Na Abel Suleiman Shiliwa.
Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza na ya pili ya somo la Yesu Kristo hakuwa muislamu, leo naendelea na sehemu ya tatu ya somo hili, ambapo nitagusia vipengele viwili.
(1) Kutawadha
(2) Kusujudu
Hivyo pia ni vipengele ambavyo waislamu hudai kuwa Yesu alikuwa muislamu, nikianza na Kutawadha, andiko ambalo wao hulitumia ni hili.
Yohana 13:5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Andiko hilo waislamu hulitumia sana, kunasibisha kutawadha kwao, na kwa YESU, wakisema kwamba, Yesu alitawadha (japo andiko halisemi hivyo) pia hudai Yesu amesema, mtu ambae hatawadhi basi hana shirika na Yesu, wao ambao hutawadha, husema kwamba ndiyo wenye shirika na Yesu, Wakristo ambao ni wavivu wa kusoma maandiko, wakisomewa hivyo, basi huamua kusilimu, wakiamini kwamba, Wakienda kwenye Uislamu, basi watakuwa na shirika na Yesu, kwa kutawadha, kitendo ambacho siyo kweli.
NENO TAWADHA lina maana ya Nawa, au Oga! tendo hilo la kutawadha kwa waislamu hutafsirika kama kunawa mbele ya kusali, yaani kabla hawajasali, hutawadha kuchukua udhu! Lakini kwa Wayahudi ni tofauti kabisa, wakati wa Musa, walio tawadha alikuwa ni Haruni na Wanae.
Kutoka 30:17 Bwana akanena na Musa, na kumwambia
18 Fanya na birika la shaba, na tako lake la shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji.
19 Na Haruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo;
20 hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike, kumteketezea Bwana sadaka ya moto;
21 basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.
Kwa hao waliokuwa na kazi ya Ukuhani, walitakiwa kuosha mikono na miguu tu, ili wasife, Musa yeye hakuambiwa afanye hivyo kwa sababu hakuwa Kuhani,
Tawadha ya Waislamu wao, huosha viungo vifuatavyo.