Friday, September 9, 2016

ALLAH SIO YEHOVA "YAHUH" ( يهوه ) MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA TANO)

ALLAH ANAAPA KWA YEHOVA ALIYE UMBA KIUME NA KIKE
ALLAH SIO YEHOVA "YAHUH" ( يهوه ) MWENYEZI MUNGU
(SEHEMU YA TANO)
Je Nani kaumba Kiume na Kike?
QURAN 92 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..
Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu? Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa katika aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah hakuumba.
Je, ni nani huyu aliye umba Kiume na Kike ambaye Allah wa Islam anaapa kwake? Endelea kusoma...kutoka Biblia Takatifu….
Yeremia 27: 5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Sasa tunamsoma Yehovah ambaye ni Mungu wa Biblia kuwa yeye ndie aliye umba kila kitu, pamoja na Kiume na Kike ambacho Allah wa Islam anaapa kwake. Kwahiyo, Jehovah aliumba kiume na kike, na Allah wa Islam anaapa kwake, sasa jaza mwenyewe nani ni Mungu?
Je, Mungu anaweza kuapa kwa Mwengine? Endelea kupata elimu …
Waebrania 6:13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
Jehova anasema hakuna Mkubwa wangu wa kuapa kwake, lakini Allah katika Kuran anasema kuwa yeye anaapa kwa aliye umba kiume na kike.
Hivyo basi leo tunafahamu kuwa aliye umba ni Jehona na Allah anaapa kwa Jehovah Mungu wa Biblia na Wakristo.
Kumbe Allah sio Mwenyezi Mungu.
Mungu awabairiki sana
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW