Saturday, July 2, 2016

WAISLAM THIBITISHENI UWEPO WA ISA BIN MARYAM KWA VITABU VILIVYOKUWEPO KABLA YA QURAN




1. Mimi naomba mtuletee ushahidi unao weza
kuthibitishika wa uwepo wa "Isa na jina la Isa bin Maryam" kwa kutumia hivyo vitabu vilivyo kuwepo kabla ya Quran.
2. Sina muda na aya za Quran. Maana Waislam mnakiri kuwa Injil iliteremshwa na Allah, hivyo basi Injil mnaweza itumia na iwe na jina la Isa.
3. Quran iliyokuja baada ya Injil siitaki. Hadith zilizo kuja baada ya Injil sizitaki. Mimi nataka mtumie vitabu vilivyo kuwepo kabla ya Quran na Muhammad.
Sasa basi. Thibitisheni uwepo wa Isa kwa kutumia vitabu vilivyo kuwepo kabla ya (1) Quran (2) kabla ya Muhammad kuzaliwa (3) kabla ya Sahih Hadith za Muhammad.
Mkinipa huo uthibitisho basi leo nitasilimu na kuwa Muislam.

UTHIBITISHO 10 KUWA YESU NI MUNGU



“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!
Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.” Kwa madai haya hata kwenye Qurana hawawezi thibitisha kuwa Allah Allah ni mungu, zaidi ya hapo, hata Utume wa Muhammad unakuwa kwenye njia panda, maana hakuna aya kwenye Quran Muhammad anasema mimi Muhammad ni mtume wa Mungu.
Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).
Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.
1. YESU ALIKUWEPO KABLA YA KUZALIWA
Ufuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO ni Mungu.
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).
Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.
2. YESU NA BABA NI WAMOJA
Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu:
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.
Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.
Yohana 14:9
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Maneno haya Yesu aliyasema baada ya kuulizwa swali lililo wazi kabisa, ambalo lilikuwa na lengo la kumjua MUNGU BABA! Imeandikwa: Filipo akamwambia, Bwana, UTUONYESHE BABA, yatutosha. Ndipo Yesu akajibu waziwazi: ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA. Maana yake ni kuwa, “Mimi ndio Baba mwenyewe.”
3. YESU NI MWANZO NA MWISHO
Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.
4. YESU NI NENO
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
Andiko hili Waislamu hawalipendi kabisa. ni kwa sababu liko wazi mno. Yesu ni Neno; na Neno ni Mungu; hivyo, Yesu ni Mungu!
5. THOMASO AKIRI KUWA YESU NI MUNGU, NA YESU HAKUKATAA KUITWA MUNGU
Yohana 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!
Tomaso aliposema hivi, Bwana Yesu hakukanusha na kusema, “Mimi sio Mungu.” Badala yake: Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. (Yoh 20:29).
Kama Thomaso alikuwa muongo, kwanini Yesu hakukataa kuitwa Mungu. Imani zote zinakiri kuwa Yesu hakufanya dhambi na hakuwa na dhambi.
6. DAMU YA YESU INAMAMLAKA
Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.
Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.
7. KATIKA YESU, KILA KITU KILIUMBWA
Wakolosai 1:16
Kwa kuwa KATIKA YEYE VITU VYOTE VILIUMBWA, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Katika Yeye Yesu vitu vyote viliumbwa. Ina maana kuwa vitu vyote vilitokana na Yesu; maana Yesu ni Neno la Mungu. Na tunajua kuwa Muumba wa vitu vyote ni Mungu; hivyo, Yesu ni Muumba – Yeye ni Mungu!!
8. KATIKA YESU, UNAKAA UTIMILIFU WA MUNGU
Wakolosai 2:9
Maana KATIKA YEYE UNAKAA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.
Sisi sote ni watu wasio wakamilifu. Tunaanguka tena na tena kwenye dhambi. Kwa hiyo, hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anaweza kujigamba kwamba yeye ametimia kama alivyo Mungu. Lakini katika Yesu “utimilifu WOTE wa Mungu unakaa.” Kwa nini? Kwa sababu Yeye ndiye Mungu huyohuyo.
9. YESU NI MUNGU PAMOJA NASI "EMMANUEL"
1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Ni Mungu gani aliyedhihirishwa katika mwili? Jibu liko wazi. Ni Yesu Kristo peke yake.
10. YESU NI MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Tito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU
Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!
Shida KUU ya Waislamu ni hii: Wanampima Mungu kwa vigezo vya kibinadamu. Mungu anasema: Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? (Yer 32:27)
Jibu liko wazo. HAKUNA!
Lakini utakuta Waislamu wanauliza maswali ya ajabu sana. Eti, kama Yesu ni Mungu, wakati amekufa, nani alikuwa anaangalia dunia?
Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO!
YESU NI MUNGU MILELE NA MILELE!!
HALELUYA!!
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua!

POSA SABA (7) ZA MUHAMMAD ZILIZO KATALIWA



1. Kwanini baadhi ya wanawake walikataa posa za Muhammad?
2. Kwanini muhammad aliendelea kuomba/toa posa na huku zikikataliwa?
Ndugu msomaji,
Leo nitakupa ushahid kadhaa kuonyesha jinsi Muhammad alivyo penda wanawake lakini wengine walikataa posa zake na kuto jali utume wake alio pewa na Mkewe.
Muhammad alimwomba amuoe Ghaziyyah kwa sababu ya uzuri wake, lakini alikataliwa. Tabari anadai kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu lakini hatoi ushahidi. al-Tabari juzuu ya 9 uk.136. Hakuna ushahidi kuwa [Ghaziyyah] hakuwa mwaminifu na kwamba Muhammad hakuwa makini kwa kutokumwadhibu, au kwamba hakuwa mwaminifu na Muhammad alimwadhibu.
Layla aligusa bega la Muhammad tokea nyuma na kumuomba amuoe. Muhammad alikubali. Ndugu za Layla walisema, "Ni jambo baya kiasi gani ulilolifanya! Wewe u mwanamke anayejiheshimu, lakini Nabii ni mpenda wanawake. Tafuta kujitengua toka kwake." Layla alikwenda kwa Nabii na kumuomba aikane ndoa hiyo na aliafikianana na hilo [ombi]." al-Tabari juzuu ya 9 uk.139.
Kutoka al-Tabari juzuu ya 9 uk.140-141, Muhammad alimposa lakini aliishia kutokumuoa:
1) Umm Hani’ bin Abi Talib [Hind] kwa sababu alikuwa na mtoto.
2) Duba’ah binti ‘Amir lakini alikuwa mzee sana.
3) Inaripotiwa kuwa alimposa Saffiyah binti Bashshamah, mateka. Alitakiwa achague mmoja kati ya Muhammad na mume wake, na alimchagua mume wake.
4) Umm Habib bint al-‘Abbas lakini kwa kuwa al-‘Abbas alikuwa kaka wa kulelewa pamoja naye kwa hiyo isingeruhusiwa kisheria kwa hiyo Muhammad aliamua kujiondoa.
5) Jamrah binti Al-Harith. Baba yake alida isivyo sahihi kuwa alikuwa anasumbuliwa na kitu Fulani. Aliporudi, alikuta ameisha kumbwa na ukoma.
Haielezwi kwa kauli moja endapo Umm Hani’ alikuwa muislam kabla au baada ya Muhammad kumwomba amuoe. al-Tabari juzuu ya 39 uk.197 na rejeo chini ya ukurasa 857 uk.197.
Ndugu msomaji ambaye ni mfuasi wa dini ya Uislam, je, unaweza tumabia kwanini posa 7 za Muhammad zilikataliwa?
Max Shimba Ministries

YESU ANAKIRI KWA MDOMO WAKE KUWA YEYE NI MUNGU


Ndugu zanguni, leo YESU anawajibu Waislam kwa mara nyingine tena kuwa yeye ni Mungu, "YESU NI MUNGU".
Hii aya hapa chini katika kitabu cha Ufunuo ni ya Yesu mwenyewee akiongea na Yohana. Yesu anakiri kuwa yeye ni Mungu. Hebu tuisome kwanza:
Ufunuo 21: 6 Yesu Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yo yote. 7 Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, NAMI NITAKUWA MUNGU WAKE, naye atakuwa mwanangu.
Mara nyingi kumekuwa na mtanashi kutoka Waislam kuwa eti Yesu hakuwai sema yeye ni Mungu. Mara zote wamekuwa wakidai kuwa, tuwaletee aya ambayo Yesu anasema yeye ni Mungu. Ingawa, Biblia imewajibu kuwa Yesu ni Mungu kutoka sehemu mbalimbali, lakini wamekuwa wabishi na kung'ang'ania waletewe aya, ili wabatizwe na kuwa Wakristo. Kwasababu Biblia imekamilika na haina shaka ndani yake. Leo Biblia inawajibu tena kuwa Yesu ni Mungu.
Aya ya 7 inasema kuwa, NUKUU: [Yeye atakayeshinda atayarithi haya yote, NAMI NITAKUWA MUNGU WAKE, naye atakuwa mwanangu.]
Yesu amekiri kuwa mtu yeyote yule atakaye urithi ufalme wake, basi ifahamike kuwa.
Moja: Yesu atakuwa Mungu wake
Pili: Wewe utakuwa Mwana wake.
Huu ni ushaidi mwingine kuwa Yesu ni Mungu. Waislam, ningependa mfahamu kuwa, Yesu ni Mungu kama ilivyo andikwa kwenye Ufunuo Sura 21 na aya ya 7.
Je, Upo tayari kumfuata Yesu ambaye ni Mungu? Kumbukeni kuwa, Yesu ndie Njia pekee ya kwenda Mbinguni. Dini haita wapeleka popote pale, lakini Yesu Kristo aliye hai ambaye sasa tunasoma kukiri kwake kuwa yeye ni Mungu, ndie njia pekee ya Uzima wa Milele.
Mpokee Yesu leo ili upate uzima wa milele.
Katika Huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Kwa Max Shimba Ministries Org 2014

ROHO, NAFSI NA MWILI


Ndugu msomaji,
Je, mwanadamu ni nani?
Kwa kifupi ninaweza kusema kuwa Mwanadamu ni Roho, ina Nafsi na inakaa ndani ya Mwili.
Ukisoma 1 Wathesalonike 5:23 Inatusaidia Kuona maeneo yote matatu ya mwanadam/mtu;
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU Mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo"
Hapa unaona Nafsi, Roho na Mwili vimetajwa kwenye hiyo aya.
ROHO NI NINI?
Roho ambayo inahusisha mambo ya Mungu.
Ni ile sehemu ya mtu yenye ufahamu wa Mungu, ambayo hufanywa hai na hutiwa nguvu na Roho wa Mungu wakati wa Wokovu. Kabla ya mtu Kuokoka, sehemu hii, haifanyi kazi kwa utimilifu kabisa kwa sababu ya dhambi. Dhambi huifanya kuondolewa nguvu ya kutenda kazi sawa sawa, kwa Amani na Roho ya Mungu. Lakini kupitia Ubatizo wa Roho Mtakatifu, mwanadamu hupokea nguvu ya kiroho, inayomwezesha kuishi maisha ya Kristo.
Roho inahusika na:-
i) Maombi na Ibada na Mungu,
ii) Ushirika na Mungu,
iii) Mapokezi ya karama za Roho,
iv) Vita vya kiroho,
v) Kuunda Mawazo na Ndoto,
vi) Dhamira, Kupambanua,
vii) Udadisi, Kuuliza,
viii) Ufahamu, Kutafsiri,
ix) Shuhuda kwa Wanadamu
NAFSI NI NINI?
Nafsi inahusika na mambo ya mtu.
Ni ile sehemu ambayo ina ufahamu wamtu mwenyewe au kiini cha ubinafsi wa mtu. Kazi yake ni:-
i) Kufikiri – Kutafakari, kuona
ii) Hisia – Kujisikia kuwa na tamaa na Upendo
iii) Utashi – Nia, Kuamua
MWILI NI NINI?
Mwili unahusika na mambo ya Ulimwengu.
Ni ile sehemu ya mwanadamu ambayo inafahamu na kukubaliana na ulimwengu wa nje. Inafanya yafuatayo:-
i) Utambuzi wa Ulimwengu, - yaani ile hali ya mwili kupokea habari kutoka Ulimwenguni kwa njia ya Ufahamu.
ii) Urejeshi – yaani ile hali ya Mwitikio wa kutenda kutokana na kutendewa kitu, kupitia utaratibu wa Maneno na Matendo.
iii) Udhihirisho – yaani ile hali ya Mwili ya kutoa habari za Ulimwengu kwa Mawazo, Kujisikia na Maamuzi ya Nafsi.''
Hivyo basi, Mtu ni Roho.
1) Mungu alimuumba mwanadamu kwanza kama roho ( Mwanzo 1:26) hapo bila mwili ndiyo maana Biblia inasema Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake kwa sababu Mungu ni Roho.
Mtu ambaye Mwanzo 1:26 inamuongelea, Biblia yenyewe inathibisha kuwa ni roho lakini yenye mwili wa rohoni (1 Korintho 15:44) ikiwa kuna mwili wa asili basi kuna mwili wa rohoni pia.
2) Mungu aliumba roho ya Mwanadamu kwanza ndio akaumba mwili wa nyama na nafsi baadae.
(Mwnzo 2:7) Mungu akauumba mwili wa Adamu kwa udongo akaichukua ile roho (kumbuka ina mwili wa kiroho) akaiweka/ingiza katika mwili kwa kuipulizia ndani ya ule udongo alio uumba, na mtu akawa nafsi hai.
Hivyo basi;
Mwanadamu amegawnyika mara tatu
1) Roho yenye ufahamu wa mambo ya Mungu. Chakula cha Roho ni neno la Mungu.
2) Nafsi ni shemu yenye ufahamu ambapo vitu vya kujifunza au elimu au kumbukumbu vinakaa. Roho huitia nafsi nguvu au kuwa mahiri kwenye eneo fulani ambalo rohoni umebarikiwa ili hicho kitu kithiirike kwenye ulimwengu wa mwili.
3) Mwili ni sehemu ya mwanadamu inayo onekana na imebeba roho na nafsi.
Bonus question.
KUFA NI NINI?
Kufa ni kitendo cha roho kuachana na mwili, kama huyo mtu(roho) alipokuwa ndani ya mwili aliishi maisha matakatifu roho yake itakwenda kwa Mungu na kama aliishi maisha yasiyompendeza Mungu huyo mtu(roho) atakwenda kuzimu.
Hivyo basi itunze sana Roho yako maana wewe ni Roho una nafsi na unaishi kwenye mwili.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo

SHEHE OMARI ASEMA QURUANI IMEJAA UCHAWI NA USHIRIKINA



*********************************************************************************************
SIRI YA WATOTO WA DAWA YAWEKWA HADHARANI NA SHEIKH OMARI
**********************************************************************************************
Sheikh Omari akifundisha hapo jana kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe jijini Dar es salaam.
Shehe Omari akielezea jinsi alivyokuwa akitengeza watoto dawa na Dalili zake.
Kwasababu ya mila nyingi za kiafrika, watu wengi sana wamejikuta wakikimbilia kwa waganga pale wanapogundua kukosa mtoto. Wakati ninasomea falaki nilijifunza namna 11 jinsi ya kumpatia mwanamke mtoto hata kama hana uwezo wa kuzaa. Wakati nikiwa mkuu wa chuo cha kichawi pale temeke, tulikuwa tukifundisha watu kwa habari ya mimba za kijini.
Kwa wakati mteja alipokuwa ananijia kwaajili ya kuaguliwa, jinni ambalo lilikuwa ndani yangu lilikuwa linapanda ndani yangu na kwenda na kumwendea mteja alafu husoma taarifa ya mteja. Baada ya muda hutoka kwa mteja na kurudi kuja kuniambia mimi tatizo la mgonjwa huyo. Baada ya hapo nilikuwa namtajia mteja tatizo lake na kumfanya aniamini kuwa nitatatua tatizo lake hapo kila nitachomwambia lazima atafanya.
Baada yakuupata (win) moyo wa mteja, nilikuwa namwagiza vitu mbalimbali vya kufanya na kuniletea kwaajili ya uaguzi. Baada ya siku kadhaa lazima mteja huyo (ambao wengi wao walikuwa wanawake) atarudi kwaajili ya uaguzi. Katika namna hii ya kwanza ya kutengeneza mtoto wa dawa; tulikuwa tunaingiza jini ndani mwanamke na jinni yule alikuwa na uwezo wa kwenda kuiba mtoto katika nyumba ya mtu wa karibu na kumwingiza katika tumbo la mwanamke yule. Matokeo ya aina hii ya mtoto wa dawa ni uwezekano wa wazazi wakitanzania kujikuta wamezaa mzungu au mtoto mwenye sura ya jirani yake.
Madhara ya aina hii, husababisha ile mimba ambayo imeibiwa kwa mtu wajirani kupotea. Na ndio maana unaweza kumwona mtu alikuwa mjauzito lakini baada ya muda mimba ile ikapotea. Na ikitokea yule jini ameshindwa kumpatia mtoto kutoka katika maeneo yale, huamua kujitengenezea nyama kutoka katika mwili wa mwanamke. Matokeo ya aina hii mwanamke anasumbuliwa sana na mimba; unaweza kuta ni muda mfupi tu wa ujauzito lakini mwanamke huyo anakuwa ameshasumbuliwa sana na magonjwa mbalimbali.
Hivyo mtoto kama huyo akizaliwa anakuwa mwili ni binadamu lakini katika roho ni jini asilimia mia moja.
Dalili za kumtambua mtoto wa dawa wa aina hii:-
1. Macho yake hayachezi mfano akigeuka huwa anageuka na shingo yote
2. shingo yake huwa inageuka polepole haigeuki kwa haraka.
3. Macho yake huwa yanameza picha/ ukiangalia kwenye kiini cha jicho lake hakionyeshi picha.
4. Safari zake za muhimu (anazozisisitizia) huelekea upande ambao haangaliani na jua.
5. Ana sifa nyingi zilizojificha/ anaweza kuwa na elimu ya juu lakini haionekani.
6. Huwa anafanya jambo zuri lakini hazingatii wakati:- mfano inawezekana wamekuja wageni nyumbani alafu yeye ndio akaanza kufagia muda ule.
7. Yeye ni mtendaji mzuri sana lakini hapendi kukubaliana. Ya
ani kama ni mtoto unaweza ukamwachia kazi afanye yeye akakataa kwa muda ule lakini jioni ukija utamkuta amefanya vyote.
8. Kwenye mikusanyiko mingi hupenda kuwa wa mwisho kutoka.
9. Ukimwangalia kwenye kipaji cha uso; kama una nguvu za Mungu utamwona kama nyama yake inatetemeka/ inatikisika
10. Huwa hafi. Kwasababu huyu ni jini hivyo hutumika katika mwili kwa muda fulani lakini baada ya muda hupotea tu bila kuonekana.
Hizo ni dalili za mtoto wa dawa anayetengenezwa kwa namna hii:
Swali: kuna madhara gani kwa wanafamilia?
Wanafamilia wanaoishi naye watapata madhara, kwasababu jini/mtoto huyu anaweza kuwa maskani ya majini na mapepo wachafu katika familia. Nakumbuka alikuwepo mama mmoja tanga tuli tulimtengenezea mtoto wa namna hii. Baada ya muda mama yule aliokoka lakini yule mtoto hakuwahi kulipuka mapepo na mara nyingi inaghalimu msaada wa Roho mtakatifu kumsaidia mtu wa namna hii.
Swali; Jini hili laweza kukua na kuwa kiongozi au kuoa?
Kiukweli linaweza kabisa kuwa kiongozi, mbunge, waziri au hata rais. Pia linaweza kuoa pia na kuzaa watoto pia; mfano mwanaume wa kijini akioa mke wa kawaida watoto wake watakuwa na ujini sana. Lakini kama mwanamke ni jini na mwanaume ni binadamu watazaa watoto wanaowasumbua sumbua sana.

KWANINI ALLAH AMBAE SIO YEHOVA ALIOGOPA KUYAAMRISHA MAJINI YAISIKILIZE TAURAT, ZABUR NA INJILI?


ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI MACHAFU YALITUMWA KWA MUHAMMAD ILI KUSIKILIZA QURAN
ALLAH HUYO HUYO ALISEMA KUWA KILA WATU WALIPEWA KITABU CHAO. HAPO TEYARI KUNA SHAKA KWENYE QURAN YA MUHAMMAD AMBAYO SASA INAKABIDHIWA MAJINI MACHAFU.
Allah kasema katika Suratil Ahqaaf aya ya 29 mpaka 32, “
]وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِنْ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنْصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِمْ مُنْذِرِينَ * قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنْزِلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُسْتَقِيمٍ * يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِي اللَّهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * وَمَنْ لا يُجِبْ دَاعِي اللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الأرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِنْ دُونِهِ أَولِيَاءُ أُوْلَئِكَ فِي ضَلالٍ مُبِينٍ[
Maana yake, “Na (wakumbushe) wakati tulipowaleta kundi la Majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana): “Nyamazeni! (Msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha somwa walirudi kwa jamaa zao kwenda kuwaonya. Wakasema “Enyi watu wetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya (Nabii) Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake na kinachoongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mlingani, (Muitaji) wa Mwenyezi Mungu na muaminini, atakusameheni (Mwenyezi Mungu) dhambi zenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na wasiomuitikia Muitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatamshinda (asiwapate) hapa katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele Yake. Hao wamo katika upotofu ulio dhahiri.”
Na kisa kingine ni cha Majini waliosikia Qurani kutoka kwa Mtume S.A.W wakati alipokuwa akiwasalisha Masahaba wake Sala ya Alfajiri. Na hii ilikuwa bila ya yeye kuwa na habari mpaka Mwenyezi Mungu S.W.T. alipomjulisha. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Jin aya ya 1 na ya 2, “
]قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنْ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا[
Maana yake, “Sema: “Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la Majini lilisikiliza (Qurani) likasema: “Hakika sisi tumesikia Qurani ya ajabu. Inaongoza katika uwongofu; kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote tena na Mola wetu.”
Makala haya yametolewa katika kitabu changu kiitwacho, "Hakika ya Majini."
MASWALI KUHUSU MAJINI:
1. Wapi katika Taurat tunajifunza kuwa Majini yaliumbwa ili kumwabudu Mungu?
2. Wapi katika Zaburi Tunafundishwa kuwa Majini yaliumbwa ili ya mwabudu Mungu?
3. Wapi katika Injil tunafundishwa kuwa Majini yaliumbwa ili kuwamudu Mungu?
JE, BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU MAJINI?
Biblia Inasema nini kuhusu uhusiano na Mapepo au Majini
Mungu ametuonya kutokuwa na uhusiano na pepo. Imeandikwa, Mambo ya Walawi 19:31 "Msiwaendee wenye pepo wala wachawi, msiwatafute ili kutiwa unajisi na wao mimi ndimi BWANA Mungu wenu."
Ilikuwa kawaida ya watu wa zamani enzi za Biblia kusali pepo. Mungu aliwaonya wana wa Israeli kuhusu uombaji wa pepo na uchawi. Imeandikwa katika Kumbukumbu la torati 18:9-12 "utakapokwisha ingia katika nchi akupayo BWANA Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto wala asionekane mtu atazamaye mbao wala mtu atazamaye nyakati mbaya wala mwenye kubashiri wala msihiri wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo wala mtu apandishaye pepo wala mchawi wala mtu awaombaye wafu kwa maana mtu atandaye hayo ni chukizo kwa BWANA kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA Mungu wako anawafukuza mbele yako."
Biblia yatupa mwanga kuhusu hali ya pepo. Imeandikwa, katika Matendo ya mitume 16:16-18 "Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele akisema watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu wenye kuwahubiria njia ya wokovu akafanya hayo siku nyingi lakini Paulo akasikitika akageuka akamwambia yule pepo nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo mtoke huyu akamtoka saa ili ile."
Pepo ni wale malaika waliomwasi Mungu kule mbinguni na kutupwa hapa duniani. Imeandikwa katika Ufunuo 12:7-9 "Kulikuwa na vita Mbinguni Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani adanganyaye ulimwengu wote akatupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye."
Kwa sababu pepo za husiana na Shetani, mtu katika israeli angeonekana akifanya pepo ilibidi auawe. Imeandikwa, katika Mambo ya walawi 20:27 "Tena mtu mme au mke aliye na pepo au aliye mchawi hakika atauawa watawapiga kwa mawe damu ya itakuwa juu yao." Isaya 8:19 yasema "Na wakati watakapokuambia tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndeye na kunong'ona je haiwabasi watu kutafuta habari kutoka kwa Mungu waoje! waende kwa watu walio kufa kwa ajili ya watu walio hai?."
JILINDE DHIDI YA MAJINI NA SHETANI
Unaweza kujilinda jinsi gani dhidi ya roho waovu-Majini-Mapepo-Mashetani? Biblia inajibu hivi: “Jitiisheni kwa Mungu; lakini mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia ninyi.” (Yakobo 4:7) Tunatii agizo hilo tunapoishi kupatana na mafundisho yaliyo katika Biblia, kitabu pekee kitakatifu ambacho kinamfichua Shetani, roho waovu, na “hila” zao. (Waefeso 6:11; 2 Wakorintho 2:11) Pia, Biblia inatuambia kwamba roho waovu pamoja na wote wanaompinga Mungu, hawatakuwapo milele. (Waroma 16:20) “Wanyoofu ndio watakaokaa duniani, na wasio na lawama ndio watakaobaki ndani yake,” inasema Methali 2:21.
JE, UMEJIULIZA HIVI?
● Je, Mungu ndiye aliyewaumba roho waovu?—2 Petro 2:4.
● Je, unaweza kuzungumza na wafu?—Mhubiri 9:5, 6.
● Unaweza kujilinda jinsi gani dhidi ya roho waovu?—Yakobo 4:7.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

MUHAMMAD ASEMA: TUMIENI MAWE MATATU KUJISAFISHA BAADA YA HAJA KUBWA


Ndugu msomaji.
Waislam wanasema kuwa eti, Uislam ni muongozo kamili wa maisha. Hakika mimi siutaki huu muongozo wa utumiaji mawe.
Soma:
Baada ya kujisaidia haja kubwa, usitumie mifupa au kinyesi kujisafisha; Bali utumie mawe kujisafisha mwenyewe ... (Sahih Bukhari, 1.4.157)
Utakapo maliza kujisaidia, tumia mawe Matatu kujisafisha sehemu zako za siri ... (Sahih Bukhari, 1. 4.162)
Tumia mawe tatu kwa kujisafisha baada ya kujisaidia ... (Sunaan Abu Dawud, 1.0040)
Baada ya kutembelea choo, beba mawe matatu na uyatumie kujisafisha wewe mwenyewe ... (Sunaan Abu Dawud, 1.1.0040)
Baada ya kujisaidia haja kubwa, tumia udongo mara mbili kujisafisha; wala usitumie kinyesi kujisafisha... (Sunaan Nasai, 1.42)
Kama unajisaidia haja kubwa katika jangwa, basi tumia mawe matatu kujisafisha baada ya haja kubwa, hakuna haja ya kutumia maji ... (Sunaan Nasai, 1.44)
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA NDUGU ZETU WAISLAMU WANAO TUMIA MAWE.

MAISHA BAADA YA KIFO


1. WAISLAM KWENDA JEHANNAM
2. WAKRISTO KUINGIA MBINGUNI
3. WAPAGANI NA WASIO NA DINI KUINGIA JEHANNAM
4. MAJINI NA MASHETANI YOTE KUINGIA JEHANNAM
Je, unaamini kwamba kuna wakati wa hukumu baada ya binadamu kukutwa na mauti?
Ndugu Msomaji,
Nivyema ufahamu nini kitakutokea punde utakapo kata roho/kufa. Swali la muhimu la kujiuliza ni hili hapa: Je, unauhakika wa wapi utakuwa baada ya kifo?
Biblia inatuambia ya kuwa baada ya mtu kufa, hupelekwa mbinguni ya Muda “Peponi” (Sio Mbingu ambayo Mungu yupo sasa ila ni –Abraham’s bosom) au Jehanamu “kuzimuni ya muda-Akhera” kulingana na hoja ya kuwa alikuwa amemkubali ama kumkataa Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wake/wako. Kwa walioamini, kufa ni kuondoka katika mwili na kuenda kukaa na Bwana “to be absent from this body is to be present with the Lord” (Wakorintho wa pili 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa wasioamini, kufa ina maana ya hukumu ya milele Jehanamu (Luka 16:22-23).
Hapa ndipo kwenye utata juu ya ni nini hufanyika baada ya kifo. Kitabu cha Ufunuo Sura 20:11-15 inaeleza juu ya wale walio kuzimu wakitupwa katika ziwa la moto. Ufunuo 21 na 22 inazungumzia juu ya mbingu mpya na dunia mpya. Kwa hivyo ina maana ya kuwa mpaka wakati wa ufufuo wa mwisho, baada ya kufa mtu hubaki katika mahali Fulani kwenye mfano wa mbinguni na kuzimu. Mahali pa mtu anapofaa kukaa milele hapatabadilika ila makazi ya muda yatabadilika “NI KAMA MAHABUSU, HALAFU MTU ANAPELEKWA JELA/ACHIWA”. Muda Fulani baada ya kufa, waumini watapelekwa katika mbingu mpya na nchi mpya (ufunuo wa Yohana 21:1) na wasioamini katika ziwa la moto (ufunuo 20:11-15). Haya ndiyo makao ya milele ya watu yanayotegemea kama mtu alimwamini Yesu Kristo pekee kwa wokovu kutokana na dhambi zake.
Wakati sisi hufa, sisi hupatana na hukumu ya Mungu (Waebrania 9:27). Kwa waumini, kuwa mbali na mwili ni kuwa pamoja na Bwana (2 Wakorintho 5:6-8; Wafilipi 1:23). Kwa makafiri kifo kinamaanisha adhabu ya milele katika jehanamu (Luka 16:22-23). “Makafiri ni wale walio kataa kuwa Yesu ni Mungu”
Mpaka kufufuka kwa mwisho, hata hivyo, kuna Mbinguni ya muda- Peponi (Luka 23:43, 2 Wakorintho 12:04) na kuzimuni ya muda-ahera (Ufunuo 1:18; 20:13-14). Kama inavyoweza kuonekana wazi katika Luka 16:19-31, katika Peponi wala katika Akhera watu hawalali. inanaweza semekana kuwa, mwili wa mtu "unalala" huku nafsi yake ikiwa peponi au kuzimuni. Wakati wa ufufuo, mwili huu "utaamshwa" na kubadilishwa hadi mwili wa milele mtu atamiliki milele, hata kama ni mbinguni au kuzimu. Wale ambao walikuwa katika peponi watapelekwa mbingu mpya na nchi mpya (Ufunuo 21:1). Wale ambao walikuwa katika kuzimu kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:11-15). Hizi ndizo hatima za mwisho na milele ya watu wote ikitegemea ikiwa mtu aliamini katika Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu au la.
Zaidi ya hapo, Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).
YOHANA 14:1-3"Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo , ningaliwaambia ; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali , nitakuja tena nitawakaribishe kwangu ; ili nilipo mimi, nanyi mwepo"
Je kuna haja ya kuogopa kifo??
“Yesu akamwambia, mimi ndiye huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je Unayasadiki hayo?” – John 11:25-26
Je, unaamini kwamba kuna maisha baada ya kifo?
Je, unaamini kwamba kuna wakati wa hukumu baada ya binadamu kukutwa na mauti?
Ikiwa ndivyo, hii ina maanisha kwamba binadamu anaishi baada ya kuondokana na mazingira ya duniani?
Je, anaishije huko?
Anakula, anakunywa, anatembea, anaongea au anasikia?
Vipi ana mwili wa nyama au roho?
Kama roho basi, ataunguaje motoni siku ya hukumu?
Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele?
YESU NDIO NJIA PEKEE YA UZIMA WA MILELE:
Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya Mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).
Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii Mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36).
BAADA YA KUFA HAKUNA NAFASI YA PILI YA KUTUBU:
Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu Msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya Kristo.
JEHANNAM:
Jehanamu, kama vile mbinguni, si mahali patajwapo kwa utisho tu bali ni mahali dhahiri. Hapa ni mahali ambapo wasiohaki watakutana na ghadhabu isiyokoma ya Mungu. Watavumilia mateso ya kihisia, kiakili, na kimwili wakiwa katika akili zao timamu huku wakijihisi kuaibika na kujuta kwa matendo yao maovu.
Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na Ziwa la Moto, liwakalo na kiberiti ambapo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (Mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.
Je unaamini kuwa kunayo maisha baada ya kifo?
Ni nini hufanyika baada ya kufa?
Je! Unaamini kuwa Jahannamu ni kitu cha kweli? Jehannamu ni ya milele?
Je, kuna ngazi mbalimbali za mbinguni?
Je, kuna viwango tofauti vya adhabu jehanamu?
Basi ungani nami katika kijarida kijacho kuhusu Maisha ya Milele.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo
For Max Shimba Ministries Org.

MUHAMMAD AKIRI KUWA YEYE NI NABII WA UONGO NA BANDIA



Muhammad alikiri kuwa yeye hakuwa na uwezo wa kufanya Miujuza
Ndugu zanguni, leo ningependa tusome kidogo kuhusu huyu Muhammad aliye dai kuwa yeye katumwa na Mungu. Hebu soma kwanza:
17. SURA AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
90. Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii.
91. Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika.
92. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyo dai; au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika uso kwa uso.
93. Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume?
(Qur-Sura 17:90-93)
Baada ya kuombwa afanye angalau muujiza mmoja tu, Muhammad alishindwa vibaya sana na kuto fanya hata muujiza mmoja.
Swali:
1. Kwanini Muhammad alishindwa kufanya miujiza kama alivyo ombwa afanye?
2. Muhammad ni Nabii peke yake alieshindwa kufanya Miujiza tokea dunia iumbwe, Je, anafaa kufuatwa na kuaminiwa?
3. Kwanini Allah nayeye hakumsaidia Nabii wake kufanya muujiza?
HAKIKA MUHAMMAD ALIKUWA NABII WA UONGO

Jesus is good because He is God

 

TRENDING NOW