Waisalmu wamekuwa ni watu wa kujivuna kujingamba kuwa wao ndiyo wenye Dini ya kweli, Ibada ya kweli na Mungu wa kweli, na kuwaona wengine kuwa ni wapagani na ni watu wasiojielewa, Kumbe wao waislamu hawajui kuwa Ibada yao hiyo na huyo mungu wao Allah wamerithi kutoka kwa wapagani wa Makka, ambapo walikuwa wakifanya baadhi ya Ibada kama ambazo leo waislamu wanazifanya na pia wakimwabudu mungu wao wa kipagani ambaye leo hii ndiye anaeitikadiwa na waislamu kuwa ndiye Muumba wa mbingu na Nchi.
Katika somo tutaangalia mambo ma 4
1) MUNGU ZAMA ZA UPAGANI
2) JENGO LA AL KAABA
3) IBADA YA KUHIJI WAPAGANI PAMOJA NA WAISLAMU
4) MIEZI YA KUHIJI YA WAPAGANI NA WAISLAMU
Hivyo ni vitu muhimu sana kwa waislamu AMBAPO katika nguzo za Uislamu Shahada ya kumkiri Allah kuwa ni mungu mmoja, ndiyo moyo wa Uislamu,
na Nguzo ya mwisho ya kwenda kuhiji Makka, ni nguzo muhimu sana kwa wale wenye uwezo kwani hupelekea wao kufutiwa madhambi yao yote, kwa mujibu wa Imani yao, kwa hivyo Matajiri na wale wenye uwezo, hufanya maovu sana huchangamkia fursa hiyo ya kwenda kuhiji Makka, ili maovu yao hayo yaweze kusameheka kupitia njia hiyo ya kuhiji
1)ALLAH MUNGU ANAEBUDIWA NA WAISLAMU ALIKUWA MUNGU WA WAPAGANI
Sasa tuanze kumuangalia huyu Allah mungu anaebudiwa na Waisalmu zama zile kabla ya Uisamu alikuwa akiabudiwa na wapagani, na ushahidi huu tunaupata kupiptia kitabu cha MAISHA YA NABII MUHAMMAD, KILICHOANDIKWA NA SHEIKH ABDULLAH SALEH FARSY, UK 57 PARAGRAPH YA 2. AMBAPO katika Paragaph ya 1 kuna habari ya Vita vikubwa ambavyo waislamu walizidiwa na Makureshi, ambao walimshambulia Muhammad kwa mawe na kumg’oa meno ya barazani, na kumzamishia misumari mashavuni, na kisha waislamu kumkimbizia kwenye Jibali ili asiuawe, kisa ikiwa ni Muhammad kutaka kuwabadili wapagani wawe waislamu, Paragraph ya 2 Nainukuu.
"Wakati huo wote walikuwa wamekwisha kupumzika, na makureshi wote wamejikusanya pamoja tayari kwa kuondoka. Mara Masahaba wakasikia sauti ya Abuu Sufyan Mkubwa wa Makureshi inanadi-inasema “Muhammad yu hai au amekufa? Muhammad yu hai au amekufa?? Mtume akawaambia masahaba zake wasimjibu. Mara ikanadi tena, “Abubakari yu hai au amekufa? Abubakar yu hai au amekufa” pakawa jii vile vile pasipatikane jawabu, Ikanadi tena kwa mara ya tatu Ikisema, “Umar yu hai au amekufa? Umar yu hai au amekufa?” Ilivyokuwa Jii Vile vile yule Abu Sufyan alisema, “Wallahi hawa wote wamekwisha kufa.” Sayyidna Umar alishindwa kustahimili kusikia haya alinyanyua sauti na kumijbu, “WOTE HAO UNAOWATAJA WA HAI, WAKO TAYARI KUKUTANA NA WEWE NA MAJESHI YAKO KILA WAKATI”
Abu Sufayan akasema, “Katukuka leo mungu mkubwa wetu-Hubal katukua leo mungu mkubwa wetu-Hubal Vita ni mapokezano siku ya hawa na siku ya wale na siku hii yetu leo ni kwa ile siku siku yenu ya Badr. Enyi Waislamu! Mtaona maiti wenu watu waliokatwa vipande vipande vipande. Mimi sikuamrisha watu wangu kufanya haya, wala sikuwakataza, wala hayakunifurahisa hayo, wala hayakunichukiza. Sasa tunakupeni habari ya kuwa tunakutakeni tena kwa mwaka wa pili mwezi wa shabani katika mtaa wa Badri” Mtume akamwamrisha Sayyidna Umar amjibu “Tayari tutakutana hapo” Tena akainuka Hind mkewe Abu Sufyan akaimba jimbo zake juu ya jabali hili, baada ya haya Abu Sufyan akamrisha watu wake washike njia kwenda zao Makka, baada ya kuwazika maiti wao 23" (MWISHO WA KUNUKUU)
Kwa mujibu wa melezo hayo tunashuhudia kuwa Huyo Abu Sufyan ambaye yeye alikuwa mpagani, aliapa baada ya kutambua kuwa Muhammad na masahaba zake wakubwa yaani Abubakar na Umar kuwa wamekwisha kufa, alisema, Wallahi, Neo HILI Wallahi linahusika leo na Mungu anaebudiwa na waislamu, na hata waislamu nao hauapa vile vile kwa kusema Wallahi kama alivyoapa Abu SUFYAN mpagani, na pia Isitoshe Abu SUFYAN ALISEMA, ametukuka Mungu mkubwa wetu, katika Lugha ya Kiarabu, ni Sub-haana Allahu Akbaru, na hata Leo waislamu pia hutumia kauli hiyo nao wakisema Sub-haaNA LLAHU, na pia husema Allahu akbaru, yaani ametukuka mwenyezi Mungu, Mungu mkubwa, kama alivyokuwa Mungu wa wapagani aliyenadiwa na mpagani ABU SUFYAN, kwa hivyo waislamu wamechukua utukufu wa mungu wa wapagani, na pia nyapo za wapagani juu ya mungu wao mkubwa. Ndiyo maana tunasema Uislamu ni upagani ulioboreshwa.
2) JENGO LA AL-KAABA
Jengo hili Waislamu hulitukuza sana kwa kudai kuwa ni jengo ambalo Ibrahimu wao feki, alilijenga yeye na mwanae Ismaili, miaka mingi. Kwa hivyo huiita nyumba Kongwe, na wakati jengo hilo lilikuwa likifanyiwa Ibada na wapagani ambao walikuwa wamejaza miungu yao nje na na ndani ya Al-kaaba; na hata Muhammad alipozaliwa babu yake alienda kumuombea kwenye hiyo miungu ya wapagani, ambapo palikuwa na miungu mingi midogo na mungu mkubwa alikuwa Hubal, ambapo Abu Sufyan alimsifu kwa kumuapia Wallahi, yaani akimaanisha huyo Hubal ndiye Allah, hebu ngoja tuangalie ushahidi huo wa kuonesha kuwa Al-kaaba lilikuwa ni Jengo la Wapagani kabla ya uislamu.
Katika Kitabu cha MAISHA YA NABII MUHAMMAD UK 3 PARAGRAPH YA 3-4 KINASEMA
A. WAZEE WAKE WANAUME