Wednesday, October 5, 2016

WAHUKUMIWA KUCHARAZWA VIBOKO 80 KWA KUTUMIA MVINYO KATIKA MEZA YA BWANA


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake….(Wakolosai 1:24)

Na Joseph DeCaro, Tehran, Iran



Mwezi huu mahakama ya Iran mjini Rasht, imewahukumu Wakristo wanne kuchapwa viboko 80 kila mmoja.

“Kosa”  lao ni kukutwa wakitumia mvinyo kukomunika, kitendo ambacho huashiria kumwagika kwa damu ya Yesu msalabani aliposulubiwa.


Lakini  waendesha mashtaka wa Iran wamewatuhumhao Behzad Taalipasand, Mehdi Omidi, Mehdi Dadkhah na Amir Hatemi kuwa waliwakuta wakinywa pombe; Wakristo hao walipatikana na hatia hiyo Jumapili na sasa wana siku kumi tu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, kwa mujibu wa Christian Solidarity Worldwide (CSW), ambayo ni taasisi ya Kikristo ya utetezi wa uhuru wa kuabudu.

"Hukumu iliyotolewa kwa waumini hao wa dini ya Kikristo inaingilia uhuru wao wa kuabudu. Inaingilia uhuru wa kutekeleza matakwa ya imani yao,” alisema Mervyn Thomas, Mtendaji Mkuu wa CSW.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Oktoba, mwaka huu vitendo vya kuteswa Wakristo, hasa Waislamu wanaobadili dini na kuwa Wakristo, vinazidi kuongezeka.

"Mamlaka za serikali zimeendelea kuyanyanyasa makanisa hata ambayo yamesajiliwa. Makanisa mengi yamelazimishwa kufungwa…zaidi ya Wakristo 300 wamekamatwa tangu mwaka 2010 na viongozi mbalimbali wa makanisa na waumini wakereketwa wamekamatwa wakihusishwa na kufanya huduma kama vile kufanya maombi na kuhudhuria semina za kiroho nje ya nchi.”

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW