Qur’an 46;9 (Surat Al-Ahqaf) Sema; mimi si kiroja (mpya) katika mitume wala sijui nitakavyofanywa, wala mtakavyofanywa ninyi, sifuati yaliyofunuliwa kwangu, sikuwa mie lolote, ila ni muonyaji tu ninayedhihirisha.
Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema, Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, “Hakuna yeyote miongoni mwenu atayeokolewa na amali yake” Wakasema hata wewe mtume wa Allah? Mtume (S.A.W) akasema, “Wala mimi isipokuwa anifunike Allah kwa rehema zake; hivyo fanyeni amali njema kwa uadilifu” (Bukhari Hadithi Na. 470, Juzuu ya
Hadithi ya Aisha kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Fanyeni yaliyo sahihi na yatekelezeni, na furahini kwa kuwa hakuna yeyote atakayeingiziwa peponi kwa amali (matendo) yake” Wakauliza ‘hata wewe mtume wa Allah?’ Mtume (s.a.w) akasema, ‘Hata mimi isipokuwa kama Allah atanifunika kwa rehema zake” (Bukhari Hadihthi Na. 474, Juzuu ya
Sasa kama mtume mwenyewe hajui hatima yake siku ya mwisho kuna haja gani Wakristo tunaojitamua kuufuata UISLAMU? Yaani tumwache Yesu mwenye uhakika na watu wake na kile atakachowapa wanaomfuata
Yohana 10;27-28
27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
28 Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
28 Nami nawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Eti tuufuate Uislamu chini ya kiongozi Muhammad ambaye hajui hatima yake kama ataenda peponi, au ataenda motoni, bila shaka kwa Mkristo anayejitambua hawezi kuwa Muislamu.
No comments:
Post a Comment