Wakati hatuwezi kuwa na hakika kabisa kwa nini Yuda alimsaliti Yesu, baadhi ya mambo fulani ni halisi. Kwanza, ingawa Yuda alichaguliwa kuwa mmoja wa wale kumi na wawili (Yohana 6:64),ushahidi wote wa maandiko matakatifu unaashiria kwamba kamwe hakuamini kuwa Yesu ni Mungu. Yeye pengine hata hakushawizika kwamba Yesu alikuwa Masihi (kama Yuda alivyoelewa). Tofauti na wanafunzi wengine waliomwita Yesu "Bwana," Yuda kamwe hakutumia jina hili kwa Yesu na badala yake alimwita "Mwalimu," ambalo lilimtambua Yesu kama tu mwalimu. Wakati wanafunzi wengine mara kwa mara walifanya fani kubwa ya imani na uaminifu (Yohana 6:68; 11:16), Yuda kamwe hakufanya hivyo na alionekana kuwa kimya. Ukosefu huu wa imani katika Yesu ni msingi kwa masuala mengine yote yaliyoorodheshwa hapa chini. Ukweli sawa na huu unatangamana nasi. Kama tutashindwa kutambua Yesu kama Mungu mwenyewe, na kwa hiyo tu wa pekee ambaye anaweza kutoa msamaha kwa ajili ya dhambi zetu-na wokovu wa milele ambao huja na hilo- tutakuwa chini ya matatizo mengine mbalimbali ambayo yanatokana na mtazamo mbaya wa Mungu.
Pili, Yuda si tu alikosa imani katika Kristo, lakini pia alikuwa na uhusiano kidogo wa kibinafsi na Yesu au aliukosa. Wakati muhtasari wa injili unaorodhesha kumi na wawili, wameorodheshwa kwa mpangilio sawa na uwiano wao(Mathayo 10: 2-4; Marko 3: 16-19; Luka 6: 14-16). Mpangilio wa jumla umeaminika kuonyesha utangamano wa karibu wa uhusiano wao kibinafsi na Yesu.Licha ya tofauti, Petro na ndugu zake Yakobo na Yohana daima walioorodheshwa kwanza, ambayo ni sawa na mahusiano yao na Yesu. Yuda daima alitajwa mwisho, ambayo inaweza kuonyesha ukosefu wake wa uhusiano binafsi wa karibu na Kristo. Kwa kuongezea, kumbukumbu ya pekee ya mazungumzo kati ya Yesu na Yuda inahusisha Yuda kukemewa na Yesu baada ya usemi wake kwa Mariamu uliochochewa na tama yake(Yohana 12: 1-8), Yuda kukataliwa na usaliti wake (Mathayo 26:25), na usaliti wenyewe (Luka 22:48).
Tatu, Yuda alitawaliwa na tamaa kwa kiwango cha kusaliti uaminifu sit u wa Yesu, bali pia wanafunzi wenzake, kama tunavyoona katika Yohana 12: 5-6.Pengine Yuda angetamani kumfuata Yesu kwa sababu tu yeye aliona umati mkubwa uliomfuata na akaamini angeweza kufaika kutoka kwa makusanyo yaliyochukuliwa kwa ajili ya kikundi. Ukweli kwamba Yuda alikuwa msimamizi wa mfuko wa pesa kwa ajili ya kundi ingeonyesha haja yake katika fedha (John 13:29).