Friday, January 5, 2018

MALAIKA NI WALINZI WAKO


Je, Malaika ni walinzi?
Na kwa kuwa malaika wanafanya kazi kwa niaba ya wanaotafuta ili kuwa watoto wa Mungu, watoto wake wa kiume na wa kike – watu wengi kuuliza kama kuna kiumbe malaika ‘walinzi’. Wakati Petro alipofunguliwa na malaika kutoka katika Gereza (Matendo 12:7-15) na akafika mlango wa nyumba ambayo walikuwemo waamini walio kutania humo; hawakuweza kusadiki kama ni Petro mwenyewe lakini walisema, ni malaika wake’. Lakini kabla ya hapo, Yesu alikuwa amekwishawaambia wafuasi wake kuwa
walio wapole wenye kutii kwa kuamini kama mtoto alivyo.
Wanaomnyenyekea Mungu wapate huduma ya watumishi wake. ‘Kwa kuwa malaika wao siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni’.
(Mathayo 18:10). Hivi ni vielelezo vya muhimu kuonyesha kuwa Mungu humlinda kila mtu kumwokoa anayeteswa na yupo tayari kuwasaidia wote wamchao Wanafunzi wa Yesu hawa huachwa na mashaka wakati wanaposoma waraka kwa Waebrania.
Sura za mwanzoni zinadhihirisha namna Mungu alivyokuwa akiwasiliana na watu, jinsi gani malaika walivyowatumishi wake na kwa namna Yesu ambaye ni Mwana wa Mungu amefanyika bora kuliko malaika na kustahili kupewa heshima na wao. Vile vile wale wote wanaofanyika wana wa Mungu na hasa wale watakaoingia katika ufalme na kuwa wafalme katika ufalme wa Mungu ule ujao watakuwa wakuu kuliko malaika.
Katika sura ya 1 mwandishi anasema kwamba Mungu ambaye alisema zamani kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi (Kwa mfano, kwa njia ya malaika waliopokea neno toka kwa Mungu na kulipeleka kwa mababu na manabii). Lakini kwa sasa anasema moja kwa moja katika mwana wake, ‘ambaye ni chapa ya nafsi yake Mungu akiwa amefanyika bora kupita Malaika kwa kadri ya jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko wao’ Mwana ni mkuu kupita Watumishi. Hata sasa mwandishi anasema, malaika
wanaendelea kufanya kazi zao.
‘Na kwa habari za malaika asema, Afanye malaika wake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa miali ya moto….Je! hao wote si roho watumikio wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? (Waebrania 1:7,14,UV)
Hii ilikuwa habari isiyo ya kawaida kwa kuwa Mariamu alikuwa hajaolewa. Hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu! Yusufu, mmewe mtarajiwa, naye pia alipokea ujumbe wa malaika uliomsihi namna ya kufanya kulingana na tukio hili la kipekee.
Wakati Yesu alipozaliwa Bethlehemu, ishara ya kuzaliwa kwake ilikuwa ishara ya uthibishto wa utukufu wa Mungu ulioonekana kwa wachungaji:
"Malaika wa Bwana (yawezekana kuwa Gabrieli?) aliwatokea na utukufu wa Bwna ukawang’arizia pande zote, wake ukiwa na hofu kuu Mara walikuwepo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbiguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia (Luka 2:9-14 U.V)
Shalom
USIKOSE SOMO LA "MALAIKA MWENYE NGUVU NYINGI"

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW