Siku Moja Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu kubwa sana ya dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Kisha akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, ambayo aliyoisimamisha.
Akamwamuru mpiga mbiu kwamba awapigie kelee watu wa kabila zote na taifa na lugha kwamba wakati watakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, ambayo mfalme Nebukadreza ameisimamisha. Ikatolewa tangazo kwamba kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
Hivyo Basi watu wote chini ya Mbingu walipoisikia sauti ya panda na filimbi, na kinubi na zeze na namna zote za ngoma wakaanguka kuisujudia ile sanamu ambayo Mfalme aliisimamisha. Lakini Marafiki zake Daniel ambao ni Shedrak na meshak na Abednego walikataa kuisujudia ile sanamu ya mfalme wakawa wakali wamesimama. Ndipo wakaldayo wakawashtaki hao wayahudi watatu kwamba wameikaidi amri ya Mfalme.
Mfalme aliposikia alikasirika sana. Akaamuru watu hao waitwe naye akawaambia hivi;”- Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Wakina Shedrack na Meshak na Abednego wakamjibu mfalme kwamba hawataisujudia sanamu aliyoisimamisha mfalme na Kwamba Hata kama Mungu akiwaokoa ama la hawataisujudia ile sanamu kamwe. Mfalme alikasirika sana akaamuru Moto uchochewe mara saba na kisha akaamuru mashujaa wa jeshi lake wawafunge Wayahudi wale watatu na kisha kuwatupa katika lile tanuru la Moto. Ndipo wayahudi wale watatu wakatupwa katika lile tanuru la Moto hali wamefungwa.
Cha ajabu ni kwamba wale waliowatupa waliungua wakafa papo hapo walakini wale wayahudi watatu waliotupwa hawakuungua hata unywele tu na Moto haukuwa na Nguvu juu yao. Mungu alimtuma Mwana wake kuwaokoa akina Shedrack na Meshak na Abednego, na Mfalme alipoliangalia tanuru aliona watu wane badala ya watatu na yule wa Nne ni kama Mwana wa Miungu.
Ndipo mfalme akaamuru watu wale watolewe. Mungu aliwatukuza wale Marafiki zake Daniel mbele ya mfalme mpagani na watu wa babeli.Mfalme akaona ukuu wa Mungu na akamtukuza Mungu wa Mbinguni na kuamuru kuwa watu wote katika ufalme wake wasimtumikie Mungu mwingine isipokuwa Mungu wa Shadrak, meshak na Abednego.
Kisa hiki kinatufundisha kuwa imetupasa kuwa waaminifu kwa Mungu bila kukengeuka hata nukta ya maagizo yake hata kama kwa kufanya hivyo itaugharimu uhai wetu. Imewapasa watu wa Mungu waone kuwa ni bora kufa kuliko kuasi maagizo ya Mungu. Walakini Mungu aliyewaokoa wale wayahudi watatu atakuwa pamoja na watu wake naye atawaokoa wale wote walio waaminifu kwake.
Siku Moja Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu kubwa sana ya dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. Kisha akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, ambayo aliyoisimamisha.
Akamwamuru mpiga mbiu kwamba awapigie kelee watu wa kabila zote na taifa na lugha kwamba wakati watakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, ambayo mfalme Nebukadreza ameisimamisha. Ikatolewa tangazo kwamba kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao.
Hivyo Basi watu wote chini ya Mbingu walipoisikia sauti ya panda na filimbi, na kinubi na zeze na namna zote za ngoma wakaanguka kuisujudia ile sanamu ambayo Mfalme aliisimamisha. Lakini Marafiki zake Daniel ambao ni Shedrak na meshak na Abednego walikataa kuisujudia ile sanamu ya mfalme wakawa wakali wamesimama. Ndipo wakaldayo wakawashtaki hao wayahudi watatu kwamba wameikaidi amri ya Mfalme.
Mfalme aliposikia alikasirika sana. Akaamuru watu hao waitwe naye akawaambia hivi;”- Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Wakina Shedrack na Meshak na Abednego wakamjibu mfalme kwamba hawataisujudia sanamu aliyoisimamisha mfalme na Kwamba Hata kama Mungu akiwaokoa ama la hawataisujudia ile sanamu kamwe. Mfalme alikasirika sana akaamuru Moto uchochewe mara saba na kisha akaamuru mashujaa wa jeshi lake wawafunge Wayahudi wale watatu na kisha kuwatupa katika lile tanuru la Moto. Ndipo wayahudi wale watatu wakatupwa katika lile tanuru la Moto hali wamefungwa.
Cha ajabu ni kwamba wale waliowatupa waliungua wakafa papo hapo walakini wale wayahudi watatu waliotupwa hawakuungua hata unywele tu na Moto haukuwa na Nguvu juu yao. Mungu alimtuma Mwana wake kuwaokoa akina Shedrack na Meshak na Abednego, na Mfalme alipoliangalia tanuru aliona watu wane badala ya watatu na yule wa Nne ni kama Mwana wa Miungu. Ndipo mfalme akaamuru watu wale watolewe. Mungu aliwatukuza wale Marafiki zake Daniel mbele ya mfalme mpagani na watu wa babeli.Mfalme akaona ukuu wa Mungu na akamtukuza Mungu wa Mbinguni na kuamuru kuwa watu wote katika ufalme wake wasimtumikie Mungu mwingine isipokuwa Mungu wa Shadrak, meshak na Abednego.
Kisa hiki kinatufundisha kuwa imetupasa kuwa waaminifu kwa Mungu bila kukengeuka hata nukta ya maagizo yake hata kama kwa kufanya hivyo itaugharimu uhai wetu. Imewapasa watu wa Mungu waone kuwa ni bora kufa kuliko kuasi maagizo ya Mungu. Walakini Mungu aliyewaokoa wale wayahudi watatu atakuwa pamoja na watu wake naye atawaokoa wale wote walio waaminifu kwake.
SWALI:
Kwenye Dan 2:38, nini inaweza kuwa ni sababu ya Danieli kusema kuwa Nebukadneza alitawala wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani?