Friday, January 5, 2018

JE, UNAMFAMU MALAIKA ANAYEWEZA KUFUNGUA MILANGO?


Matendo ya Mitume 5: 19 “lakini Malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,”

Huyu Malaika ameenda mpaka gerezani akawatoa watu wa Mungu gerezani. Tunajifunza wakati wa kwenye maombi unaweza kumtuma malaika huyu aende akafungue milango ya biashara iliyofunga, ndoa illiyofunga, kazi, milango ya kupata kiwanja, milango ya kupata visa, milango ya promotion iliyofunga na akaenda kufungua milango uliokwama kwa damu ya Yesu. Watu wa duniani kwenye Ufalme wao huenda kwa waganga wa kienyeji lakini sisi Mungu wa Ufalme wetu anazo nguvu nyingi kuliko mungu wao na tunaweza kutenda mambo makubwa kuliko wao.

Unapowatumia Malaika fahamu kwamba wana lugha zao ambazo ni Biblia(katiba) ambayo ni Neno la Mungu na kunena kwa lugha(lugha ya Ufalme), unapomtuma Malaika uwe unataja sheria inayomhusu kwenye Biblia na uombe.

Mfano Unatakiwa useme:-
“Baba Mungu katika jina la Yesu imeandikwa kwenye sheria ya Matendo ya Mitume 5:19 sheria ya kumtuma Malaika mwenye uwezo wa kufungua milango yeye aliyeifungua milango ya gereza la akina Paulo aende akafungue mlango ya magonjwa ulionishikilia, biashara yangu iliyofunga, milango ya safari iliyofunga ifunguke kwa jina la Yesu Amina.” Unaomba na kutaja maeneo uliyofungwa na Fahamu kuwa Malaika huyu atatenda sawasawa na maneno yako.

USIKOSE SOMO LA "SHERIA YA MALAIKA WA KUTOROSHA GEREZANI"

Shalom

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW