Sunday, December 23, 2018

KWANINI WAKRISTO TUNASHEREHEKEA KRISMAS? = SEHEMU YA KWANZA =

Image may contain: text
SOMO:-UKWELI KUHUSU SIKUKUU YA KRISMASI
NA
SABABU ZA MSINGI KI-BIBLIA ZINAZOTUFANYA WAKRISTO KUSHEREKEA KRISMASI .
Ili iwe rahisi kwetu kulielewa vizuri somo hili. Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vinne ambavyo ni:-
1. MAANA YA NENO KRISMASI
2. HISTORIA YA KRISMASI NA TAREHE 25/ DESEMBA
3. MAMBO YA KUYAELEWA NA KUYAZINGATIA KUHUSU HISTORIA YA KRISMASI
4. SABABU ZA MSINGI KI-BIBLIA ZA KUWAFANYA WAKRISTO TUSHEREKEE KRISMASI
Mistari muhimu ya kukumbuka :-
L U K A 2:9-11:-"Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana."
Z A B U R I 118:22-24:"Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa BWANA, Nalo ni ajabu machoni petu. Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA, Tutashangilia na kuifurahia."
Amen!.
1/ KIPENGELE CHA KWANZA
MAANA YA NENO KRISMASI
KRISMASI (pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake mwokozi Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita duniani .
Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule ukristo wa mashariki.
Kuna majina mawili yaliyo ya kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii
Neno KRISMASI linatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
Neno Noeli inatokana na neno la Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambalo limepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "No�l". Hilo ni ufupisho wa neno la Kilatini "Natalis (dies)", "(siku ya) kuzaliwa".
N.B:- IBADA NA SHEREHE YA KUZALIWA KWA YESU (KRISMASI) IKO KI-BIBLIA.
Hili si suala tu ambalo limetungwa na wanadamu fulani. La hasha! Hili ni jambo ambalo lipo ki-biblia kwa kuanzishwa na Mungu mwenyewe.
Tukio la kwanza la IBADA NA SHEREHE YA KUZALIWA KWA YESU KRISTO lilifanyika tokea Yesu alipozaliwa. Na watu wa kwanza kabisa kusherekea kuzaliwa kwake walikuwa majeshi ya malaika wa Mungu. Na pia wanadamu pia walimsifu Mungu na kumtukuza kwa kuzaliwa kwake mwokozi Yesu Kristo. Kwa hiyo suala la Krismasi liko ki-biblia
[ LUKA 2:7-14,20, 25-38].
2/ KIPENGELE CHA PILI
HISTORIA YA KRISMASI NA TAREHE 25/DESEMBA
Tarehe halisi kabisa ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake mwokozi Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.
Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200.
Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Labda kadirio la tarehe ya 25 Desemba pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
KRISMASI NA SIKUKUU YA SOL INVICTUS
Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kufanya ichukue nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika").
Lakini pengine mambo yalikwenda kinyume, yaani kwamba Makaisari walianzisha sikukuu hiyo, halafu wakaipanga tarehe ya Krismasi ili kushindana na Ukristo uliokuwa bado chini ya dhuluma ya serikali yao lakini ulikuwa unazidi kuenea.
Aliyeingiza sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" (Mitra) huko Roma ni Eliogabalus (kaisari kuanzia 218 hadi 222). Baadaye kaisari Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273, hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba.
Wakati wa kaisari Licinius (308-324) sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba.
Mwandishi wa kikatoliki MARIO RIGHETTI kwa utii kabisa anakubali kwamba, " ili kuwezesha kukubalika imani kikristo kwa wapagani , Kanisa la Roma (chini ya mfalme Constantinel aliyeongoka na kubatizwa kuwa mkristo), WAKAIGEUZA KUTOKA sikukuu ya kipagani ya kumpa heshima " Invincible sun" Mithra na mshindi wagiza , wakaona ni busara Desemba 25 kuwa ni sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo".
( Rejea :- Historia ya mwongozo wa kiliturujia, 1955, vol. 2.P.67).
Kutoka Roma, uliokuwa mji mkuu wa Dola la Roma, sherehe ya 25 Desemba ilienea kote katika Ukristo.
Wakristo wengi husheherekea tarehe 25 Desemba (Wakatoliki na sehemu ya Waprotestanti na Waorthodoksi). Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda."
Mwisho wa kunukuu
3/ KIPENGELE CHA TATU
MAMBO YA KUYAELEWA NA KUYAZINGATIA KUHUSU HISTORIA YA KRISMASI.
(1) Kama tarehe 25 Desemba hapo mwanzoni ilikuwa ni sikuu ya kipagani . Halafu Wakaibadilisha kutoka katika imani ya kipagani badala yake ili ichukue nafasi ya kusherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Jambo hilo ni sahihi kabisa mbele za Mungu.
Na katika jambo hilo. Ni ROHO MTAKATIFU aliyelitumia kanisa la Roma chini ya mfalme Constantinel kuibadilisha sikukuu ya kipagani iliyokuwepo , badala yake iwe Chrismasi.
Tendo hilo ni sawa na mtu kumtoa gizani na kumleta kwenye Nuru halisi. Kumtoa katika njia yake upotevu ili kumleta sasa katika njia sahihi ya kweli iliyoonyokaa.
Hakuna tatizo la tarehe 25 Desemba ilyobadilishwa kutoka kwenye sikukuu ya upangani, ili ije kuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Krismas). Jambo ni sahihi kabisa. Kwa mfano Biblia inasema juu ya hilo katika
MATENDO 26:16-18:-"BWANA akaniambia, mimi ni Yesu.... Lakini inuka , usimame kwa miguu yako, maana nimekutokeaa kwa sababu hii , nikuwekee wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako; nikikuokoa na watu wako, na watu wa mataifa, AMBAO NAKUTUMA KWAO; UWAFUMBUE MACHO YAO, NA KUWAGEUZA WAIACHE GIZA NA KUILEKEA NURU, waziache na nguvu za shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu Mimi".
(2) SIKU ZOOTE NI ZA MUNGU NA HAKUNA SIKU YA SHETANI.
Mtu anayeipinga sherehe ya sikukuu ya krismasi kwa kudai kwamba eti 25 Desemba ilkuwa ni siku ya sikuu ya kipagani. Na hivyo hana haja ya kusherekea Krismasi.
Mtu wa namna hiyo. Tatizo lake hajui wala kuelewa anachokisema badala yake anajidanganya mwenyewe na kujipotosha. Uelewa wake ni mdogo!
Ni muhimu kufahamu vizuri . Siku zote ni za Mungu na hakuna siku ya shetani. Inategemea tu na mtu mwenyewe binafsi anaitumia vipi siku hiyo kwa kufanya mambo ya kumpendeza Mungu au mambo ya shetani !! Lakini hakuna siku maalumu ya shetani . Bali Siku zote ni mali ya Mungu mwenyewe. Na anataka tuzitumie siku zote kumsifu, kumwabudu, kumtukuza na kumpendeza yeye .
Kwa mfano Biblia inasema juu ya hilo katika
MWANZO 1:14:-" MUNGU AKASEMA, na iwe mianga katika Anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka."
ZABURI 105:4:-" Mtakeni BWANA na nguvu zake, utafuteni uso wake SIKU ZOTE".
YOHANA 8:29:-" Naye aliyenipeleka yu pamoja nami: hakuniacha pekee yangu; kwa sababu NAFANYA SIKU ZOOTE yale yampendezayo ".
MATENDO 2:46-47:-" NA SIKU ZOOTE kwa moyo mmoja walidumu ndani ya Hekalu......... wakimsifu Mungu,, na kuwapendeza watu woote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa".
Unaweza kuona! Tusimpe siku shetani. SIKU ZOOTE NI ZA MUNGU, maana yeye ndiye aliyezifanya kuwako. . Kilichobaki ni kwa mtu mwenyewe tu binafsi anaitumia vipi hiyo siku kufanya mapenzi ya nani ya Mungu au ya shetani ?!
Na kwa maana hiyo. Kama tarehe 25 Desemba ilikuwa ni siku ya sikukuu ya wapagani. Hilo lilikuwa ni kivyaoo wenyewe kwa upotofu wa mioyo yao wenyewe walivyoamua kuitumia hiyo kufanya mambo yao ya kipangani. Lakini hilo Bado haimanisha kwamba 25 Desemba basi siku hiyo ni ya wapagani. La hasha !! Itakuwa ni ya kipagani kwetu wakristo iwapo kama tutashiriki mambo yao kipagani kama walivyokuwa wakifanya wao. Lakini siku hii tukiitumia tofauti na jinsi walivyoitumia wao. Hii siyo siku tena ya kipagani, bali ni takatifu kwa Bwana.
TAREHE 25 DESEMBA kwetu sisi wakristo tuliookoka tunaitumia siku hiyo maalumu kwaajiri ya kumuadhimisha BWANA kwa kukumbuka tukio kubwa mno la kuzaliwa kwake Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu. Biblia inasema hivi katika
WARUMI 14:4, 6-7:-" Wewe u nani umuhukumuye mtumishi wa mwingine ? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha. YEYE AADHIMISHAYE SIKU , HUIDHIMISHA KWA BWANA; naye alaye hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu ; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu . Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwenu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake."
Katika siku hii ya tarehe 25 Disemba, tunaitumia kumwadhimisha Bwana, ni siku maalumu na ya kipekee ambayo wakristo tunaitumia kutafakari mambo mengi ya ukuu wa Mungu wetu na upendo wake kwa wanadamu. Tunamshangilia , tunamsifu na kumtukuza, tunamwimbia na kumshukuru Mungu Baba yetu na MWOKOZI wetu Yesu Kristo aliyekuja kutuponya, kutuokoa na kutukomboa wanadamu kutoka kwenye gereza la Ibilisi.
" Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba YESU KRISTO ALIKUJA ULIMWENGUNI AWAOKOE WENYE DHAMBI; ambao wa kwanza wao ni Mimi".
[YOHANA 3:16-17; LUKA 2:28-34; 1TIMOTHEO 1:15-16].
IKiwa watu wengine wanaweza kukumbuka kusherekea kuzaliwa kwao na wakamshukuru Mungu. Basi ni jambo zuri na bora zaidi kupita yoote kukumbuka kusherekea kuzaliwa kwake mwokozi wetu Yesu Kristo.
(3) HATUSHEREKEI TAREHE BALI KUMBUKUMBU YA TUKIO LA KUZALIWA MWOKOZI WETU ULIMWENGUNI.
Biblia inasema
YOHANA 21:25:-" kuna na mambo MAMBO MENGINE MENGI aliyoyafanya Yesu; ambayo kama yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa. Lakini hizi zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima wa milele kwa jina lake".
Nini maana yake? Ingawa haijulikani tarehe na mwezi maalumu aliyozaliwa Yesu Kristo au kuandikwa kwenye Biblia. Ndiyo hatuoni! Kwa sababu mbele za Mungu tarehe ya kuzaliwa Yesu sio jambo la msingi, bali lilo la msingi ni TUKIO LA KUZALIWA KWA YESU, ndiomaana Mungu akaliandika. Matukio mengi aliyoyafanya Yesu hayakuandikwa na Mungu, lakini tukio lake hili la kuzaliwa limeandikwa. Hii ni kwa sababu Mungu anataka kutufundisha, tukio hili ni la msingi sana kwetu kulitafakari.
Kujua tarehe ni ipi hilo sio jambo la msingi kwetu kama ambavyo halikuwa la msingi kwa Mungu . Narudia tena Hoja ya msingi kwetu hapa sio tarehe ngapi mwezi gani , bali HOJA YA MSINGI NI KWAMBA YESU KRISTO AMEZALIWA. Full stop. Kwa sababu lilo la msingi kwetu sio tarehe bali ni kumbukumbu ya tukio lilotendeka la kuzaliwa kwa Yesu Kristo ulimwenguni .
Narudia tena kusisitiza unielewe vyema. La msingi kwetu hapa wakristo hatureshekei tarehe, bali tunasherekea kumbukumbu ya tukio la kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Mbali hata na tarehe 25 Desemba, siku zote na wakati woote tungepaswa kusherekea kukumbuka kuzaliwa kwake mwokozi wetu Yesu Kristo ulimwenguni . Biblia inasema katika
MATHAYO 28:20:-"Na kufundisha kuyashika yoote niliyowaamuru ninyi; NA TAZAMA , MIMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE, hata ukamilifu wa dahari ".
Kwa maana hiyo hiyo hata tunaposherekea 25 Desemba kuzaliwa kwake , bado Yesu yupo pamoja nasi.
4/ KIPENGELE CHA NNE
SABABU ZA MSINGI KIBIBLIA ZA KUWAFANYA WAKRISTO TUSHEREKEE KRISMASI.
Ni kwa sababu zifuatazo:-
(1) Ni taarifa ya agizo la Mungu kwetu kupitia kwa mkono wa malaika.
Biblia inasema katika LUKA 2:10-14:-" Malaika akamwambia, msiogope; kwa kuwa Mimi nawaletea HABARI NJEMA YA FURAHA KUKUU ITAKAYOKUWAKO KWA WATU WOOTE; Maana Leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwaajili yenu, mwokozi Ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia".
Unaweza kuona , hata wingi wa jeshi la mbinguni la malaika waliungamana pamoja na wanadamu kufurahia kwa kusherekea kuzaliwa kwake YESU KRISTO.
ISAYA 9:6-7:-" MAANA KWA AJILI YETU MTOTO AMEZALIWA, tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa Amani......."
Mtu yoyote ambaye anapinga kusherekea sikukuu za Krismasi. Mtu wa namna hiyo bila shaka anasema kwa kutumiwa na roho ya shetani bila kujitambua.
(2) Ni Agizo la Biblia kwamba (SIKU YA KRIMASI) tuishangilie na kuifurahia.
Biblia inasema katika
ZABURI 118:22-24:-" Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. Neno hili limetoka kwa BWANA, nalo ni la ajabu machoni Petu; SIKU HII NDIYO ALIYOIFANYA BWANA, TUTASHANGILIA NA KUIFURAHIA".
Jiwe kuu la pembeni anayetajwa hapo ni Yesu Kristo (2 Waefeso 2:20). Na siku inayotajwa hapo ni siku yake ya kuzaliwa ( Christmas).
Na Biblia inasema tena katika ZABURI 70:4:-" Washangilie, wakufurahie, wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako waseme daima, Atukuzwe Mungu".
Sasa Yesu Kristo alipozaliwa, yeye ndiye aliyefanyika wokovu wa Mungu wetu [LUKA 2:27-32; 1KOR 1:30]. Na ndiomaana wakristo Leo tunaidhimisha siku hiyo ya Krismas kwa kushangilia na kuifurahia, kwa kuzaliwa kwake mwokozi wetu Yesu Kristo , aliyetupatia wokovu. HALELUYA!!
(3) Kusherekea Krismasi sio dhambi wala kosa, bali ni mapenzi ya Mungu kwetu.
Biblia inasema katika
1 WAKORINTO 10:-" Basi , mlapo , au mnywapo, au MTENDAPO NENO LOLOTE, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu".
WAKOLOSAI 3:17:-" Na KILA MFANYALO, kwa neno au kwa tendo, FANYENI YOOTE katika jina la Bwana Yesu, mkishukuru Mungu Baba kwa Yeye".
Ndiomaana Siku ya Krismasi mbali tu na kusherekea inavyostahili. Lakini bado imekuwa ni siku maalumu na ya kipekee ambayo mambo mengi mema yanayafanyika ya kuumpa Mungu sifa, heshima na utukufu na shukrani tele, kwetu sisi wakristo tuliookoka. Na Mungu anaonekana kwa namna ya kipekee siku hii pia akiwaponya, akiwaokoa, akiwagusa na kuwatembelea watu wengi.
(4) SIKUKUU YA MWANDAMO WA MWEZI NI KIVULI CHA SIKUKUU YA KUZALIWA KWA YESU KRISTO LEO (KRISMAS).
Nyakati za Agano la kale watu waliagizwa kusherekea sikukuu ya Mwandamo wa mwezi, mara tu mwezi ulipoanza kuandama . Watu walisherekea .
Biblia inasema Katika ZABURI 81:3-4:-" PIgeni panda mwandamo wa mwezi, wakati wa mbalamwezi, SIKUKUU YETU. Kwa maana nu sheria kwa Israeli, ni hukumu ya Mungu wa Yakobo ".
Ni muhimu kuelewa Sikukuu ya Mwandamo wa Mwezi ilikuwa ni picha/mfano/ kivuli cha Yesu Kristo atakayekuja baadaye .
Biblia inasema katika WAKOLOSAI 2:16-17:-" Basi , mtu asiwahukumu ninyi kwa vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au MWANDAMO WA MWEZI, au sabato ; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo ; bali mwili ni wa Kristo ".
Sasa Yesu Kristo Leo yeye ndiye anayeitwa ni Nuru halisi ya ulimwengu. Biblia inatuambia katika YOHANA 8:12:-"Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima".
[ Soma pia YOHANA 1:9-10].
Sasa YESU KRISTO KAMA NURU HALISI iliyokuja katika ulimwengu. Mara tu Wakati huo Alipozaliwa Yesu Kristo katika ulimwengu huu uliojaa Giza . Ilikuwa ni sawa na kama nuru ndogo iliyochomoza na kuanza kuangaza katika ulimwengu huu uliojaa Giza. Na kwa maana hiyo kama katika Agano la kale walivyosherekea sikukuu ya Mwandamo wa mwezi. Jambo hilo lilikuwa ni kivuli tu cha Sherehe ya sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo, tunapoisherekea leo . HALELUYA !!
(5) Tunasherekea Krismas , kwa sababu Yesu Kristo alikuja ili tuwe na uzima tena tuwe nao tele.
Biblia inasema YOHANA 10:10:-" Mwivi (shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; Mimi Yesu nalikuja ili wawe na uzima tena wawe nao tele".
Kabla ya Yesu Kristo hajaja duniani kwa kuzaliwa kwake. Hapo mwanzoni shetani alituonea , alitutesa na kutuua bila kuwa na msaada wowote ule.
Lakini kwa kuja kwake Yesu Kristo duniani. Alikuja ili atuponye, atuokoe na kutuweka huru mbali na dhambi na vifungo vya shetani . Na kwa kila allitajaye jina la BWANA anaponywa na kuolokewa.
MATENDO 10:38:-" Habari za Yesu wa Nazaret, jinsi alivyomtia Mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na KUPONYA WOOTE WALIOONEWA NA IBILISI; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye ".
LUKA 9:1-2:-" Akawaita wale Thenashara, AKAWAPA UWEZO NA MAMLAKA juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, NA KUPONYA WAGONJWA".
[ LUKA 10::17-19 ]
Kama Yesu asingezaliwa dunia Leo . Maana yake ni kwamba uzima , uponyaji wala wokovu tusingeupata.
Lakini ashukuruliwe Mungu Baba kwa kuwa kwa kuzaliwa kwake Yesu Kristo ametupa uwezo na mamlaka, tena tumeponywa na kuweka huru mbali na vifungo vyote vya Ibliisi. Neno la Mungu linasema katika
WAKOLOSAI 1:12-14:-" Mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za Giza , AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi".
(6) Tunasherea siku ya Krismas , kwa sababu kwa kuzaliwa kwake Yesu Kristo duniani. Ametufanya sisi mataifa mengine yoote nje na Israeli, ambao hapo mwanzo tulikuwa hatuna tumaini wala MUNGU duniani. Lakini kupitia kuja kwa Yesu Kristo duniani, tumehesabika pamoja na Israel kuwa sehemu ya urithi mmoja wa watoto wa Mungu.
Maana hapo mwanzo TAIFA LA MUNGU NA WATU WAKE YEHOVA WALIKUWA NI WA ISRAELI TU . Sisi mataifa mengine tulikuwa hatuna tumaini wala Mungu duniani. Maana yake Tulikuwa ni watu wa kufa tu na kwenda Motoni moja kwa moja.
kama Yesu Kristo asingezaliwa , sisi mataifa mengine nje na Israeli, tungebaki kuwa tumetengwa mbali na uso wa Mungu milele .
Lakini kwa kuja kwake Yesu Kristo duniani alipozaliwa. Tumepatanishwa sisi na Israel kuwa kitu kimoja , SISI SOTE NI WATOTO WA MUNGU. Hakuna cha myahudi wala myunani. Biblia inasema katika WAEFESO 2:11-21; WAGALATIA 3:26-29; 1 PETRO 2:5-10.
NB.
Kwa sababu hiyo . Hizo ndizo sababu kuu za msingi ki-biblia zinazotufanya WAKRISTO TUSHEREKEE CHRISTMAS.
Kuamua kusherekea Krismasi au kuacha kusherea yote mawili sio dhambi . kwa maana hakuna Andiko linalotukaza kutoshetekea Krismasi wala hakuna sheria ya Andiko linamlolazimisha mtu kusherekea Krismasi.
Kwahiyo kama utapenda basi sherekea kwa utukufu wa Mungu. Vema. Na kama wewe moyoni mwako kwako haupendi kusherekea Krismasi. Basi acha!
La msingi tusikwazane, tusinyosheane vidole wala kuhukumiaana kwa jambo hili la Christmas. Kila mmoja atumie Uhuru wa imani yake, maadamu kwa kufanya hivyo hatendi dhambi.
Biblia inasema katika WARUMI 14:10-13, 19:-" LAKINI WEWE JE! MBONA WANUHUKUMU NDUGU YAKO? Au WEWE JE MBONA WAMDHARAU NDUGU YAKO ? kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu . kwa kuwa imeandikwa , kama niishivyo asema Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu, na kila ulimi utamkiri Mungu. Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. BASI TUSIZIDI KUHUKUMIANA, bali afadhali toeni hukumu, MTU ASITIE KITU CHA KUMKWAZA NDUGU AU CHA KUMWAGUSHA. Basi kama ni hivyo , na tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana".
La msingi tusihukumiane wala kukwazana kwa wewe unayependa kusherekea Christmas na kwa wewe ambaye husherekei. Bado wote tunabakia ni watoto wa Mungu na tunakwenda mbinguni.
Na la msingi kuliko yote tunaposherekea sikukuu ya Christmas. Ni YESU KRISTO AZALIWE UPYA NDANI YA MIOYO YETU. Tubadilike kitabia , kiusemi, kimavazi , kimwenendo na kufanyika kuwa viumbe vipya machoni pa Mungu wetu.
2 WAKORINTO 5:17:-" Hata imekuwa , MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya".
Na Hakuna maana yoyote ya kusherekea Christmas hii kama bado wewe hujaokoka. MPE YESU MAISHA YAKO NDUGU YANGU , AKUOKOE . Maana neno la Mungu linasema
MATHAYO 1:21:-" Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, YEYE NDIYE ATAKAYEWAOKOA WATU WAKE NA DHAMBI ZAO".
Mungu awabariki wote kwa kila asomaje ujumbe wa Neno hili.
Nakutakia HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA .
Ukipenda kuwasiliana nami kwa ushauri , maombezi na mafundisho zaidi ya masomo ya neno la Mungu. Karibu :-
Mtumishi wa Mungu aliye hai.
MWL, REV:-ODRICK BRYSON
SIMU:- 0759 386 988; 0717 591 466
Email:- Odrick16@gmail.com.
Whatsapp group.
"KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA"
[ 2 WAKORINTO 2:17 ]
Shalom,
By permission Rev Odrick Bryson
Max Shimba Ministries Org,

Saturday, December 22, 2018

ROHO MTAKATIFU NI PARAKLETOS IKIMAANISHA NI MSAIDIZI WETU


Image may contain: text




Mfariji/ Mshauri / Msaidizi: (Isaya 11: 2; Yohana 14:16; 15:26; 16: 7) Maneno yote matatu ni tafsiri ya Kigiriki parakletos, ambayo tunapata "Paraclete," jina jingine la Roho Mtakatifu. Yesu alipokwenda, wanafunzi wake walikuwa na wasiwasi sana kwa sababu walikuwa wamepoteza uwepo wa ufariji wake. Lakini aliahidi kutuma Roho Mtakatifu kuwatuliza, kuwafariji, na kuongoza wale ambao ni wa Kristo. Roho Mtakaatifu pia "anatoa ushahidi" na roho zetu kwamba sisi ni wa Yeye na kwa hiyo hutuhakikishia wokovu.
Kabla ya kuondoka, Yesu alimtambulisha Roho Mtakatifu kwa wanafunzi wake. Katika utambulisho huu aliourudia sehemu kadhaa, tunapata kujifunza juu ya umuhimu wa Roho wa Mungu. Huu ni moja ya mistari ambayo Yesu anamtambulisha Roho Mtakatifu kwetu:
Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu.Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. (Yohana 14:14-17)
Yesu anaahidi Roho Mtakatifu: Yohana 14:15-31
Hatua muhimu mwishoni mwa sura ya 14 ni ahadi ya kwamba wanafunzi watapokea Roho Mtakatifu kama Msaidizi wao. Neno 'Msaidizi', katika parakletos ya Kigiriki, lina maana nyingi. Wanasayansi wamejaribu kutambua asili yake katika historia ya dini kwa kusoma maandiko kutoka kwa dini mbalimbali. Mfano unaofanana unaonekana katika fasihi za Kiyahudi, na pia kati ya Wayahudi wa Qumran, na baadaye katika maandiko ya Mandaa. Utafiti wa maandiko haya haujawasaidia sana. Neno hilo ni la zamani, lakini somo ni jipya.
Hata hivyo, Roho Mtakatifu ni Mchungaji (tazama Ayubu 33:23), Msaidizi (1 Yohana 2: 1), Msaidizi na Msaidizi (hasa katika sehemu tunayozungumzia sasa) kwa Wakristo. Tunapojifunza kutoka kwa sehemu ya sasa, Roho Mtakatifu alikuwa, juu ya yote, alitumwa ili kuwasaidia Wakristo baada ya Yesu hakuwa tena kimwili miongoni mwao. Hivi karibuni Yesu alikuwa amekwenda, lakini kupitia Msaidizi, wale walio wake wanaweza bado kumwona. Tofauti na "watu wa ulimwengu", wafuasi wa Yesu wanaelewa kwamba Baba yuko ndani ya Mwanawe, Mwana ni ndani ya Baba, Yesu ni yeye mwenyewe, na yeye mwenyewe ni ndani ya Yesu - hii inatuchukua sisi juu ya mambo ya kiteolojia. Dunia haijui Msaidizi, wala haitamjua.
Kipengele kingine kikubwa katika kifungu hiki, kinachoonekana mara kadhaa, hujali utii wa waumini kushika maneno ya Mwalimu wao. Ikiwa tunampenda Yesu, ni kuonekana katika matendo yetu halisi. Tunataka kutii mapenzi ya Bwana ambayo ametuonyesha. Kuna msisitizo mkubwa sana juu ya haya yote katika maandishi ya Yohana na (tazama mfano 1 Yohana 2: 7-11). Upendo wetu kwa Bwana siyo dhana tu, lakini inamaanisha kwamba tunatenda kwa maneno yake. Hatuwezi kumpenda Yesu na, wakati huo huo, tusijali neno lake.
Katika mistari ya mwisho ya sura hii, giza huanza kuanguka juu ya utukufu. Saa iko karibu, Yesu yuko karibu kusulubiwa. Utii wa Mwana kwa mapenzi ya Baba unaonyeshwa kwa ukweli kwamba Yesu mwenyewe ni wa kweli kwa maneno, ambayo alianza tu kutangaza. Upendo kwa Baba hupimwa kwa vitendo halisi, na hivyo Bwana huweka njia ya msalaba.
Yafuatayo ni mambo mbalimbai ambayo Biblia inatufundisha kuhusu nafsi ya Roho Mtakatifu.
Parakletos (mfariji, yeye anayekuwa pamoja nasi - Yohana 14:16, 26; 15:26)
Hufahamu mawazo ya ndani ya Mungu (1 Korintho 2:10-11)
Huongea nasi (Matendo 13:2; Ebr 3:7)
Hutufundisha (Yohana 14:26)
Kama mzazi, ili kwamba tusiwe yatima (orphanos kwenye Kigiriki - Yohana 14:18)
Hutuongoza (Yohana 16:13)
Hutufundisha (Yohana 14:26; 1 Korintho 2:13)
Huishi ndani yetu (1 Korintho 3:16; 2 Tim 1:14; Rum 8:9, 11; Efeso 2:22)
Mioyoni mwetu (2 Korintho 1:22; Galatia 4:6)
Hutuombea (vitu visivyo na uhai haviombi au kuombea - Rumi 8:26-27)
Anaweza kufanyiwa jeuri (Ebrania 10:29)
Humshuhudia Kristo (Yohana 15:26)
Anao ufahamu (Rumi 8:27)
Anaweweza kuhuzunishwa (Isaya 63:10; Efeso 4:30)
Hufanya maamuzi (1 Korintho 12:11)
Hupenda (Rumi 15:30)
Anaweza kupendezwa na mambo (Matendo 15:28)
Huchunguza mambo ya ndani ya Mungu (1 Korintho 2:9-10)
Huugua (na kwa ajili hiyo hutujali - Rumi 8:26)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu kristo Mungu Mkuu. Tit0 2:13

Thursday, December 20, 2018

SHETANI NI NANI?


SHETANI NI NANI?
JE, SHETANI ALIUMBWA NA MWENYEZI MUNGU KAMA WANAVYO DAI WAISLAM?
Biblia humwita “mungu wa ulimwengu huu.” Lakini alitoka wapi? Je Mungu alimuumba kama alivyo? Je, yeye ni roho aliyeanguka? Haya hapa ni majibu kutoka katika Neno la Mungu!
Biblia inamfafanua Shetani kuwa kiumbe halisi ambaye yuko katika makao ya roho. (Ayubu 1:6) Inatueleza kuhusu sifa zake za ukatili kutia ndani matendo yake ya uovu. (Ayubu 1:13-19; 2:7, 8; 2 Timotheo 2:26)
Asili ya Shetani ni wapi au nini?
Tangu mwanzo Shetani hakuwa anaitwa Shetani, yaani hapakuapo na kiumbe kilichoumbwa na kuitwa Shetani. Alikuwa ni “mwana wa asubuhi” (Isa.14:12) yeye pamoja na jeshi lingine la mbinguni,waliumbwa wote wakiwa wakamilifu katika njia zao zote ( Ezekieli. 28:14-19). Kulikuwa na amani na umoja Mbinguni. Kisha mambo yakaharibika. Biblia haiko wazi sana juu ya swala hili ni nini hasa kulitokea na kwa namna gani, ila uovu au kutokumtii Mungu kulioneka kwa Lucifa. Mwishowe alifukuzwa kutoka Mbingini, pamoja na jeshi lake lote lililoasi, wakafukuziwa mbali kabisa kutoka mbinguni na kutupwa, na wanazunguka zunguka katika nchi (duniani).
(Wakolosai 1:15) Mungu aliumba malaika. (Ayubu 38:4-7) Wote walikuwa wakamilifu na waadilifu. Hata hivyo, mmoja kati ya malaika hao aliitwa Lusifa ndie akaja kuwa Shetani.
Malaika huyo hakuitwa Shetani alipoumbwa. Jina hilo ni la kumfafanua, na linamaanisha “Mpinzani; Adui; Mshtaki.” Alikuja kuitwa Shetani kwa sababu alichagua kumpinga Mungu. Ni sawa na kusema, Mungu hakuumba majambazi, bali Majambazi ni sifa ambayo mtu anaipata anapo fanya unyang'anyi kwa kutumia nguvu. Mungu wetu hakuumba uovu.
Kiumbe huyo wa roho akaanza kukuza hisia za kiburi na za kushindana na Mungu. Alitaka wengine wamwabudu yeye. Yesu alipokuwa hapa duniani, Shetani alimtaka Yesu ‘amfanyie tendo la ibada.’—Mathayo 4:9.
Shetani alitupwa na malaika wake?
Ufunuo 12: 7-21 Imeandikwa “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Ufunuo 12 husema juu ya Shetani na pepo wake wabaya “walitupwa katika nchi” (fu. 13). Kwa hakika sura hii imepachikwa katikati ya kitabu cha Ufunuo, na ni muhtasari mfupi wa historia ya Kanisa la Agano Jipya.
Fungu la 3 linamwelezea Shetani kama “joka” aliye “kokota theluthi ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika nchi” (fu. 4). Kumbuka kwamba “nyota” hizi zilikuwa ni theluthi ya malaika wote waliokuwa chini ya Nyota ya alfajiri kabla hajaasi.
2 Petro 2:4 hutoa kiashiria kingine juu ya huku “kutupwa chini” kwa Shetani na malaika zake “aliowakokota pamoja” naye. Angalia: “Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa [Shetani hakuwa malaika pekee aliyeasi], bali aliwatupa shimoni.” (Neno la Kigiriki hapa ni tartaros na linamaanisha aidha “gerezani” ama “kizuizini”—hii ni dunia yenyewe.) Pepo hawa wabaya pamoja na Shetani “wanalindwa hata ije hukumu,” wakiisha “kutiwa…katika vifungo vya giza.” Hii inafunua kwamba Mungu aliwatia katika gereza hili la giza pepo wengine wengi walioanguka waungane na “mkuu wa giza.”
Ufunuo 12:7-9 hueleza, kwa undani, lini Shetani na pepo wake wabaya watatupwa hata nchi kwa mara ya mwisho wasipate tena kibali cha kuingia mbinguni. Mafungu ya 12-14 yanaonyesha kwamba mwitikio wa ibilisi ni hasira kuu. Wakati huu wa kutisha unakuja kwa ulimwengu mzima hapo mbeleni kidogo!
Shetani anatushawishi vipi?:
Asili ya shetani ni roho mchafu. sio kitu kinachoweza kuonekana, lakini ni kitu ambacho tunaweza kukifahamu kwa kusoma Biblia. Biblia ilitolewa kama Neno la Mungu. Yesu Kristo alikuja kwetu kama mfano hai wa Neno la Mungu. Ni katika kusoma Biblia tu, ndipo tunaweza kutambua mazuri na mabaya, kujua juu ya utauwa, au kutambua haki na imani ya kweli, na yapi yaliyo ya shetani. Na ni nini yaliyo Mapenzi ya Mungu. Sio jambo tunaloweza kulifahamu tangu kuzaliwa au ambalo tukiwa tunazaliwa tunakuwa tunalifahamu.Wengi kati yetu tunafanya uchaguzi mbaya kwa sababu hatusomi Biblia na kulifuata Neno la Mungu, sawa sawa na Mapenzi ya Mungu.
Shetani ni roho mchafu na anatushawishi kiroho, njia moja ya kumuona shetani ni katika mawazo yetu, akilini mwetu. Tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu. Shetani sio kitu kilichoandikwa, sio kitu tunachoweza kukiona kwa macho, kukisikia, kugusa, kuonja au kunusa. Mungu ni kama hivyo kwa namna fulani na malaika wote na hata shetani pia.
Waefeso. 2:2 Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumufuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi.
Mwisho wa Shetani ni wapi?
Ufunuo 20:2 Akamshika yule joka, yule joka wa zamani, ambaye ni ibilisi na shetani, akamfunga miaka elfu.
Shetani atafungwa na hataweza kumshawishi mtu tena mwanadamu yeyote kwa muda miaka elfu moja kisha atafunguliwa tena (Ufunuo 20:7) mwisho wa hiyo miaka elfu moja. Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, shetani atafunguliwa, atoke kifungoni kwake; na kutambua ya kwamba ameshidwa; ni mnyonge hawezi kupata nguvu pasipo Mungu, na kuna vita vingine tena vitakavyotokea dhidi ya Mungu kama shetani atakavyowadanganya nakuwashawishi watu tena kama anavyofanya wakati huu wa sasa
Shetani anatupwa katika shimo (Isaya 14:15-17). Na wale wanaomwona washangaa na kustajabu ya kwamba huyu ndiye yule aliyeleta matatizo yote ya duniani na huzuni na masikitiko yote. Ghafla anabadilika na kutokuwa tena yule mnyama wa roho chafu ya kutisha na ya kuogofya ambaye hapo mwanzo alikuwa ni wa kuogofya na wa kutisha, aliyeweza kusababisha watu waamini ya kuwa ndivyo alivyo. Yeye ni mhongo aliyouadhibu uumbaji wa Mungu uliyofundishwa kumkili Mungu katika nguvu zake ambaye Yeye ni Mweza.
Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Hata hivyo shetani atatambua ya kuwa Mungu alikuwa ni wa haki wakati wote. Hili neno “shetani” maana yake ni mshitaki. Shetani ataacha kuwa mshitaki, hatakuwa shetani tena. Hatawashitaki tena ndugu, kama alivyowashuhudia kwa uongo. Mashitaka yamekwisha lakini yatakuwepo daima kama kumbukumbu. Adhabu gaini kwa shetani ! Mashitaka yake hayatasahaulika. Yatakumbukwa daima kama aliyemvunjia Mungu heshima, na kwa kuudan ganya ulimwengu. Atapata mateso yake kwa sababu atatambua makosa yake. Msamaha wetu ni muhimu sana katika kurudisha utukufu na heshima yake na katika maisha mema.
Mwishowe, kila mtu atamtambua Kristo kuwa ni Mfalme na Kuhani Mkuu anayeunganisha dunia yote na kumwakilisha Mungu. Jambo hili litakapokamilika vita kati ya mema na mabaya vitakuwa vimekwisha. Ushawishi wa shetani utakuwa umekwisha. Mauti yamekwisha. Makanisa ya uongo na manabii wa uongo na unabii wa uongo utakuwa umekwisha. Yote yatakuwa yamekwisha; wote watatambua Mpango wa Mungu na watakuwa sehemu ya Familia ya Mungu. Wote watakiri ya kwamba Mungu alijua yote, na anajua yote, na daima atajua yote.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
Image may contain: 1 person, text

Wednesday, December 19, 2018

SODOMA NA GOMORA

Image result for sodoma na gomora iko nchi gani
na Tony Alamo
Karibu na Yeriko katika Israeli ipo sehemu iitwayo Sodoma na Gomora.1 Kama unaweza kuiona, utafahamu bila shaka kwamba MUNGU ni MUNGU mwenye kuhukumu!2 Unaweza kuchukua vipande vya njano vya salfa, ambavyo huungua unapoviwasha. Ni mahali pa kutisha ambapo hujawahi kuona. Milima yaonekana kana kwamba MUNGU alivikata vilele vya milima katika vipande vikubwa-vikubwa, kisha, kwa ngumi YAKE kubwa, akaponda kila kitu na kusawazisha, akazika katika chumvi, salfa (kiberiti) na moto. Beba nyumbani kipande cha salfa (kiberiti) kama ukumbusho. Chukua kipande kingine ukiweke kwenye sanduku la kupigia kura wakati umma unaposema, “Hebu tupige kura tuone kama ndoa ya jinsia moja ni sawa.” Kamwe usithubutu kusema pamoja na halaiki ya watu kwamba NENO LA MUNGU si la kweli! Hatuwezi kujua sawa, baya, jema, au ovu bila NENO LA MUNGU!3

Eneo lote hili lina joto kuliko sehemu nyingine yoyote katika Nchi Takatifu. Pia ni sehemu ambayo haina uhai. Kuna milima mikubwa ya chumvi karibu yake.4 Haijalishi ni kiasi gani mto Yordani hutiririka na kumwaga maji yake baridi katika Bahari ya Chumvi, maji ya bahari ya Chumvi ni chumvi sana, na kamwe hayawezi kuendeleza uhai, wala kutoa samaki. Kuanguka kwa milima kumelifanya eneo hilo kuwa ukiwa sana, na kuna kreta kubwa katika ardhi karibu na hoteli. Eneo hili huitwa Engedi, likimaanisha “jicho la kondoo.” Zipo hoteli tatu kubwa huko, na nyingine ndogo kumi, zote zikiwa na mabwawa ya kuogelea. Kreta kubwa na maharibiko halisi vilikuwa kwenye barabara ya nyuma inayotoka Engedi kwenda Beer-sheba. Unaposimama juu kwenye pembe za kreta, unaweza kuona vizuri zaidi uharibifu, eneo la milima iliyoporomoka ya Sodoma na Gomora. Nyuma ya kreta, kuna milima iliyofunikwa na mawingu na ukungu juu yake. Ukimya na ukiwa humfanya mtu kuwa na hofu. Haiwezekani kabisa kuona chini kwenye kreta, ni pana sana.

Kuna kreta ngapi kubwa katika ardhi – ardhi iliyopasuka mashimo makubwa – ambayo imesababisha uharibifu na maziko ya Sodoma na Gomora? Yeriko ni lazima ihusishwe pia, kwa sababu Sodoma ni wilaya tu ndani ya Yeriko. Unaposhuka na barabara ya mlimani kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, masikio yako huzibuka, kama vile unatua na ndege. Yeriko ipo chini sana ya usawa wa bahari, sehemu iliyo chini kuliko sehemu zote za nchi. Ni kwa sababu MUNGU aliponda na kusawazisha eneo lote. Aliifanya sehemu hii kuwa chini kuliko sehemu zote za ardhi kwa sababu ya dhambi walizotenda.5

Yeriko, isipokuwa mji, karibia yote ni tupu, na isiyo na uhai, kwani ni nchi iliyolaaniwa. Inatia huzuni. Mazingira ni mabaya mno. Haijalishi ni mara ngapi watu wanajaribu kuiendeleza nchi, kwa namna fulani kuleta maisha na furaha ndani yake; lakini nchi hiyo inawashinda na haiendelei. Unaweza kuona mapango na nyumba ambazo zimeharibiwa. Watu waishio humo ni wachache, na wengi wao ni wachungaji. Mfumo wao wa maisha ni mbaya sana na wa kikatili, kama ardhi yao ilivyo katili, na nyuso zao huonekana ngumu kama mwamba.

Watu hadi leo hii, huchukua mawe ya salfa, kiberiti, ambavyo MUNGU alimwaga juu ya eneo hilo. Huchukua kumbukumbu na kuwasha mawe ya salfa kwa kiberiti. Wezi wa makaburi (Majambazi) na wanaakiolojia hutembelea maeneo haya mara kwa mara kuangalia makaburi na majeneza. Majambazi huchimba usiku, wakisaka miili, mitungi, vikombe, vito, na samani ambavyo wanaweza kuviuza kabla ya wanaakiolojia kuvipata. Wanajaribu pia kuchimba mapango yaliyoharibiwa na nyumba kutoka kwenye miamba, kiberiti na salfa.

Yeyote atakayetazama ukubwa wa uharibifu katika eneo hili hatakuwa na shaka kwamba ni uharibifu alioufanya MUNGU kulihadhibu eneo hili, kwani nchi yote ya Israeli ni ya kijani na iliyostawi, isipokuwa sehemu ya Sodoma na vijiji vinavyoizunguka. Hivi punde MUNGU ataleta uharibifu WAKE katika dunia hii tena na juu ya ulimwengu wote.6

Nchini Marekani, hatujawahi kuona tetemeko la ardhi kubwa zaidi ya 9.2 kwa kiwango cha skeli za Richter. Ni rahisi kuona kwamba, kama uharibifu alioufanya MUNGU katika Sodoma na Gomora ungepimwa leo kwa skeli ya Ritcher, ungesomeka 25.0 au zaidi. Hii ni bila hata ya kuzingatia mvua ya moto na kiberiti juu ya watu kwa sababu ya vitendo viovu vya ngono, kama ushoga na uzinzi.7

Eneo lote hili linastahili kuwa ushuhuda wa MUNGU kwa watu wote, hasa wale wapotovu wanaofanya ushoga na usagaji. Baada ya kuona yote haya, utatambua kwamba MUNGU hafanyi mzaha. Humaanisha kile Asemacho.8 Ni nyakati za mwisho, hivyo usifanye mzaha hali kadhalika unaposali sala hii kwa MUNGU:
Prayer
BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13
BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.
Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).

Mahali ilipo Sodoma na Gomora
Mwanzo 19:27-28 inasema, “Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za BWANA, naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama  moshi wa tanuru.”

Katika miaka ya 1980, mgunduzi wa kiakiolojia wa maeneo ya Kibiblia, Ron Wyatt, alibaini maono wa ajabu wa “maumbo” alipokuwa akipita katika pwani ya Bahari ya Chumvi. Kwake yalionekana kama kuta za mji na majengo, ila katika rangi nyeupe. Kwa miaka mingi hakufanya lolote kuhusu kile alichokiona, lakini mnamo 1989, Ron aligundua jambo ambalo lilimshawishi kwamba maumbo haya yenye rangi nyeupe hayakutokana na mabadiliko ya kijiolojia.

Zaidi ya Matabaka ya Kijiolojia
Ron aliona barabara ambayo vitu vyeupe vilikuwa vimekatiza na sehemu ya ndani ikiwa na vitu vilivyoonekana katika mpangilio wa tabaka ambazo zilionyesha dhahiri kwamba haya yalikuwa ni zaidi ya matabaka ya kijiolojia.

Katika kutafuta kwenye Biblia, dalili kulingana na maandiko yao, Ron na mkewe Mary Nell walipata marejeo andiko ambayo yanataja miji minne inayounda sehemu ya mipaka ya Wakanaani:
“Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha” (Mwanzo 10:19).

Itakuwa ni jambo la ajabu kwa Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu kila mmoja kuorodheshwa kama alama za mpaka kama yote ingekuwa katika eneo moja, upande wa kusini mwa Bahari ya Chumvi. Ni mantiki kwa miji iyo kuwa katika umbali kutoka mmoja hadi mwingine ili kujumuisha kila mmoja wa miji hiyo kama alama za mpaka.

Sehemu ya maeneo aliyoona Ron, kwa hakika, yalikuwa yametengana kwa umbali usiopungua maili hamsini au zaidi. Mji mmojawapo ulikuwa kaskazini mwa Yeriko, ambao kulingana na maandiko inaashiria Seboimu utakuwa kaskazini mwa Bahari ya Chumvi.

“Naye Sauli, na mwanawe Yonathani, na watu walikuwapo pamoja nao, wakakaa huko Geba ya Benyamini; lakini Wafilisti wakatua katika Mikmashi. Nao watekaji wa nyara wakatua katika marago ya hao Wafilisti, vikosi vitatu; kikosi kimoja kikageukia njia iendayo Ofra, mpaka nchi ya Shauli; na kikosi kingine kikageukia njia iendayo Beth-horoni; na kikosi kingine kikageukia njia ya mpakani ielekeayo bonde la Seboimu upande wa nyika” (1 Samweli 13:16-18).

Baadaye 1989, Ron na Mary Nell Wyatt walitembelea eneo hilo chini kidogo ya Masada na wakachukua sampuli ya vitu vyeupe ambavyo vilivunjika haraka mikononi mwao na kusambaratika katika chembe mithili ya poda ya talkum. Wakati huo, Mary Nell aliona moja ya kapsuli ya kiberiti ikiwa imegandamana na kipande cha majivu yaliyosindiliwa; hata hivyo, hakuna hitimisho lililopatikana wakati huo, kwamba kilikuwa ni kitu gani.

Mnamo Oktoba 1990, Ron Wyatt na Richard Rives walirudi katika eneo hilo. Walipokuwa wakilichunguza eneo hilo lililoko chini ya Masada, waligundua kwamba mvua ilikuwa imenyesha. Walipokuwa wakishangaa mahali hapo, Richard aliona kitu mfano wa chumba kilicho wazi au pango kwa mbali na walipokaribia pango walikutana na rundo kubwa la majivu ambalo lilikuwa limeanguka muda huo kutoka juu – labda kwa sababu ya mvua iliyokuwa imenyesha muda huo. Ron aliposimama kutazama, aliona gololi nyingi za njano ndani ya majivu yaliyosambaratika, zote zikiwa zimezungukwa na ukoko mwekundu-mweusi mithili ya pete. Alipojaribu kutoa moja, alitambua ilikuwa ni salfa. Kwa uchunguzi wa karibu, sasa akiwa anajua nini anatafuta, ilifahamika kwamba vyote vilivyokuwa ndani ya mabaki ya majivu vilikuwa ni vitu vya mviringo kama mpira vikiwa vimezungukwa na salfa (kiberiti).

Baada ya uvumbuzi wa kiberiti, utafiti wa kiakiolojia wa Wyatt ulianza kuchunguza kama kiberiti walichoona kilipatikana katika mfumo huu sehemu nyingine yoyote. Ron na Mary Nell Wyatt pamoja na Richard Rives walikwenda kwenye Taasisi ya Smithsonia, mjini Washington D.C. na kuchunguza salfa yao katika namna tofauti, hakuna iliyokuwa ya mviringo yenye poda za salfa. Na kuongeza, hakuna iliyokuwa imezungukwa na utando. Ombi liliidhinishwa na Taasisi ya Smithsonia kuchunguza salfa zilizokuwa na mwonekano tofauti. Salfa zilikusanywa kutoka sehemu mbalimbali duniani, zenye zaidi ya vielelezo hamsini. Hakuna hata moja kati ya hizo zilizoonyesha tabia sawa na salfa ya kiberiti iliyopatikana karibu na “miji ya Bonde.”
Ron Wyatt hakuwa mtu wa kwanza kugundua kiberiti karibu na Bahari ya Chumvi. Wakati William Albright na Melvin Kyle walipotoka kuiona miji ya Sodoma na Gomoara mnamo 1924, wao pia, waliona vipande vya kiberiti kusini mwa Bahari ya Chumvi.

“…sehemu ambayo kiberiti kilinyesha itaonyesha kiberiti. Naam, inaonyesha; tuliokota salfa halisi, katika vipande vikubwa kama ncha ya dole gumba langu. Imechanganyika na mchanga wa milima magharibi mwa bahari, na sasa imesambaa katika mwambao wa bahari hata upande wa mashariki wa bahari, kama maili nne au tano kutoka kwenye pembe yenye tabaka. Kwa kiasi Fulani imetawanyika mbali na kwa mapana juu ya bonde hili.” (Ugunduzi wa Sodoma na Dk. Melvin Kyle, 1928, uk. 52-53)

Wala Melvin Kyle hakuwa wa kwanza kuona mabaki ya majivu. Kumbukumbu nyingine ya miji hii inatoka kwa Josephus katika kitabu chake cha Nne, Wars of the Jews, (Vita ya Wayahudi), Sura ya VIII:
“Sasa nchi hii imeteketezwa kwa namna ya kuhuzunisha, na hakuna anayetamani kuikaa;…ilikuwa nchi ya kale yenye furaha sana, kwa matunda iliyozaa na utajiri wa miji yake, ingawa yote sasa imeteketezwa. Inatokana na ukengeufu wa wakaazi wake, ulichomwa kwa radi; Kutokana na madhara hayo bado yamo mabaki ya moto ule wa Mungu; na athari (au vivuli) vya miji mitano bado huonekana...”
Maelezo ya Josephus yanaeleza vizuri kabisa kile kinachoweza kuonekana katika sehemu hizi za majivu:
“...imeteketezwa yote.”

Maelezo ya uharibifu wa Sodoma, Gomora, na “Mabonde yote” havikuwa hadithi za kale. Lilikuwa tukio la kihistoria ambalo lilitokea hasa kama maelezo ya Kibiblia yalivyobainisha.
http://www.wyattmuseum.com/cities-of-the-plain.htm

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:
Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 
P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078
Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362
Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.
Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.
Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.
Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.
Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo
Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.
Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.
MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)
USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.
Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:
© Hatimiliki Aprili 2015 Haki zote zimehifadhiwa, Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo ® Imesajiliwa Aprili 2015
SWAHILI—VOLUME 21200—SODOM AND GOMORRAH

footnotes:
1. Mwa. 18:20-33, 19:1-29, Kum. 29:23 return
2. Mwa. sura. 6-7, Hes. 11:1, Kum. 4:24, 10:17, 32: 4, 15-16, 19-26, 35:43, Zab. 2:1-5, 12, 7:11-12, 11: 5-6, 21:8-9, Isa. 30:1-3, 30, 33, 66: 15-16, 24, Yer. 7:20, 10:10, 21:11-14, Omb. 4:11, Nah. 1:2-8, Mat. 25:31-46, 2 Kor. 5:10-11, Ebr. 10:30-31, 2 Pet. 2:4-9, Yud. 7, Ufu. 14:9-11, 20:11-15 return
3. Kut. 20:1-7, Kum. 5:1-21, Yos. 1:8, Zab. 119:9, 104-105, 130, Mit. 6:23, Mal. 4:4, Yoh. 5:24, 8:31-32, 12:48, 15:3, 2 Tim. 3:15-17, Yak. 1:21-25, 2 Pet. 1:19 return
4. Mwa. 19:24-26, Kum. 29:23, Isa. 13:19-22, Yer. 50:40, Omb. 4:6, Sef. 2:9 return
5. Mwa. 13:13, 18:20-21, 19:1-13, 24-25, Eze. 16:49-50, Yud. 7 return
6. Isa. 13:3-13, 24:1-21, 34:1-10, Eze. 22:25-31, 24:6-14, sura 38, Yoe. 1:13-15, Zef. 3:8, Mal. 4:1, Mat. 24:3-7, 21-22, 29-34, Lk. 17:24-30, 2 Thes. 1:7-10, 2 Pet. 3:3-12, Ufu. 6:15-17, 8:7-13, 9:1-19, 11:18, 16:1-11, 17-21, 19:11-21 return
7. Mwa. 19:4-13, Law. 18:20, 22, 20:13, Kum. 22:5, 23:17-18, Amu. 19:22-28, 1 Fal. 14:22-24, Rum. 1:18, 24-32, 1 Kor. 6:9-10, 18, 10:8, 2 Kor. 12:21, Gal. 5:19-21, Efe. 5:3-6, Kol. 3:5-7, 1 Thes. 4:3, 1 Tim. 1:9-10, Ebr. 13:4, Yud. 7, Ufu. 2:21, 9:21, 22:15return
8. Hes. 23:19, 1 Sam. 15:29, Zab. 119:89, Mit. 19:21, Muh. 3:14, Isa. 14:24, 40:8, Yer. 4:28, Eze. 24:14, Dan. 4:35, Mat. 5:17-18 return

Prayer footnotes:
1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return
2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return
3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return
4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return
5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return
6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return
7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return
8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return
9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return
10. Heb. 11:6 return
11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return
12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return
13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return

Friday, December 7, 2018

WAPI YESU KASEMA WATU WAWE WAKRISTO?




WAPI YESU KASEMA WATU WAWE WAKRISTO?
Hili ndilo swali dhaifu linalo ulizwa na ndugu zetu kila kukicha. Leo nawajibu kwa aya ili wanyamaze milele yote.
Marko 9: 39 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;
40 kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.
41 Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
Katika aya ya 41, Yesu anasema sisi ni watu wa Kristo. Je, mtu wa Kristo ni nani kama sio Mkristo?
Je, hawa watu waliomfuata Yesu waliitwa Wakristo?
Matendo 11: 26 hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
Neno la Mungu linakujibu kuwa, wanafunzi wa Yesu ambao ni sisi tunaitwa Wakristo.
Je, dai la Ukristo ni dini linathibitishika kama wanavyo lazimisha Waislam?
3.Suurat Al 'Imran 99. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliye amini NJIA ya Mwenyezi Mungu mkiitafutia kosa, na hali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda.
Waislam wanakiri kuwa NJIA YA MWENYEZI MUNGU NI DINI. YAANI DINI NI NJIA. JE, NJIA HII YA MWENYEZI MUNGU NI IPI?
Soma: "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." Yohana 14:6
YESU ANASEMA YEYE NI NJIA. WAISLAM WANASEMA DINI NI NJIA, KUMBE BASI UKRISTO KWA TAFSIRI YA WAISLAM NI DINI.
1 Petro 4:16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
KUMBE JINA LA UKRISTO NI LA KUMTUKUZA MUNGU KAMA ILIVYO THIBITISHWA KWENYE PETRO HAPO JUU.
Sasa tusome Tafsir ya Bharwani hapa chini: 1.Suurat An Nahl 125
Maelezo: Suuratun Nah'l * 125. Ewe Nabii! Lingania, uwite watu kwenye Njia ya Haki ambayo Mola wako Mlezi amewataka watu wako waifuate. Na katika huo Wito wako pita njia ambayo inamnasibu kila mmoja wao. Waite wenye vyeo vya juu katika wao kwa maneno ya hikima kwa mujibu wa akili zao. Na watu wa kawaida walio baki kati yao walinganie kwa kuwapa mawaidha yanao waelekea, na kuwapigia mifano ya mambo wanayo pambana nayo ya kuwapeleka kwenye Haki, na uwaongoze kwenye njia fupi inayo wanasibu. Na jadiliana na watu wa dini zilizo tangulia katika watu wa Biblia, yaani Mayahudi na Wakristo, kwa kutumia hoja za kiakili, Mant'iqi, na maneno laini, na majadiliano mazuri, si maneno ya ukali na matusi, ili uwakinaishe na uwavutie. Hii ndiyo njia ya Daa'wa (Wito), kuwaita watu kumwendea Mwenyezi Mungu -watu wa mila zote. Basi ifuate njia hii unapo waita, na baada ya hayo yaliyo baki mwachilie Mola wako Mlezi, ambaye anamjua aliye zama katika upotovu kati yao na akawa mbali na njia ya uwokovu, na nani ambaye aliye salimika, akaongoka, na akayaamini hayo uliyo waletea.
ALLAH ANASEMA UKRISTO NI DINI ILIYO TANGULIA. KUMBE UISLAM HAUKUWEPO KABLA YA UKRISTO. http://www.iium.edu.my/deed/quran/swahili/without/c16.htm…
JE , NIKWELI UKRISTO NA KANISA VILIKUWEPO KABLA YA UISLAM.
Tumsome Musa, Je aliingia KANISANI?
Matendo ya Mitume 7: 37 Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye.
38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Musa anawajibu waislam kuwa yeye aliingia Kanisa alipo kuwa Jangwani. Kumbe Musa hakuwa Muislam wala hakuwai ingia Msikitini.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

UISLAMU SI MAHALI SALAMA PENYE UHURU NA USAWA

Image may contain: one or more people and textHata tukidhani kimakosa kuwa uislam ulianzia Afrika na kwamba Nabii wake alikuwa mweusi, hii pekee yake haitakuwa sababu nzuri kwa weusi kuasiri uislam.
Hata haitakuwa sababu nzuri kwa wazungu kuasiri uislamu kwasababu tu Muhammad alikuwa mweupe. Tunapaswa kuuangalia uislamu wenyewe.
Nisingependa niwe Muislam kwa sababu uislam hupingana na uhuru, kitu ambacho kipo karibu sana na mioyo na nia za Waamerika wenye asili ya Kiafrika, ukizingatia dhuluma waliyoipata hapo zamani.
Kitu kimoja ambacho uislam hauamini ni uhuru wa kidini. Ikiwa uislam utaichukua Amerika hapatakuwa na uhuru wa kidini. Koran inasema, "Ikiwa mtu yeyote ataka dini nyingine licha ya uislam, jambo hili halitakubaliwa kwake kamwe; na katika maisha yajayo mtu huyu atakuwa katika kundi la waliopotea (Sura 3:85).
Mafundisho mengi ya uislam hayaendani na na maendeleo na nyakati. Na pia hayaendani na haki za binadamu, haki za kiraia au haki za kikatiba.
Ifuatayo ni mifano michache ya uislam Wanaume ni bora kuliko wanawake (Sura 2:228) Wanawake wana haki nusu ya zile za wanaume:
haki za kutoa ushahidi mahakamani (Sura 2:282) haki za mirathi (Sura 4:11)
Mwanaume aweza kumpiga mkewe (Sura 4:34) Mwanaume aweza kuoa wake hadi wanne kwa wakati mmoja (Sura 4:3) Waislam lazima wapigane mpaka wapinzani wao wajisalimishe kwenye uislam (Sura 9:5) Muislam asiwe na rafiki Myahudi wala Mkristo (Sura 5:54) Mtu anayeasi uislamu lazima auawe (Sura 9:12) Wizi huadhibiwa kwa kukata mikono (Sura 5:41) Ugoni huadhibiwa kwa kupigwa mijeredi hadharani (Sura 24:2) Hakuna utengano kati ya kanisa [dini] na serikali. (Sura 2:193) Hakuna upinzani utakaoruhusiwa hata kidogo (Sura 4:59)
Mwamerika mwenzangu mwenye asili ya Kiafrika
Kwa kusema kuwa uislam ni dini ya mtu mweusi, wakereketwa wa uislam wanaonyesha tu chuki yao halisi na ubaguzi wa rangi. Usiliache hili likakurubuni.
Waislam hawajali rangi ya ngozi yako, wanatumia usemi huo tu ili wapate kukuteka. Maana kama Waislam wangelikuwa wanajali watu weusi, kwa nini Waislam weusi wanawateka ndugu zao Wakristo weusi huko Sudan siku hizi, wakiwachinja wanyonge na kuwauza wenye afya kama watumwa (angalia taarifa ya Idara ya Taifa [State Dept]: Habari za Mtandao wa Kimataifa; Mei 26, 1993).
Zingatia, upande mwingine, kuwa Yesu Kristo alikuja kutupa uzima wa milele, ambapo kila mmoja ni sawa mbele za Mungu.
"Hapana Myahudi wala Myunani. Hakuna mtumwa wala aliyehuru. Hakuna mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu" (Wagalatia 3:28).
Tofauti kati ya mafundisho ya kiislam na mafundisho ya Yesu Kristo ni kubwa. Uchaguzi uko wazi, na uchaguzi huu ni wako mwenyewe.
IJUE KWELI
IFUATE KWELI
ISAMBAZE KWELI

JE, MOHAMMAD ALITABIRIWA KWENYE AGANO JIPYA KAMA MSAIDIZI AU ROHO MTAKATIFU, KAMA AMBAVYO BAADHI YA WAISLAM WANADAI?

No automatic alt text available.Kwenye Yohana 14:16-26; 15:26; 16:5-15,
Je Muhammad alitabiriwa kwenye Agano Jipya kama Msaidizi au Roho Mtakatifu, kama ambavyo baadhi ya Waislam wanadai?
Jibu: Hapana. Kama jambo hili lingekuwa kweli, basi Waislam wangeamini mambo haya matano (ambayo hawayaamini)
1. Muhammad alimtukuza Yesu. (Yohana 16:14)
2. Mungu alimtuma Muhammad kwa jina la Yesu. (Yohana 14:26)
3. Muhammad alikuwa ametumwa na Yesu pia. (Yohana 16:7)
4. Muhammad alitwaa hekima ya Yesu na kuifanya ifahamike kwetu. (Yohana 16:15)
5. Muhammad alikuwa "ndani ya" mitume. (Yohana 16:17)
Kwa hiyo, hakuna Muislam mwenye ueleo wa mambo atakayeamini kuwa mistari hii inamuongelea Muhammad. Mistari hii lazima iwe inamwogelea mtu mwingine aliyetumwa na Mungu.
Kwa upande mwingine, pengine Waislam wanapaswa kumtukuza Yesu, kama wanadhani kuwa Muhammad alifanya hivyo, kulingana na mistari hii.
Kama wazo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) naye alizungumzia jinsi ambavyo Msaidizi kwenye Yohana 14-16 ni Mungu Roho Mtakatifu kwenye Disputation with Manes sura ya 34-35 uk.208-209
Tazama When Cultists Ask uk.182-183 na When Critics Ask uk.419-420 kwa maelezo zaidi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds

  BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds. The targets included a Radwan Force training facility used for weapons drills ...

TRENDING NOW