Kati ya watu wanaowasumbua sana ndugu zetu Waislamu ni shujaa wa Bwana Yesu, Mtume Paulo. Na hii haikuanza kwa Waislamu pekee, bali kuanzia kwa washika torati waliokuwako wakati wake, yaani mafarisayo, wakuu wa makuhani, waandishi pamoja na Wayahudi wa kawaida waliofuata dini ya Kiyahudi.
Waislamu wanaendeleza tu ili roho ya upinzani dhidi ya Injili iokoayo ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo Waislamu wanasema zinawafanya wamkatae Mtume Paulo, kama nilivyozitoa kwenye facebook kwenye post mojawapo ya ndugu mmoja wa Kiislamu.
Wanasema:
MOJA: Eti aliweka amri ya watu wasitahiriwe, ndio maana Wakristo wengi leo wana magovi
JIBU:
Tohara ni suala la afya ya kawaida wala halina uhusiano na kwenda mbinguni. Yaani, ukitaka kufanyiwa tohara, ni faida kwa mwili wako tu na wala sio kwa roho yako. Kinachoenda mbinguni ni mwili na wala sio roho. Mwili uwe umetahiriwa au haujatahiriwa, ukifa ni kuozea tu ardhini. Kwa hiyo, Mungu alilitumia hilo suala la tohara kama ishara ya mambo halisi ya rohoni, na sio ya mwilini:
(Kumb 10:16) Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu.
(Kumb 30:6) BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.
(Yer 4:4) Jitahirini kwa BWANA, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
MBILI: Eti alikuwa gaidi wa kuwaua wanafunzi wa Yesu kisha akadai ni mtume wao ili azidi kuwaua kifkra
JIBU
Hii ni hoja kichekesho. Tangu lini mkawa na huruma na wanafunzi wa Yesu? Mnasemaje kuhusu makundi yenye itikadi kali ambayo yanaua Wakristo duniani hivi leo, yanavunja makanisa na kuwalazimisha kufuata miungu yao? Je, nayo mnayalaani?
Paulo alikuwa muuaji KABLA ya kumjua Kristo kama ambavyo SISI SOTE nasi tulikuwa wenye dhambi kabla ya kumjua Kristo. Na Yesu anasema:
(Luk 5:31-32) Yesu akajibu akawaambia, wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.
Yesu anawaita wenye dhambi ili Yeye ndiye awape mioyo mipya iliyojaa upendo, huruma na msaada kwa wanadamu wengine. Yeye hakuja kumtafuta Paulo asiye na dhambi, maana hakuna Paulo wa hivyo au mwanadamu yeyote wa hivyo.
Kama Paulo alikuwa mwuaji, wa kulalamika alitakiwa awe Kristo Yesu mwenyewe na wala sio wewe uliye na chuki na Paulo.
TATU: Eti ndiye aliyeleta ushoga duniani
JIBU
Huu ni uongo kutoka kwenye shimo la kuzimu. Paulo anasema:
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, (1Kor 6:9)
Jipime mwenyewe kama usemayo ni mambo yanayoingia akilini au la. Unayejidanganya ni wewe mwenyewe wala si mtu mwingine.
NNE : Eti ndiye aliyesema pombe ni dawa ya magonjwa.
JIBU :





.jpg)


