Friday, March 18, 2016

JE KUSALI NA VIATU KATIKA JENGO LA IBADA NI MAKOSA?



Ndugu msomaji,
Ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na sauti zinazopazwa kila kona ya ncha ya dunia toka kwa ndugu na rafiki zetu wapendwa wa Kiislam, wakihoji juu ya kile wanachokiita kuwa ni tendo la Wakristo kupuuzia au kutotii ukweli wa Biblia kwa madai kwamba maandiko matakatifu ya Biblia kupitia agizo fulani lililotolewa kwa nabii Musa yanaelekeza Wakristo kutekeleza matendo yao ya ibada kwa kuvua viatu vyao waingiapo makanisani.
Katika mada hili tutaangazia mambo muhimu yatakayo saidia kutoa mwangaza na majibu ya msingi juu ya hoja hiyo tete.
Mapitio ya mada:-
Chimbuko la hoja hiyo katika Biblia na Qur an.
Farsafa juu ya tukio Musa kuvua viatu / nini kusudi la tukio hilo?
Je’ Musa alivua viatu katika matendo halisi ya ibada katika utumishi wake?
Je’ mtume Muhammad naye alisali na viatu au bila viatu?
Bwana Yesu / Manabii na Mitume katika farsafa ya ibada na kuvaa viatu.
Kwa kuatilia kwa makini vipengele hivyo vya uchambuzi hadi mwisho ni imani yangu kuwa hautabaki kama ulivyo ikiwa u Muislam au ni Mkristo, ninachokusihi ni kufungua moyo wako ili kweli za maandiko zipate nafasi ndani yako.
Uchambuzi wa mada
Hebu sasa bila ya kupoteza muda tuanze kwa kuangalia kipengele namba moja kama vilivyoainishwa katika muongozo wa mapitio ya mada:-
Chimbuko la hoja hiyo katika Biblia na Qur an.
Kuibuka kwa hoja hii chanzo chake ni matokeo ya ndugu zetu na marafiki wa Kiiislam kugeukia matumizi ya Biblia katika harakati zao mbali mbali za uenezi wa Uislam duniani.
Kuanzia kule Durban - Afrika ya kusini’ mwana mihadhara mashuhuri marehemu Ahmed Deedat ndiye mwanzilishi mkuu wa hoja hizi chini ya shirika lake la uenezi wa Uislam IPC – (Islamic Propagation Centre), bwana Deedat ameandika majarida na vitabu vingi vinavyohoji na kukosoa msingi mzima na misimamo wa mafundisho ya teolojia ya Kikristo, ambapo katika kitabu kimojawapo pia ameibua hoja hii juu ya kile anachodai kutokuwepo kwa uhalali wa mtu kuingia kwenye jengo la ibada akiwa na viatu miguuni mwake.
Katika hoja yake hiyo Deedat kama ilivyo wanaharakati wengine wa uenezi wa Uislam hivi leo ananukuu kile anachokiita kuwa ni ushahidi wa katazo hilo la kusali na viatu katika kitabu hiki cha nabii Musa ndani ya Biblia:-
Kutoka 3:4-5
Bwana alipoona kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa’ Musa’ naye akasema mimi hapa. (5) Naye akasema, usikaribie hapa. Vua viatu vyako miguuni mwako, maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Katika maandiko ya kitabu cha msahafu pia maelezo ya kisa hicho cha Musa yamenukuliwa kama tunavyosoma:-
Qur an 20:11
Basi alipofika akaitwa, ewe Musa, bilashaka mimi ndiye Mola wako’ basi vua viatu vyako kwa kuwa wewe huko katika bonde takatifu la tuwa...
Hivyo kupitia maelezo ya maandiko hayo Wanaharakati hao wa uenezi wa dini wamesikika wakifundisha kwa ujasiri kuwa jamii ya Wakristo imepotoka kwa kuingia katika majengo ya ibada na viatu huku wakiacha maelekezo hayo ya Biblia kupitia tukio hilo la Musa maelekezo ambayo kwa mtazamo wao huyaona kuwa ndiyo yanayotoa muongozo wa ibada ya kusali bila ya kuvaa viatu miguuni.
Katika uchambuzi wa mada hii tutaangalia mawazo hayo kwa ulinganifu wa kina ili kuondokana na utata huu uliotawala katika masikio ya watu wengi.
Farsafa juu tukio hilo la Musa kuvua viatu, na je’ nini kusudi lake?
Wazo la wajenga hoja juu ya tukio hilo linaangukia moja kwa moja katika dhana ya fundisho la ibada.
Na kwa kiwango cha usomaji na uchunguzi wao wamejikuta wakihitimisha hoja hiyo kwa kuondoka na wazo hilo kwamba kusudi la andiko hilo lilkuwa ni kuelekeza namna ya kuabudu kwa kutovaa viatu miguuni.
Ukweli halisi
Pamoja na maelezo au niite mapendekezo ya waalimu hao mbalimbali, binafsi kadri ya uchunguzi wa kina nilioufanya ili kuelewa farsafa au muktaza halisi wa tukio hilo, nimegundua kuwa hakuna usahihi au uhalali wowote wa kuhusisha tukio hilo la Musa kuamriwa kuvua viatu machungani ( mlima horebu) na fundisho la mfumo wa ibada makanisani au kwenye majengo mengine ya ibada.
Ili kupata ufumbuzi wa hilo hebu turejee kwanza historia ya maisha ya Musa
Musa alikuwa mtoto wa tatu kati ya watoto wa mzee Amrani na mkewe mcha Mungu aliyeitwa Yokobedi, historia inaonyesha kuwa Musa alizaliwa kwa 593 KK katika bara la Afrika nchini Misri, akiwa mtoto wa miezi mitatu aliokotwa na binti wa Farao na kulelewa katika jumba la kifalme Misri (Matendo 7:20-22).
Musa aliishi katika himaya hiyo ya Kifalme kwa miaka 40’ yaani toka mwaka 593 KK hadi 1553 KK, na baadae alikimbilia Midiani baada ya kumuua Mmisri mmoja aliyemkuta akimpiga Mwebrania alipokuwa ameenda kutazama ndugu zake huko, na huko Midiani aliishi kwa mkwewe Yethro aliyekuwa akifanya kazi ya Ukuhani ambaye ndiye aliyemwolea binti yake mmoja wa mwisho miongoni mwa mabinti 7 aliyeitwa Sipora, Musa aliishi hapo ukweni kwa muda wa miaka 40’ tangu mwaka 1553 KK hadi 1513 KK na ndipo akiwa na umri wa miaka 80’ alitokewa akiwa machungani na kutakiwa kwenda kuwakomboa Israel toka nchi ya Misri (Kutoka 3:1-15).
Mambo machache ya msingi tunajifunza katika historia hiyo ya Musa.
Musa alikwenda kutazama ndugu zake na kukuta Mmisri akimpiga Mwebrania na ndipo akampiga Mmisri yule na kumuua ( Kutoka 2:11).
Kama sehemu ya makimbilio Musa akakimbilia Midiani – ambapo ni mwisho wa magharibi mwa jangwa la Arabu, Ghuba ya Akaba kuingia mkono wan chi ya Sinai kwa mkwewe aliyeitwa ‘ Reueli au Yethro.
Mkwe wa Musa Yethro alikuwa ni kuhani, hivyo Musa aliishi na kuhani kwa miaka “40’.
Mambo ya kiugunduzi
Kadri ya historia ya maisha na mizunguko hiyo ya Musa tunaweza kugundua mambo ya msingi yanayoweza kujenga msingi wa ufumbuzi wa mada hii, lakini kubwa zaidi ni kuwa Musa baada ya kufanya kosa lile la kuua alikimbia na kwenda kuishi kwa kuhani Yethro.
Tendo hilo la Musa kuishi kwa kuhani Yethro’ linatupa msingi wa kuelewa kusudi hasa la Musa kutakiwa kuvua viatu kama lililenga fundisho la mfumo wa ibada au la’_ufumbuzi huo tunaupata kwa kujiuliza maswali yafuatayo;-
Endpo Musa aliishi kwa kuhani’ swali Je’ nini kazi ya kuhani?
Kadri ya Biblia tunagundua kuwa kuhani kazi yake ni:-
- Kusimamia na kuendesha ibada za upatanisho wa dhambi kadri ya mfumo na utaratibu uliowekwa na Mungu katika hekalu la dunia/ kwa kifupi ni msimamizi na mwendeshaji wa ibada.
Hivyo kutokana na jukumu hilo la kuhani tunaweza kupiga picha ifuatayo juu ya maisha ya Musa akiwa kwa kuhani huyo tukilinganisha na tukio la mlima Horebu, kwa kuzingatia mwenendo wa maisha ya makuhani kuwa:-
- Kwa kuishi huko na kuhani’ basi huenda nabii Musa alikuwa akihusishwa au kushiriki katika maisha ya ibada za nyumbani kwa kuhani huyo kwa kuzingatia msimamo wa makuhani katika matendo ya kidini tokea katika ngazi ya familia.
- Kwa hali hiyo kama kuvua viatu ingalikuwa ni sehemu ya mfumo wa ibada basi Musa angekuwa ameshajifunza au kuona kwa kuhani huyo Yethro’ katika ibada za nyumbani na hivyo kusingekuwa na haja ya Mungu kutoa maelekezo tena kwa Musa juu ya kuvua viatu pale Horebu endapo pia kusudi la kuwepo kwake kule porini lingekuwa ni kutekeleza matendo ya ibada.
Lakini pamoja na hoja hizo za msingi bado inapaswa ieleweke kuwa tukio hilo la agizo la kuvua viatu kwa Musa lilitolewa kwa Musa pindi akiwa katika shughuli za kawaida za kimaisha za kuchunga wanyama tena kipindi ambacho bado hakuwa na nafasi yeyote ya utumishi kwakuwa uteuzi wake ulikuwa bado, na kwa hali halisi Musa alikuwa mlimani tena kwenye mapori kwakuwa alikuwa akilisha wanyama na hakuwa kanisani wala katika eneo la mazingira ya kiibada.
Pamoja na hayo kile kinachoonekana kuwachanganya wapendwa wangu na ndugu Waislam ni agizo tu kwa Musa kutakiwa kuvua viatu vyake, na kwa hali hiyo kulichikulia kwamba tendo hilo kuwa ndicho kinapaswa kuwa kielelezo cha mifumo ya ibada zetu za makanisani na katika majengo mengine ya ibada.
Sababu ya kina / kwanini kuvua viatu katika Biblia?
Kile nilichotangulia kusema awali ni swala la uaminifu na moyo wa dhati katika kusoma maandiko, kimsingi Biblia ina majibu kwa kila swali la imani hivyo jukumu letu ni kuichunguza kwa makini tu.
Na katika kufikia kina halisi cha uchunguzi wa neno la Mungu hasa kwa hoja zenye utata kama hii, ni vyema kanuni ya usomaji wa Biblia inayoelekezwa na kitabu cha Mhubiri ikazingatiwa.. rejea:
Mhubiri 7:27
Tazama, asema mhubiri, “mimi nimeyaona hayo kwa kulinganisha na hili, ili kuitafuta jumla.”
Mhubiri anaweka bayana kuwa kanuni ya msingi katika usomaji wa maandiko imejengwa katika mfumo wa kanuni ya kulinganisha maandiko mbalimbali katika harakati za kutafuta fafsiri au maana ya kile ulichosoma, na kwa kutumia kanuni hiyo ya Biblia nitaomba sasa tuungane kusoma nukuu hii ya andiko la kitabu cha nabii Ruthu ili kugundua chimbuko na sababu ya kina juu ya tamaduni hii ya kuvua viatu, na yakuwa ilikuwa na madhumuni gani basi kwa wana wa Israel na hata Mungu amtokee Musa kwa kuanza na agizo hilo hilo la kuvua viatu.
Ruthu 4:7
Basi ilikuwa desturi zamani za kale katika Israel, kwa habari za kukomboa na kubadiliana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israel.
Pamoja na kwamba kinachoshikiliwa zaidi na wajenga hoja ni utakatifu wa eneo kuwa ndiyo sababu iliyofanya Musa kutakiwa kuvua viatu, lakini kile anachoeleza Ruthu ndiyo sababu ya kiasili na kina hasa, kwakuwa kimsingi Biblia kama tutakavyoona mbele bado tena inaonyesha Mungu akiagiza yeye mwenyewe na wakati mwingine kupitia malaika akiwataka manabii na mitume kuvaa viatu vyao katikati ya utakatifu na uwepo wake.
Katika andiko hilo nabii Ruthu anataja mambo kadhaa yanayolengwa au kukusudiwa katika tendo la kuvua viatu kama ifuatavyo:- Ruthu 4:7.
- Ilikuwa ni utekelezaji wa desturi ya zamani katika Israeli
- Ilikuwa ni uthibisho wa utayari wa kazi ya kukomboa au mambo ya rehani.
- Ilikuwa ndiyo ishara ya kuthibitisha mambo katika Israeli
Kwa kile kinachomaanishwa kupitia tendo hilo la kuvua viatu kwa Waisrael kadri ya ufafanuzi wa andiko hilo la Ruthu, utangundua kuwa wale wanaojenga hoja ya kuwalaumu wale wanaoingia katika majengo ya ibada na viatu hivi leo, wanafanya hivyo ikiwa ni matokeo tu ya kutotumia muda wa kutosha kuchunguza mambo kwa kina kabla ya kuibua hoja au mafundisho.
Hivyo kile alichofanya Musa kwa kutii agizo hilo la kuvua viatu ilikuwa ni kuonyesha utayari wake wa kuwa kiongozi wa njia kwa Wana wa Israel katika harakati za kuwakomboa toka katika utumwa wa Farao. Vinginevyo kama dhana kuu ingekuwa ni utakatifu wa eneo basi tungekuwa na swali la kujiuliza kwamba:-
“Kwakuwa nchi yote ilikuwa ni takatifu je’ Musa alihifadhi viatu hivyo wapi?
Au je ni wapi imeandikwa kuwa Musa alikimbia kutoka nje ya ardhi hiyo ya Horebu kwenda kutupa viatu vyake ili kutonajisi utakatifu wa eneo hilo?”
Na kwa msingi huo basi ni bayana kuwa tendo hilo la kuvua viatu lililenga zaidi kupima utayari wa Musa kwaajili ya kupatiwa jukumu hilo la kuwakomboa wana wa Israel kama ambavyo kitabu cha Ruthu kinaeleza kuwa ilikuwa ni uthibisho pia kwa habari ya kukomboa.
Hata hivyo kwajumla tukio lenyewe halikuwa tukio la Musa kuabudu au kufundishwa mfumo wa ibada badala yake kile kinachoonekana hilo lilikuwa ni tukio la kumtawadha nabii Musa kwa jukumu la kukomboa watu wa Mungu.
Tukio kama hilo linaweza kufanana na kile tunachofanya mara kadhaa tunapokamilisha kuchagua viongozi wetu kwa upande wa uongozi wa Serikali..
Jifunze kwa mfano;
Kwa kawaida huwa baada ya kumchangua raisi wa nchi pamoja na taratibu nyingine, huwa anapoapishwa huonekana pia akivalishwa shuka begani na kushikishwa ngao na mkuki na wazee wa jadi kisha kuketi katika kigoda.
Kimsingi tendo hilo ni tendo linalotendwa kwa siku moja tu likiwa na lengo la kutoa kiashiria kuwa huyo aliyeko mbele sasa ni kiongozi wa nchi. Na baada ya hapo kiongozi huyo huvua mavazi hayo na kuendelea na majukumu yake....
Hivyo kile kilichotendeka kwa Musa kama ilivyo kwa tamaduni zetu hizo, ni tukio la kutawadhwa na kuthibitishwa kuwa sasa ni kiongozi wa umma wa Israel na hivyo matukio hayo ya kumthibitisha maana yake inakomea katika eneo husika la tukio hilo... hivyo kwamaana hiyo tendo hilo lisingepaswa kuhusianishwa na mifumo ya kawaida ya ibada.
Je’ Musa alivua viatu katika matendo halisi ya ibada katika utumishi wake?
Hii ni moja ya sehemu muhimu sana katika uchambuzi wa mada hii, katika sehemu hii ndipo pia tunaweza kukaza wazo la msingi juu ya dhumuni hasa la agizo la Musa kuvua viatu kama tulivyokwishaona hapo nyuma, kwakuwa kimsingi kama agizo hilo lililenga mfumo endelevu wa ibada basi niwazi kwamba hatutarajii kuona Mungu huyo huyo akitoa agizo jingine la kumtaka tena Musa kuvaa viatu katika matendo ya ibada.
Lakini hapa ni kinyume, na ndipo pia tunakuwa bayana na kuona ukweli wa uchambuzi tuliofanya hapo nyuma na kuona jinsi ambavyo tukio hilo halikulenga kuelekeza mfumo wa ibada ya kuvua viatu katika majengo yetu.
Matukio ya mbele yote yanayohusu ibada za nabii Musa yanataja jinsi Musa alivyofanya au kuruhusiwa kuyafanya ibada zake akiwa amevaa viatu vyake, na tukio kubwa maarufu zaidi ni lile la ibada ya kwanza ya pasaka katika nchi ya Misri, kumbuka ibada hiyo ndiyo imefanya msingi wa ibada ya leo ya pasaka kupitia kafara ya damu ya Yesu ambayo inaadhimishwa na Wakristo karibu katika makanisa yote. Ibada hii Musa aliambiwa aifanye akiwa amevaa viatu...
Kutoka 12:11-12
Tena mtamla hivi, mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, “mmevaa viatu vyenu miguuni”, na fimbo zenu mikononi mwenu, nanyi mtamla kwa haraka ni pasaka ya Bwana (12) maana nitapita katika nchi ya misri usiku huo.....
Maelezo hayo ya Biblia ni bayana, tena Mungu mwenyewe kwa kinywa chake anamwagiza nabii Musa kuendesha ibada ya pasaka na tena basi ibada hiyo anatakiwa kuifanya yeye na Wana wa Israel wakiwa wamevaa viatu vyao.........
Kwa andiko hilo tungeweza hata kuhitimisha mada hii kwakuwa kila kitu sasa kiko bayana, lakini tunaweza kuendelea kufanya mikazo zaidi ili kwamba ndugu msomaji wangu umalize mashaka yote juu ya hili, na basi kwa kulinganisha agizo lile la kuvua viatu lililodhaniwa kuwa ndiyo fundisho la mfumo wa ibada na tukio hili halisi la ibada tunaweza kujiuliza maswali ya fuatayo:-
- Kama tendo la Musa kuambiwa vua viatu vyako lililenga mambo ya ibada na kumtaka Musa awe akivua viatu katika matendo ya ibada:
Je’ sasa ni Mungu yupi tena anayemtaka Musa kuvaa viatu katika ibada hiyo ya pasaka na tena Mungu huyo akiahidi kupita hapo Misri usiku huo na huku tayari wana wa Israel wakiwa wamevaa viatu vyao?
- Na je’ inaaminisha nini vitabu vyetu vinapomtambulisha Mungu kuwa si mwenye kigeugeu endapo kama maagizo hayo ni ya kujipinga? Rejea; (Qur an 17:77/ Yakobo 1:16-18)
Ndugu msomaji wangu hayo ni maswali ya changamoto na kumsha ufahamu wetu, lakini kama tulivyokwishaona ni kuwa kamwe agizo lile la kuvua viatu halikulenga kuelekeza mfumo wa ibada kwa Wakristo , na badala yake ilikuwa ni tukio la kumtawadha Musa ili kupewa dhamana ya kuwakomboa Israeli toka utumwa wa Farao. (Rejea’ Ruthu 4:7 Basi ilikuwa desturi zamani za kale katika Israel, kwa habari za kukomboa na kubadiliana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israel.)
Nabii Musa akiwa jangwani
Baada ya kutoka Misri chini ya nabii Musa wana wa Israel walikuwa na mikutaniko mbalmbali ya kiibada Jangwani...
Qur an 7:138
Na tukawavusha wana wa Israil baharini ( wakasalimika na balaa za Firauni) na wakawafikia watu waliokuwa wakiabudu masanamu yao. Wakasema “Ewe Musa! Tufanyie waungu na sisi ( yaani masanamu....(Nabii Musa akasema) Hakika ninyi ni watu mufanyao ujinga...........
Matendo 7:38
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani, pamoja na yule malaika aliyemtokea..
Maandiko hayo kimsingi yanaweka bayana juu ya kuwepo kwa matendo ya ibada kwa wana wa Israil baada ya kuvuka bahari ya shamu na kuendelea na msafara jangwani, andiko la Qur an linataja jaribio la watu waasi kuwataka wana wa Israel kujihusisha na ibada ya sanamu tendo linalotajwa na Qur an kuwa lilikataliwa na nabii Musa.
Kwa upande mwingine maandiko ya Biblia nayo yanaonyesha kuwa wana wa Israeli walikuwa katika umoja wa kanisa ambao kimsingi ni umoja wa watu walioitwa kutoka gizani na kujiunganisha pamoja wakimwabudu Mungu.(Greec: Ekllessia)
Habari gani juu ya viatu?
Kumbukumbu 29:4-5
- Lakini Bwana hakuwapa macho ya kuona..
- Name miaka arobaini nimewaongoza jangwani..
- Nguo zenu hazikuchakaa mwilini..
- Viatu vyenu havikuchakaa miguuni mwenu...
Andiko hilo la kumbukumbu linaonyesha muujiza ambao Mungu aliwatendea wana wa Israeli, ambapo miongoni mwa matendo hayo ya miujiza ni tendo la kufanya viatu vya wana wa Israel kutochakaa katika miguu yao, kipindi chote cha miaka arobaini ya jangwani.
Hivyo hoja ya msingi hapo ni kuwa kumbe wana wa Israel wakiwa hapo jangwani bado walikuwa na viatu, swali la msingi ni kuwa:-
je’ ni mahali gani katika maandiko ambapo Mungu aliwalekeza wana wa Israel waingiapo kwenye kanisa la jangwani wawe wanavua viatu hivyo vinavyotajwa?
Na endapo ushahidi huo wa kutakiwa kutovaa viatu hivyo wakati wa ibada basi wale wanaojenga hoja ya kukosoa wanaoingia na viatu hawatakuwa na uhalali wa kujenga hoja hiyo kwakuwa ni hoja isiyo na utetezi wa kimaandiko.
Je’ mtume Muhammad naye alisali na viatu au bila viatu?
Hii ni hoja ya msingi sana katika uchambuzi wote wa mada hii, kwakuwa pamoja na mitazamo yetu juu ya maswala ya kidini lakini tunakubaliana kuwa manabii tunaowaamini kadri ya makundi ya imani zetu ndiyo wanaotoa sura nzima ya kanuni na masharti juu ya mwenendo wa wafuasi katika imani zao hivyo kadri ya vile inavyoaminika kuwa wao hupokea maelekezo kwa Mungu...
Hivyo katika kipengele hiki tutaangalia kwa upana wake juu ya ibada za mtume Muhammad anayeaminiwa na jamii ya ndugu zetu Waislam ili kuona naye anatoa kielelezo gani kitakacho tusaidia kupata suluhisho la utata wa hoja hii katika ulimwengu wetu wa imani.
Maandiko mawili ya msingi katika Qur an ndiyo yatakayotupatia kanuni na njia ya kutafiti hoja hii:-
Qur an 33:21
Bilashaka mnao mfano mwema (riwadha nzuri) kwa mtume wa Mwenyezi Mungu....
Katika andiko hilo la kwanza tunaona kuwa Qur an ikimtaja Muhammad kama ndiye anayepaswa kuwa mfano au kilelezo katika matendo ya kidini na hivyo jamii ya Waislam inapaswa kuiga toka kwake.
Andiko hilo pamoja na mambo mengine linatupatia kibali au uhalali wa kuchunguza ili kuona mwenendo wa ibada za mtume Muhammad mwenyewe ambazo kimsingi ndizo zinapaswa kuigwa na wapendwa wetu Waislam. Hata hivyo ni vyema ieleweke kuwa maandiko ya masahafu wa Qur an hayataji kwa upana mwenendo wa matendo ya ibada ya mtume, lakini yanatoa mwongozo wa kanuni ya kufanya. Hebu soma ayah ii:-
Qur 42:10
Mkihitirafiana katika jambo lolote, rejeeni katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za mtume.
Hivyo njia inayotajwa na andiko hilo ni kutafuta ufumbuzi juu ya hoja yeyote kwa kurejea katika vitabu vilivyo nje ya Qur an vilivyopitishwa kama vitabu halali vya teolojia ya Uislam, vinavyoitwa vitabu vya hadithi.
Hebu sasa tuandalie katika vitabu hivyo vya hadithi kuelewa ukweli huo:-
Nukuu 1’
Book’ Sahih Al-Bukhari (Arabic English – Dr Muhsin Khan – Islamic University, Al Medina Al Munawwra / Al Maktabat Al Salafiat)
Vol 1’ Chapter 24/ (Hadith) no 383’
Narrated Abu Maslama, Sai’id Yazid Al Azid: I asked Anas bin Malik whether the Prophet had ever prayed with His shoes on. He replied “Yes.”
Tafsiri
Imesimuliwa na Abu Maslama, Sai’id Yazid Al Azid; Nilimuuliza Anas bin Malik endapo mtume alishawahi wakati wowote kusali na viatu vyake. Akajibu“ Ndiyo.”
Simulizi hiyo isiyo na maneno mengi inaweka bayana juu ya namna mtume Muhammad alivyoendesha ibada zake za swala, na yakuwa kumbe Muhammad mwenyewe aliabudu na viatu vyake na hakuwa akivua viatu wakati wa ibada.
Hebu tuone nukuu nyingine:
Book’ Sahih Al-Bukhari (Arabic English – Dr Muhsin Khan – Islamic University, Al Medina Al Munawwra / Al Maktabat Al Salafiat)
Vol 1’ Chapter 25/ (Hadith) no 384 / 385
(384)Narrated Ibrahim: Hammam bin Al Harith said, “I saw Jarir bin ‘Abdullah urinating. Then he performed ablution and passed his (wet) hands over his Khuffs, stood up and prayed. He was asked abaut it. He replied that he had seen the Prophet doing the same.”
Tafsiri
Imesimuliwa na Ibrahimu; Hammam bin Al Harith alisema, nilimuona Jarir bin‘ Abdallah akiungana na wengine na kisha akatawadha na kupitisha mkono uliolowa maji juu ya viatu vyake, kisha akasimama na kuswali. Alipoulizwa juu ya hilo. Alijibu kwamba alimuona mtume akifanya kitendo kama hicho”.....
(385)Narrated Al –Mughira bin Shu’ba: Ihelped the Prophet in perfoming ablusion and passed his wet hands over his kuhuffs and prayed.
Tafsiri
Imesimuliwa na Al – Mughira bin Shu’ba: nilimsaidia mtume katika kutawadha na ndipo akapitisha mikono yake iliyoloana juu ya viatu vyake na kusali.
Kwajumla haditi zote hizo zinazotambuliwa na kukubalika katika teolojia ya Uislam, zinaweka wazi juu ya hali halisi ya mfumo wa ibada wa mtume Muhammad kuwa desturi yake ilikuwa ni kusali akiwa na aina hiyo ya viatu vyake vinavyotambuliwa kama Khuffu’ hivyo hoja hiyo iko bayana kabisa.
Bwana Yesu / Manabii na Mitume katika farsafa ya ibada na kuvaa viatu.
Nikualike ndugu msomaji wangu tunapolekea ukingoni mwa achambuzi wa mada hii baada ya kujipatia majibu ya msingi juu ya hoja hii ya kusali au kutokusali na viatu.
Katika sehemu hii ya mwisho tutapitia kwa kifupi ili kuona jinsi mitume na manabii walivyotenda huko nyuma kwa habari ya matendo mbalimbali ya kidini na swala hili la uvaaji wa viatu, hii ikiwa ni pamoja na kujibu hoja ya msingi inayohusiana na dhana kwamba huenda panapokuwepo utakatifu basi viatu havipaswi kuwepo.
Hebu kabla hatujaenda mbali turejee kidogo kuangalia matukio machache ya manabii katika uhusiano na swala la uvaa wa viatu.
Ezekieli 24:17
Ugua lakini si kwa sauti ya kusikiwa, usifanye matanga kwaajili yake aliyekufa; jipige kilemba chako; ukavae viatu vyako.....
Katika andiko hilo nabii Ezekieli anaelekezwa na Mungu juu ya kanuni sahihi ya ibada na hapo hoja kuu ilikuwa ni juu ya ibada ya maombolezo, katika maelekezo yake kwa Ezekiel Mungu ana ainisha yaliyo sahihi kufanyika katika ibada hiyo ya maombolezo nay ale yasiyopaswa kufanyika..
Yaliyokatazwa:
- Ugua lakini si kwa sauti ya kusikiwa
- Usifanye matanga kwaajili ya aliyekufa
Yaliyoruhusiwa”
- Jipige kilemba chako ( hiyo ni kadri ya desturi ya Kiyahudi)
- Kavae viatu vyako..
Hivyo kadri ya andiko hilo Mungu mwenyewe ndiye anayetoa maelekezo kwa Ezekieli kumkumbusha kuvaa viatu vyake katika ibada hiyo ya maombolezo, na maelekezo hayo yalifuatia baada ya kumjulisha yasiyopaswa kufanywa katika ibada hiyo ya maombolezo, na hivyo basi tendo la kuvaa viatu linaangukia katika upande ule wa matendo yaliyoruhusiwa kufanywa wakati wa ibada hiyo ya maombolezo, hivyo hakukuwa na shida yeyote ya swala la uvaaji wa viatu mbali na tukio tu la Musa lililolenga kumtawadha kuwa kiongozi wa Israel
Kisa kingine katika Biblia ni kile kinachomhusu nabii Isaya ambaye aliagizwa kutembea akiwa hana viatu tena uchi, ikiwa ni tukio la kidini la kuonya juu ya uovu wa wanadamu na ugumu wao wa kuamini na kutubu, tendo hilo lililohusisha pamoja na kutembea uchi lakini Isaya kutotakiwa kuvaa viatu linatajwa na Biblia kuwa ni tendo la Ishara ya ajabu. ( rejea Isaya 20:3)
Je” eneo lenye utakatifu viatu haviruhusiwi?
Hii ni hoja ya msingi kuiangalia walau kwa kifupi, sababu ya kuangalia hoja hii pamoja na mambo mengine lakini ni tendo la kigezo hiki kuchukuliwa kama ndiyo sababu kuu ya kukaza madai ya kuvua viatu wakati wa ibada.
Lakini katika sehemu hii tutaona kisa kimoja tu kinachotoa jibu zima la hoja hii nacho ni kile kinachohusu tukio la Petro gerezani; hebu tuone kwa kifupi:-
Matendo 12:5-9
- Petro alikuwa amefungwa gerezani..
- Kanisa lilikuwa likomba kwaajili yake..
- Malaika alitumwa kumtoa Petro gerezani..
- Ndipo chumba cha Petro “kikajaa nuru kutoka mbunguni”....
- Akiwa katika nuru hiyo (takatifu) ya mbinguni, Malaika akamwamuru avae viatu vyake kisha amfuate....
Kisa hicho cha Petro kinajibu hoja hiyo bila ya kuacha swali lolote, kadri ya kisa hicho Biblia inaweka wazi kuwa mara Malaika alipoingia tu kwenye chumba cha gereza ndipo nuru ikafurika mle mchumbani, na jambo la kushangaza ni tendo la Malaika katikati ya nuru hiyo anamwagiza Petro kuvaa viatu vyake’ yaani maana yake ni kuwa Petro alivaa viatu hivyo huki akizungukwa na nuru hiyo takatifu aliyokuja nayo Malaika toka mbinguni.
Hivyo hiyo ni kumaanisha kuwa hapakuwa na tatizo lolote juu ya uwepo wa viatu katika nuru hiyo takatifu ya mbinguni iliyofurika katika chumba hicho cha gereza, na kubwa zaidi ni tamko la Malaika lililomtaka Petro kumfuata mara baada ya kumaliza zoezi la kuvaa viatu yaani kwa lugha nyingine ni kuwa Malaika bado aliendelea kumtaka Petro kudumu katika mafuriko ya nuru hiyo akiwa na viatu vyake kwa tendo hilo la kudumu kuambatana naye hadi nje ya gereza hilo.Wito wangu kwa watu wa Mungu bado ni kuwasisitiza kusoma maandiko kwa usahihi, ili kuepuka kuwaondoa wengine kwenye hali ya Mungu.
Kwa ushahidi huo ni wazi hakuna tatizo kuingia na viatu mahala penye utakatifu.
JE, YESU ALIVUA VIATU ALIPO INGIA KWENYE MAHEKALU?
Hakuna ushahidi wa Yesu kuvua viatu katika majengo ya ibada.
Biblia inaonyesha kuwa Yesu alikuwa akivaa viatu na hakuna mahali alipovua viatu hivyo ili kutekeleza kwanza matendo ya ibada, ni vyema ikiwa ni mkristo au hata kama ni Muislam kuzingatia kuwa hoja yoyote unayojenga ikiwa ina lengo la kutaka kuonyesha mapungufu ya Wakristo katika utekelezaji wa maamrisho ya kidini, lazima kwanza hoja hiyo iwe na vyanzo vya kimandiko ikihusisha maelekezo ya kiongozi mkuu wa Ukristo yaani Bwana Yesu mwenyewe.
Rejea; Qur an 5:47
Watu wa injili wahukumu kwa yale aliyotelemsha Mwenyezi Mungu ndani yake, na wasiohukumu kwa (kufuata) yale aliyotelemsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio maasi.
Andiko hilo la Qur an linaweka bayana kuwa hukumu zozote dhini ya watu wa Injli zinapaswa kutokana na msingi wa Injili yenyewe, hivyo hii ni kumaanisha kuwa kama swala la kusali na viatu lingekuwa linapingana na msingi wowote wa mafundisho ya Injili ya Yesu basi hoja hiyo ya kusali na viatu ingekuwa sahihi na yenye nguvu.
Hivyo hii ni tofauti na wale wanaohoji leo kuonekana kutokuwa na kipengele chochote cha kusonda jamii ya Wakristo katika hoja hii kuwa kwa tendo la kusali na viatu wamekiuka kanuni Fulani zilizoamriwa na maandiko hayo.
Lakini badala yake tunaona Yesu mwenyewe akiwa na viatu ambavyo hakuna kifungu cha maandiko kinachoonyesha kuwa aliwahi kuvua viatu hivyo kwaajili ya kutekeleza ibada;
Matendo 13:25....Siwezi kulegeza viatu vya miguu yake...
Hitimisho:Nichukue fursa hii mpendwa msomaji wangu kukushukuru kwa kutumia muda wako kufuatilia uchambuzi huu, ni wito wangu endapo hapo nyuma uliyumbishwa kiufahamu juu ya hoja hii sasa usimame imara, na kama huenda hukuwahi kuwa Mkristo na huenda hoja hii ilichangia kusitisha maamuzi yako sasa fungua moyo wako umpokee Yesu.
Biblia inamaliza kwa kusema:
Yeremia 2:25: Zuia mguu wako usikose kiatu......
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 18, 2016

Thursday, March 17, 2016

MUHAMMAD AKIRI KUWA BABA YAKE YUPO MOTONI

Ndugu msomaji,
Huu ni MSIBA MKUBWA sana kwa Waislam. Muhammad ambaye baba yake anaitwa Abdullah ikimaanisha "mtumwa wa Allah" imethibitshwa kuwa yupo Jehanna/motoni akichomeka.
Haya si maneno yangu na wala mimi simsingizii baba ya Muhammad, bali haya ni maneno ya Muhammad.
Soma uthibitisho hapa.
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeuka kuondoka, akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni. (Sahih Muslim, Kitabu 001, Namba 0398).
Na swali ambalo tungependa wajiulize Waislam ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
ZAIDI YA HAPO,
1. Kwanini Muhammad anakiri kuwa baba yake yupo Motoni?
2. Je, huyu Abdullah/abdallah alipata wapi hili jina lenye Allah ndani yake?
3. Je, inamaanisha kuwa Allah ambaye ni mungu wa kipagani alikuwepo kabla ya Muhammad?
Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).
Tunaambiwa kwamba:
Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Quraish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).
Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:
….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).
Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, ….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).
Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).
Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).
… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).
…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).
…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).
Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.
Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.
Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba.
Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."
Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.
Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?
Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.
Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.
Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?
Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).
Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!
Kumbe basi Kaaba ni nyumba ya kipagani.
Kumbe basi baba yake Muhammad yupo Motoni.
Kumbe basi Waislam wote wanao enda kuhiji wataingia motoni.
Kumbe basi Allah ni mungu wa kipagani.
Hakika Uislam ni dini ya wapagani ndio maana Muhamamd alikiri kuwa baba yake yupo motoni.
Nawakaribisha kwa Mungu Mkuu aliye hai, YESU MWOKOZI WETU.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 17, 2016

Saturday, March 12, 2016

KUMBE ADAM NA HAWA WALITUMIA LUGHA YA KIEBRANIA NA SIO KIARABU

Ndugu msomaji,
Katika somo letu hili, tutajifunza na kujibu swali kuhusu; ni lugha ipi Adam na Hawa walitumia wakati wakiwa katika Bustani ya Edeni?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Adam na Hawa walitumia Kiebrania kwasababu ya majina mawili ambayo Adam alimpa Hawa ambayo yanaweza kuwa yakinifu pekee katika lugha ya Kiebrania. Adam alimuita Hawa jina la “ISHA” ikiwa na maana ya MWANAMKE kwasabau ya kuwa alitoka kwa “ISH” ikiwa na maana ya MWANAUME , zaidi ya hapo, Adam alimuita mkewe “CHAVA” [HAWA] ikiwa na maana ya mama wa watu wote “CHAI” [UHAI].
Zaidi ya hapo, jina la ADAM linatokana na neno la Kiebrania “ADAMAH” likimaanisha “udongo”, hili jina linathibitisha kuwa Mungu alimuumba Adam kutoka kwenye udongo, kama ambavyo Biblia inasema katika Kitabu cha Mwanzo Mlango 2 na aya ya 7. Hivyo basi, tokea wakati wa Adam na Hawa mpaka wakati wa Mnara wa Babeli, watu wote walitumia lugha ya Kiebrania. Bereshet 2:23, 3:20, Midrash Bereshet Rabbah 38
Wasomi wa Kiyahudi na wa Kikristo wanaendelea kuthibitsiha kuwa Lugha ya Kiebrania ndio ilikuwa lugha ya kwanza, na majadiliano makali yalifanywa zamani na watafiti kama Dante Alighierl (1265-3121), Guillaume Postel (1510-1581) Claude Duret (1570-1611), Etienne Guichard (wakati huo huo wa ATHANASIUS Kircher (1602-1680) na Franciscus Mercurius van Helmont (1614-1698) wana sema kuwa, lugha ya Kiebrania ndio ilitumika na Adam na Hawa. Kwa mfano Mtaalam Guichard alisema kuwa neno la Kilatini “divider” likimaanisha tenganisha au kutenganisha limetokana na neno la Kiebrania la “batar” likimaanisha kukata katika sehemu mbili, hili neno lilifanana na la “tarab” ambalo lilikuja neno la Kilatini la “tribus” likimaanisha “kabila “tribe”
Hebu tuangalie ushahid mchache kutoka Biblia:
Matendo ya Mitume 26:14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya KIEBRANIA, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
Yohana 19: 17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa KIEBRANIA, Golgotha.
Matendo ya Mitume 22: 2 Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema,
Kutoka 2:6 Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.
Katika kitabu cha Kutoka hapo juu, tunajifunza kuwa MUSA ANAITWA MTOTO WA KIEBRANIA “Eevriym in Hebrew” na katika kipindi chote watoto wa Kiisraeli waliitwa kama WAEBRANIA ambao ni watoto au wajukuu wa Ibrahim na Musa. Soma Mwanzo 10:24. Zaidi ya hapo, katika kitabu cha Mwanzo 14:13 tunasoma kuwa Ibrahim anaitwa Muebrania (Eevriy in Hebrew).
Huu ni ushahid tosha kuwa Lugha ya Mungu kwa Adam na Hawa ilikuwa ni Kiebrania na sio Kiarabu au lugha nyengine.
Je, Kwanini Mungu alitumia Kiebrani alipo zungumza na Adm na Hawa?
Kwanini Adam na Hawa walitumia Kiebrania walipo kuwa katika Bustani ya Edeni?
Hapa pana hitaji ufunuo wa hali ya kuu kufahamu kwanini Mungu alitumia lugha ya Kiebrania ambayo ni tofauti kabisa na Allah anaye tumia Kiarabu tu.
Kumbe sababu za Allah kutumia Kiarabu ni kupinga Mungu wa Biblia ambaye alitumia Kiebrani na kuwapinga Waisraeli ambao waliitwa wana wa KIEBRANIA.
References:
1. Merrill F. Unger, "Tower of Babel," Unger's Bible Dictionary, 1977 ed.: 115. (BCE - Before the Common Era, equivalent to BC)
2. J.I. Packer, Merril C. Tenney, William White, Jr., Nelson's Illustrated Encyclopedia of Bible Facts (Nashville: Thomas Nelson, 1995) 337.
3. Madelene S. Miller and J. Lane Miller, "Sumer," Harper's Bible Dictionary, 1973 ed.: 710.
4. Unger, "Scythian," 987.
5. Unger, "Egypt," 288.
6. William Smith, "Hebrew Language," Smith's Bible Dictionary, 1948 ed.: 238.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 12, 2016

DINI NA MADHEHEBU NI MZIGO USIO WA LAZIMA


MAANA YA DINI
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford: 2004) inaeleza neno ‘dini’ kama mfumo fulani wa imani inayohusiana na mambo ya kiroho na njia ya kuabudu, kusali au kuheshimu/kutii Muumba.

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa kifupi kwamba, dini ni utaratibu anaotumia mwanadamu katika kumwabudu Mungu.

Zipo dini mbalimbali duniani. Japokuwa zote zinaweza kusema zinamwabudu Mungu aliyeumba vitu vyote, lakini kile kinachozitofautisha ni “utaratibu” zinazotumia katika huko kumwabudu Mungu – ndiyo sababu zikawa ni dini au madhehebu mbalimbali.

Utaratibu maana yake ni kanuni mahususi zinazotakiwa kufuatwa katika kufanya jambo fulani. Mathalani, unapotaka kujiunga na chuo, utatakiwa kulipa gharama za usajili, kujaza fomu, kufanya hivyo katika muda maalum, kuwasilisha maombi yako kwenye ofisi maalum, nk. Hali kadhalika kwa upande wa dini, ili muumini ahesabike kuwa ametekeleza ibada kwa Mungu, upo utaratibu au kanuni mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa. Kanuni hizo ni pamoja na:
Kusema sala maalum;
Kusema sala mara idadi maalum;
Kusimama au kukaa kwa wakati maalum;
Kuvaa mavazi maalum;
Kutazama welekeo maalum; n.k.

YESU ALIANZISHA DINI GANI?
Ukisoma Biblia kwa makini, utagundua kwamba Yesu Kristo hakuanzisha Ukristo kama dini au madhehebu. Wakati Bwana Yesu alipokuja, kulikuwa na dini ya Kiyahudi (Judaism). Hii ni dini ambayo ilikuwa na utaratibu wake wa kumwabudu Mungu kama ilivyo kawaida ya dini yoyote kuwa na utaratibu.

Lakini ni wazi kwamba, Bwana Yesu hakukubalika kabisa ndani ya dini hii. Walikuwa ni wakuu wa dini hiyohiyo ndio waliomshitaki Bwana na kuwachochoea watu wa kawaida waanze kupiga kelele za kusema: asulubiwe, asulubiwe! Kati ya mashtaka yao, walisema: Sisi tulimsikia akisema, Mimi nitalivunja hekalu hili lililofanyika kwa mikono, na katika siku tatu nitajenga jingine lisilofanyika kwa mikono. (Mk. 14:58).

Lakini ni kwa nini walikuwa hawamtaki? Ni kwa sababu alikuwa anaonekana anavunja utaratibu wa dini. Pia ni kwa sababu alionekana kujizolea umaarufu mwingi kuliko wakuu wa dini. Kwa hiyo, waliona kwamba nafasi zao ziko hatarini. Kwa hiyo, walimchukia na kumtungia hila nyingi ili waweze kupata sababu ya kumwua.

Tunaona jambo hilohilo hata baadaye katika huduma ya mtume Paulo. Kabla ya kuokoka, Paulo alikuwa ni mshika dini ya Kiyahudi. Yeye mwenyewe anasema kwamba: Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu. (Gal. 1:14).

Lakini pale alipoitwa na Bwana Yesu kwenye huduma, mambo yaligeuka kabisa. Wayahudi walitafuta kumwua Paulo kwa sababu waliona kwamba tayari yuko kinyume na dini yao. Mathalani, Paulo alipokuwa ameshikiliwa na utawala wa Kirumi, mjomba wa Paulo alienda kumwambia jemadari wa Kirumi kwamba: ...Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi. Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hata watakapomwua; nao sasa wako tayari wakitazamia ahadi kwako. (Mdo. 23:20-21).

Na ndiyo maana baadaye Paulo anasema: Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumwa wa Kristo. (Gal. 1:10).

Hapa Paulo anamaanisha kwamba, kabla ya kumjua Kristo alikuwa ni mshika dini tu ambapo wakati huo uhusiano wake na washika dini ulikuwa wa amani kabisa. Lakini baada ya kuachana na dini, ndio maana wakamchukia. Na anasema sasa, kama angekuwa bado anawapendeza wanadamu wale washika dini, basi asingekuwa anateseka hivyo kwa ajili ya Kristo.

Mtume Paulo anaonyesha kwamba kutoka kwenye dini kwa ajili ya Kristo kuna neema kubwa. Anasema: Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri mataifa habari zake. (Gal. 1:15-16).

Kumbe Mungu anaita dini kuwa ni mapokeo ya mababa (Gal. 1:14). Na kumbe, alipomwita Paulo katika huduma, hakutaka Paulo abakie tena humo ndani ya dini. Na kwa kuwa sasa Paulo alitoka nje ya dini, alijikuta akizalisha maadui wengi sana.

Watu waliokuwa wakimpinga Bwana Yesu na wale waliompinga Paulo hawakuwa wakitetea maslahi ya kisiasa, bali walikuwa wakitetea dini yao.

Friday, March 11, 2016

ALLAH NA UISLAM NI DINI YA WAFU

Ndugu msomaji,
Ukisoma Biblia takatifu ambayo ndio NENO la Mungu, inasema: Mungu ni Mungu wa walio hai na sio wa wafu. Soma Mathayo 22 aya ya 32 ..... Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."
Marko 12:27 Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.
Kama Biblia ilivyo tuhakikishia kuwa Mungu si Mungu wa Wafu kama ambavyo Marehemu Muhammad wa kwenye Quran ambaye anaombewa kila siku na Allah na Malaika wake. Hebu tusome aya kutoka Quran.
Surat Al Ahzab 56. Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.http://www.quranitukufu.net/033.html
Waislam wameamrishwa kuombea Marehemu Muhammad ambaye mpaka hivi leo yupo kaburini akisubiri hukumu kutoka kwa Yesu muumba wake.
Imam Amirul Mu’minin Ali (a) alisema:
Watembeleeni wafu Makaburini, maana wanajisikia furaha mnapo watembelea. Omba unacho taka katika kaburi la Baba yako na mama yako baada ya kuwaombea. Al-Akhlaq wa al-Aadab al-Islamiyyah compiled by Hay’at Muhammad al-Amin, Qum:
Imam al-Sadiq (a) anawataka Waislam watembelee makaburi, kwasababu hao wafu kwa kupitia Allah wanafahamu mnapo watembelea makaburini na wanasikia furaha mnapo kwenda kuwatembelea. Abu Muhammad Zaynu’l ‘Abidin, Manifestations of the All-Merciful:
Wafu wanashukuru mnapo watembelea makaburini, na wanajisikia upweke unapo ondoka. http://www.alseraj.net/3/index2.shtml?91&100&92&1&15
Ushuhuda hapo juu unathibitsiha kuwa, UISLAMU ni dini ya wafu na wanaamini kuwa Wafu walio oza na kuliwa na Mchwa makaburini wanawasikia na wapo kwenye hayo makaburi. Lakini, nini hutokea usiku wa kwanza unapo zikwa, soma hiki kisa cha ajabu sana kutoka Sahihi hadith.
USIKU WA KWANZA WA MUISLAM KABURINI:
[Hasan: At-Tirmidhee from Abu Hurairah.]
Nabii wa Allah (sallAllahu 'alaihi wa sallam) anasema, mtu aliye kufa anapo zikwa, Malaika wawili mmoja wa Mweusi na mwengine wa Bluu, mmoja anaitwa Al Munkar na mwengine an Makeer, na wanamsemesha maiti na kumuuliza; Nini ulikuwa unasema kuhusu huyu mtu? Hivyo husema alicho kuwa ansema, Mtume wa Allahm nashuhudia kuwa mwenye haki ya kuabudiwa ni Allah na Muhammad ni mtume wake. Na wale Malaika watasea, hakika tulijua utasema hivyo, hivyo kaburi lake litaongezwa na kufikia upana wa Sabini kwa Sabini, na anafanyiwa nuru kwake, na litasema lala. Na yeye atasema nitakwenda kwa familia yako na kuwafahamisha..........
Muhammad anasema; Marehemu anapozikwa kaburini, husikia sauti za nyayo za ndugu zake ........ [Saheeh: Al-Bukhaaree (2/422), Muslim, Ahmad, Abu Daud, an-Nasaa.ee: from Anas.],
Al-Baraa b. 'Azib anasema, tulenda Makaburini na tulikuta mmtu moja wa Nasar hajazikwa, basi Nabii wa Allah akamuuliza maiti, asema najisalimisha kwa Allah.....[Saheeh: Ahmad, Abu Dawud (3/4735) Ibn Khuzaimah, al-Haakim, al-Baihaqee in 'Shu'ab ul-Imaan', ad-Diyaa: from al-Baraa.]
Hadithi hapo juu zinatuthibitishia kuwa Uislam ni DINI YA WAFU wakati Biblia inasema kuwa Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.
ENDELEA:
Ada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomaliza kuzika alikuwa anasimama kaburini na husema: “Muombeeni msamaha ndugu yenu kwa Allaah na amfanye thabiti kwani hivi sasa anahojiwa” (Abu Daawuud).
SASA WAISLAM WANAMSWALIA MAITI QURAN
Maiti huswaliwa kwa kufuata utaratibu huu:
Atasimama Imaam (kiongozi wa Swalah) upande wa kichwa, kama maiti ni mwanaume, na hii imethibiti katika Hadiyth ya Abu Ghaalibi al-Khayyaat, amesema:
“Nimemshuhudia Anas bin Maalik akiswalia maiti ya kiume akasimama usawa wa kichwa chake.”
Pia Imaam atasimama usawa wa katikati wa ikiwa maiti ni mwanamke, kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Samurah bin Jundub, anasema:
“Nimeswali nyuma ya Mtume (Rehma na amani ya Allaah ziwe juu yake) naye akimswalia mama wa Ka’ab….akasimama katikati yake.”
Kisha, Imaam ataleta takbira kwa kusema, ‘Allaahu Akbar’, (Allaah ni mkubwa) mara nne au tano au tisa, kwani aina zote hizi zimethibiti kutoka kwa Mtume (Rehma na amani ya Allaah ziwe juu yake). Lakini mara nyingi Mtume (Rehma na amani ya Allaah ziwe juu yake) alileta takbira nne.
Allah na Muhammad wanaendelea kusema kuwa eti Muombeeni MSAMAHA MAITI ...............“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumuombee uthabiti, kwani hakika sasa hivi anaulizwa maswali”[36] kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Affaan.
Inamaanisha kuwa, wewe Muislam endelea kutenda dhambi, bila wasiwasi wowote ule, maana ukifa tu NDUGU ZAKO Watakuombea msamaha, huu jamani ni UONGO MKUBWA SANA.
Kuombea wafu huwafanya wenye dhambi kuendelea kutenda dhambi wakiamini kwamba baada ya kufa kanisa litaomba ili wao waingie mbinguni. Ndugu nakuambia tena WOKOVU NI SASA.
Katika Luka 16:26…Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'' Biblia inatuonyesha watu waliokufa wengine wako pema peponi na wengine wako kuzimu,’’ ’’
BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU WAFU?
MUNGU humpokea mwenye dhambi ambaye hutubu kwa woyo na kujitakasa kwa msingi wa imani peke yake katika damu ya YESU KRISTO. Hivyo humpa uzima wa milele. 2 Kor 6:2’’(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa) ‘’
Biblia inatuambia ya kuwa baada ya mtu kufa, hupelekwa Mbinguni au Jehanamu kulengana na hoja ya kuwa alikuwa amemkubali ama kumkataa Kristo kama mwokozi. Kwa walioamini, kufa ni kuondoka katika mwili na kuenda kukaa na Bwana (wakorintho wa pili 5:6-8; wafilipi 1:23). Kwa wasioamini, kufa ina maana ya hukumu ya milele jehanamu (Luka 16:22-23).
Hapa ndipo kwenye utata juu ya ni nini hufanyika baada ya kifo. Ufunuo wa Yohana 20:11-15 inaeleza juu ya wale walio kuzimu wakitupwa katika ziwa la moto. Ufunuo wa Yohana 21 na 22 inazungumzia juu ya mbingu mpya na dunia mpya. Kwa hivyo ina maana ya kuwa mpaka wakati wa ufufuo wa mwisho, baada ya kufa mtu hubaki katika mahali Fulani kwenye mfano wa mbinguni na kuzimu. Mahali pa mtu anapofaa kukaa milele hapatabadilika ila makazi ya muda yatabadilika. Muda Fulani baada ya kufa, waumini watapelekwa katika mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo wa Yohana 21:1) na wasioamini katika ziwa la moto (ufunuo wa Yohana 20:11-15). Haya ndiyo makao ya milele ya watu yanayotegemea kama mtu alimwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu kutokana na dhambi zake.
Waislam, baada ya kifo ni hukumu na hakuna kuombea maiti msamaha. Muda thabiti wa kutengeneza maisha yako ni huu ulio nao sasa na sio kusubiri kuombewa rehemea baada ya kifo. Huo ni mtego wa Shetani aliye iketia njia iliyo nyooka ya Allah.
Vipi mwenzangu? Umejitayarishaje kwa ajili ya kifo?
Maisha ya hapa duniani hayana uhakika kwamba tutaishi na kuiona kesho. Kifo huja ghafla, Biblia inatuonya “Haya basi, ninyi msemao, leo au kesho tutaingia mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho.
Uzima wenu nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, na kisha hutoweka,” Yak. 4:13-14. Biblia tena inasema, “Kwa maana asema wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa,” 2 Kor. 6:2. Anza leo, wakati kuna nafasi, mwamini Yesu Kristo Mwana wa Mungu, Yoh. 8:24. Yeye ni njia ya kweli na uzima, Yoh. 14:6. Kwa jina la Yesu Kristo pekee ndilo tunaloweza kuokolewa kwalo, Mdo. 4:11-12. Tubu dhambi zako zote, Mdo. 17:30-31. Mkiri Yesu Kristo kuwa ni Mwana wa Mungu, Mdo. 8:37. Uzikwe pamoja naye katika ili upate ondoleo la dhambi, Rum. 6:4; Mdo. 22:16. Kisha mtumikie Kristo katika Kanisa lake kwa maisha yako yote yaliyosalia na utabarikiwa.
Leo tumejifunza tofauti ya KIFO katika Uislam na UKRISTO. Waislam wanaamini kuombea maiti msamaha na Wakristo wanaamini kuwa, wokovu ni sasa.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 11, 2016

Wednesday, March 9, 2016

ALLAH ATEUA MTUME WA MAJINI NA MPINGA KRISTO 666

1. Allah ateua Mtume kwa Majini Quran 6: 130
2. Allah ateua Mtume wa Wanyama Surat An Naml 82
Ndugu zanguni,
Allah anasema katika Quran kuwa, ameteua Mtume kwa kila kiumbe mpaka Majini machafu. Hebu soma aya hapa chini
ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI YANA MTUME WAO
Quran 6: 130. Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.
Swali lamsingi kwa Allah :
Jina la Mtume wa Majini ambaye ni Jini ni nani?
Kwasababu kila Umma ulipewa kitabu na mtume wake, Je, umma wa Majini walipewa kitabu gani?
Lakini nilipo soma Hadith nikagundua kuwa, Muhammad alikuwa anaongea na Majini na kuyafundisha Quran.
MTUME MUHAMMAD AKUTANA NA MAJINI USIKU
Allah S.W.T. ametuhakikishia wazi kuwa ujumbe aliopewa Mtume S.A.W. ulikuwa kwa Wanadamu na Majini na Mashetani pia. Na katika Qurani na Hadithi za Mtume S.A.W. kuna dalili zilizo wazi zinazoyakinisha kuwa Mtume S.A.W. alikuwa akikutana nao na kuwafundisha dini. Na hata wakati mwingine Majini walikuwa wakitoa majibu mazuri zaidi kuliko Binadamu kwenye masuala ya dini. Na mfano ni wakati waliposomewa Suratir Rahmaan. Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na iliyotolewa na Ttirmidhi kasema, “Wakati ambapo Mtume S.A.W. alipowasomea Majini Suratir Rahmaan, “
لَقَدْ قَرَأْتُهَا ‘‘يعني سُورَةَ الرَّحْمَنِ’’ عَلَى الْجِنِّ …، فَكَانُوا أَحْسَنَ مَرْدُودًا مِنْكُمْ ، كُنْتُ كُلَّمَا أَتَيْتُ عَلَى قَوْلِهِ ]فَبِأَيِّ آلاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ[ قَالُوا: لا بِشَيْءٍ مِنْ نِعَمِكَ رَبَّنَا نُكَذِّبُ ، فَلَكَ الحمد
Maana yake, “Hakika nimewasomea Majini (yaani Suratir Rahmaan)…wamejibu vizuri zaidi kuliko nyinyi. Kila nilipofikia kauli Yake (Mwenyezi Mungu S.W.T.) “Fabiayyi A-alaai Rabikumaa Tukadhibaan.) Maana yake, “Basi ipi katika neema za Mola wenu ambayo mnayoikanusha kuwa si kweli?” (Basi Majini) walijibu “Laa bishaay Min Niamika Rabbana Nukadhibu, Falakal Hamdu.” Maana yake, “Hakuna neema yoyote katika neema Zako Mola wetu tunayoikadhibisha, bali tunashukuru.” Na Mtume S.A.W. alipowasomea Wanadamu hawakujibu chochote, akawaambia, “Ndugu zenu wa Ki-Jini wamejibu jawabu nzuri waliposikia haya.” Na dalili nyingine kuwa Mtume S.AW. pia alikuwa ametumwa kwao ni kisa cha baadhi ya Majini ambao baada ya kuisikiliza Qurani waliiamini na wakarejea kwao na kuanza kuwaita wenzao kwenye dini ya Kiislamu.
ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI YALITUMWA KWA MUHAMMAD ILI KUSIKILIZA QURAN
ALLAH HUYO HUYO ALISEMA KUWA KILA WATU/VIUMBE/WANYAMA WALIPEWA MTUME WAO. HAPO TEYARI KUNA SHAKA KWENYE QURAN YA MUHAMMAD AMBAYO SASA INAKABIDHIWA MAJINI MACHAFU.
Allah kasema katika Suratil Ahqaaf aya ya 29 mpaka 32, “
]وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِنْ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنْصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِمْ مُنْذِرِينَ * قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنْزِلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُسْتَقِيمٍ * يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِي اللَّهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * وَمَنْ لا يُجِبْ دَاعِي اللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الأرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِنْ دُونِهِ أَولِيَاءُ أُوْلَئِكَ فِي ضَلالٍ مُبِينٍ[
Maana yake, “Na (wakumbushe) wakati tulipowaleta kundi la Majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana): “Nyamazeni! (Msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha somwa walirudi kwa jamaa zao kwenda kuwaonya. Wakasema “Enyi watu wetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya (Nabii) Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake na kinachoongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mlingani, (Muitaji) wa Mwenyezi Mungu na muaminini, atakusameheni (Mwenyezi Mungu) dhambi zenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na wasiomuitikia Muitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatamshinda (asiwapate) hapa katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele Yake. Hao wamo katika upotofu ulio dhahiri.”
Na kisa kingine ni cha Majini waliosikia Qurani kutoka kwa Mtume S.A.W wakati alipokuwa akiwasalisha Masahaba wake Sala ya Alfajiri. Na hii ilikuwa bila ya yeye kuwa na habari mpaka Mwenyezi Mungu S.W.T. alipomjulisha. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Jin aya ya 1 na ya 2, “
]قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنْ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا[
Maana yake, “Sema: “Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la Majini lilisikiliza (Qurani) likasema: “Hakika sisi tumesikia Qurani ya ajabu. Inaongoza katika uwongofu; kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote tena na Mola wetu.”
Makala haya yametolewa katika kitabu changu kiitwacho, "Hakika ya Majini."
ALLAH SASA ATEUA MTUME KWA WANYAMA = 666. KUMBE BASI ALLAH NA MUHAMMAD NA DINI YAKE NDIO 666
Surat An Naml 82. Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu
Kifungu kuu katika Biblia ambacho kinataja "alama ya mnyama" ni Ufunuo 13:15-18. Marejeo mengine yanaweza kupatikana katika Ufunuo 14: 9, 11, 15:2, 16:2, 19:20, na 20:4. Alama hii hutumika kama muhuri kwa wafuasi wa Mpinga Kristo na nabii wa uongo (msemaji wa Mpinga Kristo). Nabii wa uongo (mnyama wa pili) ndiye ambaye husababisha watu kuchukua alama hii. Alama hasa huwekwa katika mkono au paji la uso na sio kadi mtu atabeba.
Je, jina la Mtume wa Wanyama ambaye ni Mnyama ni nani?
Je, wanyama walipewa kitabu gani?
SIRI IMESHA FUNGUKA, SASA TUNAFAHAMU KUWA, ALLAH NDIE ATAKAYE LETA MPINGA KRISTO 666, NA ALLAH AMEKIRI KATIKA SURAT AN NAML KUWA YEYE AMESHA TEUA MTUME AMBAYE NI MNYAMA NA HUYO MTUME ANASOMA QURAN YA MUHAMMAD.
KAMA kweli Quran ni maneno ya Allah, na aliiteremsha, basi, leo tunafahamu kuwa Allah sio tu ataleta Mpinga Kristo, bali Allah na Muhammad ndio Mpinga Kristo.
Ndugu msomaji utakaesoma mpambano huu sitanukuu moja kwa moja maandiko lakini nitakachokiandika, mashahidi mtakuwa wenyewe kuona kama ni kweli au uongo ya kuwa vitabu hivi vinapambana kiasi hicho..nami sitaandika uongo kamwe.
Hebu tuanze:
BIBLIA: ‘Yesu Kristo alisulubiwa. QURAN: hapana hapana walimsulubisha mwandaazimu mwingine wakizani ndiye!!.
BIBLIA: Yesu ni Mwana wa Mungu. QURAN: ni uongo kwa kuwa Mungu hana mwana wala hazai!!.
BIBLIA: ’tunapata msamaha wa dhambi kupitia damu ya Yesu. QURAN: sivyo kabisa…Mnyaai Mungu ndiye akusameheni madhambi yenu pale mtakapoenda Makka japo mara moja kuhiji. (kiswali chandu cha uzushi..wale masikini je?..Ndiyo kusema pepo ni ya matajiri tu?!!).
BIBLIA: Majini wana asili ya mashetani, ni kundi au jeshi la yule muovu, msishirikiane nayo katika ibada wala kuwatolea sadaka.QURAN: ALLAH asema: nimekuumbeni na majini ili mpate kuniabudu!! (swali la uzushi:Shetani na majini yake yanaabudu na waisilamu ili yaende wapi wakati wao walisha laaniwa na wanachosubiri ni jehanam tu!!).
Huu ni Msiba Mwengine katika dini ya Allah ambayo sasa tumejifunza kuwa ni ya Mpinga Kristo.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 6, 2016

MAJINI MACHAFU NA MASHETANI YANAMWABUDU ALLAH

1. QURAN INASEMA KUWA MAJINI YANAZALIANA NA KUFA KAMA BINADAMU
2. ALLAH AYARUHUSU MAJINI KUZAA NA WAISLAMU
3. QURAN INAKIRI KUWA MAJINI NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD.
4. MAJINI MACHAFU YANAMWABUDU ALLAH
5. KILA MUISLAM AMEPAGAWA NA MAJINI KATIKA MWILI WAKE
Leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu Majini au Mashetani katika Uislam.
JINI NI NINI?
Katika lugha ya kiarabu, neno Jini linamaanisha kitu kilichofichwa au kisichoonekana QURAN 1:71 Neno hili hutumiwa na Waarabu kwa ajili ya kutaja jina fulani. Kwa Waarabu, Jini anayevaa sura ya kike humwita Jinivya, hivyo majini Ghul/Ghilan, nao hujifunua kwa sura ya kike.
Katika imani ya Kiislamu, wao huamni kwamba Majini hutofautiana na Mashetani. Majini waliosilimu wao huitwa majini mazuri na hawa wakiwa katika hali kujionyesha kwa wanadamu, hao huitwa AJINU na wale walioacha kusilimu mwaka 610 AD (Baada ya Kristo) katika safari ya mtume Muhamad alipotoka Taif , wao wanaitwa Mashetani . Hivyo, wao wanapokuwa katika hali ya kutoonekana huitwa ALBAHATWA lakini pia Majini wote wanapokuwa katika hali ya kutoonekana waweza kuitwa ALBAHATWA, yaani PEPO.
QURAN INASEMA KUWA MAJINI YANAZALIANA NA KUFA KAMA BINADAMU
Muislamu huamini kwamba kuna majini ya kike na kiume. Lakini pia , huamini kuwa Majini huoana na kuzaliana QURAN 55:56 na kuwa Majini huzaa sana kuliko binadamu na kwamba, Jini mmoja anaweza kuzaa watoto 300, na kuwa Jini huzaa watoto 3 hadi 4 kwa mkupuo. Somo QURAN 55:26-28 na kuwa Majini wanaweza kuishi miaka 400-1,000 kisha wanaweza kufa. Tofauti yao na binadamu ni kwamba wao wanaishi miaka mingi kuliko binadamu. Lakini pia, huamini kuwa wapo Majini wanaokula, wanaomeza, wanaokunywa, ila tofauti yao na wanadamu ni kwamba wao hula kwa kutumia mkono wa kushoto.
ALLAH AYARUHUSU MAJINI YANAZAA NA WAISLAMU
Pia hiamini kuwa Majini wana uwezo wa kuzaa na Wanadamu. Soma QURAN 17:64. Waislamu huamini kwamba mtu anauwezo wa kuoa au kuolewa na Jini bila kujua, na mwanadamu anauwezo wa kumuua Jini. Soma QURAN 57:14-15
SURATULJINN
Ndani ya QURAN pia imo sura inayoitwa Suratuljinn (QURAN 72). Sura hiyo huitwa hivyo kwa sababu ni sura ya Majini (Mapepo).
Kwa nini wanatajwa Majini katika imani ya Kiislamu?
QURAN INAKIRI KUWA MAJINI MACHAFU NI MAISLAM NA YALISILIMU PALE QURAN ILIPO TEREMSHWA KWA MUHAMMAD.
Majini wanatajwa sana katika dini ya Kiislamu kwa kuwa ni waislam kwa kusilimu, kwa kuiamini Quran tukufu aliyopewa mtume Muhamad.
Majini walisilimu na kuwa Waislamu mwaka 610 AD(Baada ya Yesu) SOMA 72:1-14 QURAN. Hivyo basi, unapotumia neon jinni maana yake unatumia lugha ya Kiarabu ukimaanisha Pepo mchafu. Ni kama Spoon/kijiko, vyote ni kitu kimoja. Ndani ya Quran, neon “PEPO” limetumika kama Paradiso, mbinguni. Lakini pia, tunapata neon jingine liitwalo AKHERA ila neno hilo halimaanishi PARADISO, bali kwa lugha ya Kiarabu neno hili “AKHERA” lina maana ya KUZIMU.
Lakini pia ukiangalia ndani ya SURALJINN ( QURAN 72:1-2, 8-9, 12 ) Mapepo hawa wanajieleza waziwazi kabisa kuwa mwanzo waliishi Mbinguni, walipogeuka kwa kuasi, walitegwa na Mungu. Linganisha na maandiko haya katika Biblia ( UFUNUO WA YOHANA 12:7-9; YUDA 1:6-8; UFUNUO 20:10; UFUNUO 21:8 ). Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, hawa majini ( Mapepo ) waliotegwa na Mungu Mbinguni wakiwa Malaika huko na kutupwa Duniani baada ya kuasi huko, sasa, wakati wa mtume Muhamad katika safari yake ya kurudi Taif mwaka 620 AD (baada ya Yesu) wapo walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu ya kuwatangazia neema ya kuabudu. Katika vol 8-9, husema , wanapojaribu kwenda Mbinguni ( walikotoka zamani ), hukuta ile Mbingu imezungushiwa vimondo vya moto. Hivyo, hudai kuwa mbingu yao iko Akhera, yaani Kuzimu, maana Mbingu ya juu ina moto na hawana uwezo wa kwenda huko. SOMA (QURAN 72:9), Mbingu ina utisho wa moto ila Akhera ( kuzimu ) hakuna shida kwao.
MAJINI MACHAFU YANAMWABUDU ALLAH
Hivyo basi, kulingana na jinsi Allah asemavyo ndani ya Quran kuwa nimeumba binadamu na majini ili muniabudu ( QURAN 57:58 ; 51:56) na kuwa , mbinguni mwao Majini wanaabudu (Majini waliosilimu mwaka 620 AD) ,SOMA QURAN 72:14, ambao ni wema wanaosafiri na kurithi uzima wa milele upatikanao Akhera ( Kuzimu ). Lengo kubwa la Shetani na Majini ni kufanya urafiki na wanadamu wengi ili kwa wingi huo apate watu wengi wa kwenda nao JEHANAMU ( QURAN 6:128 ). Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba moto wa milele hakuwekewa Mwanadamu bali ni Shetani na malaika zake wote ( Majini au mapepo ). Hawa, hawana nafasi tena ya kuungama au kutubu.
Yesu Kristo anayetambuliwa na Waislam kama Mtume tu, hakuwa na urafiki wowote na Shetani wala Mapepo ( Majini ). Aliyaamuru Majini kutoka ndani ya watu waliokuwa wakiteswa nayo ( MATHAYO 8:29: MARKO 5 N,K )
Wakati Yesu anaondoka hapa duniani, alichukuliwa na wingu na kupaa kuelekea juu. Mbinguni ni juu kama Quran inavyothibitisha. Yesu aliweza kupaa na kuingia Mbinguni lakini Majini ( Mapepo ) walioslimu wakijaribu tu, wanakutana na moto mkali. Tumeona kuwa Majini ambao ni Waislamu kwa kusilimu, wanaishi AKHERA yaani Kuzimu. Je, Waislamu wengine unadhani wataishia wapi milele? Katika imani ya Kiislam huamini kuwa, Muislam akifa anakuwa na Majini wawili wa Kumlinda humo Kaburini.
KILA MUISLAM ANA JINI KATIKA MWILI WAKE
Majini wamepewa ruhusa ya kukaa katika mwili wa Muislam yeyote, hivyo kila Muislam ana Jini kuanzia moja na kuendelea. Vile vile Majini wameruhusiwa kukaa katika nyumba za Waislam. Katika nyumba yoyote ya Muumini wa dini hiyo, kuna Jini au Majini wanaokaa humo. Ni ukweli usiopingika kuwa bila Majini hakuna Uislamu kama vile pasipo Roho Mtakatifu hakuna Ukristo. Majini ndiyo yaliyomchukua mtume Muhamad kwa muda wa siku 40 akiwa Mabondeni walikompeleka na kuanza kumuagiza kuhusiana na kuanzisha imani hiyo ya Kiislamu.
USHAURI WANGU KWA WA WAKRISTO:
Ushauri wangu wa bure kwa Mkristo ni huu, USIMUACHE KAMWE KRISTO NA KUINGIA KATIKA IMANI ZA MASHETANI (1TIMOTHEO 4:1-2 ).
Majini au Mashetani ni kitui kimoja na wala hakuna tofauti yao. Wote hao Mashetani/Majini yalimpinga Mungu na kutupwa duniani. Biblia inasema kuwa Hakuna Msamaha kwa Majini maana wao walisha hukumiwa na wanacho subiri ni kutupwa Jehannam.
Shetani bado ni “mfalme wa nguvu za anga” (Waefeso 2:2). Hii inamaanisha kwamba Shetani na Malaika wengine walioasi wanaweza kushawishi mia zetu na mawazo yetu kupitia miziki, runinga, mijadala, nk. Tumeambiwa kujihadhari katika mawazo na nia zetu (2Wakorintho 10:3-5). 2Wakorintho 4:4 inatuambia kuwa mungu wa dunia hii amepofusha mawazo ya watu ili wasiamini.
Shetani ndiye yuko nyuma ya dini zote za uongo na dini za dunia. Shetani atafanya na kila kitu katika uwezo wake ili ampinge Mungu na wale wote wanaomfuata. Ingawa hatima ya Shetani imewekwa muhuri kuwa tanuru la moto milele (Ufunuo Wa Yohana 20:10).
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

LEO TUANGALIE JUHUDI ZA WAHADHIRI KUTAFUTA UTABIRI WA MUHAMMAD MWANA WA ABDALAH KWENYE BIBLIA:

Nabii Isaya ameandika kwamba: Kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi (Isaya 29:12).
Waislamu walipoona andiko hili wakadhani kuwa tayari wameshapata ushahidi kuwa Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia kwa kuwa Muhammad alikuwa ni mtu ambaye hakuwa amesoma.
Ukifuatilia sura nzima ya 29 na mantiki iliyozaa mstari huu wa 12, unaweza kuishia kucheka tu, ingawaje hili si jambo la kucheka.
Wanachofanya Waislamu ni upotovu mkubwa ambao unaangamiza mamilioni ya watu wa Mungu milele katika jehanamu ya moto. Watu wanaaminishwa uongo na wao wanaukumbatia kana kwamba ni ukweli.
Kwa ujumla, ukisoma sura ya 29 ni sura ambayo inatamka hukumu juu ya Ariel (Yerusalemu) kutokana na uasi wao juu ya sheria na maagizo ya Mungu, Yehova. Hebu tusome sura hiyo kwa Taratibu:
1 Ole wa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi alifanya kituo chake ndani yake; ongezeni mwaka baada ya mwaka; sikukuu na zirudi wakati wake,
2 ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.
3 Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke.
4 Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong'ona toka mavumbini.
5 Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.
6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.
7 Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.
8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
9 Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo.
10 Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji.
Mbali na hukumu hizo hapo juu, Mungu bado akaendelea kusema kuwa, kutokana na uasi wao, hata neno lake hawatalielewa. Yaani hawataweza kusikia au kujua Mungu anasema nini hata kama watasoma au kusikia neno lake. Hii ni pamoja na wale ambao ndio wanatarajiwa kuwa wenye kuelewa neno hili – yaani manabii na waonaji – ukiachilia mbali wale wasio na maarifa juu ya neno la Mungu, yaani watu wa kawaida. Kwa hiyo, anaendelea kusema:
11 Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri;
12 kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.
Sasa basi, kama kweli Muhammad ndiye anayetajwa kwenye Isaya 29:12, kimantiki ina maana kuwa yeye ni kati ya wasioelewa lolote kwa kuwa wako chini ya hukumu ya Mungu; maana kama tulivyoona, sura hii ni tamko la hukumu ya Mungu kutokana na uasi. Si vibaya hata hivyo! Ndiyo maana nikasema kwamba unaposoma hoja hii ya Waislamu unaweza kuishia kucheka tu.
Lakini ebu tazama CHUO hiki ni WATU humpa mtu asiye na maarifa?
Sasa kama chuo hiki kinakusudiwa ni Qurani?
Je WATu hawa waliompa Muhammad chuo hiki ni kina nani?
Hivi kumbe Quran imetoka kwa WATU wakumpa Muhammad?
Hata hivyo, kwa kuwa sasa Muhammad ni nabii asiyeelewa chochote kutokana na kuwa chini ya hukumu ya Mungu kulingana na mantiki ya andiko hili, maana yake ni kuwa ujumbe alioleta kwa wanadamu hautoki kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi. Ndiyo! Labda kama, kwa makusudi tu, hutaki mantiki iliyopo. Kwa nini basi umfuate mtu wa namna hiyo?
Fanya maamuzi; nafsi yako ni ya gharama Mpendwa
By permission from Mwalimu Chaka
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH NA MUHAMMAD WAKIRI KUWA YESU NI MWOKOZI NA SHETANI NDIE KIONGOZI WA DINI YA UISLAMU

1. QURAN YAKIRI KUWA YESU NDIE MWOKOZI
2. QURAN YAKIRI KUWA WAISLAM WANABEBA MIZIGO MIBAYA SANA.
3. QURAN YAKIRI KUWA SHETANI ANAKAA KWENYE NJIA ILIYO NYOOKA – UISLAMU.
4. MUHAMMAD AMSILIMISHA SHETANI NA KUWA MUISLAMU.
Ndugu msomaji,
Waislam wamekuwa wakisema kuwa, mtu mwengine hawezi kukubebea mizigo yako, lakini, hayo madai yanapingwa na aya kadhaa za Quran.
Nasi tulipousikia uwongofu tuliuamini; basi anayemwamini Mola wake hataogopa kupunjwa wala kutwikwa (kubebeshwa) dhambi (za mtu mwengine).” (Qurani 72:13)
Quran inasema kuwa, anaye mwamini Mwenyei Mungu, hawezi kuogopa kubebeshwa dhambi za mtu mwengine.
Je, kuna watu wanaweza kubeba dhambi za Mtu mwengine?
Soma Quran Surat An Nahl(16) aya ya 25. Kuna watu wanawapoteza wengine Ili wabebe mizigo ya madhambi Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni mibaya mno hiyo mizigo wanayo ibeba!
Allah kupitia Quran anawaambia Waislam wote kuwa, hiyo mizigo ya dhambi wanayo beba, NI MIBAYA MNO, na wamepotezwa ili waibebe wenyewe mpaka siku ya kiyama.
SASA, kama kubeba Mizigo siku ya kiyama mbaya mno, je, tuipeleke wapi hiyo mizigo, SASA SOMA Zaburi 55: 22 Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
BIBLIA INAWAJIBU WAISLAM KUWA, MTWIKE BWANA MZIGO WAKO. Ndio maana Wakristo wote tumegundua hili, ENDELEA KUSOMA Yohana 13:13 INASEA: Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
Yesu anasema kuwa, NINYI MNANIITA MWALIMU NA BWANA, NANYI MWANENA VEMA. Endelea KUSOMA Yeremia 10:10 Bali Bwana ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.
YEREMIA 10:10 INAWAJIBU WAISLAM KUWA, HUYO BWANA NDIE MUNGU WA KWELI. SASA, Waislam wanashanga kivipi Yesu awe Mungu na Yesu huyo huyo afe Msalabani, ENDELEA KUSOMA
Quran 55:29 INAENDELA KUKUJIBU 29. Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
QURAN inakujibu kwa ufasaha kuwa KILA KITU KILICHOPO MBINGUNI NA ARDHINI VINAMWOMBA YESU. Haya Mwislamu unaendelea kushangaa, Sasa angalia nini kilitendeka na au tokea Msalabani
SOMA: 1 Petro 3: 18 - 19 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
Neno la Mungu linasema kuwa MWILI WAKE NDIO ULIUWAWA BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA. Sasa hakuna kushangaa tena maana tufahamu ulio uwawa ni Mwili wake to bali Roho yake haikuuwawa.
Maandiko yanasema kuwa MUNGU NI ROHO, sasa aliye UWAWA NI MWILI TU BALI ROHO YAKE AKAHUISHWA
1 Timotheo 6:15-16 15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina
Kumbe basi Yesu aliungama maungamo mazuri mazuri SOMA aya ya 13 katika 1 Timotheo 6: Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, Ushaihid zaidi soma Luka 18: 31.
LAKINI ndugu zetu Waislam wanasema kuwa MSALABA NI ALAMA YA SHETANI, HEBU TUANZE NA QURAN 7:16 16. Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.
SHETANI ANAMWAMBIA ALLAH KUWA, Kwa kuwa umenihukumia upotofu, BASI NITAWAVIZIA KATIKA NJIA YAKO ILIYO NYOOKA.
SHETANI AMEAPA KUWA ATAKETI KATIKA NJIA YA ALLAH ILIYO NYOOKA.
SASA HII NJIA YA ALLAH ILIYO NYOOKA AMBAYO SHETANI ameapa atakaa kwenye hiyo njia, ni ipi?
QURAN 6: 126. Na hii Dini ya Uislam, ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi ILIYO NYOOKA. Tumezipambanua Aya kwa watu wanao kumbuka.
KUMBE SHETANI AMEKETI KWENYE NJIA ILIYO NYOOKA AMBAYO NI DINI YA UISLAMU, QURAN 7:16.
Kwasababu Shetani kaketi huko kwenye njia iliyo nyooka, ndio maana Shetani ana dini, au unabisha?
MUHAMMAD AMSILIMISHA SHETANI
Kitabu Asili ya Majini Ukurasa wa 20 INASEMA: Ni bahati mbaya kwamba Adam na Hawa hawakufanya jitihada za kumwezesha Shetani na wanawe kuomba Msamaha kwa Mwenyezi Mungu, NI MTUME MUHAMMAD TU NDIE ALIYE MSILIMISHA SHETANI AKAWA MUISLAMU.
Haya sio maajabu, maana tumesoma hapo kwenye Quran Surat Al Anaam kuwa Shetani anakaa kwenye NJIA ILIYO NYOOKA YA ALLAH. Na Njia iliyo nyooka ni UISLAMU Quran 6 aya ya 126 Na hii Dini ya Uislam, ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi Iliyo nyooka. Tumezipambanua Aya kwa watu wanao kumbuka.
Ndugu zanguni, kwa mara nyingie tumejifuza kuwa Shetani ndie kiongozi wa dini ya Uislam. Shetani ndie yupo kwenye NJIA ILIYO NYOOKA NA AMEKETI HAPO. ZAIDI YA HAPO, SHETANI AMESILIMISHWA NA MUHAMMAD kama tulivyo soma katika Kitabu cha Asili ya Mini Ukurasa wa 20.
Huu ni Msiba Mwengine katika dini ya Allah ambayo sasa tumejifunza kuwa Shetani anakaa kwenye Njia Iliyo nyooka na alisilimu na kuwa Muislam.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 9, 2016

Tuesday, March 8, 2016

MALAIKA WALIO FANYA DHAMBI

1. Je, Shetani aliumbwa kma Shetani au alikuwa na jina lingine?
2. Je, Majini yaliumbwa kama Majini au yalikuwa na majina mengine?
Ndugu msomaji,
Katika somo hili, tutajifunze kuhusu Malaika walio tenda dhambi, na matokea yao baada ya kufanya hivyo.
Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Roho na kwamba viumbe wake wa kwanza walikuwa roho. (Yohana 4:24; Waebrania 1:13, 14) Isitoshe, Biblia pia inataja kwamba kuna roho waovu. (1 Wakorintho 10:20, 21; Yakobo 2:19) Lakini haifundishi kwamba Mungu ndiye aliyewaumba roho waovu. Basi wao ni nani, na walitokea jinsi gani?
Katika Biblia tunasoma kuwa, kuna Malaika walitenda dhambi na kufukuzwa Mbiguni. Mungu mwenye upendo, alipowaumba viumbe wa roho, viumbe hawa, aliwaumba wakiwa na uhuru wa kuchagua ikiwa watatende mema au mabaya.
Roho wa kwanza kuasi na mwenye sifa mbaya zaidi alikuwa Lucifer ambaye anajulikana sasa kwa jina la Shetani.
Ni nini kilichomchochea Shetani kumwasi Mungu?
Shetani alianza kutamani ibada ambayo ilikuwa hasa ya Muumba-Mungu, kisha akajikweza kutokana na tamaa hiyo na kujifanya kuwa mungu. Isaya 14: 11 Fahari yako yote imeshushwa mpaka kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako na minyoo imekufunika. 12 Tazama jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya asubuhi, mwana wa mapambazuko! Umetupwa chini duniani, wewe uliyepata kuangusha mataifa! 1 3 Ulisema moyoni mwako, “Nitapanda juu hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, ataketi nimetawazwa juu ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya juu sana vya mlima Mtakatifu.
Biblia inamfafanua Shetani kuwa kiumbe halisi ambaye yuko katika makao ya roho. (Ayubu 1:6) Inatueleza kuhusu sifa zake za ukatili kutia ndani matendo yake ya uovu. (Ayubu 1:13-19; 2:7, 8; 2 Timotheo 2:26) Pia inasimulia mazungumzo kati ya Shetani na Mungu na pia kati yake na Yesu.— Ayubu 1:7-12; Mathayo 4:1-11.
Kiumbe huyo mwovu alitoka wapi? Mungu aliumba viumbe “roho” wanaoitwa malaika. (Ayubu 38:4-7) Wote walikuwa wakamilifu na waadilifu. Hata hivyo, mmoja kati ya malaika hao akaja kuwa Shetani.
Malaika huyo hakuitwa Shetani alipoumbwa kama nilivyo sema hapo mwanzo na/au hakuumbwa akiwa Shetani, kama imani zingine zinavyo sema, bali alikuwa Malaika muadilifu mbele za Mungu. Jina hilo Shetani ni la kumfafanua, na linamaanisha “Mpinzani; Adui; Mshtaki.” Alikuja kuitwa Shetani kwa sababu alichagua kumpinga Mungu.
Kiumbe huyo wa roho akaanza kukuza hisia za kiburi na za kushindana na Mungu. Alitaka wengine wamwabudu yeye. Mwana mzaliwa wa kwanza wa Mungu alipokuwa hapa duniani, Shetani alimtaka Yesu ‘amfanyie tendo la ibada.’— Mathayo 4:9.
Katika Bustani ya Edeni, Shetani amdanganya Hawa:
Shetani “hakusimama imara katika kweli.” (Yohana 8:44) Alidai kwamba Mungu alikuwa mwongo, ilhali kwa kweli, yeye ndiye alikuwa mwongo. Alimwambia Hawa kwamba angekuwa kama Mungu, lakini ni yeye hasa aliyetaka kuwa kama Mungu. Na kupitia mbinu zake za ujanja, alitosheleza tamaa yake yenye ubinafsi. Alimfanya Hawa amwone kuwa mkuu kuliko Mungu. Kwa kumtii Shetani, Hawa alimkubali kuwa mungu wake.—Mwanzo 3:1-7.
Kwa kuchochea uasi, malaika huyo ambaye awali alikuwa mwenye kuaminika akawa Shetani, yaani, mpinzani na adui ya Mungu na wanadamu. Neno “Ibilisi,” linalomaanisha “Mchongezi,” likawa pia jina la malaika huyo mwovu. Malaika huyo ambaye aliongoza katika kutenda dhambi mwishowe aliwachochea malaika wengine wakose kumtii Mungu na wamwasi kama yeye. (Mwanzo 6:1, 2; 1 Petro 3:19, 20) Kwa kufanya hivyo malaika hao waliwaongezea wanadamu shida. Kwa sababu ya kuiga njia za Shetani zenye ubinafsi, “dunia ikajaa jeuri. Na uovu”—Mwanzo 6:11; Mathayo 12:24.
Ingawa ni wazi kwamba roho waovu wamezuiwa wasijigeuze kuwa wanadamu, bado wana nguvu na uvutano mwingi juu ya akili na maisha ya watu. Kwa kweli, Shetani, na roho wake waovu, ‘anaipotosha dunia nzima inayokaliwa.’ (Ufunuo 12:9; 16:14) Kwa njia gani? Hasa kupitia “mafundisho ya roho waovu.” (1 Timotheo 4:1) Mafundisho hayo ya uwongo, ambayo mengi ni ya kidini, yamepofusha akili za mamilioni ya watu wasitambue ukweli kumhusu Mungu. (2 Wakorintho 4:4) Fikiria mifano kadhaa.
Unaweza kujilinda jinsi gani dhidi ya roho waovu?
Biblia inajibu hivi: “Jitiisheni kwa Mungu; lakini mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia ninyi.” (Yakobo 4:7) Tunatii agizo hilo tunapoishi kupatana na mafundisho yaliyo katika Biblia, kitabu pekee kitakatifu ambacho kinamfichua Shetani, roho waovu, na “hila” zao. (Waefeso 6:11; 2 Wakorintho 2:11) Pia, Biblia inatuambia kwamba roho waovu pamoja na wote wanaompinga Mungu, hawatakuwapo milele. (Waroma 16:20) “Wanyoofu ndio watakaokaa duniani, na wasio na lawama ndio watakaobaki ndani yake,” inasema Methali 2:21.
Jinsi shetani anavyotenda kazi:

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW