Friday, October 7, 2016

YESU KRISTO HAJAWAHI KUWA MUISLAMU NA KAMWE HATOKUJA KUWA MUISLAMU (SEHEMU YA TATU)


Na Abel Suleiman Shiliwa.
Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza na ya pili ya somo la Yesu Kristo hakuwa muislamu, leo naendelea na sehemu ya tatu ya somo hili, ambapo nitagusia vipengele viwili.
(1) Kutawadha
(2) Kusujudu
Hivyo pia ni vipengele ambavyo waislamu hudai kuwa Yesu alikuwa muislamu, nikianza na Kutawadha, andiko ambalo wao hulitumia ni hili.
Yohana 13:5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Andiko hilo waislamu hulitumia sana, kunasibisha kutawadha kwao, na kwa YESU, wakisema kwamba, Yesu alitawadha (japo andiko halisemi hivyo) pia hudai Yesu amesema, mtu ambae hatawadhi basi hana shirika na Yesu, wao ambao hutawadha, husema kwamba ndiyo wenye shirika na Yesu, Wakristo ambao ni wavivu wa kusoma maandiko, wakisomewa hivyo, basi huamua kusilimu, wakiamini kwamba, Wakienda kwenye Uislamu, basi watakuwa na shirika na Yesu, kwa kutawadha, kitendo ambacho siyo kweli.
NENO TAWADHA lina maana ya Nawa, au Oga! tendo hilo la kutawadha kwa waislamu hutafsirika kama kunawa mbele ya kusali, yaani kabla hawajasali, hutawadha kuchukua udhu! Lakini kwa Wayahudi ni tofauti kabisa, wakati wa Musa, walio tawadha alikuwa ni Haruni na Wanae.
Kutoka 30:17 Bwana akanena na Musa, na kumwambia
18 Fanya na birika la shaba, na tako lake la shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji.
19 Na Haruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo;
20 hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike, kumteketezea Bwana sadaka ya moto;
21 basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.
Kwa hao waliokuwa na kazi ya Ukuhani, walitakiwa kuosha mikono na miguu tu, ili wasife, Musa yeye hakuambiwa afanye hivyo kwa sababu hakuwa Kuhani,
Tawadha ya Waislamu wao, huosha viungo vifuatavyo.

(2) mikono
(2) Mdomo
(3) Pua
(4) Uso
(5) Miguu
(6) Kichwa
(7) Masikio
Wakiosha mikono na miguu tu hauwi udhu huo, na tena wao wakikosa maji hutumia mpaka mchanga.
Quran Suratul Maidah
ﻳَﺎ ﺃَﻳُّﻬَﺎ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺁﻣَﻨُﻮﺍْ ﺇِﺫَﺍ ﻗُﻤْﺘُﻢْ
ﺇِﻟَﻰ ﺍﻟﺼَّﻠﻮﺓِ ﻓﺎﻏْﺴِﻠُﻮﺍْ ﻭُﺟُﻮﻫَﻜُﻢْ
ﻭَﺃَﻳْﺪِﻳَﻜُﻢْ ﺇِﻟَﻰ ﺍﻟْﻤَﺮَﺍﻓِﻖِ ﻭَﺍﻣْﺴَﺤُﻮﺍْ
ﺑِﺮُﺅُﻭﺳِﻜُﻢْ ﻭَﺃَﺭْﺟُﻠَﻜُﻢْ ﺇِﻟَﻰ ﺍﻟْﻜَﻌْﺒَﻴﻦِ
ﻭَﺇِﻥ ﻛُﻨﺘُﻢْ ﺟُﻨُﺒًﺎ ﻓَﺎﻃَّﻬَّﺮُﻭﺍْ ﻭَﺇِﻥ ﻛُﻨﺘُﻢ
ﻣَّﺮْﺿَﻰ ﺃَﻭْ ﻋَﻠَﻰ ﺳَﻔَﺮٍ ﺃَﻭْ ﺟَﺎﺀ ﺃَﺣَﺪٌ
ﻣَّﻨﻜُﻢ ﻣِّﻦَ ﺍﻟْﻐَﺎﺋِﻂِ ﺃَﻭْ ﻻَﻣَﺴْﺘُﻢُ ﺍﻟﻨِّﺴَﺎﺀ
ﻓَﻠَﻢْ ﺗَﺠِﺪُﻭﺍْ ﻣَﺎﺀ ﻓَﺘَﻴَﻤَّﻤُﻮﺍْ ﺻَﻌِﻴﺪًﺍ
ﻃَﻴِّﺒًﺎ ﻓَﺎﻣْﺴَﺤُﻮﺍْ ﺑِﻮُﺟُﻮﻫِﻜُﻢْ ﻭَﺃَﻳْﺪِﻳﻜُﻢ
ﻣِّﻨْﻪُ ﻣَﺎ ﻳُﺮِﻳﺪُ ﺍﻟﻠّﻪُ ﻟِﻴَﺠْﻌَﻞَ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢ ﻣِّﻦْ
ﺣَﺮَﺝٍ ﻭَﻟَﻜِﻦ ﻳُﺮِﻳﺪُ ﻟِﻴُﻄَﻬَّﺮَﻛُﻢْ ﻭَﻟِﻴُﺘِﻢَّ
ﻧِﻌْﻤَﺘَﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻜُﻢْ ﻟَﻌَﻠَّﻜُﻢْ ﺗَﺸْﻜُﺮُﻭﻥَ
6. Enyi mlioamini! mnaposimama kwa (ajili
ya ) swala, basi osheni nyuso zenu, na mikono
yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu
na miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na
janaba, basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au
safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au
mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji,
basi tayamamuni mchanga ulio safi na mpake
nyuso zenu na mikono yenu Mwenyeezi Mungu
hapendi kukutieni katika taabu, lakini anataka
kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili
mpate kushukuru.
Hiyo ndiyo tawadha ya waislamu, wanapotaka kusali, ikitokea wana janaba (wamefanya ngono) au wametoka chooni, wakataka kutawadha wakakosa maji basi watayamamu, kwa kutumia mchanga, mchanga wenyewe waupake usoni! chooni kimetumika kingine kutoa kinyesi, ila mchanga unapakwa usoni!
kilichomwingilia mwanamke ni kingine, halafu mchanga unapakwa usoni, (sitaki kukaa sana hapo) hiyo ndiyo tawadha ya waislamu.
Tawadha kwa Wayahudi ni tofauti kabisa na Tawadha ya Waislamu.
Historia inaonyesha kuwa katika nchi ya uyahudi ambayo hali ya jangwa sehemu ya mazingira yake kulikua na vumbi sana hivyo walikua wanaweka mabalasi ya kutawadhia ili watu wanawe sio mikono tuu bali hata miguu ili wawe safi ndio waingie ndani ya nyumba ya mtu
Yohana 2:6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
Kwa hivyo kutawadha hakujaanza na waislamu bali kulikuwepo hata kabla ya uislam hivyo kutawadha kusihusishwe na uislamu kwa kuwa wayahudi ndio chimbuko la destuli hii ya kutawadha na bila shaka hata sasa wayahudi wanadumisha destuli hii.
Tawadha ya Yesu kwa wanafunzi ilikuwa na funzo kubwa la utumishi! yaani kutumikiana! na alifanya jambo hilo wakati wa Chakula cha jioni, na siyo wakati wa kusali.
Yohana 13:1 Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.
2 Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti;
3 Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
HILO TENDO LA KUWATADHA WANAFUNZI YESU HAKUWAHI KULIFANYA, ALIVYOANZA KUWATADHA WANAFUNZI WAKE, WENGINE WALIRIDHIA, ALIPOENDA KWA PETRO, IKAWA HIVI
6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
PETRO ALIONA KWAMBA, YEYE KUTAWADHWA NA BOSI WAKE, NI KITENDO CHA KUJIDHALILISHA KWA YESU, ALITAKA WAO WANAFUNZI NDO WAMTAWADHE YESU, ALIPOTIA SHAKA YESU AKASEMA, NILIFANYALO UTALIFAHAMU BAADAE, YAANI ARIDHIE KUTAWADHWA NA BOSI WAKE HUYO, BAADA YA TUKIO HILO, BAADAE ATAJUA MAKUSUDI YA YESU KUWATADHA, BADALA YA WAO KUMTAWADHA YEYE PETRO HAKURIDHIKA
8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.
PETRO ALIPOONA VILE, AKAONA KWA NIMI AWE NJE NA USHIRIKA WA YESU, AKATAKA YESU ASIISHIE TU KWENYE MIGUU, BALI NA KICHWA CHAKE PAMOJA NA MIGUU, YESU AKAMJIBU
10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.
YESU AKAFUNDISHA KUWA MTU ALIYEKWISHA KUOGA ANATAKIWA KUTAWADHA MIGUU TU, SASA JE! WAISLAMU HUFANYA HIVYO? WAO WAWE WAMEOGA WAWE HAWAJAOGA, NI LAZIMA WATAWADHE VIUNGO VYOTE, KUONYESHA KWAMBA WAPO TOFAUTI NA MAFUNDISHO YA YESU
11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.
12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
BAADA YA YESU KUMALIZA KUWATAWADHA, WANAFUNZI WAKE, HAPO KAWAULIZA SWALI, JE! WANAJUA HICHO ALICHOWATENDEA? AKAAMUA KUSEMA DHUMUNI LAKE
13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
Yesu hapo alikuwa anawapa kielelezo wanafunzi wake, kwamba, yeye atakapoondoka, asije akainuka mmoja wao na kujifanya yeye ndiye mkubwa, akataka atumikiwe, bali akawataka wote wajione sawa, watumikiane, waheshimiane, mkubwa ajishushe kwa wadogo, ndiyo maana akasema, "Mimi niliye mwalimu na Bwana nimewatendea hivi, imewapasa ninyi nanyi kutendeana hayo, tawadha hiyo haikuwa na mahusiano na kusali, maana alifanya hivyo wakati wa Chakula.
Na katika maandiko hayo , hakuna sehemu ambayo Yesu ametawadha, ni ajabu sana kuona Waislamu wakilihusisha tendo hilo na Uislamu, ni Lini na wapi Muhammad aliwahi kuwatawadha masahaba zake? Au ni msikiti gani Duniani ambapo Waislamu wao kwa wao hutawadhana? Ili tujue kwamba tendo hilo ni Uislamu? tunawaona waislamu wakigombea makopo kila mmoja anajitawadha mwenyewe, hivyo ni uongo ulio dhahiri kusema kwamba Yesu alikuwa Muislamu, kwa tendo tu la kuwadha wanafunzi wake.
(2) KUSUJUDU
Huo pia ni miongoni mwa uongo wa waislamu, hudai kwamba Yesu alisujudu, kwa mujibu wa andiko hili.
Mathayo 26:38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Hapo kwenye kuomba wao husema akasujudu, na tena wametengeneza mpaka picha ya Yesu akisujudu kama wanavyofanya wao, japo andiko halisemi kwamba Yesu alisujudu, bali akaanguka kifulifuli (Kifudifudi)
Kusujudu:- ni tendo ambalo linahusisha viungo vifuatavyo.
Magoti
viganja vya mikono
Vidole vya miguuni
Uso
pua.
Viungo vyote hivyo ni lazima viguse chini, mahali ambapo unapatumia kusujudia, wakati huo tumbo, mikono kifua mapaja havigusi chini.
Kifulifuli:- Ni kulala hali ya kuwa tumbo, mikono, mapaja, kifua, uso vipo chini, ni tukio la kuomboleza, mtu mwenye huzuni hulala kifulifuli, ishara ya kuhuzunika.
Kuanguka kifulifuli, siyo kusujudu, Yesu hajawahi kusujudu, bali yeye alisujudiwa.
Mathayo 2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Mathayo 28:17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Yohana 9:35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?
37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.
Kwa hivyo YESU KRISTO hajawahi kuwa muislamu, wala hajawahi kusujudu, na hata kama ingetokea akasujudu, bado isingekuwa ni sababu ya kuwa muislamu, kwa sababu kusujudu siyo Uislamu.
Usikose sehemu ya 4 ya somo hilo, ili ujue kama hakuwa muislamu alikuwa nani? na mtu anakuwaje muislamu?

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW