Saturday, May 13, 2017

JE, KUNAYO MAISHA BAADA YA KIFO?


Je, unaamini kwamba kuna wakati wa hukumu baada ya binadamu kukutwa na mauti?
Ndugu Msomaji,
Nivyema ufahamu nini kitakutokea punde utakapo kata roho/kufa. Swali la muhimu la kujiuliza ni hili hapa:
Je, unauhakika wa wapi utakuwa baada ya kifo?
Biblia inatuambia ya kuwa baada ya mtu kufa, hupelekwa mbinguni ya Muda “Peponi” (Sio Mbingu ambayo Mungu yupo sasa ila ni –Abraham’s bosom) au Jehanamu “kuzimuni ya muda-Akhera” kulingana na hoja ya kuwa alikuwa amemkubali ama kumkataa Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake/wako. Kwa walioamini, kufa ni kuondoka katika mwili na kuenda kukaa na Bwana “to be absent from this body is to be present with the Lord” (Wakorintho wa pili 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa wasioamini, kufa ina maana ya hukumu ya milele Jehanamu (Luka 16:22-23).
Hapa ndipo kwenye utata juu ya ni nini hufanyika baada ya kifo. Kitabu cha Ufunuo Sura 20:11-15 inaeleza juu ya wale walio kuzimu wakitupwa katika ziwa la moto. Ufunuo 21 na 22 inazungumzia juu ya mbingu mpya na dunia mpya. Kwa hivyo ina maana ya kuwa mpaka wakati wa ufufuo wa mwisho, baada ya kufa mtu hubaki katika mahali Fulani kwenye mfano wa mbinguni na kuzimu. Mahali pa mtu anapofaa kukaa milele hapatabadilika ila makazi ya muda yatabadilika “NI KAMA MAHABUSU, HALAFU MTU ANAPELEKWA JELA/ACHIWA”.
Muda Fulani baada ya kufa, waumini watapelekwa katika mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo wa Yohana 21:1) na wasioamini katika ziwa la moto (ufunuo 20:11-15). Haya ndiyo makao ya milele ya watu yanayotegemea kama mtu alimwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu kutokana na dhambi zake.
Wakati sisi hufa, sisi hupatana na hukumu ya Mungu (Waebrania 9:27). Kwa waumini, kuwa mbali na mwili ni kuwa pamoja na Bwana (2 Wakorintho 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa makafiri kifo kinamaanisha adhabu ya milele katika jehanamu (Luka 16:22-23). “Makafiri ni wale walio kataa kuwa Yesu ni Mungu”
Mpaka kufufuka kwa mwisho, hata hivyo, kuna Mbinguni ya muda- Peponi (Luka 23:43, 2 Wakorintho 12:04) na kuzimuni ya muda-ahera (Ufunuo 1:18; 20:13-14). Kama inavyoweza kuonekana wazi katika Luka 16:19-31, katika Peponi wala katika Akhera watu hawalali. inanaweza semekana kuwa, mwili wa mtu "unalala" huku nafsi yake ikiwa peponi au kuzimuni. Wakati wa ufufuo, mwili huu "utaamshwa" na kubadilishwa hadi mwili wa milele mtu atamiliki milele, hata kama ni mbinguni au kuzimu. Wale ambao walikuwa katika peponi watapelekwa mbingu mpya na nchi mpya (Ufunuo 21:1). Wale ambao walikuwa katika kuzimu kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:11-15). Hizi ndizo hatima za mwisho na milele ya watu wote ikitegemea ikiwa mtu aliamini katika Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu au la.
Zaidi ya hapo, Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).
YOHANA 14:1-3"Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo , ningaliwaambia ; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali , nitakuja tena nitawakaribishe kwangu ; ili nilipo mimi, nanyi mwepo"
Je kuna haja ya kuogopa kifo?
“Yesu akamwambia, mimi ndiye huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je Unayasadiki hayo?” – John 11:25-26
Je, unaamini kwamba kuna maisha baada ya kifo?
Je, unaamini kwamba kuna wakati wa hukumu baada ya binadamu kukutwa na mauti?
Ikiwa ndivyo, hii ina maanisha kwamba binadamu anaishi baada ya kuondokana na mazingira ya duniani?
Je, anaishije huko?
Anakula, anakunywa, anatembea, anaongea au anasikia?
Vipi ana mwili wa nyama au roho?
Kama roho basi, ataunguaje motoni siku ya hukumu?
Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele?
YESU NDIO NJIA PEKEE YA UZIMA WA MILELE:
Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya Mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).
Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii Mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36).
BAADA YA KUFA HAKUNA NAFASI YA PILI YA KUTUBU:
Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu Msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya Kristo.
JEHANNAM:
Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na Ziwa la Moto, liwakalo na kiberiti ambapo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (Mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.
Je unaamini kuwa kunayo maisha baada ya kifo?
Ni nini hufanyika baada ya kufa?
Je! Unaamini kuwa Jahannamu ni kitu cha kweli? Jehannamu ni ya milele?
Je, kuna ngazi mbalimbali za mbinguni?
Je, kuna viwango tofauti vya adhabu jehanamu?
Basi ungani nami katika kijarida kijacho kuhusu Maisha ya Milele.
Mungu awabariki sana,
Dr. Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW