Na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima
Utangulizi:
Wakristo wengi huwa hawazungumzii neno kafara kwasababu wanahisi kuwa ni la waganga wa kienyeji, lakini hili neno limeandikwa kwenye biblia mara nyingi sana. Hii ni kuonyesha kuwa wapo watu wanatoa kafara.
KAFARA KWENYE BIBLIA:
Baada ya Yoshua na wana wa Israeli kuangusha ukuta wa Yeriko, Yoshua aliweka agano kuwa atakayeamua kujenga ukuta ataanza kwa kufiwa na mwanawe wa kwanza na akasema akimaliza atafiwa na mwanae wa pili.Yoshua 6:20-27. Lakini miaka mingi baadaye mtu mmoja akatoa kafara ya wanawe ili aweze kujenga ngome ya Yeriko kwa upya, Kumbe kafara yaweza kutolewa kwa ajili ya kujenga kitu duniani. Imeandikwa katika 1Wafalme 16:38.
2Wafalme 3:20-27, Hapa tunaona habari ya Huyu Mfalme ambaye baada ya kuona anashindwa vita dhidi ya wana wa Israeli, akaamua kumtoa kafara mwanaye na hilo jambo likawa hasira juu ya Israeli na kashinda vita. Kumbe kafara inaweza ikamwezesha mtu kushinda vita. Ukisoma maandiko haya kwa haraka hutoweza kuelewa lakini ukikaa ukatafakari utaona kuna jambo la muhimu sana hapo.
Kafara ya mtu kwenye biblia; 2Wafalme17:17,“Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha” kumpitisha mtoto motoni ni kumchoma moto kama kafara yaani ukisoma biblia ya kingereza inatumia neno “sacrifices “ Ezekieli 16:20-21, kumbe jambo la kafara lipo kwenye biblia,na hapa Ezekieli anasema wakawatoa kafara wanao kuwa chakula; na pia neno hili limeoneka na pia katika kitabu cha Ezekieli 20:31-32.
KWELI KUHUSU KAFARA:
Mtoto au mtu akitolewa kafara anakuwa ameuwawa Mwili na kupewa majini au mashetani, katika biblia shetani anayehusika na mambo ya kafara, Mambo ya Walawi 18:21; ukisoma biblia ya Kiswahili unaweza ukahisi moleki ni mtu lakini tuangalie kwenye biblia ya kingereza “do not give out your children to be sacrifices..” Mambo ya Walawi 20:2 “who sacrifices.. kumbe inawezekana unaumwa na upo kwenye ugonjwa kumbe ndio unatolewa kafara hivyo..
Kumbe sasa waweza kumwona mtu amekufa na ugonjwa Fulani kumbe ni kafara, mwingine anatoa kafara kwa ajili ya utajiri. Mambo ya Walawi 20:3, pia tunaona kuwa kumbe wachawi hawa wanatoa ndugu na si mtu ambaye hamjui. Yaani kama una ndugu wa karibu au wa mbali ambaye ni mchawi, Yule ndiye anayeweza kukutoa kafara, na kwenye kitabu cha Mambo ya walawi shetani aliyekuwa anahusika na kafara aliitwa Moleki. Walawi 20:4,5 2Wafalme 20:10
Hayo maandiko ni ya agano la kale lakini pia katika agano jipya jambo hili limetajwa pia; 2Wakorintho 10:20 “.”
KWANINI WATU WANATOA KAFARA:

















