Saturday, May 13, 2017

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 5

Image may contain: one or more people, people standing, sky and text
NAWEZAJE KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU?
Baadhi ya wakristo hawawezi kupambanua kati ya "kujazwa na Roho Mtakatifu" na "Kuwa na Roho Mtakatifu" Ama wengine pia hufikiri" Kujazwa na Roho Mtakatifu" ni sawa na kuwa na "Karama za Roho Mtakatifu". Ni maombi yangu kwamba Mungu atatusaidia kuelewa maana halisi ya kujazwa na Roho Mtakatifu.
ROHO MTAKATIFU NI NANI?
Roho mtakatifu ni Mungu(Mungu nafsi ya tatu), Roho anapatikana kila mahali kwa wakati mmoja
( Matendo 5: 3-4) " 3 Lakini Petro akasema:“Anania, kwa nini Shetani amekupa ujasiri wa kuidanganyai roho takatifu na kujiwekea kwa siri kiasi fulani cha bei ya shamba? 4 Kabla ya kuuza je, haikuwa mali yako, na baada ya kuuza je,haikuendelea kuwa mikononi mwako? Kwa nini ukakusudia tendo kama hili katika moyo wako? Umedanganya, si wanadamu, bali Mungu."
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NI ZIPI?
Mwalimu, kiongozi, Fumbo ya siri za Mungu (1.Korintho 2:10)
"Kwa maana ni kwetu sisi Mungu ameyafunua kupitia roho yake, kwa maana roho huchunguza ndani ya mambo yote, hata mambo mazito ya Mungu."
Mtoa habari wa mambo yajayo, msemaji wa mambo ya Mungu, Mkumbushaji, Kutupa nguvu.
Huchunguza yote, mwombezi (Warumi 8:26)
"26 Vivyo hivyo Roho pia hujiunga kutoa msaada kwa ajili ya udhaifu wetu; kwa maana lile tatizo kuhusu tunalohitaji kusali hatujui, lakini roho yenyewe hutuombea pamoja na kuugua kusikotamkwa."
UNAWEZAJE KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU?
Kumtii MUNGU katika sheria zake
Moyo wote utawala wake unakuwa wa Roho mtakatifu, roho anakusaidia kuishi kwa neno
(Waefeso 5:18)
"Pia,msiwe mkilewa divai, ambayo ina upotovu ndani yake, bali endeleeni kujazwa na roho,"
Utajazwa kwa Maombi, maisha ya kulitafuta neno,maisha ya kunyenyekea, kutii.
(1 Samwel 15:21)
"Nao watu wakachukua kutoka katika nyara kondoo na ng’ombe, walio bora zaidi kati yao kama kitu kilichotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, ili wamtolee Yehova,Mungu wako dhabihu katika Gilgali."
(Isaya 1:19)
"Ninyi mkionyesha utayari na kusikiliza,mtakula mema ya nchi."
(Yakobo 4:17)
"Kwa hiyo, ikiwa mtu anajua jinsi ya kufanya yaliyo sawa na bado hayafanyi, hiyo ni dhambi kwake."

Kinachozuia kujazwa na Roho Mtakatifu
Dhambi katika maisha ya muumini, hakuna kujazwa kama unadhambi (Waefeso 4 : 30)
"Pia, msiwe mkiihuzunisha roho takatifu ya Mungu, ambayo kupitia hiyo mmetiwa muhuri kwa ajili ya siku ya kuachiliwa huru kupitia fidia"
(1 Thesalonike 5:19)
"Msiuzime moto wa roho"
Kifungu cha maana katika kuelewa juu ya kujazwa na Roho Mtakatifu in Yohana 14:16, mahali ampapo Yesu anaahidi kukaa kwa Roho Mtakatifu kwa wakristo, na huyo atadumu si kwa muda. Ni kitu cha maana kutofautisha kati ya kukaa kwa Roho Mtakatifu na kujazwa na Roho Mtakatifu. Kudumu kwa Roho Mtakatifu aupo kwa baadhi ya wakristo, bali ni kwa Wakristo wote. Kuna sehemu nyingi katika Bibilia zinazo pongeza huu msimamo wetu.
Kwanza, Roho Mtakatifu ni zawadi iliyopewa Wakristo wote katika Kristo Yesu bila kupagua, na hakuna sheria za kutimiza ila tu ni kuwa na imani katika Kristo Yesu (Yohona 7:37-39).
Pili, Roho Mtakatifu unapokewa wakati wa kuokoka (Waefeso 1:13). Wagalatia 3:2 inasisitiza ukweli huu pia, kwa kusema kwamba kutiwa muhuri na kujazwa na Roho Mtakatifu ulitokea wakati wa kuokoka.
Tatu, Roho Mtakatifu unakaa kwa Wakristo milele. Wakristo wamepewa Roho Mtakatifu kama mtaji ama tibitisho la utukufu wao katika siku zijazo katika Kristo (2 Wakorintho 1:22; Waefeso 4:30).
Hili ni linganisho la kujazwa kwa Roho Mtakatifu ambao Waefeso 5:18 yazungumzia. Kikamilifu ni lazima tuzame katika Roho Mtakatifu ili atumiliki na katika hali hiyo atujaze. Warumi 8:9 na Waefeso 1:13-14 za sema kwamba anakaa kwa kila Mkristo, lakini anaweza kuhusunishwa (4:30), na kazi yake ndani yetu unaweza poa (1Wathesalonike 5:19). Wakati tunaruhusu haya kutokea hatuwezi kuhisi kikamilifu Roho Mtakatifu ukifanya kazi na nguvu zake ndani yetu.
Kujazwa na Roho Mtakatifu haimaanishi tendo la nche pekee; pia yamaanisha tendo la kimawazo ambalo latutia moyo kwa kila tendo tutendalo. Zaburi 19:14 yasema, “Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wnagu.”
Dhambi ndiyo huzuia kujazwa kwa Roho Mtakatifu, na kumtii Mungu ndio njia pekee Roho anaweza kutunzwa. Waefeso 5:18 yatwaamuru kwamba tujazwe na Roho Mtakatifu; bali si kwa kuomba ili tujazwe na Roho Mtakatifu ambayo itawezesha kukamilisha kujazwa kwa Roho. Ni utiifu wetu wa sheria za Mungu wawezesha Roho kufanya kazi kwa huru ndani yetu. Kwa sababu tumeadhirika kwa dhambi, ni vigumu kujazwa na Roho wakati wote. Wakati twatenda dhambi ni lazima tutubu papo hapo kwa Mungu na tufanye upya mkataba wa kujazwa na Roho na kuongozwa na Roho Mtakatifu.
FAIDA ZA KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU
Kutoufuata mwili , Hakuna kuufata mwili, kuhuishwa kwa miili yetu( Warumi 8 : 9 -10)
"Hata hivyo, ninyi hampatani na mwili, bali mnapatana na roho, ikiwa kweli roho ya Mungu inakaa ndani yenu. Lakini ikiwa mtu yeyote hana roho ya Kristo, mtu huyo si wake. 10 Lakini ikiwa Kristo yuko katika muungano pamoja na ninyi,mwili kwa kweli umekufa kwa sababu ya dhambi, bali roho ni uzima kwa sababu ya uadilifu. 11 Basi, ikiwa roho ya yule aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu inakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua KristoYesu kutoka kwawafu ataifanya pia miili yenu inayoweza kufa iwe hai kupitia roho yake inayokaa ndani yenu"
Ikiwa maisha ya dhambi yatatawala, na Roho Mtakatifu kuhuzunika na baadae kupoa. Mkristo hupoteza nguvu ya kushinda dhambi. Kwamba muumini anayeishi katika dhambi ni lazima kutubu kwa Mungu na kufanya upya mkataba ili kujazwa tena na Roho Mtalktifu.
"Kwa kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, Hao ndio wana na Mungu" (Warumi 8:14)
Ukiwa na swali lolote au kitu kinakutatiza kuhusiana na Somo hili tafadhali andika au toa maoni yako hapa chini na wachungaji na viongozi wa dini watalijibu mara moja na haraka iwezekanavyo.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

BIBLIA INAKATAZA ULEVI

Image may contain: one or more people and text
Je, Bibilia Ya Sema Nini Kuhusu Ulevi?
Bibilia yalinganisha ulevi na upumbavu (Mithali 26:9) na inapeyana onyo hili: Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo. (Isaya 5:11). Ole wake yeye ambaye jirani yake kileo, akiimimina kutoka kwenye kiriba cha mvinyo mpaka wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi. (Habakkuk 2:15).Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo nao walio hodari katika kuchanganya vileo, (Isaya 5:22).
Amkeni, enyi walevi, mlie!
Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo, (Joel 1:5).
Mtume Paulo aliwaonya watu ya kuwa hakuna mlevi atakaeingia katika Ufalme wa Mungu (1 Wakoritho 6:10). Ulevi ni kitendo cha kawaida cha utu alisi wa dhambi hakuna awayeyeyote aishie
katika njinsi hii atakae urithi ufalme wa mungu (Wagalatia 5:19-21).
“DIVAI ni mdhihaki, kileo husababisha msukosuko, na kila mtu anayepotezwa nacho hana hekima.” Je, andiko hilo la Biblia linalopatikana katika Methali 20:1, linaonyesha kwamba ni vibaya kunywa kileo? Wengine wanafikiri hivyo. Ili kuthibitisha hilo, wao hutaja masimulizi ya Biblia ambapo watu walifanya mambo mabaya kwa sababu ya matumizi mabaya ya kileo.—Mwanzo 9:20-25.
Maandiko yana ilani nyingi juu ya kunywa kileo (Mambo ya Walawi 10:9; Hesabu6:3; Kumbukumbu la Torati 29:6; Waamuzi 13:4,7,14; Samueli wa kwanza 1:15; Methali 20:1; 31:4,6; Isaya 5:11;22; 24:9; 28:7; 29:9; 56:12; Mika 2:11; Luka 1:15).
Biblia inaonya kuhusu matokeo mabaya ya kunywa kileo kupita kiasi. Waefeso 5:18 inasema: “Pia, msiwe mkilewa divai, ambayo ina upotovu ndani yake.” Vilevile, Methali 23:20, 21 inahimiza hivi: “Usiwe kati ya watu wanaokunywa divai mno, kati ya watu wanaokula nyama kwa ulafi. Kwa maana mlevi na mlafi watakuwa maskini.” Na Isaya 5:11 inasema: “Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema ili watafute tu kileo, wanaokawia mpaka giza la jioni sana hivi kwamba divai inawawasha!”
Kile Mungu anachowaamuru Wakristo juu ya kileo ni wajizuie na ulevi (Waefeso 5:18).
Biblia inakataza ulevi na athari zake (Methali 23:29-35).
Wakristo wanakatazwa kuachilia miili yao itawalwe na vitu vinginevyo. (Wakorintho wa kwanza 6:12; Petro wa pili 2:19). Kunywa kileo kingi kunaathiri mtu. Maandiko yanakataza chochote kile ambacho kwa kukifanya unasababisha wengine kujikwaa (Wakorintho wa kwanza 8:9-13). Kwa mujibu wa haya ni vigumu mkristo kukiri kuwa anakunywa kileo kwa utukufu wa Mungu (Wakorintho wa kwanza 10;31).
Mungu anatuamuru kuwa tusiwe walevi (Waefeso 5:18) Kwa wakati pia Mungu atuamuru tukane kabisa vinywaji vizito. Kama ilivyo kwa wachungaji (Mambo ya Walawi 10:9) Sheria za wanazareti (Hesabu 6:3) Hekima ya waongozao (Mithali 3:4) Nabii Danieli (Daniel 1:8) Yohana mbatizaji (Luka 1:15) Waumini wote katika hali tofauti tofauti (Warumi 14:21)
Kama umekuwa mlevi fungua moyo wako kwa Mungu mfalme kisha uombe ombi hili “ Mfalme wa mbingu na nchi naja mbele yako kwa jina la Yesu kristo.
Natubu dhambi zangu. Nakiri kwamba nimekosa mbele yako na nimeharibu maisha kwa ajili ya pombe Naomba unisamehe na unisafishe. Namchukua Yesu kama mfalme na mkombozi kwa
njia ya imani kupitia kwa damu yake. Nguvu za dhambi zimevunjwa .
Nakuhitaji kwa ukombozi. Nakemea roho wa ulevi na kuzivunja nguvu za kishetani, huku nikijuwa kwamba neno la Mungu lasema “Jisalimishe kwa Mungu.
Mkatae shetani na atakutoroka (Yakobo4:7) Asante kwa kunipa
ukombozi na neno lako lihimidiwe milele na milele. Amina.”
Kwa sababu umekuwa mkristo, umezaliwa tena kupitia kwa roho
mtakatifu, yafaa ukomae katika uhusiano wako na Mungu.
Yafaa ujifunze kuisikia sauti ya Mungu na ufuate njia zake:
1). Soma Biblia
2). Omba na uongee na Mungu moyoni mwako
3). Batizwa na ujiunge na Kanisa linalompendaza Yesu kristo.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

JE, TUNAWEZA AMINI UNABII NA MANABII WA SIKU ZA MWISHO? SOMO LA PILI

No automatic alt text available.
Somo la Pili:
Tunaanza na mwanamume ambaye anaheshimiwa na Waislamu, Wakristo, na Wayahudi. Alikuwa Mwebrania aliyeishi kuanzia mwaka wa 2018 hadi 1843 K.W.K.* Aliitwa Abrahamu.*
Abrahamu alihusika moja kwa moja katika baadhi ya unabii ulioandikwa mapema sana katika Biblia—unabii unaotuhusu sisi pia leo. Kulingana na kitabu cha Biblia cha Mwanzo, unabii huo ulitaja mambo yafuatayo:
(1) Uzao wa Abrahamu ungekuwa taifa kubwa.
(2) Ili wawe taifa kubwa, wangekuwa watumwa katika nchi ya kigeni.
(3) Wangekombolewa na kumiliki nchi ya Kanaani. Acheni tuchunguze mambo hayo kwa undani zaidi.
Unabii Mbalimbali Wenye Kustaajabisha
UNABII WA KWANZA:
“Nitafanya taifa kubwa kutokana nawe [Abrahamu].”—Mwanzo 12:2.
Utimizo: Wazao wa Abrahamu kupitia Isaka na Yakobo (ambaye pia anaitwa Israeli) walikuja kufanyiza taifa la kale la Israeli—taifa lililojitawala likiwa na wafalme wake.
Historia inafunua nini?
● Biblia inaonyesha waziwazi ukoo wa Abrahamu, kupitia Isaka, Yakobo, na wana 12 wa Yakobo. Nasaba hiyo ilitia ndani wafalme wengi waliotawala katika Israeli au Yuda. Kati ya watawala hao, 17 wanatajwa katika vitabu ambavyo si vya Biblia, na hilo linapatana na maandishi ya Biblia ya jinsi wazao wa Abrahamu kupitia Isaka na Yakobo walivyokuja kuwa taifa.*
UNABII WA PILI:
“Uzao wako [Abrahamu] utakuwa mkaaji mgeni katika nchi isiyokuwa yao, nao watawatumikia watu wale . . . Lakini katika kizazi cha nne watarudi hapa.”—Mwanzo 15:13, 16.
Utimizo: Kwa sababu ya njaa kali huko Kanaani, vizazi vinne vya wazao wa Abrahamu viliishi nchini Misri, kwanza wakiwa wakaaji wageni lakini baadaye wakiwa watumwa waliolazimishwa kutengeneza matofali kutokana na udongo na nyasi. Kwa mfano, tunaweza kufikiria kuhusu ukoo mmoja—ule wa Lawi, kitukuu wa Abrahamu, aliyehamia Misri pamoja na baba yake aliyezeeka—vizazi vyake vinne ni (1) Lawi, (2) mwana wake Kohathi, (3) mjukuu wake Amramu, na (4) kitukuu wake Musa. (Kutoka 6:16, 18, 20) Katika mwaka wa 1513 K.W.K., Musa aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri.—Ona orodha ya matukio iliyo hapo chini pamoja na sanduku “Kuweka Wakati kwa Usahihi.”
Historia inafunua nini?
● Kulingana na James K. Hoffmeier, profesa wa Agano la Kale na Uchimbuaji wa Vitu vya Kale vya Mashariki ya Kati, maandishi ya Misri na uthibitisho wa vitu vya kale vilivyochimbuliwa unaonyesha kwamba wazao wa Shemu (kama vile Waebrania wa kale) waliruhusiwa kuingia Misri wakiwa na mifugo yao kulipokuwa na njaa. Lakini je, Waisraeli waliwahi kuwa watumwa huko, waliolazimishwa kutengeneza matofali?
● Ingawa maandishi ya Wamisri hayawataji Waisraeli moja kwa moja, michoro katika makaburi ya Misri na vitabu vya kukunjwa vinathibitisha kwamba Wamisri waliwatumia wageni kutengeneza matofali kutokana na udongo na nyasi. Sawa tu na maandishi ya Biblia, maandishi ya Wamisri yanaonyesha kwamba wasimamizi wa kazi waliandika rekodi za kuonyesha idadi ya matofali yaliyotengenezwa. (Kutoka 5:14, 19) Hoffmeier anasema: “Maandishi ya Misri yanathibitisha kwamba wageni walilazimishwa kuwa watumwa . . . katika kipindi kilekile ambacho Waisraeli walikuwa wakikandamizwa. Hivyo basi, inaonekana kwamba ni sahihi kusema kuwa Waebrania wa kale waliingia Misri . . . wakati wa njaa na baadaye wakalazimishwa kuwa watumwa.”
UNABII WA TATU:
‘Nitawapa wazao wako nchi yote ya Kanaani.’—Mwanzo 17:8.
Utimizo: Ingawa Musa aliongoza taifa changa la Israeli kutoka Misri, Yoshua mwana wa Nuni ndiye aliyewaongoza kuingia nchi ya Kanaani katika mwaka wa 1473 K.W.K.
Historia inafunua nini?
● Ingawa huenda wachimbuaji wa vitu vya kale wakatoa tarehe zinazotofautiana, “tunapaswa kuzungumzia hasa kuingia kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani, na kukaa humo,” anaandika K. A. Kitchen, profesa aliyestaafu wa mambo ya Misri.
● Biblia inaonyesha kwamba Yoshua ‘aliteketeza jiji la Kanaani la Hasori katika moto.’ (Yoshua 11:10, 11) Katika magofu ya jiji hilo, wachimbuaji wa vitu vya kale wamechimbua mahekalu matatu ya Wakanaani ambayo yalikuwa yameharibiwa kabisa. Pia walipata uthibitisho kwamba jiji hilo liliteketezwa katika miaka ya 1400 K.W.K. Mambo hayo hakika yanapatana na Biblia.
● Jiji lingine la Kanaani linalostahili kufikiriwa ni Gibeoni, lililoko kilomita 9.6 hivi kutoka Yerusalemu. Wachimbuaji wa vitu vya kale waligundua jiji hilo walipopata jina lake likiwa limechongwa juu ya vishikio 30 hivi vya mitungi. Tofauti na wakaaji wa Hasori, Wagibeoni wa kale walikuwa wamefanya amani pamoja na Yoshua. Kwa sababu hiyo, akawafanya kuwa “watekaji wa maji.” (Yoshua 9:3-7, 23) Kwa nini aliwapa mgawo huo? Masimulizi yanayopatikana katika 2 Samweli 2:13 na Yeremia 41:12 yanaonyesha kwamba Gibeoni lilikuwa eneo lenye maji mengi. Basi kupatana na simulizi hilo la Biblia, kitabu Archaeological Study Bible, New International Version kinasema: “Kitu chenye kutokeza zaidi katika eneo la Gibeoni ni kwamba kulikuwa na maji mengi sana: chemchemi moja kubwa na saba ndogo.”
● Maandishi mengi ya kihistoria yamethibitisha kwamba watu wengi wanaotajwa katika Biblia waliwahi kuishi. Kama ilivyotajwa awali, orodha hiyo inatia ndani majina ya wafalme 17 waliokuwa wazao wa Abrahamu na wakatawala Israeli au Yuda. Kati yao Ahabu, Ahazi, Daudi, Hezekia, Manase, na Uzia. Kwa wazi, kuwepo kwa familia za kifalme kunakazia hoja ya kwamba taifa linaloitwa Israeli liliingia katika nchi ya Kanaani na kuimiliki.
● Mnamo 1896, wachunguzi walipata Jiwe la Merneptah huko Thebesi, Misri. Jiwe hilo lina maandishi yanayomsifu Farao Merneptah kwa kampeni yake ya kijeshi ya kuingia Kanaani karibu na mwaka wa 1210 K.W.K. Hayo ndiyo maandishi ya kwanza yasiyo ya Biblia yanazungumza kuhusu Israeli, jambo linalounga mkono hata zaidi kuwepo kwa taifa hilo.
Faida ya Kuwa na Habari Hususa
Kama vile ambavyo tumeona, Biblia ina habari nyingi hususa kuhusu watu, mahali, na matukio. Habari hizo hususa zinatuwezesha kuilinganisha Biblia na maandishi mengine, na hivyo kutusaidia kuthibitisha utimizo wa unabii wa Biblia. Kuhusiana na Abrahamu na uzao wake, mambo hakika yanaonyesha kwamba ahadi za Mungu zilitimizwa—uzao wa Abrahamu ulikuwa taifa, walifanywa kuwa watumwa nchini Misri, na baadaye waliimiliki nchi ya Kanaani. Mambo yote hayo yanatukumbusha maneno ya Petro, mwandikaji mmoja wa Biblia, ambaye alisema hivi kwa unyenyekevu: “Unabii haukuletwa wakati wowote kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu walisema yaliyotoka kwa Mungu kama walivyoongozwa na roho takatifu.”—2 Petro 1:21.
Baada ya Israeli kuimiliki nchi ya Kanaani, historia ya taifa hilo ilianza kubadilika sana, na kukawa na matokeo mabaya sana. Matokeo hayo mabaya yalitabiriwa pia na waandikaji wa Biblia, kama toleo linalofuata litakavyoonyesha.
“K.W.K.” inamaanisha “Kabla ya Wakati wa Kawaida.”
Mwanzoni Abrahamu aliitwa Abramu. Jina la Abrahamu alipewa baada ya kuitwa Baba wa Mataifa yote.
Ona 1 Mambo ya Nyakati 1:27-34; 2:1-15; 3:1-24. Wakati wa utawala wa Rehoboamu, mwana wa Mfalme Sulemani, taifa la Israeli liligawanywa kuwa ufalme wa kaskazini na ufalme wa kusini. Baada ya hapo, wafalme wawili walitawala Israeli wakati uleule.—1 Wafalme 12:1-24.
BARAKA KWA “MATAIFA YOTE”
Mungu aliahidi kwamba watu wa “mataifa yote” wangejibariki kupitia kwa uzao wa Abrahamu. (Mwanzo 22:18) Sababu kuu ambayo Mungu alifanya uzao wa Abrahamu uwe taifa ilikuwa kutokeza Masihi, ambaye angetoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu wote.* Kwa hiyo, ahadi ya Mungu kwa Abrahamu inakuhusu! Yohana 3:16 inasema hivi: “Mungu aliupenda ulimwengu sana hivi kwamba akamtoa Mwana wake mzaliwa-pekee, ili kila mtu anayemwamini asiangamizwe bali awe na uzima wa milele.”
Unabii unaohusiana moja kwa moja na utambulisho wa Masihi utazungumziwa katika Sehemu ya 3 na ya 4 ya mfululizo huu.
KUWEKA WAKATI KWA USAHIHI
Mfano unaoonyesha umuhimu wa Biblia kuweka wakati kwa usahihi unaonyeshwa katika 1 Wafalme 6:1, andiko linaloonyesha wakati ambapo Mfalme Sulemani alianza kazi ya ujenzi wa hekalu huko Yerusalemu. Tunasoma hivi: “Ikawa kwamba katika mwaka wa 480 [miaka 479 kamili] baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne [wa utawala wa Sulemani], katika mwezi wa Zivu, yaani, mwezi wa pili, baada ya Sulemani kuwa mfalme juu ya Israeli, akaanza kumjengea Yehova nyumba.”
Mfuatano wa matukio ya Biblia unaonyesha kwamba mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani ulikuwa mwaka wa 1034 K.W.K. Mwaka huo unatusaidia kufahamu wakati ambapo Waisraeli walitoka Misri kwani unapohesabu kurudi nyuma miaka 479 kamili inatufikisha kwenye mwaka wa 1513 K.W.K.
ABRAHAMU NI MTU ANAYETAJWA KATIKA HISTORIA
● Mabamba ya udongo ya mapema ya milenia ya pili K.W.K. yanaorodhesha majiji yaliyo na majina ya watu wa ukoo wa Abrahamu. Majiji hayo yanatia ndani Pelegi, Serugi, Nahori, Tera, na Harani.—Mwanzo 11:17-32.
● Kwenye Mwanzo 11:31, tunasoma kwamba Abrahamu na familia yake walihama kutoka “Uru la Wakaldayo.” Magofu ya jiji hilo yaligunduliwa kusini-mashariki mwa Iraki. Biblia pia inasema kwamba baba ya Abrahamu, Tera, alikufa katika jiji la Harani, ambalo huenda sasa liko nchini Uturuki, na kwamba mke wa Abrahamu, Sara, alifia huko Hebroni, ambalo ni moja kati ya majiji ya zamani zaidi ambayo bado watu wanaishi katika Mashariki ya Kati.—Mwanzo 11:32; 23:2.
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
ORODHA YA MATUKIO YANAYOHUSU UZAO WA ABRAHAMU NA KUTOKA KWA WAISRAELI MISRI
(K.W.K.)
1843 Abrahamu anakufa
Vizazi vinne vya
wazao wa Abrahamu
Lawi
1728 Yakobo anahamisha
familia Misri
1711 Yakobo anakufa Kohathi
1657 Yosefu anakufa Amramu
1593 Musa anazaliwa
1513 Musa anawaongoza
Waisraeli kutoka Misri
1473 Musa anakufa.
Yoshua anawaongoza
Waisraeli kuingia
Kanaani
Kipindi cha Waamuzi
1117 Samweli anatia mafuta
Sauli kuwa mfalme wa kwanza wa Israeli
1107 Daudi anazaliwa
1070 Daudi anakuwa mfalme wa Israeli
1034 Sulemani anaanza kujenga hekalu
Jiwe hili la ushindi lenye maneno “Nyumba ya Daudi,” ni moja kati ya maandishi 17 yanayowataja wafalme waliokuwa wazao wa Abrahamu na waliotawala Israeli au Yuda
[Hisani]
© Israel Museum, Jerusalem/The Bridgeman Art Library International
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

KWANINI DINI YA UISLAM INARUHUSU KUKEKETA "KUTAIRIWA" WANAWAKE?


Ndugu msomaji,Image may contain: one or more people and text
Naanza kwa swali kwa Waislam:
Wapi kwenye Taurat au Zaburi au Injili panasema kuwa Wanawake wakeketwe?
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema, “Itakapogusa [kitakapokutana] kilichotahiriwa kimoja kugusa kilichotahiriwa kingine, basi yapasa kuoga.” [Al-Bukhaariy].
Na amesema tena Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), “Vitakapokutana viwili vilivyotahiriwa, basi ni wajibu kuoga.” [Ibn Maajah 611].
Na vilivyotahiriwa viwili hapo makusudio ni sehemu ya ngozi inayokatwa katika utupu wa mwanamme na ile ya utupu wa mwanamke. Na ni ushahidi kuwa wanawake walikuwa wakitahiriwa. [Rejea Swahiyh Fiqhus Sunnah mj.1, uk.99].
Pia katika kauli nyingine ya Imaam Hanbal ni 'Makrumah' kwa Hadiyth ya Mtume aliposema, “...kata kipande kidogo na wala usimalize”, na Hadiyth “Khitaan ni Sunnah kwa wanaume na Pendezo kwa wanawake.” [Hadiyth hizi tumeeleza juu hukmu zake].
Sahih hadith moja inasema kuwa: Muhammad alikutana na mwanamke aliye kuwa anamkeketa msichana ndogo, Muhammad akamwambia "AONDOE kisimi 'clitoris' (clitorectomy) chote pamoja na sehemu ya 'labia minora', ambacho kinashonwa chote na kubakiza uwazi"
Au kuondosha kisimi 'clitoris' chote, 'labia minora' na sehemu ya kati ya 'labia majora', pamoja na sehemu yote ya kiungo cha mwanamke kushonwa na kubakizwa tundu dogo tu. Na utaratibu huu unahitaji kumfunga miguu mtoto kwa kiasi cha wiki tatu.
Huu ndio UISLAM unao fanya TOHARA kwa WANAWAKE ili kumfuraisha Mwanaume tu. Hakika hii ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu.
Wapi kwenye Taurat au Zaburi au Injili panasema kuwa Wanawake wakeketwe?
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE, KUNAYO MAISHA BAADA YA KIFO?


Je, unaamini kwamba kuna wakati wa hukumu baada ya binadamu kukutwa na mauti?
Ndugu Msomaji,
Nivyema ufahamu nini kitakutokea punde utakapo kata roho/kufa. Swali la muhimu la kujiuliza ni hili hapa:
Je, unauhakika wa wapi utakuwa baada ya kifo?
Biblia inatuambia ya kuwa baada ya mtu kufa, hupelekwa mbinguni ya Muda “Peponi” (Sio Mbingu ambayo Mungu yupo sasa ila ni –Abraham’s bosom) au Jehanamu “kuzimuni ya muda-Akhera” kulingana na hoja ya kuwa alikuwa amemkubali ama kumkataa Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake/wako. Kwa walioamini, kufa ni kuondoka katika mwili na kuenda kukaa na Bwana “to be absent from this body is to be present with the Lord” (Wakorintho wa pili 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa wasioamini, kufa ina maana ya hukumu ya milele Jehanamu (Luka 16:22-23).
Hapa ndipo kwenye utata juu ya ni nini hufanyika baada ya kifo. Kitabu cha Ufunuo Sura 20:11-15 inaeleza juu ya wale walio kuzimu wakitupwa katika ziwa la moto. Ufunuo 21 na 22 inazungumzia juu ya mbingu mpya na dunia mpya. Kwa hivyo ina maana ya kuwa mpaka wakati wa ufufuo wa mwisho, baada ya kufa mtu hubaki katika mahali Fulani kwenye mfano wa mbinguni na kuzimu. Mahali pa mtu anapofaa kukaa milele hapatabadilika ila makazi ya muda yatabadilika “NI KAMA MAHABUSU, HALAFU MTU ANAPELEKWA JELA/ACHIWA”.
Muda Fulani baada ya kufa, waumini watapelekwa katika mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo wa Yohana 21:1) na wasioamini katika ziwa la moto (ufunuo 20:11-15). Haya ndiyo makao ya milele ya watu yanayotegemea kama mtu alimwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu kutokana na dhambi zake.
Wakati sisi hufa, sisi hupatana na hukumu ya Mungu (Waebrania 9:27). Kwa waumini, kuwa mbali na mwili ni kuwa pamoja na Bwana (2 Wakorintho 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa makafiri kifo kinamaanisha adhabu ya milele katika jehanamu (Luka 16:22-23). “Makafiri ni wale walio kataa kuwa Yesu ni Mungu”
Mpaka kufufuka kwa mwisho, hata hivyo, kuna Mbinguni ya muda- Peponi (Luka 23:43, 2 Wakorintho 12:04) na kuzimuni ya muda-ahera (Ufunuo 1:18; 20:13-14). Kama inavyoweza kuonekana wazi katika Luka 16:19-31, katika Peponi wala katika Akhera watu hawalali. inanaweza semekana kuwa, mwili wa mtu "unalala" huku nafsi yake ikiwa peponi au kuzimuni. Wakati wa ufufuo, mwili huu "utaamshwa" na kubadilishwa hadi mwili wa milele mtu atamiliki milele, hata kama ni mbinguni au kuzimu. Wale ambao walikuwa katika peponi watapelekwa mbingu mpya na nchi mpya (Ufunuo 21:1). Wale ambao walikuwa katika kuzimu kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:11-15). Hizi ndizo hatima za mwisho na milele ya watu wote ikitegemea ikiwa mtu aliamini katika Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu au la.
Zaidi ya hapo, Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).
YOHANA 14:1-3"Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo , ningaliwaambia ; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali , nitakuja tena nitawakaribishe kwangu ; ili nilipo mimi, nanyi mwepo"
Je kuna haja ya kuogopa kifo?
“Yesu akamwambia, mimi ndiye huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je Unayasadiki hayo?” – John 11:25-26
Je, unaamini kwamba kuna maisha baada ya kifo?
Je, unaamini kwamba kuna wakati wa hukumu baada ya binadamu kukutwa na mauti?
Ikiwa ndivyo, hii ina maanisha kwamba binadamu anaishi baada ya kuondokana na mazingira ya duniani?
Je, anaishije huko?
Anakula, anakunywa, anatembea, anaongea au anasikia?
Vipi ana mwili wa nyama au roho?
Kama roho basi, ataunguaje motoni siku ya hukumu?
Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele?
YESU NDIO NJIA PEKEE YA UZIMA WA MILELE:
Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya Mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).
Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii Mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36).
BAADA YA KUFA HAKUNA NAFASI YA PILI YA KUTUBU:
Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu Msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya Kristo.
JEHANNAM:
Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na Ziwa la Moto, liwakalo na kiberiti ambapo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (Mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.
Je unaamini kuwa kunayo maisha baada ya kifo?
Ni nini hufanyika baada ya kufa?
Je! Unaamini kuwa Jahannamu ni kitu cha kweli? Jehannamu ni ya milele?
Je, kuna ngazi mbalimbali za mbinguni?
Je, kuna viwango tofauti vya adhabu jehanamu?
Basi ungani nami katika kijarida kijacho kuhusu Maisha ya Milele.
Mungu awabariki sana,
Dr. Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
For Max Shimba Ministries Org.

UTATA MKUBWA KUHUSU UTUME WA MUHAMMAD

Image may contain: 1 person, text
Ndugu msomaji,
Katika Biblia shetani ametajwa kuwa anaweza kujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
2 Wakorintho 11:13-15 “Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu, maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakajigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao”.
Muhammad akiwa Medina aliulizwa na Wayahudi ikiwa ufunuo wake umetoka kwa Mungu wa Kweli kwa kumtaka atoe sifa za manabii. Akijibu swali hilo alisema:
Mkweli Mwaminifu Juzuu 3-4 Uk.63. Hadithi Na. 880. “Kasema Mtume (s.a.w):- (Mambo) manne ya sheria za mitume (Kuwa na) na haya,na kujipaka mafuta mazuri,na kuowa (wake), na kupiga mswaki.
Hizi si sifa za Ki-Mungu kwa nabii na mtume bali ni za kibinadamu tu.
Manabii na watu mbalimbali katika Biblia hawakuona haya. Soma Isaya 50:7 “ Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimeukaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya”.
Zaburi 34:5 “ Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya”
Zab 119:46 “ Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu”
Warumi 1:16 “ Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye kwa Myahudi kwanza , na kwa Myunani pia” 1Petro 4:16 “ Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Zaidi ya hayo tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu kuathirika na nguvu za giza yaani uchawi.. Je nabii au mtume wa Mwenyezi Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Katika Qur’an Suratul Ban-Israel, 17:47 “ Tunajua sana, sababu wanayosikiliza, na wanaponong’ona, wanaposema hao madhalimu. Nyinyi hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa”
Pia katika Suratul Falaq, 113:1-5 “ Ninajikinga kwa mola wa ulimwengu wote na shari ya Alivyoviumba, na shari ya giza la usiku liingiapo, na shari ya wale wanaopulizia (vivia) mafundoni (wakavunja) mashikamano yaliyo baina ya watu yaani shari ya mafatani, Na shari ya hasidi anapohusudu”
Tunasoma tukio hilo katika ufafanuzi wake uliyomo ndani ya Qur’an chapa ya nane uk.977 unaofafanua Sura ya 113-114 “Athari ya uchawi juu ya mtume (s.a.w). Swali la pili lijitokezalo kuhusu sura mbili hizi ni kwamba kwa mujibu wa hadithi uchawi ulifanywa dhidi ya mtume (s.a.w) naye akawa mgonjwa, na ili kuiondoa athari hiyo ya uchawi Jibril (a.s) alikuja na kumpa maelekezo Mtume (s.a.w) ya kusoma sura mbili hizi. Watafiti wengi zamani na wa sasa wamelifanyia upinzani jambo hilo, kwamba ikiwa hadithi zitakubaliwa, basi mfumo wote wa sharia utakuwa ni wa kutiliwa shaka, kwa sababu kama mtume (s.a.w) aliweza kuathirika kwa uchawi, na kwa mujibu wa hadithi hizi kweli uchawi huo ulionesha athari yake, basi hatuwezi kukaidi au kukana hadi kiwango gani maadui waliweza kumfanya Mtume (s.a.w) aseme na atende mambo kwa nguvu ya uchawi, na katika mafundisho yake mambo mangapi yatoka kwa Allah na mangapi yatokana na athari ya uchawi juu yake.
Si hiyo tu, bali pia wasema kuwa baada ya kuyatambua hayo kuwa ni kweli katu haitawezekana hata kule kukaidi kuwa (s.a.w) alishawishiwa kudai utume kwa mauzauza ya kinjozi kuwa alimjia malaika. Pia wanasema hadithi hizi zapingana na Qur’an, na kama ilivyo katika Qur’an kuwa tuhuma hiyo batili kwa makafiri ilivyotajwa kuwa mtume s.a.w amerogwa naye ameathirika na uchawi: wanaposema hao madhalimu, ‘Ninyi hamumfuati isipokuwa mtu aliyerogwa’.” (17:47), lakini hadithi hizi zinathibitisha madai ya makafiri kuwa kwa kweli aliathirika na kuongozwa na uchawi……Kadri historia inavyohusika,ukweli kuwa kiasi fulani cha athari ya uchawi juu ya Mtume (s.a.w) ni hakika iliyothibiti; na kama kwa ustadi wa ubishi inawezekana kuthibitisha kuwa kweli.
Limesimuliwa jambo hilo na Bukhari, Muslim, Nasai, Ibn Majah, Ahmad, ‘Abdur Razzaq, Humaid, Baihaqi, Tabarani, Ibn Sa’d, Ibn Marduyah, Ibn Abi Shaibah, Hakim, Abd bin Humaid na Muhadithina wengine toka kwa Bi. ‘Aisha (r.a), Zaid bin Arqam, Ibn ‘Abbas kupitia silsila nyingi mno kiasi kwamba jambo lenyewe limefikia hali ya ufululizo kamili, isipokuwa kila Hadithi, yenyewe ni ripoti kamili.
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata. Ikiwa na wao Waislamu kwa mujibu wa hadithi hizi hawajui ni mambo mangapi Muhammad aliyoyasema yanatoka kwa Allah na mangapi aliyasema akiwa ameshinikizwa na wachawi , Je ufunuo na utume wake utakuwa umetoka kwa Mungu wa Kweli? Tafakari !!
Ndani ya Biblia Takatifu hakuma kurogwa kwa mtu wa Mungu. Hesabu 23:23 “ Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israel. Sasa habari za Yakobo na Israel zitasemwa , Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!”
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia Takatifu, manabii na mitume wa kweli wa Bwana Mungu wanatoka katika taifa la Israel.
Kitabu cha Ezekiel 13:9 “ Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na kutabiri uongo;hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika maandiko ya nyumba ya Israel, wala hawataingia katika nchi ya Israel; Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU” .
Pia kwa mujibu wa kitabu cha Qur’an manabii na mitume ni lazima watoke kwa Yakobo ambaye ni mtoto wa Is-haqa ambaye naye ni mtoto wa Ibrahim. Qur’an Suratul Al-Ankabuut, (Buibui), 29:27 “ Na tulimpa (kumzaa nabii) Is-haqa na (kumjukuu nabii) Yakubu na tukauweka katika kizazi chake unabii na (kupata) kitabu, na tukampa ujira wake katika dunia; naye katika akhera kwa yakini atakuwa miongoni mwa watu wema”.
Aya hii, inaendelea kusisitiza kuwa ni kupitia kizazi cha Yakobo ndiko uliko unabii na kupata kitabu. Kwa bahati mbaya Muhammad ibn Abdullah, hatoki katika kizazi hicho wala kwa Ishmael kama wanavyodai Waislamu . Kwa sababu Ishmael ni Mwebrania kama baba yake mzee Ibrahim alivyo Mwebrania (Mwanzo 14:13) na Muhammad ni mwarabu kutoka kabila la Maqureysh. Kwa kutambua hilo ndipo tunamwoma Muhammad akiwaonya watu wengine wajiepushe na watu wa kabila lake.
Sahih Al-Bukhari Vol.1.Hadithi Na. 801 na Al-Lu’lu Kitabu cha 3. Uk.1089.Hadithi Na.1846 inasomeka“Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema ,“Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, Kabila hili la Makuraish litawateketeza watu.’ Wakauliza, ‘Unatushauri nini?’ Akasema, Nashauri watu wajitenge nalo.”
Kumzamisha nzi kwenye kinywaji
Bukhar vol. 4 Hadith 537 “ Narrated Abu Huraira: The Prophet said: If a house fly falls in the drink of any one of you, he should dip it (in the drink) for one of its wings has a disease and the other has the cure for the disease”
Tafsiri: Ilisimuliwa na Abu Huraira: Nabii alisema kama nzi akiangukia ndani ya kinywaji cha mmoja wenu, anapaswa kumzamisha kabisa (ndani ya kinywaji) kwa kuwa bawa lake moja lina ugonjwa na bawa lake jingine lina dawa
Mitume wa Yesu ndani ya Biblia Takatifu walikwisha kutuonya kuhusu uchafu huo. Katika 2 Kor 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org.

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 6

Image may contain: 3 people, text
JE, NINI MAANA NA FAIDA YA KUNENA KWA NDIMI?
Tuanze kwa kusoma Biblia:
“Hata ilipotimia Siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine [zingine – KJV], kama Roho alivyowajalia kutamka.
Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja ALIWASIKIA WAKISEMA KWA LUGHA YAKE MWENYEWE. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi SISI KUSIKIA KILA MTU LUGHA YETU TULIYOZALIWA NAYO? Waparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia [Libya] karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na Waongofu, Wakrete na Waarabu; TUNAWASIKIA HAWA WAKISEMA KWA LUGHE ZETU matendo makuu ya Mungu.” Matendo 2:1-
11.
Siku ya Pentekoste, mitume walizungumza kwa lugha. Matendo sura ya 2 inaweka wazi kwamba mitume walikuwa wakisema kwa lugha ya binadamu (Matendo 2:6-8). Neno lilotafsiriwa "lugha" katika zote Matendo sura ya 2 na 1 Wakorintho sura ya 14 ni glossa/ndimi ambalo lina maana ya "lugha."
Kuzungumza katika lugha ilikuwa ni uwezo wa kuongea katika lugha ambayo msemaji haijui, ili kutangaza injili kwa mtu ambaye anazungumza lugha hiyo. Katika eneo la kitamaduni la Korintho, inaonekana kwamba Karama ya lugha ilikuwa ya thamani na maarufu. Waumini Wakorintho walikuwa na uwezo bora wa kuwasilisha injili ya Neno la Mungu kama matokeo ya karama ya lugha. Hata hivyo, Paulo aliiweka wazi kwamba hata katika matumizi ya hii lugha, ilikuwa ya kutafsiriwa au "imetafsiriwa" (1 Wakorintho 14:13, 27). Muumini Mkorintho atanena kwa lugha ngeni, kutangaza ukweli wa Mungu kwa mtu ambaye alizungumza lugha hiyo, na pia huyo muumini, au muumini mwingine katika kanisa, alikuwa atafsiri yale aliyosemwa ili mkutano wote uweza kuelewa kile ambacho alisema.
KUNENA KWA LUGHA NI USHAHIDI WA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU:
Kuna matukio matatu katika kitabu cha Matendo ya Mitume ambapo kunena katika lugha kunafuatana na kupokea Roho Mtakatifu- Matendo 2:4, 10:44-46, na 19:06. Hata hivyo, hafla hizi tatu ndio sehemu pekee katika Biblia ambapo kunena kwa lugha ni ushahidi wa kupokea Roho Mtakatifu. Katika kitabu cha Matendo, maelfu ya watu wanamwamini Yesu na hakuna mahali kumesungumziwa kuhusu kunena kwa lugha (Matendo 2:41, 8:5-25, 16:31-34, 21:20). Katika Agano Jipya inafundishwa kwamba kunena kwa lugha ni ushahidi tu mtu imepokea Roho Mtakatifu. Kwa kweli, Agano Jipya hufundisha kinyume. Tunaambiwa kwamba kila muumini katika Kristo ana Roho Mtakatifu (Warumi 8:9, 1 Wakorintho 12:13; Waefeso 1:13-14 ), lakini si kila muumini hunena lugha ngeni (1 Wakorintho 12:29-31).
Hivyo, kwa nini kuzungumza katika lugha kulikuwa ushahidi wa Roho Mtakatifu katika hivyo vifungu vitatu katika Matendo? Matendo 2 yanakili mitume wanabatizwa kwa Roho Mtakatifu na kuwezeshwa na Yeye kwa kutangaza habari njema. Mitume kuliwezeshwa kusema kwa lugha nyingine (lugha ) ili waweze kushiriki kweli na watu katika lugha yao wenyewe. Matendo 10 imerekodi Mtume Petro kupelekwa kushiriki injili na watu wasio Wayahudi.
Matendo 10:44-47 inaeleza hiya: "Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
FAIDA YA KUNENA KWA LUGHA:
Kunena na au kuomba kwa lugha mpya kuna faida sana katika maisha yako. Shetani anajua umuhimu na nguvu ya maombi kupitia ndimi/lugha. NI rahisi sana kwa Shetani kukutibua ukiwa unaomba kwa akili, lakini Shetani hana ujanja wa kukutibua ukiwa unaomba kwa roho nikimaanisha kwa lugha/ndimi. Mtume Paulo katika Wakirontho alisema, "Nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia....." (1 Wakorintho 14:14,15).
Hivyo basi, mtu akiomba kwa roho yaani kwa lugha, ni Roho Mtakatifu anayetoa hiyo lugha (Anaye kuongoza katika Maombi), hivyo ni Roho Mtakatifu atakayekusaidia ni jambo gani kuombea sawasawa na uhitaji wako. Zaidi ya hapo, Roho Mtakatifu atakusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu juu ya jambo hilo. (Warumi 8:26, 27).
Kuomba kwa akili (sio kwa lugha) kunachosha mapema na huwa kuna kurudiarudia maneno, mwishowe inakuwa upayukaji tu ili uombe muda mrefu, lakini mtu anapoomba kwa lugha panakuwa na uwezesho wa ajabu wa kudumu katika maombi kwa muda mrefu bila kuchoka, maana si akili inayoomba bali ni roho ya mtu, na roho haijui uchovu wa mwili, (Yesu alisema roho i radhi lakini mwili huu dhaifu, akawauliza yaani mmeshindwa kuomba hata kwa lisaa limoja?) Unaona tatizo la kuomba kwa ktumia akili?
JE, LUGHA ZILIZONENWA ZILIJULIKANA AU HAZIKUJULIKANA?
Lugha iliyotumika kuelezea Matendo 2:4 inasema kwamba wale walioipokea karama ile ya lugha walisema “kwa lugha nyingine [zingine – KJV],” yaani, walisema kwa lugha zaidi ya zile walizozitumia kwa kawaida kama lugha zao za kuzaliwa nazo.
Wakati ule wa Pentekoste walikuwapo “Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.” Fungu la 5. Wayahudi wale walikuwa wametawanyika miongoni mwa mataifa kwa kipindi kirefu sana, na wengi wao hawakuweza kusema tena Kiebrania au Kiaramu. Karama ile ya lugha iliwawezesha kutoa hotuba na ushuhuda kuhusu “matendo makuu ya Mungu” (fungu la 11) aliyotenda kwa njia ya Yesu wa Nazareti, kiasi kwamba Wayahudi wale waliokuwa si wa nchi ile ya Palestina, yaani, wahujaji wale waliokuja katika Mji ule Mtakatifu wa Yerusalemu, waliweza kuelewa yote yaliyosemwa katika lugha za mahali kwao walikotoka.
Ni dhahiri kwamba lugha zilizonenwa pale ni zile tu zilizojulikana na watu. Wasikilizaji wale walishangaa sana “kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.” Matendo 2:6.
“Kila lugha inayojulikana ilikuwa imewakilishwa na wale waliokusanyika pale. Lugha zile mbalimbali zingekuwa kipingamizi kikubwa kwa utangazaji wa injili ile; kwa hiyo Mungu kwa njia ya mwujiza aliujazia upungufu waliokuwa nao wale mitume. Roho Mtakatifu aliwafanyia kile ambacho wasingeweza kukipata katika maisha yao yote. Kuanzia sasa [wakati ule] wangeweza kuzitangaza mbali kweli zile za injili, wakisema kwa usahihi lugha za wale waliokuwa anawahudumia.”
Kuomba katika lugha si kitu ambacho huamua wokovu wako, la hasha. Zaidi ya hapo, Kuomba katika lugha si kitu kiinamtofautisha Mkristo kukomaa kutoka kwa Mkristo machanga. Kwahiyo, usijisikie vibaya kama bado haujaanza kunena kwa lugha.
USIKOSE SEHEMU YA SABA: Matunda ya Roho Mtakatifu ni gani?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UNABII NI NINI?


Image may contain: text
JE, UNAJUA MAANA YA UNABII NA JINSI UNAVYOPATIKANA?
Unabii ni ujumbe ulioongozwa na Roho ya Mungu, ufunuo kutoka kwa Mungu. Biblia inasema kwamba manabii “walisema yaliyotoka kwa Mungu kama walivyoongozwa na Roho Mtakatifu.” (2 Petro 1:20, 21) Kwa hiyo, nabii ni mtu anayepokea ujumbe kutoka kwa Mungu na kuwapitishia wengine ujumbe huo.— Matendo 3:18.
JE, MANABII WALIPATE UJUMBE KUTOKA KWA MUNGU?
Mungu alitumia njia kadhaa kuwapitishia manabii wake mawazo yake:
KWA KUTUMIA MAANDISHI:
Mungu alitumia njia hii angalau pindi moja alipompa Musa zile Amri Kumi zikiwa zimeandikwa.—Kutoka 31:18.
KUPITIA MALAIKA WAKE:
Kwa mfano, Mungu alitumia malaika kumletea Musa ujumbe ambao alipaswa kumpelekea Farao wa Misri. (Kutoka 3:2-4, 10) Wakati ambapo maneno hususa yalikuwa muhimu, Mungu aliwaongoza malaika wamwambie mtu maneno hususa ya kuandika, kama alivyofanya alipomwambia Musa hivi:
“Jiandikie maneno haya, kwa sababu ninafanya agano pamoja nawe na Israeli kupatana na maneno haya.”—Kutoka 34:27. *
KUPITIA MAONO:
Nyakati nyingine nabii alipokea maono alipokuwa macho na akiwa anafahamu kabisa kinachoendelea. (Isaya 1:1; Habakuki 1:1) Maono mengine yalikuwa halisi kabisa hivi kwamba wahusika waliyashiriki. (Luka 9:28-36; Ufunuo 1:10-17) Pindi nyingine, maono yalipitishwa mhusika akiwa katika njozi. (Matendo 10:10, 11; 22:17-21) Pia Mungu aliwasilisha ujumbe wake katika ndoto wakati ambapo nabii alikuwa amelala.—Danieli 7:1; Matendo 16:9, 10.
KUPITIA AKILI-KUIONGOZA AKILI:
Mungu aliongoza mawazo ya manabii wake ili kupitisha ujumbe wake. Hiyo ndiyo maana inayotolewa na maneno haya ya Biblia: “Andiko lote limeongozwa na roho ya Mungu.” Maneno hayo yanayosema “limeongozwa na roho ya Mungu” yanaweza pia kutafsiriwa “lenye pumzi ya Mungu.” (2 Timotheo 3:16; Union Version) Mungu alitumia roho yake takatifu, au kani ya utendaji, kuingiza mawazo yake katika akili za watumishi wake. Ujumbe ulikuwa wa Mungu, lakini manabii ndio waliochagua namna ya kuyapanga maneno.—2 Samweli 23:1, 2.
Je, nyakati zote unabii unahusisha kutabiri wakati ujao?
Hapana, unabii wa Biblia hautabiri tu kuhusu mambo ya wakati ujao. Hata hivyo, ujumbe mwingi kutoka kwa Mungu unahusiana na wakati ujao, hata ikiwa si moja kwa moja. Kwa mfano, manabii wa Mungu waliwaonya Waisraeli wa kale kuhusu njia zao mbaya. Maonyo hayo yalifafanua baraka za wakati ujao ikiwa watu wangetii, na pia yalitaja madhara ambayo wangepata kwa kutotii. (Yeremia 25:4-6) Matokeo yalitegemea njia ambayo Waisraeli waliamua kufuata.—Kumbukumbu la Torati 30:19, 20.
Mifano ya unabii wa Biblia usiohusisha utabiri
Pindi moja Waisraeli walipomwomba Mungu msaada, alituma nabii kueleza kwamba kwa kuwa walikataa kutii amri za Mungu, basi Mungu alikataa kuwasaidia.—Waamuzi 6:6-10.
Wakati ambapo Yesu alizungumza na mwanamke Msamaria, alifunua mambo kuhusu maisha yake ya zamani ambayo hangeweza kuyajua bila kufunuliwa na Mungu. Mwanamke huyo alitambua kwamba Yesu alikuwa nabii hata ingawa hakuwa ametabiri kuhusu wakati ujao.—Yohana 4:17-19.
Wakati wa kesi ya Yesu, maadui wake walimfunika uso, wakampiga, kisha wakamwambia: “Toa unabii. Ni nani aliyekupiga?” Hawakuwa wakimwambia Yesu atabiri wakati ujao bali kwa msaada wa Mungu aseme ni nani aliyempiga.—Luka 22:63, 64.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Tuesday, May 9, 2017

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 3

Image may contain: cloud, sky, bird and text
ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA.
Kila Mkristo au mtu aliyeokoka, hana budi kuwa na lengo la kufikia kimo na cheo cha utimilifu wa Kristo katika tabia na Utumishi wa Mungu (Waefeso 4:11-15 ). Kufikia kiwango cha Yesu Kristo katika tabia ni jambo linalowezekana, Kama siyo, tusingetakiwa kuwa wakamilifu na watakatifu kama Baba wa mbinguni alivyo Mtakatifu (Mathayo 5:48;1`Petro 1:15-16) Neno la Mungu pia, linatufundisha uwezekano wa kuwa na viwango vya utumishi vya Yesu alipokuwa duniani, na hata kuzidi (Yohana 14:12).
Hata hivyo haya yote hayawezekani kama sisi siyo waombaji kama Yesu alikuwa mwombaji namba moja. Alifanya maombi alfajiri na mapema (Marko 1:35). Alijitenga na shughuli mchana na kufanya maombi (Luka 5:15-16) Aliomba jioni (Mathayo 14:23) Wakati mwingine alifanya maombi usiku kucha (Luka 6:12).
Je,sisi tunaweza kuwa waombaji kiasi hiki? Kwa nguvu na jitihada zetu hatuwezi.
Tunaweza tu, tukisaidiwa na Roho Mtakatifu. Ndiyo maana tunajifunza somo hili muhimu leo katika mfululizo wa masomo haya ya Roho Mtakatifu, na kichwa cha somo la sasa ni
 ”ROHO MTAKATIFU, ATUSAIDIAYE KUOMBA”, NA TUTAJIFUNZA SOMO HILI KATIKA VIPENGERE VINNE:-
A. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
B. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
C. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
D. ROHO MTAKATIFU,MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
A. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
Shetani ndiye adui yetu mkuu. Kazi yake ni kuiba chochote kizuri cha kiroho tulicho nacho, na tena kuchinja au kuua na kuharibu yote mema kwetu kiroho na kimwili.Tukiwa peke yetu, kamwe hatuwezi kupambana na shetani na kumshinda. Hatuna budi kuwa na Mungu katika maisha yetu ili tumshinde ibilisi. Daudi alimshinda Goliathi kwa Jina la Bwana.
Hakumshinda kwa nguvu zake. Kwa maana nyingine hatuwezi kuzaa matunda yoyote mema ya kiroho kama hatuko ndani ya Yesu. Usalama wetu na ushindi wetu wa kiroho, unategemeana sana na sisis kukaa ndani yake Yesu, yaani sisi kuwa na uhusiano au ushirika na Kristo. Pasipo yeye, sisi hatuwezi kufanya neno lolote. (Yohana 15:4-5). Kukaa ndani ya Yesu, kunafananishwa na tawi lililounganishwa na shina.
Kuunganishwa huko ndiyo uhai wa tawi.
Tawi likijitenga na shina, linanyauka na kufa. Sasa basi, tunaunganisha na Mungu na Mungu tunapokuwa tunawasiliana naye katika maombi. Tukiwa hatuna maisha ya maombi, kimsingi ni kwamba tunakuwa ni tawi lililojenga na shina, na hivyo tunanyauka na hatimaye kufa kiroho. Hatuwezi kuwa na kitu tusipoomba (Yakobo 4:2)
Tutaingia majaribuni tusipoomba (Mathayo 26:41).
Tutapepetwa kama ngano na ibilisi na mazuri yote ya kiroho yataondoshwa, na imani yetu itatoweka (Luka 22:31-32).
Shetani atatumeza na kuturudisha katika ufalme wake (1Petro 5:8).
Hatuwezi kuwaleta watu kwa Yesu, tusipokuwa waombaji, maana Shetani hatawaachia (Zaburi 2:8).
Hatuwezi kuona watu wakifunguliwa katika vifungo vya shetani vya kimwili (Luka 13:16) na vile vinavyotokana na mambo ya rohoni (Matendo 12:5-17). Kwa ufupi tutachukuliwa na mafuriko ya Shetani (Zaburi 32:6).
B. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
Maandiko yanatufahamisha kwamba makao ya Mungu mbinguni, ni Mahali palipoinuka, na Mlimani kwenye kiti cha enzi cha Mungu (Isaya 57:15; Kutoka 24:12-13 ; Ufunuo 7:9-10). Ingawa Mungu wetu yuko mlimani, maandiko yanasema tukimwomba, yeye husikia huko mbinguni na kutujibu maombi yetu kwa kuyatenda tunayoyataka (1Wafalme 8:32; Zaburi 76:8;1 02:19).
Hata hivyo, hatuna budi kufahamu pia kwamba katika mazingira fulani Mungu hushuka kutoka mlimani na kuja duniani katika hali isiyo ya kawaida. Mungu anaposhuka kwa jinsi hii, hutenda mambo ya kutisha, na ya kushangaza, yasiyo ya kawaida na hivyo kuwavuta wengi mno kwake (Waamuzi 4:12-16,5:13; Isaya 31:4; Hesabu 11:23-25,31-32).
Uamsho hutokea Mungu anaposhuka, na watu wagumu wa mioyo huvutwa kwa Yesu, walio vuguvugu huwa moto, mambo mengine makubwa ya kuitikisa jamii kama mamia ya wenye ukimwi kupona kwa mpigo, hutokea, Mungu akishuka.
Hata hivyo kushuka kwa Mungu hutokea baada ya maombi ya kuugua na kulia kwa uchungu mkubwa (Kutoka 2:23-24;3:7-8;
Matendo 7:32-34). Wakati wote Yesu Kristo alimfanya Mungu kushuka katika huduma yake kwa kuwa aliomba kwa kulia sana
na machozi (Waebrania 5:7), na wengine walimuombolezea kwa kilio na uchungu mkubwa (Luka 23:27).
Kulia kwa kuugua katika maombi hushusha majibu ya maombi namna ya kipekee (2Nyakati 34:27; Zaburi 34:17;39:12;51:1-2,17;72:12;12;88:1-2; Isaya 58:9; Yeremia 31:9; Luka 18:7).
Sasa basi ni rahisi kuomba maombi kwa kulia na kuugua?
Jibu ni la ,bila msaada wa Roho Mtakatifu, itakuwa kama tunaigiza tu.
C. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU.
Tunajifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na maombi kwa kuyaangalia maisha ya maombi ya Yesu, na mafundisho yake kuhusu maombi:-
§ Yesu Kristo alikuwa na wakati wa kuomba pamoja na wanafunzi wake (Luka 9:18), Lakini pia alikuwa na muda mrefu wa maombi ya peke yake (Luka 5:16; Marko 6:45-46). Ni muhimu kujiunga na kikosi cha maombi cha Kanisa na kushiriki maombi ya pamoja na wengine, lakini ni lazima kila mmoja kuwa na muda wa kuomba mwenyewe.
§ Yesu hakukubali kuchukuliwa na huduma za kushauri watu, kuwaombea watu n.k na kuziruhusu zimkoseshe kuomba.
Alijua bila maombi, huduma hizo zitakuwa hazina nguvu. Aliziacha huduma, akafanya maombi (Luka 5:15-16). Kabla ya kuzungumza na watu, alizungumza na Mungu KWANZA. Alifanya maombi ya alfajiri na mapema sana na baadaye alipokutana na watu ilikuwa rahisi mno kwake kuponya ukoma na kutoa pepo. (Marko 1:35-42).
§ Kabla ya Yesu kutembea juu ya maji, na kukomesha upepo, alikuwa na kipindi kirefu cha maombi (Marko 6:46-51). Vipindi virefu vya maombi vinaweza kutupa uwezo wa kuona yasiyowezekana yakiwezekana!
§ Utukufu wa Yesu ulitokana na maombi! (Luka 9:28-29) Hatuna utukufu wa Mungu kwa kuwa siyo waombaji! Mwombaji, utukufu wake humwogopesha shetani
§ Alipokuwa na huzuni aliomba hakunung'unika tu na kulalamika, na ghafla alipata ujasiri wa kukabili lolote lile (Mathayo 26:36-39; 47-49). Hatuna ujasiri na tumejaa woga kwa kuwa hatuombi
§ Maombi yake yalikuwa ni vita hasa. Alipokuwa akiomba, alitoka jasho (hari) kama matone ya damu (Luka 22:44).
Maombi ni mapambano dhidi ya shetani anayezuia majibu yetu (Danieli 10:12-13). Ni lazima iwe ni vita. Mwili ni lazima tuushughulishe kama wapiganaji hasa, tukiwa katika roho Maombi yenye matokeo makubwa, ni yale ya kutoka jasho! Ni lazima tumkabili shetani katika vita ya maombi kabla hata hajatushambulia.Katika vita ya siku sita kati ya waisraeli na wamisri, miaka kadha iliyopita; Waisraeli walishinda Wamisri ingawa walikuwa na ndege nyingi zaidi za kivita kuliko wao,kwa kuwa walizipiga KABLA hazijaondoka katika vituo vyao.
Tusingoje matatizo ndio tuombe!
§ Imani yetu na ya ndugu zetu,inaweza kutokutindika,ikiwa tu tutakuwa waombaji;kinyume cha hapo ni rahisi kumezwa na
shetani (Luka 22:31-32;1Petro 5:8-9)
§ Maombi ndiyo yanafanya tuutunze utakatifu wetu,na kuwa mbali na dunia. Bila maombi ni rahisi kuvutwa na masumbufu
ya dunia (Luka 21:34-36).
§ Yesu aliliombea Kanisa (Yohana 17:14-15). Ni muhimu kuliombea kanisa na siyo kujiombea wenyewe tu wakati wote.
Je tunaweza kuyatendea kazi yote haya kwa nguvu zetu? Jibu ni la kwa nguvu zetu hatuwezi ,bila msaada wa Roho Mtakatifu.
D. ROHO MTAKATIFU MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
Shetani anafahamu sana umuhimu wa maombi, na hivyo atatuzuia sana kufanya maombi kuliko yote mengine, ili tubaki kama matawi ambayo hayajaunganishwa na shina. Anajua pasipo Mungu, sisi hatuwezi neon lolote. Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi. Tunaweza kuomba sisi hatuwezi neno lolote. Kwa kujifunza tu juu ya maombi, bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi. Tunaweza kuomba siku mbili, tatu, halafu basi. Pamoja na wanafunzi wa Yesu kuhimizwa kuomba na Yesu mwenyewe, bado walishindwa kuwa waombaji (Mathayo 26:37-43).
Ndipo hatimaye akawaambia atakuja Msaidizi ambaye kazi yake mojawapo, ni kutusaidia kuomba (Yohana 16:7; Warumi 8:26-28). Yeye Roho, kwa kuwa hutuombea kwa kuugua, na tena ni Roho ya neema na kuomba, huweza kutupa msaada wa kutuwezesha kuomba kwa kuugua na kulia (Zakaria 12:10) Baada ya Roho Mtakatifu kuja na kuwasaidia wanafunzi wa
Yesu, maisha yao ya maombi yalibadilika (Matendo 10:9). Siri ni hii, usitumie nguvu zako kuomba. Kabla ya kuingia katika maombi, mwombe Msaidizi akusaidie kuomba.
Shalom
USIKOSE SEHEMU YA NNE SOMO 4: UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

YESU NI MUNGU. UTHIBITISHO WA AYA TU.

Image may contain: text
1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Ufunuo 1:8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
Wakolosai 1:16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 20:28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!
Wafilipi 2:6-7 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Ufunuo 22:13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ufunuo 21:6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. 7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
Leo nimetoa aya tu. Sasa nakuomba uzisome na utafakari.
Barikiwa sa na Yesu aliye hai.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds

  BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds. The targets included a Radwan Force training facility used for weapons drills ...

TRENDING NOW