Tuesday, December 3, 2013

KATIKA SIKU YA PILI YA MKUTANO MKUBWA WA KIHISTORIA TANGA NA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA

WATU ZAIDI YA KUMI WATOA USHUHUDA WA KUOKOLEWA KUTOKA MSUKULENI


Katika siku ya pili ya Mkutano Mkubwa wa kutokea katika mkoa wa Tanga kumekuwa na matendo makuu na maajbu ambayo Mungu ameyatenda kupitia kwa Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, wa Kanisa la Glory of Christ (T)  Church- Ufufuo na Uzima.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea maelfu ya watu katika uwanja wa Tangamano.

Wakati wa maombezi maelfu ya watu walikuwa wanafunguliwa kwa jinsi ya ajabu kwa jina la Yesu, kutoka katika vifungo vya shetani.

Roho wa Mungu akiendelea kuwafungua watu wa Mungu

Mchungaji Gwajima akiwabariki na kuwawekea ulinzi maelfu ya watu ili wasichukuliwe au kudhuriwa tena na shetani kwa Jina la Yesu
HALIMA ALLY
Anatoa ushuhuda wake na kuelezea kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na Bibi mmoja aitwaye  Nyatanga ambaye ni mchawi, na alikuwa amemuweka kwenye shimo kubwa jeusi.
Halima aliendelea kuelezea akiwa na machungu sana huku akilia kutokana na mateso makali na mambo ya kikatili aliyoyaona huko msukuleni, aliuelezea uamti kuwa chakula alichokuwa anakula ni Pumba za mahindi na za mtama...na shughuli yake kubwa ilikuwa ni kutumikishwa mambo ya kichawi na kuwadhuru wanadamu.

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa na HALIMA ALLY akiwa anatoa ushuhuda wake kwa machungu sana huku akibubujikwa na machozi ya kwikwi.

Mama yake mzazi aliweza kuitwa na kujitokeza na akaelezea kuwa mtoto wake alikuwa hana maendeleo mazuri shuleni wala nyumbani na alikuwa hajui hasa chanzo ni nini.

Mama yake Halima alitoa kauli nzito za kulaani vitendo vya kichawi na akamshukuru sana Mungu kwa kumuokoa mtoto wake kutoka utumwani mwa shetani, na wote wawili walimpokea Yesu na wameahidi kummpa Yesu maisha yao milele yote.

HUSSEIN OMARY
Ni kijana ambaye anaishi Tanga mjini alifika siku ya Pili ya mkutano, maisha yake yalikuwa na mikosi isiyoisha.
Lakini baada ya maombezi ya Mchungaji Josephat Gwajima ikaja kugundulika kuwa nafsi ya  Hussein ilikuwa imechukuliwa msukule kwa njia za kichawi na alikuwa anatumikishwa kulima mashambani huko Bumbuli. 


Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na Hussein Omari mbele ya maelfu ya watu akiwa anatoa ushuhuda wake.

Mama yake Hussein akilia kwa uchungu huku akielezea furaha yake moyoni kwa kummpata tena mwanae wa mwisho Hussein,Pia Hussein akiwa analia kwa furaha kwa kuweza tena kumuona mama yake Mzazi
Hussein akimshukuru Mungu na kuahidi kumkabidhi bwana Yesu maisha yake milele.

Mama yake mzazi Hussein (mwenye nyekundu) na Mama mdogo katikati wakimlaki mtoto wao baada ya kurudishwa kutoka msukuleni.

ENDELEA KUSOMA USHUHUDA HAPA CHINI

UFUFUO NA UZIMA MEGA GOSPEL CRUSADE WITH SENIOR PASTOR JOSEPHAT GWAJIMA

Binti Aliye Angusha Meli ya Mv. Spice Aokolewa na Yesu katika Mkutano wa Ufufuo na Uzima Tanga

BINTI AITWAYE THERESIA AMBAYE ALIKUWA ANATUMIKISHWA NA SHETANI AELEZEA JINSI ALIVYOSHIRIKI KATIKA KUIZAMISHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER KWA NJIA ZA KISHETANI.
Theresia akiombewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ili kumuweka huru kutoka katika kifungo cha kumtumikia shetani, pia alikuwa anamatatizo ya miguu na hapa anaombewa kwa jina la Yesu.

Theresia ni binti aishiye Jijini Tanga na Mama yake mzazi, na siku hii ambayo alifunguliwa kutoka kuzimu kwa shetani alikuwa amekuja kwenye Mkutano wa Injili uliokuwa umeandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima Jijini Tanga na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.

Theresia akiwa analia kwa uchungu punde tu..baada ya kutoka kufunguliwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anamuhakikishia kuwa kwa sasa tayari yuko salama na hatochukuliwa tena...kwa maana kwa Yesu ni salam Daima..

Na baada ya Mchungaji Josephat Gwajima kuanza kuwaombea maelfu ya watu ambao walikuwa mkutanoni wengi walifunguliwa, na waliokuwa katika vifungo vya shetani, na  msukuleni walifunguliwa na kurejeshwa katika hali zao za kawaida.

Mchungaji Kiongzoi Josephat Gwajima akiwa na Binti Theresia pamoja na Mama mzazi wa binti Theresia

Theresia akiwa tayari kuanza kuelezea habari nzima..


ALIFIKAJE KUZIMU 
Siku moja nilikuwa nimetumwa dukani na mama yangu mkubwa, wakati navuka barabara ghafula nikakutana na mtu ana kila kiungo katika mwili wale kikiwa kimoja kimoja , akajitambulisha kwa jina la Lucifer akanipa mkono ila nikakataa, akauchukua mkono wangu kwa nguvu akanikumbatia, nikajikuta chini ya bahari. Akaja mwenyewe  nikaogopa sana akaniambia nimekuchagua kwa sababu nimekuchagua hata kabla hujazaliwa. Kwa sababu una akili sana. 
Theresia akiwa anaelezea ushuhuda wa yale aliyaona katika ulimwengu wa kishetani.
Akaniambia nilipozaliwa aliniwinda sana ila alishindwa kunichukua kwa sababu bibi yangu alikuwa ananiombea sana . Lucifer akaniambia anataka niwe mke wa mtoto wake. Tukafunga ndoa  na baada ya miezi 6 baba yake akaniambia anaweza  kunipa nguvu nyingi sana lakini anataka nimtumikie yeye. Baada ya miaka 6 akanipeleka shemu Fulani ndani ya bahari ya pacific lakini ni chini sana, sehemu hiyo ni mji kama ilivyo miji ya huku.
Tukaingia sehemu Fulani tukamkuta dragon ambae alianza kuongea na Lucifer, nikafunga macho na nikajisikia kujawa na  nguvu sana, akaniambia amenipa nguvu na mamlaka ya kumiliki na kutawala fahamu za wanadamu.

Mama mzazi wa Theresia alianza kulia kwa uchungu sana baada ya kunza kusikia habari hizi za kutisha ambazo mwanae wa kuzaa ameyapitia.


Siku moja niliamka asubuhi nikiwa na njaa sana kwa sababu usiku wake sikula chakula, Lucifer akaniambia kuna meli inaitwa Mv spice nikaenda na baadhi ya watu tukatega nyaya za kopa, ile meli ikawa inakuja tukatega pale maji yanapogawanyikia  ili watu waseme ni mkondo wa maji, kuna maneno nikayasema halafu nikasimama pembeni, ile meli ikaanza kuzama mpaka kwenye kina cha chini kabisa cha bahari ambacho nilitaka mimi, kisha  tukaunganisha mabomba mpaka kule pacific na tukapata damu nyingi sana. Mimi nilikuwa nahitaji kunywa damu kiasi cha tani 5000 kwa siku ili niwze kutena kazi kwa nguvu nyingi.

Theresia akiendelea kuelezea huku mama mzazi akiwa anaendela kusikiliza kwa umakini wakiwa na Mchungai Josephat Gwajima

Pia kazi yetu nyingine ilikuwa kuwafanya watu wanaompenda Mungu waache kabisa na kuanza kuwaza vitu vilivyo tofauti kabisa na mapenzi ya Mungu, na waliuwa wakiifanya kazi hii kwa ku-control akili na fikra za wanadamu, yani utawala mkubwa  wa shetani ni kuzishika na kuzikamata fikra za wanadamu ili watende mambo ya kumchukiza Mungu na kujiondolea neema ya Mungu, na walikuwa na uwezo wa kumfanya binadamu atende jambo lolote baya iwe kuuwa,kulewa kutokwenda kanisani.

ULITOKAJE HUKO?

Monday, December 2, 2013

Malaika Waliofanya Dhambi


Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Roho na kwamba viumbe wake wa kwanza walikuwa roho. (Yohana 4:24; Waebrania 1:13, 14) Isitoshe, Biblia pia inataja kwamba kuna roho waovu. (1 Wakorintho 10:20, 21; Yakobo 2:19) Lakini haifundishi kwamba Mungu ndiye aliyewaumba roho waovu. Basi wao ni nani, na walitokea jinsi gani?

Katika Biblia tunasoma kuwa, kuna Malaika walitenda dhambi na kufukuzwa Mbiguni. Mungu mwenye upendo, alipowaumba viumbe wa roho, viumbe hawa, aliwaumba wakiwa na uhuru wa kuchagua ikiwa watatende mema au mabaya.

Roho wa kwanza kuasi na mwenye sifa mbaya zaidi alikuwa Lucifer ambaye anajulikana sasa kwa jina la Shetani.

Ni nini kilichomchochea Shetani kumwasi Mungu?
Shetani alianza kutamani ibada ambayo ilikuwa hasa ya Muumba-Mungu, kisha akajikweza kutokana na tamaa hiyo na kujifanya kuwa mungu. Isaya 14: 11Fahari yako yote imeshushwa mpaka kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako na minyoo imekufunika. 12Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko! Umetupwa chini duniani, wewe uliyepata kuangusha mataifa! 1 3Ulisema moyoni mwako, “Nitapanda juu hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, ataketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya juu sana vya mlima Mtakatifu.

Biblia inamfafanua Shetani kuwa kiumbe halisi ambaye yuko katika makao ya roho. (Ayubu 1:6) Inatueleza kuhusu sifa zake za ukatili kutia ndani matendo yake ya uovu. (Ayubu 1:13-19; 2:7, 8; 2 Timotheo 2:26) Pia inasimulia mazungumzo kati ya Shetani na Mungu na pia kati yake na Yesu.—Ayubu 1:7-12; Mathayo 4:1-11.

Kiumbe huyo mwovu alitoka wapi? Mungu aliumba viumbe “roho” wanaoitwa malaika. (Ayubu 38:4-7) Wote walikuwa wakamilifu na waadilifu. Hata hivyo, mmoja kati ya malaika hao akaja kuwa Shetani.

Malaika huyo hakuitwa Shetani alipoumbwa kama nilivyo sema hapo mwanzo na/au hakuumbwa akiwa Shetani, kama imani zingine zinavyo sema, bali alikuwa Malaika muadilifu mbele za Mungu. Jina hilo Shetani ni la kumfafanua, na linamaanisha “Mpinzani; Adui; Mshtaki.” Alikuja kuitwa Shetani kwa sababu alichagua kumpinga Mungu.

MAAJABU BINTI ASHUHUDIA KUIANGUSHA MELI YA MV SPICE MKUTANO WA GWAJIMA TANGA




Soma habari hii kama ilivyoandikwa na mwandishi wa kanisa la Ufufuo aliyepo mkoani Tanga.
Ni binti aitwae Theresia (pichani akiwa amekumbatiana na mama yake) alichukuliwa na kuwekwa bahari ya Pacific. Pamoja na mambo yote jambo lililoshangaza watu ni kudai kuwa alihusika katika kuiangusha meli ya MV Spice.

akielezea jinsi alivyofanya binti huyo alisema kuwa walitumwa kutoka baharini na kufanya kazi hiyo. Akiwa na wenzake wanne kati yao yeye akiwa Master Mind, alisema kuwa aliishusha meli hadi kwenye kina kirefu na kukusanya damu za watu.

Binti huyo ambaye alikuwa anaongea lugha ya kingereza mara kwa mara, alisema kuwa pamoja na kuangusha meli hiyo alikuwa na uwezo wa ku control fahamu za watu jambo ambalo walilifanya kwa vijana wengi.

Kilio kilitanda katika familia yake baada ya Theresia kusema kuwa hajawahi kumuona mama yake tangu 2007. Na ya kwamba mama yake alikuwa akiishi kitu kingine na sio yeye. 

Sunday, December 1, 2013

WAISLAM LETENI AYA KUTOKA KORAN AU BIBLIA INAYOSEMA KUWA PAULO HAKUWA MTUME WA MUNGU.

Leo nimeamua kukata ngebe za Wafilisti kuhusu Mtume Paulo ambaye anawanyima usingizi kila siku Waislam na Allah wao. Paulo alikuwa Mtume wa Mungu, hebu tusome Biblia:

Wagalatia 1:1 Paulo, mtume, si mtume wa wanadamu aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu 

Biblia ipo wazi kabisaa, kuwa Paulo alitumwa na Mungu, wakati Muham-mad alitumwa na Jibril ambaye si Mungu. Koran inakiri kuwa Muham-mad alikutana na Jibril na hakuwai kukutana na au ongea na Mungu. Lakini tunasoma katika Biblia kuwa, Paulo alipewa utume na Mungu mwenyewee. 

Warumi 1:1 Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, ALIYEITWA KUWA MTUME na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu

Ningependa kuanzia leo, ieleweke kuwa Waislam wanafuata kanyaboya. Muham-mad hakuwai ongea na Mungu. Muham-mad hakutumwa na Mungu. Muham-mad ni Mtume Bandia asie na hili wale lile.

Mitume wote ambao tunawasoma katika Biblia, waliongea na Mungu moja kwa moja na bila ya kutumia msaada wa Malaika. Lakini Muham-mad anatumia msaada wa Jibril, kiumbe kinacho daiwa kuwa ni Malaika aliye tumwa na Allah. Kwanini Muham-mad ndie mtume pekee anayetumia c/o katika mawasiliano yake na mungu wa Islam? Je, Allah ni Mungu? Kama ni Mungu, mbona anatumia usaidizi katika kuongea na Muham-mad wa Islam? Mbona Mungu wa Biblia hakutumia usaidizi kuongea na Mitume wake? 

Mkishindwa kutuletea aya kutoka Koran au Biblia inayo sema Paulo si Mtume wa Mungu, basi kushindwa kwenu ndio ushaidi tosha kuwa Muham-mad alikuwa Mtume Bandia na Paulo ni Mtume wa Mungu.

Waislam, tuleteeni aya ambayo inasema kuwa Paulo hakuwa Mtume.

Swali limeenda shule hilo

Max Shimba Ministries

MTUME PAULO AENDA UARABUNI BAADA YA KUOKOKA


Kufuatana na kitabu cha Wagalatia, Mtume Paulo baada ya kuokoka alikwenda Uarabuni. Hebu tuisome Biblia kwa ushaidi yakinifu:

Wagalatia1: 17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla 
yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.

Kwanini Mtume Paulo alikwenda Urabauni baada ya kuokoka?

Mtume Paulo alikwenda kufanya nini Uarabuni?

Ndugu Wasomaji, Ukumbi ni wenu kujadili.

Max Shimba Ministries

Saturday, November 30, 2013

Televangelist Paul Crouch, founder of TBN, dies at 79

Source: LA Times

By Elaine Woo 

Paul Crouch, a pioneering televangelist who founded Trinity Broadcasting Network, the world’s largest Christian TV network, died today, according to the network's website. He was 79. 

The church reported in October that Crouch had fallen ill and was taken to a Dallas-area hospital while on a visit to a TBN facility in Colleyville, Texas. He had "heart and related health issues," the church said, and he was later returned to California for continued treatment. 

The son of a Missouri missionary, Crouch moved to California in the early 1960s to manage the movie and television unit of the Assemblies of God. A decade later, after receiving what he believed was a message from God, he began to buy television stations, cable channels and satellites and developed enough Christian programming to sustain a 24-hour network. 

By the mid-1980s, Orange County-based TBN was “the country’s most-watched religious network,” according to J. Gordon Melton and Jon R. Stone in their book “Prime-Time Religion: An Encyclopedia of Religious Broadcasting.” 

Read more: http://www.latimes.com/obituaries/la-televangelist-paul-crouch-who-founded-the-world-famous-trinity-broadcasting-network-dies-at-79-20131130,0,5660860.story 

Friday, November 29, 2013

ALLAH NI MUONGO KUTOKANA NA BIBLIA NA KORAN


Je, Allah na Shetani ni yule yule mmoja?

Katika ujumbe wa leo, nitaweka ushaidi wa Kibiblia na Koran ambao unatuambia kuwa, Allah ambaye ndie mungu wa dini ya Kiislamu ni muongo.

Biblia inasema kuwa MUONGO ni yeyote yule anaye sema Yesu si Kristo na anaye mkana Baba(Jehovah) na Mwana (Yesu).

Hebu tusome kwanza Biblia:
1 Yohana 2:22-26; Je, mwongo ni nani? Mwongo ni yule anayekana kwamba Yesu si Kristo. Mtu huyo ndiye mpinga-Kristo, anayemkana Baba na Mwana. 23 Mtu anayemkana Mwana hawezi kumjua Baba; mtu anayemkiri Mwana anamjua na Baba pia. 24 Hakikisheni kwamba ujumbe mliosikia tangu mwanzo unadumu mioyoni mwenu. Ujumbe huo ukikaa mioyoni mwenu, ninyi pia mtadumu ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Na yeye ametuahidi uzima wa milele. 26 Ninawaandikia mambo haya kuhusu wale wanaojaribu kuwapo tosha.

Biblia inatufundisha kuwa, mwongo ni mtu yeyote yule anaye pinga kuwa Yesu si Kristo, zaidi ya hapo, Biblia inaendelea kutufundisha kuwa mtu anaye mkana Yesu hawezi kumjua Baba yake. Kumbe ndio maana Waislam wanasema kuwa Mungu hawezi kuwa Baba na wala hana Mwana!

Allah wa Koran anamkata Yesu kama Mwana na anakana kuwa Jehovah si Baba wa Yesu. Soma Quran hapa chini.

Quran 19:35. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. 

Katika Surah Maryam hapo juu, Allah anasema kuwa Mwenyezi Mungu hana Mwana, jambo ambalo ni kinyume na aya tuliyo isoma kutoka Biblia kuwa, Muongo ni mtu na au kiumbe chechote kile kinacho pinga kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na anaye mkana Baba yake (1Yohana 2: 22-26). Allah amesha mkana Baba, hivyo basi Allah teyari amenyakuwa sifa ya uongo.

Je, Allah ni Mungo? Hebu tuendelee kusoma Koran. Quran 1539. Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenipotosha na kunitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, 

Katika aya hapo juu, Shetani anasema kuwa, Allah ndiye aliye mpotosha na kumfanya awe mbaya. Kumbe Allah ndie mwanzislishi wa upotoshaji/uongo? Ushaidi zaidi utaupata katia Surah na aya zifuatazo 3:54, 3:54, 7:123, 13:42, 14:46, 16:26, 16:45, 27:50, 40:45, 71:22 impf. act. 6:123, 6:123, 6:124, 8:30, 8:30, 8:30, 10:21, 12:102, 16:127, 27:70, 35:10 n.vb. 7:99, 7:99, 7:123, 10:21, 10:21, 12:31, 13:33, 13:42, 14:46, 14:46, 14:46, 27:50, 27:50, 27:51, 34:33, 35:10, 35:43, 35:43, 71:22 pcple. act. 3:54, 8:30

katika Surat-Nisai 171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu.

Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka.

Allah anasema kwamba watu wa Kitab ambao ni Wakristo wasisema mabaya kuhusu Allah ila, wakiri kuwa Yesu ni Mtume tu na wasiseme kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, wala wasiseme kuwa Kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Allah anaendelea kuonyesha tabia yake ya uongo katika aya hapo juu.

Sasa endelea kusoma Biblia na ufahamu sifa zaidi za muongo.
Yohana 8:44 Ninyi ni watoto wa baba yenu shetani; kwa hiyo mnapenda kufanya maovu kama yeye. Tangu mwanzo yeye alikuwa muuaji na hana uhusiano wo wote na mambo ya kweli; kwa maana hana asili ya kusema lililo kweli. Shetani anapodanga nya anadhihirisha asili yake kwa kuwa yeye ni mwongo na ni baba wa uongo.

Katika aya hapo juu tunafundishwa kuwa, watoto wa Shetani wanapenda kufanya maovu kama baba yao. Ndio maana tunasoma kwenye Koran kuwa, Allah ametoa amri kwa wafuasi wake kuuwa mtu yeyote yule anayekataa kuwa Muislam. Kuuwa ni kufanya maovu, lakini kwa Allah kuuwa ni kufanya jambo jema Quran 2:244, 3:151, 4:74, 4:89, 4:95, 4:104, 5:33, 8:12. 

Allah akatika Surat An Nisaai anatimiza yale yote yaliyo semwa katika Yohana 8:44, ambayo ni adhama zote za Shetani: 

Quran 4 Surat An Nisaai Allah anasema 74. Basi nawapigane katika Njia ya Allah wale ambao wanao uza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Allah kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.

Hii surah ambayo iliteremka Makkah inaonyesha dhahir tabia ya Allah ambayo haina tofauti na Shetani aliye semwa katika Biblia. Yesu anasema jinsi gani Shetani anafanya kazi, na nini hasa hufanya kwa binadamu. Soma Yohana 10:10 Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi nimekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele.

Hiyo ndiyo kazi ya Shetani ambayo tunaiona katika Allah wa Koran. Shetani ni Baba wa Uongo, vivyo hivyo, Allah naye ni Baba wa Uongo katika Uislam. Shetani ni muuaji, vivyo hivyo, Allah nayeye anatoa amri ya kuuwa Makafir wote katika Koran 9:14, 9:20, 9:38-39. Suran 9:14. Piganeni nao, Allah awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.

Ndugu wasomaji, Allah ameonyesha adhama zote za Shetani kuwa ni zake. Mungu huwa hasemi uongo wala achonganishi watu ili wapigane kwa ajili yake. Allah si Mungu.

Nimategemeo yangu kuwa, utafanya utafiti zaidi ili uweze kuona tofauti zilizopo kati ya Mungu wa Biblia na Allah wa Koran.

Katika huduma yake

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Wednesday, November 27, 2013

YESU HAKUWA MUISLAM


USHAIDI WA KIBIBLIA NA KORAN

Waumini wa dini ya Kiislam wamekuwa na tabia ya kuseka kuwa, eti, Yesu alikuwa ni Muislam. Madai haya ya Waislam yamekuwa yakisemwa katika mihadhara yao ya kidini bila ya kuwa na ushaidi yakinifu kusaidia madai yao.
Leo nitajibu madai haya kwa kutumia Biblia na Koran kama ifuatavyo:

YESU HAKUWAI SEMA SHAHADA
Kufuatana na sharia za Kiislam, ili mtu awe Muislam lazima aseme na au afanya shahada. Yesu hakusema SHAHADA (La ilaha illallah) na hakuna ushaidi wa Kibiblia au Koran unao sema kuwa Yesu alisema SHAHADA. Hivyo basi, Yesu hakuwa Muislam.  

YESU HAKUWAI KUMWABUDU ALLAH
Yesu hakuwai kuomba na au kumwabudu “Allah”, lakini kutokana na Biblia, Yesu aliomba kwa Baba yake, Yohana 17:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe. Koran na Uislam unakiri kuwa Allah si Baba na hakuna hata aya moja inayo mwita Allah Baba. Yesu hakuwa Muislam.

YESU HAKUWAI KUOMBA HUKU AKIANGALIA MAKKAH
Yesu hakuwai kusujudu huku akiangalia Makkah, jambo ambalo ni moja ya masharti katika kumwomba na au abudu “ALLAH”. Quran 2:149. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. 150. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka.

Sasa tumsome Yesu katika Biblia, wapi aliangalia wakati akiomba.
Yesu aliomba huku akiangalia Mbinguni soma: Marko 6: 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote. 
Katika aya tuliyo isoma hapo juu, imetupa ushaidi kuwa Yesu aliangalia Juu Mbinguni ambapo Baba yake alipo na si Makkah.

YESU HAKUFUNDISHA KUHUSU KAABA
Yesu hakuwai sema na au fundisha wanafunzi wake kuhusu “KAABA”. Jambo ambalo tunaona linafanywa na Waislam na lilifundishwa na Muhammad mtume wa Allah.

YESU HAKUFUNGA SWAUMU KILA MWAKA
Yesu hakuwa anafunga Ramadhani/Saumu kila mwaka, jambo ambalo ni sehemu ya Uislam kufunga ramadhani kila Mwaka. Quran 2:183, Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.

Hakuna hata sehemu moja katika Biblia ambayo tunasoma kuwa Yesu alitoa amri kwa wafuasi wake kuwa ni lazima wafunge swaumu kila mwaka, lakini tunasoma kuwa Mathayo 6:16-18: Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; 
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 

YESU HAKUFANYA JIHAD
Yesu hakufanya Jihad kama ilivyo amri ya kila Muislam kufanya Jihad. Quran 2:216. Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. Lakini Yesu alisema yafuatayo kuhusu kupigana: Yohana 18: 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 

Katika aya hapo juu, Yesu anatufundisha kuwa Ufalme wake si wa hapa Duniani bali Mbinguni, hivyo basi hawezi kufanya Jihad kama Allah alivyo waamrisha Waislam. Yesu hakuwa Muislam na hakufanya Jihad.

YESU ALISEMA PENDENI ADUI ZENU, WAKATI ALLAH ANASEMA WACHUKIENI WAKRISTO NA WAYAHUDI
Yesu hakuwachukia watu ambao walikuwa wanampinga, lakini aliwapenda na kuwaombea, kinyume na maamrisho ya Allah kwa Waislam wote. Soma Mathayo 5:44.  lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.

Sasa Msome Allah anavyo panda chuki kwa wafuasi wake. Quran 5:51. Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

YESU HAKUFUNDISHA KUPIGA WAZINZI MAWE
Yesu hakupiga watu Mawe na wala hakufundisha kuwa Wazinzi wapigwe Mawe kama ambayo inafundishwa kwenye dini ya Uislam. Msome Yesu hapa: Yohana 8: 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 

Lakini katika Uislam tunamsoma Muhammad akitoa amri ya kupigwa mawe mdhinifu: Volume 2, Kitabu 23, Namba 413:
Alisimulia 'Abdullah bin' Umar:
Myahudi kuleta kwa Mtume Muhammad watu wawili Mwanaume na mwanamke ambao walikamatwa wakifanya uzinzi kinyume cha sheria za ngono. Mtume Muhammad aliamrisha wote wawili wapigwe mawe mpaka kifo, karibu na mahali pa sadaka ya sala ya mazishi iliyopo kando ya msikiti.

Hivyo basi Yesu hakuwa Muislam na hakupiga wazinzi mawe lakini tunamsoma Muhammad akipiga watu mawe na akifundisha kupigwa mawe kwa Wazinzi katika Uislam.

YESU HAKUFUNDISHA WATU WATAWADHE KABLA YA KUOMBA
Yesu hakufanya na au fuata sharia za kuosha na au kutawadha kama ambavyo Waislam wanafanya kila siku. Msome Yesu katika Mathayo 15:2-11. Lakini Allah anafanya mila za kuosha na au kutawadha mwili kabla ya kumwabudu. Quran 5:6. Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.

Yesu hakuwa anatawadha kabla ya kumwomba Baba yake kama ilivyo katika Uislam. Yesu hakuwa Muislam.

YESU HAKUWAI TUMIA MANENO “SAW” AU “PBUH”
Yesu hakuwai waambia watu waandike vifupisho “SAW” na “PBUH” baada ya kutaja majina yao, kinyume chake Allah na Mtume wake wanafundisha kusema hivyo katika Uislam baada ya kutaja majina ya Mitume na Manabii.
Ndugu wasomaji, leo tumemsoma Yesu na tumesoma tabia yake  na mafundisho yake machahe ambayo yote yanapinga sheria na mila za kiislam.
Ni mategemeo yangu kuwa, kijarida hiki kitakusaidia kuelewa kuwa Yesu hakufuata mila za Kiislam na wala hakumwabudu Allah.

Mungu awabairiki sana


Katika Huduma Yake

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

TRENDING NOW