo wa Yesu ulikuwa tofauti na ufufuo wowote uliotangulia. Watu waliofufuliwa mapema walifufuliwa wakiwa na miili ya kibinadamu na hatimaye walikufa tena. Yesu alifufuliwa akiwa na mwili wa roho ambao haungeweza kuharibika. (Soma Matendo 13:34.) Petro aliandika kwamba Yesu “aliuawa katika mwili, lakini akafanywa kuwa hai katika roho.” Zaidi ya hayo, “yuko mkono wa kuume wa Mungu, kwa maana alienda zake mbinguni; na malaika na mamlaka na nguvu vilitiishwa kwake.” (1 Petro 3:18-22) Ufufuo wowote uliotangulia ufufuo wa Yesu ulikuwa muujiza wenye kustaajabisha, lakini ufufuo wa Yesu ulikuwa muujiza mkubwa hata zaidi.
TUNAJUAJE KWAMBA YESU ALIFUFULIWA?
Ufufuo wa Yesu ulitokeaje “kulingana na Maandiko”?
Kwanza, tunajua kwamba Yesu alifufuliwa kwa sababu ufufuo wake ulitokea “kulingana na Maandiko.” Neno la Mungu lilitabiri ufufuo huo. Kwa mfano, Daudi aliandika kwamba mtumishi “mshikamanifu” zaidi wa Mungu hataachwa katika Kaburi. (Soma Zaburi 16:10.) Katika siku ya Pentekoste ya mwaka 33 W.K., mtume Petro alionyesha kwamba maneno hayo ya kinabii yalimhusu Yesu. Alisema hivi: “[Daudi] aliona kimbele na kusema kuhusu ufufuo wa Kristo, kwamba hakuachwa katika Kaburi wala mwili wake haukuona uharibifu.”—Matendo 2:23-27, 31.
Pili, tunajua kwamba Yesu alifufuliwa kwa sababu tuna ushuhuda wa mashahidi wengi. Kwa siku 40, Yesu aliyefufuliwa aliwatokea wanafunzi wake katika bustani ambamo kaburi lake lilikuwa, na pia aliwatokea njiani wakielekea Emau, na wakiwa sehemu nyingine. (Luka 24:13-15) Katika pindi hizo, aliongea na mtu mmoja-mmoja kutia ndani Petro, na pia aliongea na vikundi vya watu. Hata pindi fulani, Yesu aliyefufuliwa alitokea umati wa watu zaidi ya 500! Ushuhuda wa mashahidi wengi hivyo waliomwona Yesu aliyefufuliwa hauwezi kukanushwa.
Tatu, tunajua kwamba Yesu alifufuliwa kwa sababu wanafunzi wake walitangaza ufufuo wake kwa bidii. Walinyanyaswa, wakateswa, na kuuawa kwa sababu ya kutangaza kwa bidii ufufuo wa Kristo. Kama Yesu hangekuwa amefufuliwa, yaani, ikiwa huo ulikuwa uwongo, kwanini Petro alihatarisha uhai wake kwa kuwatangazia viongozi wa kidini kuhusu ufufuo wa Kristo ilhali viongozi hao walimchukia Yesu na kupanga njama auawe? Kwa sababu Petro na wanafunzi wengine walikuwa na uhakika kwamba Yesu alikuwa hai na alikuwa akiongoza kazi ambayo Mungu alitaka ifanywe. Isitoshe, ufufuo wa Yesu uliwahakikishia wafuasi wake kwamba wao pia wangefufuliwa. Kwa mfano, Stefano alikufa akiwa na uhakika kwamba wafu watafufuliwa.—Matendo. 7:55-60.
Ufufuo wa Kristo unatupatia ujasiri wa kuhubiri. Kwa miaka 2,000, maadui wa Mungu wametumia kila aina ya silaha kukomesha kazi ya kuhubiri habari njema—wametumia uasi-imani, dhihaka, vikundi vyenye ghasia, marufuku, mateso, na kuwaua watumishi wa Mungu. Hata hivyo, hakuna chochote, yaani, hakuna ‘silaha yoyote iliyofanywa juu yetu’ imekomesha kazi yetu ya kuhubiri kuhusu Ufalme na kufanya wanafunzi. (Isaya 54:17) Hatuwaogopi watumishi au watumwa wa Shetani. Yesu yuko pamoja nasi, na anatusaidia kama alivyoahidi. (Mathayo 28:20) Hatuna sababu yoyote ya kuogopa kwa kuwa hata adui zetu wafanye nini, hawataweza kamwe kutunyamazisha!
Yesu alisema: “Mimi ndiye ufufuo na uzima. Yule anayeniamini, hata akifa, atarudi kwenye uzima.” (Yohana 11:25) Kwa hakika, maneno hayo yenye kusisimua yatatimia. Yesu ana Mamlaka yote Mbinguni na Duniani ya kuwafufua wale wanaopata uhai wa kiroho mbinguni, na pia kuwafufua mabilioni ya watu wanaotumaini kuishi milele. Dhabihu ya Yesu inayofunika dhambi na pia ufufuo wake unatuhakikishia kwamba kifo hakitakuwapo tena. Je, kujua mambo hayo hakukupi nguvu za kuvumilia jaribu lolote lile na hata kukabili kifo kwa ujasiri?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

KWA NINI WAISRAELI WANASHEREHEKEA PASAKA KWA ZAIDI YA MIAKA 3500?

Image may contain: one or more people, crowd, outdoor and text
“Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaisherehekea ikiwa sherehe kwa Yehova.”— Kutoka 12:14.
Ni sherehe ya Pasaka. Ilikuwa sherehe ya kukumbuka kukombolewa kwa taifa la kale la Israeli kutoka utumwani huko Misri. Tukio hilo linapaswa kuwa muhimu kwako. Kwa nini? Kwa sababu linahusiana na mambo fulani muhimu maishani mwako.
Hata hivyo, huenda ukasema: ‘Wayahudi ndio wanaosherehekea Pasaka, lakini mimi si Myahudi. Inanihusuje?’
Maneno haya muhimu yanajibu swali hilo: “Kristo pasaka yetu ametolewa dhabihu.” (1 Korintho 5:7) Ili tuelewe vizuri umuhimu wa maneno hayo ya kweli, tunahitaji kuijua Pasaka ya Wayahudi na kuona jinsi inavyohusiana na amri fulani waliyopewa Wakristo wote.
Ni nini kilichotukea kabla ya Pasaka ya kwanza?
Baada ya Waisraeli kuwa watumwa kwa miaka mingi huko Misri, Mungu alimtuma Musa na Haruni ndugu yake, wakamwambie Farao awaachilie huru watu Wake. Mtawala huyo wa Misri mwenye kiburi alikataa kuwaruhusu Waisraeli waende zao, hivyo Mungu akaipiga nchi ya Misri kwa mfululizo wa mapigo yenye kuangamiza. Mwishowe, Mungu alileta pigo la kumi lililoua wazaliwa wote wa kwanza Wamisri, na hivyo Farao akawaacha Waisraeli waende zao.— Kutoka 1:11; 3:9, 10; 5:1, 2; 11:1, 5.
Hata hivyo, Waisraeli walipaswa kufanya nini kabla ya kuachiliwa huru?
Ulikuwa wakati wa majira ya kuchipua ya mwaka wa 1513 K.W.K., katika mwezi wa Kiebrania wa Abibu, uliokuja kuitwa Nisani, wakati ambapo saa za mchana hulingana kwa urefu na saa za usiku. * Mungu alisema kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huo, Waisraeli walipaswa kuanza kujitayarisha kufanya mambo fulani Nisani 14. Siku hiyo ilianza jua lilipotua kwa kuwa kulingana na Waebrania, siku ilianza na kwisha jua lilipotua. Katika Nisani 14, kila familia ilipaswa kuchinja kondoo dume (au mbuzi), kuchukua sehemu ya damu na kuipaka juu ya miimo ya mlango na sehemu ya juu ya mlango wa nyumba. (Kutoka 12:3-7, 22, 23) Kila familia ilipaswa kumla mwana-kondoo aliyechomwa kwa moto, mboga, na mkate usiotiwa chachu. Malaika wa Mungu angepita katikati ya nchi na kumchinja kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, lakini Waisraeli waliotii wangelindwa, kisha Farao angewaruhusu waende zao.—Kutoka 12:8-13, 29-32.
Hivyo ndivyo ilivyotukea, na Waisraeli walipaswa kuendelea kukumbuka ukombozi wao.
Mungu aliwaambia hivi: “Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaisherehekea ikiwa sherehe kwa Yehova katika vizazi vyenu vyote.
Nanyi mtaisherehekea kama sheria mpaka wakati usio na kipimo.” Mwadhimisho huo uliofanywa siku ya 14 ulifuatiwa na sherehe ya siku saba. Nisani 14 ndiyo iliyokuwa siku ya Pasaka, lakini siku zote nane za sherehe hiyo ziliitwa pia Pasaka. (Kutoka 12:14-17; Luka 22:1; Yohana 18:28; 19:14) Pasaka ilikuwa mojawapo ya sherehe rasmi (Sikukuu) ambazo Wayahudi walipaswa kusherehekea kila mwaka.—2 Nyakati 8:13.
Acheni tufikirie tena kilichotukia Misri. Musa alisema kwamba watu wa Mungu wangeendelea kusherehekea Pasaka; ilipaswa kuwa sharti “mpaka wakati usio na kipimo.” Wakati wa sherehe hiyo ya kila mwaka, watoto waliwauliza wazazi wao maana ya tukio hilo. (Soma Kutoka 12:24-27; Kumbukumbu 6:20-23) Kwa hiyo, Pasaka ingekuwa “ukumbusho” hata kwa watoto.—Kutoka 12:14.
Wakristo wa kweli hawasherehekei Pasaka ya Kiyahudi. Sherehe hiyo ilikuwa sehemu ya Sheria ya Musa, na hatuko chini ya Sheria hiyo. (Roman 10:4; Kolosai 2:13-16) Hata hivyo, tunakumbuka kwa uthamini kifo cha Mwana wa Mungu. Lakini kuna mambo fulani katika sherehe ya Pasaka iliyoanzishwa huko Misri yaliyo na maana kwetu.
Mwana-kondoo alipochinjwa kwa ajili ya mlo wa Pasaka, Waisraeli hawakupaswa kuvunja mfupa wake wowote. (Kutoka 12:46; Hesabu 9:11, 12)
Namna gani YESU “Mwana-Kondoo wa Mungu” aliyekuja kutoa fidia?
(Yohana 1:29) Alitundikwa mtini katikati ya wahalifu wawili. Wayahudi walimwomba Pilato aagize mifupa ya wanaume hao waliotundikwa ivunjwe. Hilo lingefanya wafe haraka na hivyo kuondolewa juu ya miti kabla ya Nisani 15, siku ya Sabato kuu. Askari-jeshi walivunja miguu ya wahalifu wawili waliotundikwa, “lakini walipokuja kwa Yesu, kwa kuwa waliona kwamba tayari alikuwa amekufa, hawakuivunja miguu yake.” (Yohana 19:31-34) Vivyo hivyo, mwana-kondoo wa Pasaka hakuvunjwa miguu. Kwa njia hiyo, mwana-kondoo huyo alikuwa “kivuli” cha jambo ambalo lingetukia Nisani 14, mwaka wa 33 W.K. (Ebrania 10:1) Isitoshe, mambo hayo yalitimiza Zaburi 34:20, na hilo linapaswa kuimarisha uhakika wetu katika unabii.
Ndio maana hii leo, sisi Wakristo tunasherekea Pasaka kwasabau Yesu ni dhabihu bora zaidi inayoweza kuokoa uhai milele.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Friday, April 14, 2017

Muslims Are Taking Countless Africans As Slaves, Starving Them To Death, Selling Them And Taking The Women To Rape Them

Related image
Muslim smugglers are taking countless Africans as slaves, with many instances of people being starved to death and women being raped. Under Gaddafi, blacks in Libya were protected, but as soon as he was toppled, the Libyans began to enslave them and put them in cages. This was all thanks to American policy, a policy that I fear is continuing unchanged.  As we read in one report:
Large numbers African migrants, mostly from Nigeria, Senegal and Gambia, are being traded in slave markets, with many subjected to sexual exploitation and others left to starve in Libya, a United Nations agency has said.
The International Organisation for Migration says West African migrants have recounted being bought and sold in garages and car parks in the southern city of Sabha, one of Libya’s main migrant smuggling hubs.
They are traded for between $200 and $500 and are held on average for two or three months.
Othman Belbeisi, head of the IOM’s Libya mission, told journalists in Geneva: “Migrants are being sold in the market as a commodity.
“Selling human beings is becoming a trend among smugglers as the smuggling networks in Libya are becoming stronger and stronger.”
The migrants are captured as they head north towards Libya’s Mediterranean coast, where some try to catch boats for Italy.
Armed groups and smuggling networks often try to extort money in exchange for allowing migrants to continue, and most of those seized are used as day labourers in construction or agriculture. Some are paid and others are forced to work without pay.
“About women, we heard a lot about bad treatment, rape and being forced into prostitution,” Belbeisi said.
The IOM said it had spoken to one Senegalese migrant who was held in a Libyan’s private house in Sabha with about 100 others, who were beaten as they called their families to ask for money for their captors.
He was then bought by another Libyan, who set a new price for his release.
Some migrants who cannot pay their captors are reportedly killed or left to starve to death, and when migrants die or are released, others are purchased to replace them, the IOM said.
Migrants are buried without being identified, with families back home uncertain of their fate.
“What we know is that migrants who fall into the hands of smugglers face systematic malnutrition, sexual abuse and even murder,” Mohammed Abdiker, IOM’s Director of Operations and Emergencies, said in a statement. “We are hearing about mass graves in the desert.”
Libya is the main gateway for migrants attempting to reach Europe by sea, with more than 150,000 people making the crossing in each of the past three years.
So far this year an estimated 26,886 migrants have crossed to Italy, over 7,000 more than during the same period in 2016. More than 600 are known to have died at sea, while an unknown number perish during their journey north through the desert.

http://shoebat.com/2017/04/12/muslims-are-taking-countless-africans-as-slaves-starving-them-to-death-selling-them-and-taking-the-women-to-rape-them/

GERMANY: As expected, a MUSLIM has been arrested in the pipe bomb attack on the Bourussa Dortmund soccer team bus


An Iraqi Muslim has been arrested over Bourussa Dortmund team bus bombing where 3 roadside bombs were detonated by mobile phone. Police found three letters claiming the attack was carried out in the name of Islam. 

UK Daily Mail  (h/t bleeps) A Muslim suspect has been arrested in connection with the pipe bomb attack on Borussia Dortmund’s team bus as authorities say they are treating it as a ‘terrorist attack’. German police searched properties belonging to ‘two suspects from the Islamist spectrum’ on Wednesday and arrested a 25-year-old Iraqi Muslim man from Wuppertal – not far from Dortmund – meaning another man is still on the loose.

The explosive devices used in the attack contained metal pins, one of which was found buried in a headrest on the vehicle, according to Frauke Koehler, a spokeswoman for federal prosecutors. 

Ms Koehler said it was lucky ‘that nothing worse happened’, adding that investigators are still working to determine how the devices were detonated and what substance was used.

The second suspect is a German (Muslim?), aged 28, from Froenderburg, near Unna, also in the state of North Rhine-Westphalia.

They have both reportedly been on the police and intelligence services radar for affiliation to ISIS while it has been claimed that one of them was seen in the vicinity of the crime scene shortly before the pipe shrapnel bombs were detonated.

Elsewhere police said three letters claiming responsibility for the attack have been found, all of them saying that it was carried out in the name of Islam. Another letter claiming to be from the far-left group Antifa had been discounted as a fraud.

At least one of the notes made reference to the Berlin Christmas market attack, in which an ISIS fanatic drove a stolen truck into shoppers, killing 12.

“According to Der Spiegel, that letter was written in German starts with the phrase ‘In the Name of Allah, the Gracious, the Merciful’ and ends with two demands.

First, ‘tornadoes’, a reference to German reconnaissance planes, must be withdrawn from Syria, and second the US base in Ramstein, Rhineland-Palatinate, should be closed….The letter also claims that German combat aircraft are involved in killing Muslims in the ‘Islamic State’, adding that athletes and other celebrities ‘in Germany and other Kreuzfahrer (crusader) nations’ are now on a ‘death list.’”



UNIVERSITY OF TEXAS-Dallas: Qurans found in toilet of Student Union


Police are looking for possible suspects who put two Islamic books of hate – Qurans – in the toilet of a bathroom at the University of Texas at Dallas between 6 p.m. and 7 p.m. on March 28th.

NBCdfw  The Muslim Student Association (MSA) (North American front group for the terror-linked Muslim Brotherhood) withheld its regular board meeting and discussed the incident. Mohammad Syed, president of the MSA, strongly condemned the act.

“Given the current political climate and how Muslims are portrayed in the media, it makes certain individuals act in this hateful way,” Muslim Student Association president Mohammad Syed told The Mercury. (Um, NO! The way Muslims behave around the world is causing certain individuals to show their hatred in a non-violent way…unlike Muslims)

DEAD BODY of first female Muslim judge on NY Court of Appeals found washed up on the side of the Hudson River


Sheila Abdus-Salaam, 65, was discovered floating in the water near 132nd Street and Hudson Parkway at around 1:45 p.m., according to police sources. Witnesses had spotted her fully clothed body and called 911, police said.

NY Post  Sources told The Post that Abdus-Salaam, who is an associate judge of the Court of Appeals, had been reported missing from her home in Harlem earlier in the day. Her husband later identified her body. Sources said it showed no obvious signs of trauma or injuries indicating criminality or foul play, and that her death appeared to be a possible suicide.

In addition to being the country’s first Muslim female judge, Abdus-Salaam was the first ever African-American woman to be appointed to the state’s Court of Appeals.

After receiving her degree from Columbia Law School, she began her legal career working as a staff attorney at East Brooklyn Legal Services. Abdus-Salaam rose through the state ranks before eventually being elected to the New York Supreme Court in 1993.

She was then appointed to the Court of Appeals by Cuomo in 2013. Former US Attorney General Eric Holder, who went to Columbia with Abdus-Salaam, was in attendance for her historic swearing-in ceremony and described how she had “defined herself by her relentless pursuit of excellence.” 

AUSTRALIA: Sen. Pauline Hanson ridiculed for advising people not to eat Islamic ‘halal-certified’ chocolate for Easter


One Nation Senator Pauline Hanson notes that Cadbury chocolate is halal-certified before plugging its competitors that are “not Halal certified” and is mocked for it on far left The Project TV by Muslim spokesjihadist, Waleed Aly.

“Don’t call me moderate”  In 2007 Waleed Aly published a book and there’s a whole chapter in there called ‘don’t call me moderate’ because it’s a term he hates. I don’t like what it implies, and so if people are calling me a “moderate” Muslim it annoys me. In other words, there is no radical Islam. There is no moderate Islam. Islam is Islam and it is inherently radical.

Sharia-compliant Cadbury axes the word “Easter” from its halal-certified Easter eggs.

Not only has Cadbury gone ‘halal,’ starting this year, the British chocolate maker also crucified the word Easter, in ‘honor’ of Easter, in order not to offend Muslim religious ‘sensibilities.’ From now on, there will be no more ‘Easter’ eggs or ‘Easter’ bunnies on these halal-certified products, because the company obviously doesn’t give a damn about offending your Christian ‘sensibilities.’

All references to the Easter bunny have been removed, too, Easter bunnies are now simply chocolate bunnies, you can eat all year long, especially during Ramadan. Easter is out but ‘HALAL’ is in, with halal certification language clearing showing on the ‘unEaster’ Easter eggs.

Perhaps next year, Cadbury will rename the Easter eggs and bunnies ‘Halal’ eggs and bunnies, which Muslim children can enjoy while they are watching the blood drain out of the necks of the writhing in pain animals that their elders have just slaughtered in celebration of Eid. 

KWANINI WASABATO NA WAISLAM HAWAITAMBUI PASAKA?

Image may contain: cloud, sky and text
“Siku Hii Itakuwa Ukumbusho Kwenu”
TORATI INAITAMBUA PASAKA:
“Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaisherehekea ikiwa sherehe kwa Mungu Yehova.”—Kutoka 12:14.
“Kristo Pasaka yetu ametolewa dhabihu.” (1 Korintho 5:7)
Nisani 14 ndiyo iliyokuwa siku ya Pasaka, lakini siku zote nane za sherehe hiyo ziliitwa pia Pasaka. (Kutoka 12:14-17; Luka 22:1; Yohana 18:28; 19:14) Pasaka ilikuwa mojawapo ya sherehe rasmi (“sikukuu,” Union Version) ambazo Wayahudi walipaswa kusherehekea kila mwaka.—2 Nyakati 8:13.
YESU ALISHEREKEA PASAKA, LAKINI WASABATO NA WAISLAM WANAIPINGA PASAKA:
Yesu na mitume wake walisherehekea Pasaka kila mwaka kwa sababu walikuwa Wayahudi na hivyo walikuwa chini ya Sheria ya Musa. (Mt. 26:17-19) Mara ya mwisho waliposherehekea Pasaka, Yesu alianzisha mwadhimisho mpya ambao wafuasi wake wangekumbuka kila mwaka, yaani, Mlo wa Jioni wa Bwana. Lakini walipaswa kuuadhimisha siku gani?
Kwa kuwa Yesu alianzisha Mlo wa Jioni wa Bwana baada tu ya Pasaka hiyo ya mwisho, mwadhimisho huo mpya ulifanywa katika siku ambayo Pasaka ilikuwa ikisherehekewa.
Kristo aliwaambia hivi Petro na Yohana: “Nendeni mkatutayarishie pasaka ili tule.” (Luka 22:7, 8) ‘Mwishowe, saa ikafika’ ya mlo wa Pasaka, baada ya jua kutua mnamo Nisani 14, ilikuwa Alhamisi jioni. Yesu alikula mlo huo pamoja na mitume wake, kisha akaanzisha Mlo wa Jioni wa Bwana. (Luka 22:14, 15) Usiku huo, alikamatwa na kushtakiwa. Yesu alitundikwa mtini karibu saa sita mchana Nisani 14, naye akafa siku hiyohiyo alasiri. (Yohana 19:14)
Hivyo, ‘Kristo pasaka yetu akatolewa dhabihu’ siku ileile ambayo mwana-kondoo wa Pasaka alichinjwa. (1 Korintho 5:7; 11:23; Mt. 26:2) Yesu alizikwa mwishoni mwa siku hiyo ya Kiyahudi, kabla ya Nisani 15 kuanza. *—Lawi 23:5-7; Luka 23:54.
Baada ya kusoma aya zote hapo juu, kwanini Wasabato "SDA" na Waislam wanaikataa sikukuu hii ya Sabato iliyo kwenye Torati?
Kama kweli Wasabato na Waislam wanaitambua TORATI, Kwanini wanasema PASAKA ni sikukuu ya WAPAGANI?
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration

The Angelic Guardianship in Psalm 91:11: A Scholarly and Inspirational Exploration By Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological Institute A...

TRENDING NOW