Ndugu zanguni:
Leo ningependa tuangalie kiundani kidogo kuhusu, “nani alikuwa Muislam wa Kwanza” kutokana na Koran iliyo teremshwa na Allah.
Kwa mujibu wa vifungu kadhaa katika Quran, Muhammad ni Muislamu kwanza :
Quran 6: 14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 161. Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. 162. Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. 163. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. (Wa ' Ana ' Awwalu Al- Muslimin ). S. 6:161-163
Sema (Ewe Muhammad): Hakika Mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, kwa kumsafishia Dini Yeye ( tu ). Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wale ambao ni Waislamu ( kujisalimisha kwake ). S. 39:11-12 Pickthall
Sura hizo hapo juu na aya hizo ulizo zisoma zinapingana vibaya sana na sura zingine katika Koran hiyo hiyo ambazo ziliteremshwa na Allah huyo huyo na kusema Manabii walio tangulia kabla ya Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
Kuran inadai kwamba Adam, Ibrahim, Nuhu, mababu, makabila kumi na mawili ya Israeli, Musa, Yesu nk, hao wote walikuwa waumini wa Allah na walikuwa Waislam, kumbuka hao wote waliishi kabla ya Muhammad ambaye anadai kuwa yeye ni Muislam wa Kwanza: