Sunday, September 10, 2017

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU








Ili tuweze kuwa mashahidi wa Mungu,tunahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka na kutakaswa. Ili tumtendee Mungu kazi kikamilifu, ni lazima tupokee nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8;Luka 24:49). Kwa sababu hili, somo hili, ni la muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mtendakazi mzuri wa Mungu. Tutaligawa somo hili katika vipengere vinne:-
A. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
B. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
C. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
D. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
E. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
F. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
A. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Baada ya mtu kuokolewa,inambidi kubatizwa kwa maji kwa jina la baba,Mwana na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19). Hata hivyo,huo siyo ubatizo wa mwisho.Baada ya mtu kutakaswa,anahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:11) Ubatizo wa maji, unamfanya mtu azamishwe ndani ya maji na kuzungukwa na maji pande zote. Vivyo hivyo, Ubatizo wa Roho Mtakatifu unamfanya mtu aliyeokoka,kuzamishwa ndani ya Roho Mtakatifu na kuzungukwa na Roho Mtakatifu pande zake zote.Roho Mtakatifu,anakuwa msaidizi wake (Yohana 15:26). Ubatizo wa maji,tunabatizwa na wanadamu waliopewa Agizo la Mungu lakini Ubatizo wa Roho Mtakatifu, tunabatizwa na Yesu mwenyewe (Mathayo 3:11).
B. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU, UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
Neno “mashahidi” katika (Matendo 1:8), linatokana na neno la lugha ya Kiyunani “Martus” ambalo linatafsiriwa katika Kiingereza" Martyr” ambalo maana yake ni “Mtu anayekuwa tayari kuteswa sana au hata kuuawa kwa sababu ya imani yake,pamoja na hayo, hawezi kuiacha imani yake”.Bila ubatizo wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kuwa mashahidi kama walivyokuwa Stefano na Antipa (Matendo 22:20; Ufunuo 2:13). Kabla ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu,Petro alisema asingemkana Yesu hata ikibidi kuuawa, lakini kinyume chake alimkana mara tatu,na yeye pamoja na wanafunzi wenzake walipoyaona mateso yanakuja,walimwacha na
kumkimbia Yesu (Mathayo 26:31-35,56) Lakini baada ya ubatizo walikuwa na ujasiri mkubwa. Matendo 4:13
C. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
§ Maji (Yohana 7:37-39)Hakuna maisha bila ya maji.Mwanadamu ni asilimia 60%maji.Kuharisha na kutapika sana humfanya mtu kupoteza maji mengi na huweza kusababisha mtu kupoteza uhai. Vilevile sisi tunaosema tumeokoka, hatuwezi kabisakuwa na maisha ya kiroho yaliyo hai yenye nguvu, bila Ubatizo wa Roho Mtakatifu.Ni lazima tunyweshwe Roho (1Wakorintho 12:13).
Jambo jingine, maji ni muhimu katika usafi wa miili yetu hutuondolea kunuka n.k Roho Mtakatifu hutumulikia dhambi au uchafu wowote.
§ Moto (Mathayo 3:11).Kuwepo kwa moto ni alama ya uwepo wa Mungu (Kutoka 3:1-5; Matendo 2:2-3). Moto vilevile,unangarisha madini kama dhahabu na fedha (Malaki 3:2-3). Ubatizo wa Roho Mtakatifu hufanya uwepo wa Mungu uwe dhahiri kwa mtu na pia humng’arisha mtu na kuwa mtumishi wa Mungu anayeng’aa . Siyo hayo tu, moto huleta mwanga.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa mwanga mkubwa wa maandiko yaani Biblia na kutupa mwanga wa uzuri wa mbinguni na ubaya wa Jehenam.Ukiwa na mwanga huo hakutakuwa na gharama kubwa yoyote ya kukufanya ushindwe kufanya mapenzi ya Mungu. Moto pia huleta nguvu ya kuendesha, magari, treni, Ndege n.k vifaa vyote hivyo huendeshwa kutokana na moto unaotokea baada ya cheche za umeme kuunguza mafuta.
Kazi ya Mungu inaendeshwa kwa nguvu ya moto, ubatizo wa Roho Mtakatifu na kwa moto. Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu, moto unawake ndani yake na hawezi kuacha kushuhudia au kuhubiri na kufundisha (Yeremia 20:9; Isaya 62:1; Matendo4:20). Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu,maneno yake huwa moto unaoteketeza kila ugumu wa mioyo ya watu kwa kuwa Roho Mtakatifu hushuhudia pamoja naye na hivyo matokeo yake ya utumishi wake huwa makubwa. Ni nguvu kwa ajili ya Utumishi (Yeremia 5:14; Yohana 15:26-27;16:6-8;Mika 3:8).
§ Upepo (Yohana 3:8) Upepo wakati wote unatembea, na uko mahali pote. Roho Mtakatifu hakufanya kazi wakati wa mitume tu, hata sasa anatembea na yuko kwetu tayari, ni wajibu wetu kumpokea tu. Upepo huvuma upendako.
Ni vigumu kuubadilisha mkondo wa upepo tunavyotaka sisi,jahazi hufuata mkondo wa upepo. Ni muhimu kutakaswa kwanza kabla ya Ubatizo huu.
Utakaso humfanya mtu kuwa mtii mno katika yote na Roho Mtakatifu ni mshirika wa wale wamtiio(Matendo 5:32) Upepo pia hutuletea hewa safi inayotuburudisha wakati wa joto, moshi n.k Mazingira yoyote magumu tukiyakabili katika utumishi wa Mungu, Roho Mtakatifu huwa hewa safi kwetu inayorekebisha mazingira.
§ Mafuta (Luka 4:16-21) Roho Mtakatifu hututia mafuta au kutuweka katika utumishi wa Mungu (1Samweli 16:13; Kutoka 30:30; 1Wafalme 19:16;Yohana 2:27) Rais kabla hajaapishwa huitwa Rais mteule na hana mamlaka sana wakati huo kisheria.
Kuapishwa kwa leo ndiyo kutiwa mafuta kwa zamani.Bila ubatizo huu,mamlaka yetu huwa hafifu. Mafuta yanalainisha na kuzuia msuguano.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa hekima ya kuvuta roho za watu(Mithali 11:30) mafuta huufanya mwili uwe laini.
Ubatizo wa Roho Mtakatifu hulainisha ukavu wa maombi yetu (Warumi 8:26).
§ Mvua (Zaburi 72:6;Hosea 6:3) Nchi haiwezi kutoa matunda bila mvua.Mtu aliyeokoka hawezi kuwa na matunda mengi bila mvua yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu (Yohana 15:16).
§ Mvinyo (Waefeso 5:18;Matendo 2:12-13) mvinyo kwa walevi unasahaulisha shida. Ubatizo wa Roho Mtakatifu, humwezesha mtu kudharau majaribu na kuondoa wasiwasi na kubabaishwa na mambo madogo madogo tu. Mvinyo kwa walevi, pia unawapa ujasiri wa kufanya lolote lile, aibu, woga vinatoweka. Ubatizo wa Roho Mtakatifu humfanya mtu kuwa jasiri kama simba na mtu aliye kuwa mwoga kama Petro, kuwa jasiri (Mithali 28:1; Mathayo 26:31-35,56; Matendo 4:13).
§ Hua (njiwa)- (Yohana 1:32) Ubatizo wa Roho Mtakatifu haufanyiki kwa mtu wa ulimwengu huu yaani ambaye
hajaokoka. Njiwa hakutua kwenye ulimwengu,alirudi safinani kwa waliookoka (Mwanzo 8:8-9)Roho Mtakatifu ni mweupe, kama hua.Ni Mtakatifu,huja kwa watakatifu waliotakaswa.
§ Muhuri (Waefeso 1:13) Muhuri ni alama ya mamlaka.Bila muhuri barua hupungua mamlaka yake. Ubatizo wa Roho Mtakatifu humfanya mtu kuwa na mamlaka ya Yesu kwake na shetani husema “ Yesu namjua na Paulo namfahamu (Matendo 19:15) Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni mamlaka au uwezo kutoka juu wa kuzifanya kazi za Yesu.
§ Arabuni (2Wakorintho 1:21-22)Neno arabuni maana yake- Uhakikisho au uthibitisho wa Uimara.Ubatizo wa Roho Mtakatifu, hutufanya kuwa na uthibitisho wa uimara wa Neno la Mungu, hutuongezea imani ya kufanya maajabu.Shetani hawezi kumpeperusha huku na kule mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu.
D. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
Kuokoka au kuzaliwa mara ya pili.Mafuta haya hayatiwi kwa mtu mgeni ambaye jina lake haliko katika kitabu cha Uzima mbinguni (Kutoka 30:31-33)
Kutakaswa (Yohana 17:17;1Wathesalonike 5:23) Wanafunzi 120 orofani,walitakaswa kabla ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Kuwa na Imani kama Roho Mtakatifu yuko kwetu tayari na kwamba ni ahadi ya Mungu kwetu(Matendo 2:38-39); Luka 11:10-13)
Kuwa na kiu ya kumtumikia Mungu (Isaya 44:3)
Kuomba kwa kufumbua sana kinywa na kutokuruhusu kutumia akili,wala kuwaza kwambatutasema lugha ya mapepo. (Luka 11:10-13; Zaburi 81:10).
E. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
Mtu akibatizwa kwa Roho Mtakatifu,kutakuwa na mambo ya kusikia kwake na ya kuyaona kwake(Mathayo 3:16-17).
Ishara ya kwanza ni kusikia kutoka kwake kabla ya kuona mengine. Atasema au ananena kwa lugha mpya asiyoifahamu
ambayo siyo ya dunia hii (Matendo 2:4;10:44-46;19:6). Ni muhimu mno kwa mtu aliyeokoka kuomba kwa kunena kwa lugha hii (1Wakorintho 14:2,4-5,15). Hata hivyo hatupaswi kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasioelewa kitu. Watadhani sisi ni wendawazimu (1Wakorintho14:18-25)
Kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasiojua kitu nikuwapa mbwa kilicho kitakatifu na kutupa lulu zetu mbele ya nguruwe matokeo yake watatudhihaki kwa kuwa hawajui maana (Mathayo 7:6).
F. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
Moto bila kuchochewa huzimika (Mithali 26:20). Hatuna budi kuwa waombaji na kuomba kwa Roho, yaani kunena kwa lugha katika maombi mara kwa mara katika maombi yetu binafsi (1Wakorintho 14:14-15; Yuda 1:20) Vile vile hatuna budi kudumu katika usafi kwa Neno (Zaburi 51:4,11;119:11; Yohana 15:3).
Hatuna budi pia kujihusisha katika kushuhudia na kuwaleta watu kwa Yesu (Mika 3:8).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: one or more people and text
Chunguza burudani yako. Je, wewe hutazama sinema au programu za televisheni au hutembelea vituo vya Intaneti vyenye kusisimua kingono? Kwa hekima, mtunga-zaburi alisali kwa Mungu: “Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.”*—Zaburi 119:37.
Sali kuhusu jambo hilo. Mtunga-zaburi alisali hivi kwa Yehova: “Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.” (Zaburi 119:37) Yehova Mungu anataka ufaulu, naye anaweza kukupa nguvu za kufanya yaliyo sawa!—Wafilipi 4:13.
Zungumza na mtu. Mara nyingi kuchagua mtu unayeweza kumfunulia moyo wako husaidia sana kushinda zoea hilo. (Methali 17:17) Andika hapa chini jina la mtu mkomavu ambaye unaona ni rahisi kumweleza jambo hilo.
ATHARI ZA KUJICHUA "PUNYETO"
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.
Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.
Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa
kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.
Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.
Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!
Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.
“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.
USIKOSE SEHEMU TA NNE
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA NNE)

Image may contain: food
Mpendwa:
Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke wakiwa na uvutano wenye nguvu kati yao, na hakuna ubaya wa kutosheleza tamaa za ngono katika mpango wa ndoa. Kabla ya kufunga ndoa, huenda ukawa na tamaa kali za ngono. Hilo likitokea, usidhani kwamba wewe ni mtu mwovu au kwamba huwezi kuishi maisha safi. Unaweza kudumisha usafi wa kiadili ukiamua kufanya hivyo! Lakini ili ufanikiwe, utahitaji kudhibiti mawazo yako kuhusu watu wa jinsi tofauti. Unaweza kufanya hivyo jinsi gani?
Epuka kujifurahisha kwa mambo machafu. Bila shaka, haimaanishi kwamba sinema zote, au miziki yote ni mibaya. Hata hivyo, katika ulimwengu wa leo burudani nyingi zimekusudiwa kuamsha tamaa zisizofaa za ngono. Biblia inatoa shauri gani? “Acheni tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Epuka kabisa burudani zote zinazoweza kuchochea tamaa zisizofaa za ngono.
UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.
MFADHAIKO:
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili.
KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza.
Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe.
Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.
Baadhi yao, hubaki wakiwa baada ya wahusika wao kuwagomea katikati ya safari. Zipo athari nyingi zaidi ya hizo,
kutegemea na namna tatizo lilivyokomaa na aina ya jinsia.
Baadhi ya madhara ya Waathirika wa Upigaji Punyeto na Kujichuwa.
• Kupiga Punyeto Kunapelekea kufika mshindo kabla na bila kujijua na husababu matatizo ya Nguvu za Kiume.
• Kutokwa na manii usingizini bila kujijuwa.
• Maumivu ya mgongo.
• Punyeto usababisha udhaifu wa mwili.
• Kuwa na sura ya ujuvi.
• Udhaifu wa Macho, kutoona vizuri.
• Nywele Kutokuwa na Afya.
• Kupungua uzito chini ya kiwango.
• Uchovu na udhaifu wa mwili, wa mara kwa mara
• Kupata maumivi kwenye kinena.
• Maumivu kwenye mapumbu.
• Mbegu za uzazi kuwa dhaifu.
• Kutosikia raha ya mapenzi/jimai.
• Kupungua kwa hamu ya kula.
• Matatizo ya kusimamisha.
• Kupotea/kutosikia njege.
• Kufikia mshindo mapema, dakika moja hoi.
TUMEFIKIA TAMATI YA MADA YETU KUHUSU KUJICHUA SEHEMU YA SIRI.
JE, UPO TAYARI KUACHA MCHEZO HUU BAADA YA KUSOMA HII MADA?
INAWEZEKANA NA NJIA RAHISI NI KUOMBA KWA MUNGU AKUSAMEHE DHAMBI HII NA KUTOA HILI PEPO LA KUJICHUA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

BIBLIA INARUHUSU KULA NYAMA YA NGURUWE

Image may contain: grass, outdoor and nature
JE, KULA NYAMA YA NGURUWE NI DHAMBI?
1. Je, kuna aya yeyote ile katika Agano Jipya inayo mkataza Mkristo kula nyama ya Nguruwe?
2. Je, kuna sheria yeyote ile kwenye Agano Jipya inayo kataza kula nyama ya Nguruwe?
3. Je, Yesu alisema au waamrisha Wafuasi wake wasile Nyama ya Nguruwe?
4. Je, Yesu alipo vitakasa vyakula vyote [Marko 7 :15-19] kunapingana na sheria ya hapo mwanzo kwenye Mambo ya Walawi?
Ndugu msomaji,
Katika hili somo, tutajifunza kuhusu ulaji wa Nyama ya Nguruwe na kwanini Wakristo wanakula Nyama ya Nguruwe.
Tuanze moja kwa moja kwa kusoma aya za Biblia:
"Bwana Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawambia Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, kila mnyama wa katika nchi watawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani pamoja na viti vyote vilivyojaa katika ardhi,na samaki wote wa baharini vimetiwa mikononi mwenu, kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani ,kadhalika hivi vyote ,balo nyama pamoja na uhai ,yaani damu yake msile" {Mwanzo 9:1-4}
Ndugu msomaji wangu maandiko yamefunua wazi kwamba Mungu alitoa wanyama wote kuliwa baada ya mboga za majani walakini hatuoni Mungu akitoa sheria ama akiwabagulia wanyama wa kuliwa yaani walio safi na wasio safi, bali maandiko yametuonyesha kuwa Mungu alitoa wanyama wote kuwa chakula kwa wanadamu kama ilivyo shuhudiwa katika Mwanzo Mlango wa 9 aya ya 1-4.
Je sheria inayohusiana na wanyama safi na wasio safi ilitolewa wapi?
Ndugu msomaji kama ambavyo nilivyokwisha kutangulia kusema kuwa sheria hii inayohusiana na vyakula haikutolewa tangu mwanzo kwa ushaidi wa andiko ambalo nimekupa limeonyesha hivyo, swali la lini sheria hii ambayo ilihusiana na vyakula ilitolewa maandiko yapo wazi kabisa eneo ilo ni baada ya wana Israel kutolewa utumwani Misri ndipo tunaona katika biblia sheria inayohusiana na wanyama walio safi na wasio safi kwaiyo kabla ya hapo wanyama wote walikuwa chakula {Mambo ya Walawi 11 :1-7} kupitia fungu ili la biblia tunaona kuwa Mungu anatoa sheria inayohusiana na wanyama wanaopaswa kuliwa na wasiopaswa kuliwa?
Ni kweli kabisa Mungu alitoa hiyo kuwa ni sheria kwao wana wa Israel walakini tusiishie tu hapo katika kuangalia sheria kuwa ni sheria tusafiri pamoja kifikra,utakumbuka kuwa watu ambao kiasili sio wayahudi walikuwa hawana desturi za usomaji wa torati?
Je hii sheria iliyohusiana na wanyama safi na wasio safi ilifahamika kwao?
Bila shaka jibu ni hapana labda utajiuliza kwanini?
Napenda tujifunze ili jambo na kutokuacha historia ya vizazi pia na chanzo cha kusambaa kwa wanadamu duniani kote
Theolojia inatueleza kwamba vizazi vya ulimwengu huu vimetokana na wana watatu wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu, na Yafethi sasa katika historia ya chanzo cha mataifa mbalimbali kama inavyoelezwa kwamba wanadamu yaani mataifa yote yaliotokana na watoto wa Nuhu walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na waliishi pamoja, wanadamu hawa ikumbukwe kwamba hawakupewa sheria yoyote inayohusiana na wanyama wapasao kuliwa na wasiopaswa hawakupewa na hapa tunaelezwa ndio chanzo cha mataifa mbalimbali maana baada ya Mungu kuwachafulia lugha walisambaa kila mmoja mahali pake (Mwanzo 11:1-9}
Sasa swali la kujiuliza je wanadamu hawa waliondoka na ufahamu upi kuhusiana na vyakula, kwamba Nguruwe haramu ama?
Maana ifahamike kuwa kwao walipewa wanyama wote kuwa chakula kwa sababu hawakuwa na sheria inayohusiana na vyakula safi na visivyo safi kwao wanyama wote ni safi tu waliondoka na imani hiyo kama walivyopokea huu ndio ukawa mwanzo wa mpishano wa vyakula baina ya watu walioitwa wa mataifa na wayahudi baada ya wao kupewa sheria iliyohusiana na wanyama walio safi na waschakula.
Wayahudi walipata tabu sana kushiriki katika kalamu za watu ambao kiasili hawakuwa wasomaji wa torati na kuishi katika nchi zao, kwa sababu walipishana katika desturi za vyakula ,wayahudi hata wale ambao walikuja kuwa wafuasi wa Kristo walipata ugumu mno katika eneo ilo,sababu wao wayahudi walipewa sheria kuhusiana na wanyama safi na wasio safi ila mataifa kwao wanyama wote walikuwa safi sasa mtume Paulo hali akiwa na ufunuo wa Kimungu aliwaeleza wale wayahudi waliokuwa wakristo zama zile na walikuwa wakiambatana na mitume katika uinjilisti alisema maneno haya
" Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila ya kuuliza uliza kwa ajiri ya dhamiri ,maana ,dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo, mtu asiyeamini akiwaalika ninyi mnataka kwenda ,kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila ya kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri" {1 Wakorintho 10:25-28}
Kwanini mtume Paulo awaagize wale kila kitu ikiwa wapo wanyama waliozuiliwa je alikuwa anapingana na Mungu? Lah hasha! hakuwa akipingana na Mungu, bali Mtume Paulo alifahamu kesi kuhusiana na vyakula, Yesu aliye kielelezo cha imani yetu aliitatua kupitia Marko 7 :15-19 pale alivyovitakasa vyakula vyote, akamaliza utata huo, hivyo baada ya hapo kila chakula kilikuwa halali kuliwa rejea tena kusoma Mwanzo 9:1-4
" Akawaambia hivi hata ninyi hamna akili ?
Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia mtu unajisi , kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni kisha chatoka kwenda chooni?
Kwa kusema hivi ali itakasa vyakula vyote ,akasema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho mtu unajisi ,kwa maaana ndani ya mioyo watu hutoka mawazo mabaya ,uasherati,wivi uuaji,uzinzi, tamaa mbaya"
Kwa sababu Yesu alivitakasa vyakula vyote ndio maana tunaona agizo lake kwa Wayahudi aliokuwa akiambatana nao kwa ajili ya kueneza ujumbe wa Mungu kuwa wakialikwa katika majumba ya wasio amini na wakawapikia nyama ambazo mmezuiliwa msile na torati kuleni kwa sababu unajisi haupo ndani ya nguruwe wala ngamia ila unajisi upo mioyoni mwa watu
Ndugu pamekuwa na hoja juu ya nguruwe kuwa na madhara jamani kwani ni nguruwe tu ana madhara?
Je Ng'ombe hawa wa leo nyama zao hazina madhara?
Je Kuku wa kizungu na mayai yake hawa madhara kiafya?
Je chumvi za viwandani na mafuta pamoja na mavinywaji havina madhara?
Watu wa Mungu kimsingi kupitia Agano Jipya, Wakristo, hatuna sheria yoyote inayotuagiza kutokula Nguruwe hivyo basi sio dhambi kula Nguruwe ,dhambi katika tasfiri ya Biblia ya Union Version kupitia 1 Yohana 3:4 imetafsiriwa kuwa " dhambi ni uhasi wa sheria" kwaiyo ili dhambi iwepo lazima pawepo na uvunjifu wa sheria je katika agano jipya Wakristo tumepewa sheria inayotutaka kutokula Nguruwe ama ngamia kwa wanaokula?
Kama hakuna basi kula Nguruwe ama Ngamia sio dhambi?
Mungu tangia mwanzo alipotoa agizo la wanadamu kula nyama, alitoa wanyama wote kuwa chakula itakuwaje dhambi kwao?
Maana hakuwapa sheria iliyowabagulia wanyama wa kuliwa na wasio paswa kuliwa kwao wanyama wote walikuwa chakula sawa kama ambavyo Mungu ametoa wanyama wote kuwa chakula kwao, kama kweli alitaka wasiliwe nguruwe angewataza wasiliwe kabla hakuwapa wanadamu wanyama wote
Biblia inasema kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna kiumbe cha kukataliwa ,kama kitapokelewa kwa shukrani ,kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba {1Timotheo 4:4-5}
Kama hakuna kiumbe cha kukataliwa maana viumbe wote ni vizuri sasa ubaya wa Nguruwe ni nini?
Kama hacheuwi hii ndio sababu ndio Mungu ametaka awe hivyo!!!!!!! Ukianzia mistari ya juu utaona anaonya watu ambao wanawazuia wengine na baadhi ya vyakula kwa kisingizio cha wanyama wazuri na wabaya, sasa hawa leo ambao wanawataka watu kujitenga na baadhi ya vyakula tunawaweka kundi gani?
Biblia inasema viumbe vyote ni safi unganisha na Mwanzo 9:1-4 upate maana halisi, hivyo kula nguruwe sio dhambi ni halali kabisa
Sio vyakula ambavyo vinatuudhurisha mbele za Mungu tunakula kwa ajili ya miili yetu sio kwa ajili ya Mungu (Warumi 15:17 na Marko 7:15-19)
Hakuna kosa kula Nguruwe kwa mujibu wa Agano Jipya asanteni mbarikiwe nyote.
Mungu awabariki sana.
By permission: Pastor Samuel J. M, Christ Nations Org, Max Shimba Ministries Org, NKJV, Gideon Bible 1960, Green Island Tabernacle Inc., Rev. Dr. J. E. Grant
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 25, 2016

WAZAZI WA MUHAMMAD WALIKUWA MAKAFIRI NA WALIKUFA MAKAFIRI


Ndugu msomaji,

KUMBE MAMA YAKE NABII MUHAMMAD ALIKUFA KAFIRI
Bi Amina mamake na Muhammad kafa kafiri. tunasoma
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((اسْتَأْذَنْتُ رَبِّي أَنْ أَسْتَغْفِرَ لأُمِّي فَلَمْ يَأْذَنْ لِي ، وَاسْتَأْذَنْتُهُ أَنْ أَزُورَ قَبْرَهَا فَأَذِنَ لِي )) مسلم
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Niliomba ruhusa kutoka kwa Allaah kumuombea msamaha mamangu, lakini Hakunipa ruhusa. Nikamuomba idhini nilizuru kaburi lake (mamangu), Naye Akanipatia ruhusa)) [Muslim]
Inaelezwa katika Kitabu cha ‘Awn al-Ma’abuud:
“Kauli yake (Muhammad) ((lakini Hakunipa ruhusa)) ina maana kuwa (mama yake) alikuwa kafiri na hairuhusiwi kumuombea maghfirah kafiri.”

Huu ni msiba mwengine kwa Waislam. Wazazi wake Muhammad wote wamekufa na dhambi kubwa kubwa na huku wakiwa MAKAFIRI.

Hivi huyu Allah mbona aliwachukiwa sana wazazi wa Muhammad?
Je, unafahamu kuwa baba yake Muhammad na yeye alikufa akiwa KAFIRI na yupoe Jehannam?
Hakika kuna mambo ya ajabu ajabu kwenye uislamu.

LAKINI HATUSOMI KUWA MAMA YAKE YESU ALIKUFA NA DHAMBI.
MUHAMMAD AKIRI KUWA BABA YAKE YUPO JEHANNAM
Huu ni MSIBA MKUBWA sana kwa Waislam. Muhammad ambaye baba yake anaitwa Abdullah ikimaanisha "mtumwa wa Allah" imethibitshwa kuwa yupo Jehannam/motoni akichomeka.
Haya si maneno yangu na wala mimi simsingizii baba ya Muhammad, bali haya ni maneno ya Muhammad.
Soma uthibitisho hapa.

Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeuka kuondoka, akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni. (Sahih Muslim, Kitabu 001, Namba 0398).

Na swali ambalo tungependa wajiulize Waislam ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?

Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
ZAIDI YA HAPO,
1. Kwanini Muhammad anakiri kuwa baba yake yupo Motoni?
2. Je, huyu Abdullah/abdallah alipata wapi hili jina lenye Allah ndani yake?
3. Je, inamaanisha kuwa Allah ambaye ni mungu wa kipagani alikuwepo kabla ya Muhammad?
Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).
Tunaambiwa kwamba:
Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Quraish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).

Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:
….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).

Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, ….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).

Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).
Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).
Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).
… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).

…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).

…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).

Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.

Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.
Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba.

Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."

Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.

Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?

Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.

Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.
Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?
Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).
Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!
Kumbe basi Kaaba ni nyumba ya kipagani.
Kumbe basi baba yake Muhammad yupo Motoni.
Kumbe basi Waislam wote wanao enda kuhiji wataingia motoni.
Kumbe basi Allah ni mungu wa kipagani.
Hakika Uislam ni dini ya wapagani ndio maana Muhamamd alikiri kuwa baba yake yupo motoni.
Nawakaribisha kwa Mungu Mkuu aliye hai, YESU MWOKOZI WETU.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

SINAGOGI SIO MSIKITI SEHEMU YA KWANZA

Image may contain: sky, text and outdoor
Tunazidi kuchambua HOJA ZA MIHADHARA ya Kiislamu
LEO TUANGALIE SINAGOGI!!
Kwa miaka mingi afrika mashariki na kati kunakosemwa Kiswahili kumetokea mafundisho ambayo ni mapotofu sana ya kukejeli, na lengo lao hasa ni kuangusha mwili wa Yesu Kristo (Kanisa) na mafundisho yake. Na kupitia mafundisho hayo wengi wameacha imani iliyo ya kweli nakufuata imani zingine ambazo mwisho wao ni mauti. Na hawa siyo wengine bali ni wahadhiri wakiislamu. Wao hudai kuwa wanafuata mafundisho ya Bwana Yesu. Unukuu aya hii Mathayo 11:29-30 pale Yesu alisema jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapa raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Pia wanasema Yesu aliingia kwenye sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake siku ya Sabato Luka 4:16.kupitia kwa tendo hili la Yesu kwingia kwenye Sinagogi , wahadhiri hawa wanadhai jambo ili linamfanya Yesu kuitwa muislamu. Tafadhali ndugu yangu ukitaka kujua ukweli fuatilia somo hili hadi tamati.. hii ni sehemu ya kwanza. Biblia ya Kiswahili katika maneno magumu imetaja kuwa Sinagogi ni msikiti wa Kiyahudu. hapa majamaa wanakesha!!
Historia ya sinagogi:
Ukitaka kujua mtu Fulani ni lazima uangazie mambo kadha wakadha ikiwemo historia yake, pasina historia ni vigumu watu kufahamu mambo yaliyofichika. Hivyo nimeonelea kuwa ni bora sana kuangazia historia ya sinagogi na chanzo chake. Jambo la msingi kwanza ni kujua maana ya Sinagogi. Neno hili Sinagogi maana yake ni mahali pa watu kukutania. Sinagogi lilianzia pale wana wa Israeli walipokuwa utumwani kule Babeli kwa miaka sabini kulinga na unabii wa nabii Jeremia, Jeremia 25:11-13.
baadaye nitaeleza tofauti ya Sinagogi na Hekalu.
Sababu ya wayahudi kuanzisha sinagogi ni hizi.
• kule utumwani hawengeweza kurudi kule Yerusalemu ambapo palikuwa na hekalu kwa minajili ya mambo ya ibaada. Kwa hivyo Wayahudi walitafuta jinzi ya kuendelesha ibaada na miandamo ya sikukuu zao.
• Kuendelesha utamaduni wao kama vile kutahiri mtoto wa kiume akiwa na siku nane kulingana na amri ya Mungu Mwanzo 17:9-12
• Ili kuzingatia sheria za Mungu kufundishana habari za torati na manabii.
Uongozi
Sinagogi lilikuwa likianzishwa na wazee wapatao saba au kumu wa kiyahudi, kila Sinagogi lilikuwa na viongozi wapatao wawili au zaidi. Na vyongozi hao huchaguliwa na wazee wa Sinagogi.
Katika karne ya agano jipya kulikuwepo masinagogi mengi sana yapatao 480 ambazo zilikuwa zikiingiwa na watu wa wamataifa mbalimbali ambao walikubali kufuata taratibu zote za dini ya kiyahudi.
Kazi ya Sinagogi:
Malengo makubwa ya Sinagogi yalikuwa kujikumbusha sheria na pia kuangalia utamaduni wao. Tusomapo Biblia na kuichunguza tunaona mambo yafuatayo;
Malaki 4:4
Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliomwamuru huko Horebu kwa ajili ya watu wangu Israeli wote naam, amri ya hukumu.
Mathayo 5:17
Yesu alifundisha hivi:- Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii la sikuja kutangua, bali kutimiliza
Hivyo basi kwa habari za torati na manabii wayahudi walikuwa wakifundisha watoto wao kwenye Sinagogi. Matendo 15:21. kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
Hapa tunaona Mtume Paulo naye anamkumbusha Timotheo habari ya mafundisho dhabiti alioyapata kutoka utotoni.
2 Timotheo 3:14-15
Baki wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; naya kuwa tangu utoto umeajua mandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Kulikuwa na masinagogi mengine yalikuwa na vyongozi zaidi ya wawili na mmoja wao alikuwa na cheo cha (Heb gr archi synagogue) au kasisi mkuu.
Kasisi huyu ilikuwa na kazi mbalimbali kwa mfano:-
• Kujenga na kutunza mali yao
• Kuangalia namna ya ibaada vile inavyofanywa ikiwemo kutunza sheria, Luka 13:10-14 nanukuu aya (14) Basi mkuu wa Sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu alimponya mtu siku ya sabato, akamjibu, akawambia makutano, kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si siku ya sabato.
• Kuchagua mtu mwenye kusoma na kuomba.
• Kualika wageni kutoka masinagogi mengine ili aje awahutubie watu na kutilia nguvu mambo yanayohusu jamii na dini yao.Matendo 13:13-15 na nukuu aya (15) kasha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa Sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwambia, Ndugu kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.
Kweli Sinagogi kuna mtu mmoja ambaye kazi yake ni kutunza kile chuo cha torati manabii na pia huangalia usafi wa Sinagogi kwa ujumla, nayeye hulipwa kwa kazi hiyo anayoifanya. Na kwa kiibrania huitwa (hazzan). Luka 4:20. akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi na watu wote waliokuwamo katika Sinagogi wakamkazia macho.
Mtumishi huyo kazi yake nyingine ilkuwa ni kutangaza mwanzo wa sabato na mwisho wake.husimamia ujenzi wa Sinagogi au kurekebishwa kwake, kwa hivyo inambidi aishi kwenye Sinagogi.
Fuatilia hapo kesho majaliwa tuangazie hoja za wahendesha mihadhara kuhusu Sinagogi
Mratibu Mwalimu Chaka wa Musa.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozo wetu.

OMBA KWA JINA LA YESU KRISTO SEHEMU YA KWANZA

https://www.facebook.com/MaxShimbaMinistry/videos/843400799142857/
Kila Mkristo anapenda awe na maisha ya maombi yaliyo na mafanikio – anapenda akiomba kitu kwa Mungu ajibiwe. Lakini mara nyingi nimewasikia wakristo kadhaa wakisema wameomba jambo Fulani kwa Mungu lakini hawajajibiwa. Wengine wanapofikia hali ya namna hii, hukata tama – hata wokovu unaanza kupoa utamu wake.
Kuna sababu nyingi ambazo zimeandikwa ndani ya Biblia zinazoeleza chanzo cha kutijibiwa maombi ya watu. Sababu mojawapo ni kutokuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu – au kwa tafsiri nyingine kuomba kinyume na maagizo ya Mungu (Yohana 5:14-15)
Yesu Kristo alituachia maagizo mbalimbali juu ya maombi katika kulitumia Jina lake – mojawapo ni hili;
Tumuombe Baba kwa jina la Yesu Kristo.
Katika kitabu cha Yohana 16:23-24; Yesu Kristo alisema; “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.”
Wazo la kwanza tunalopata katika agizo hili ni kuelekeza mawazo na maombi yetu kwa baba Yetu aliye mbinguni wala si kwa malaika wala kwa wanadamu. Ndiyo maana imeandikwa; “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Waebrania 11:6)
Yesu Kristo alipokuwa anawafundisha kuomba alisema; “basi ninyi saline hivi; Baba yetu uliye mbinguni….” Jambo kubwa alilotaka wanafunzi waone ni umuhimu wa kujua na kuelekeza mawazo na maombi yao kwa BABA MUNGU. Watu wengi wamekwama kwenye maombi kwa kuwa katika mawazo yao wamewategemea sana watu katika kupata majibu ya maombi yao badala ya kumtegemea Baba Mungu.
Sisemi ni vibaya kushirikiana na watu wengine katika maombi – hapana. Bali nataka ujue kuwa hata ukiwashirikisha watu wakusaidie kuomba – wewe elekeza mawazo yako kwa Baba Mungu na kumtegemea Yeye kukujibu.
Wazo la pili tunalolipata katika maagizo ya Yesu Kristo juu ya maombi yaliyoandikwa katika (Yohana 16:23-24) ni tuombe kwa Jina lake. Hakusema tuombe kwa ajili yake au kwa niaba yake, bali alisema tuombe kwa jina lake.
“Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.” (Yohana 16:23-24)
Mara kwa mara utawasikia watu wakimaliza maombi yao kwa kusema “kwa ajili ya Yesu Kristo, amina”. Lakini sioni mahali ambapo Yesu Kristo alisema tuombe kwa ajili yake. Hebu fikiri mtu anaomba uponyaji wa tumbo halafu aombe akisema “Naomba tumbo langu lipone kwa ajili ya Yesu Kristo”. Je! Ni Yesu Kristo anayehitaji uponyaji au ni wewe?
Yesu Kristo alisema tuombe kwa Jina lake na siyo tuombe kwa ajili yake wala kwa niaba yake – kumbuka hilo kila wakati unapolitumia jina la Yesu Kristo katika maombi. Lakini kama unataka mtu apone kwa ajili ya Yesu Kristo, basi omba kwa jina la Yesu Kristo – ili Jina hili litukuzwe.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

JE, YESU ALIMAANISHA NINI ALIPO SEMA MSIDHANI KUWA NIMEKUJA KUTENGUWA TORATI AU MANABII; LA, BALI KUTIMIZA?

Image may contain: text and nature
Hoja nyingine kutoka kwa wasabato hujengwa katika kitabu cha Mathayo 5:17-18 inayosema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, BALI KUTIMILIZA. Kwa maana, amini, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”
Hoja inayojengwa na wasabato katika andiko hili, ni kwamba, Bwana Yesu anakiri hajakuja kutangua torati wala manabii bali amekuja kuitimiliza, yaani wakimaanisha kuwa, naye amekuja kuishika sabato.
Watoto wa Mungu, hii hoja ni ya undanganyifu. Kuupata ukweli, ni vizuri turudi kwenye Biblia ya Kiingereza ya toleo la King James ili tupate tafsiri nzuri zaidi. Mathayo 5:17, “Do not think that I came to destroy the law or the prophets. I did not come to destroy but to FULFILL…..” Kadhalika na matoleo mengine ya Kiingereza, neno ‘Kutimiliza’ kwa Kiingereza limetumika ‘FULFILL’. Kulingana na kamusi ya Kiingereza, neno ‘fulfill’ lina maana zifuatazo; maana ya kwanza ya ‘fulfill’ ni ‘fill up’ yaani ‘jazia.’ Kwa hiyo inaleta maana ya kwamba, Bwana Yesu, hakuja kuitangua bali amekuja kuijazia (fill up), kwani kulikuwa kuna mapungufu katika lile agano. Na ndiyo maana katika kitabu cha Waebrania 8:7 tunasoma, “Maana kama lile la kwanza, lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.”
Maana ya pili ya ‘fulfill’ ni ‘an act of doing something to satisfaction’ ikiwa na maana kwamba ni kitendo cha kufanya kitu ili kifike kwenye utoshelevu. Kwa hiyo, Bwana Yesu hakuja kuitangua torati na manabii, bali amekuja kuboresha ili ifikie utoshelevu, maana bado torati na manabii, haikuleta utoshelevu wala kuleta matokeo mazuri kwa watu, kwani kila kukicha watu walikuwa wakiuawa kwa kushindwa kuiishi torati. Maana ya tatu ya ‘fulfill’ ni ‘an act of achieving goal’ kwa Kiswahili inamaanisha ni kitendo cha kufanya kitu kifike kwenye malengo.
Kwa hiyo kwa lugha nyingine tungeweza kusema kwamba, Bwana Yesu amekuja kuifanya torati na manabii iweze kufikia malengo aliyokusudia, kwa sababu bado ilikuwa na shida kulingana na uwezo wa mwanadamu. Sasa kwa lugha fasaha ni kwamba, Bwana Yesu, hakuja kuiondoa torati na manabii, bali alikuja kufanya maboresho, marekebisho, masahihisho; ikiwa na maana kwamba kilichotakiwa kuondoka kiliondoka, na kilichotakiwa kubaki, kilibaki; na hii ilifanya na chekecho la msalaba. Mfano, mambo ya kushika sabato yaliondolewa, kwa sababu sabato ilikuwa ni amri ya ishara, ilikuwa ni kivuli, ikimuashira Yeye Bwana Yesu mwenyewe kama pumziko la kweli la kiroho. Hivyo, kwa vile Yeye pumziko halisi amekuja, sabato haikuwa na kazi tena. Bwana Yesu anasema, “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao, na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” (Mathayo 11:28)
Upungufu wa Agano la lake unaozungumziwa katika Waebrania 8:7, haupo katika torati, kwani torati kwa asili, haina tatizo na ni njema maana ni maagizo ya Mungu mwenyewe. Tatizo lilikuwa kwenye uwezo wa wanadamu wenyewe katika kuifuata torati yote kwa nguvu zao; maana kipindi cha agano la kale, walipewa sheria na hukumu tu, lakini hawakuwa na neema ya kuwafanya washike hiyo sheria. Kwa hiyo, kimsingi wana wa Israeli waliipenda torati (sheria) na hukumu walizopewa na Mungu, na waliikubali hiyo torati (sheria) na hukumu, na ndiyo maana walikubali kufanya agano na Mungu, kwa kuwa kila agano ni lazima kuwepo kwa makubaliano katika pande mbili.
Mioyoni mwao waliikubali na kuipenda torati (sheria) na hukumu zake, lakini mwili uliwazuia kuitekeleza hiyo torati, kwa kuwa walipewa torati (sheria) na hukumu tu bila neema au kiwezesho cha kuiishi sheria. Sasa hapo ndipo tunapopata upungufu wa Agano la kale.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

SHETANI ANAWAPENDA SANA WAISLAM

Image may contain: one or more people and text
Mfikirie Yesu asiyekuwa na Dhambi
Tofauti na Muhammad, aliye jiita nabii bila ya kufanya unabii wowote ule.
Yesu alitimiza mamia ya unabii na maana zake. Yesu hakuwahi kusamehewa dhambi kwasababu hakuwa na dhambi wala hakuwai tenda dhambi kama Muhammad nabii wa Allah.
Yesu hakuwahi kuua, wala kutishia maisha ya msafiri yeyote yule.
Alikuwa na kiwango cha juu sana cha uadilifu (hakuruhusu ufanyaji tendo la ndoa kwa kutumia nguvu)
Yesu aliahidi kulipa adhabu ya dhambi zetu, aliteseka na kufa kwa ajili yako, na hana kaburi, kwani alifufuka kutoka katika wafu.
Wakristo hawasemi kuhusu Yesu kuwa: "amani ya Mungu na iwe juu yake", Yesu ndiye mfalme wa amani; amani ya Mungu ipo juu yake. Lakini, tumaini langu ni kuwa utaweza kujua namna ya kuona kuwa amani na upendo vya Yesu vinaishi moyoni mwako.
SASA TUMSOME NABII WA ALLAH AITWAYE MUHAMMAD
Muhammad Mwenye Mafanikio:
Muhammad pamoja na watu wake waliteka nyara misafara ya wafanya biashara na wasafiri mbalimbali.
Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 37 sura ya 8 na.495 uk.280 inasema "wakati Allah alipomfanya mtume kuwa tajiri kutokanana na ushindi" 1/5 ya mateka ya vita iliwekwa katika hazina na Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 5 sura ya 401 na.2348 uk.519 inasema familia ya Muhammad ilikuwa na hisa ndani yake.
Utekaji nyara wa mali za watu wa kwanza kufanywa na Waislam ulijulikana kama Nakha la Raid. Wakati wa mwezi wa kusimamisha vita kwa muda, wafuasi wake waliushambulia msafara kwa kuuvamia na kuua mtu mmoja, na kuwafanya watu waliosalia kuwa watumwa, na kuchukua nyara.
Muhammad mwenyewe aliongoza uvamizi wa pili pale Badr. Muhammad aliongeza utajiri wake kwa kuyashambulia makazi ya Wayahudi ya Khaibr. Yeye na wafuasi waliokuwa waaminifu kwake walijitwalia nyara na wake (Je Muhammad alihitaji mke mwingine?) wa Wayahudi wanaume 700-1000 wa kabila la Banu Quraiza waliowakata vichwa baada ya kujisalimisha.
Ndio maana nasema Shetani anawapenda sana Waislam.
Ili kuweza kufahamu chimbuko halisi la Uislam inafaa kuyafahamu mazingira ya Uarabuni kabla ya Uislam, mtu aliyeitwa Muhammad na historia ya mwanzo ya Uislam. Elimu kale (akiolojia), Kurani na Hadithi vina mengi ya kusimlia ambayo watu wengi wanaweza kuwa hawajui.
SHETANI ANAWAPENDA SANA WAISLAM NDIO MAANA AKASILIMU NA KUWA MUISLAM:
Ni bahati mbaya kwamba Adamu na Hawa hawakufanikiwa kufanya jitihada za kumwezesha shetani na wanae kuuomba msamaha kwa mwenyezi Mungu na kuwa Waislamu, ni mtume Muhammad tu ndiye aliyemsilimisha shetani akawa muislamu… (KITABU CHA ASILI YA MAJINI UK 20)
Kama unapenda kuwa na Shetani basi bakia hukohuko kwenye Uislam maana Shetani alisha silimishwa na Muhammad na Shetani anaupenda Uislam na ni Muislam.
Kama hupendi uwe na Shetani maishani mwako basi mpokee Yesu ambaye anakupenda na amekutayarishia maisha mazuri baada ya kifo.
Uchaguzi ni wako, kumpenda shetani ambaye ni Muislam au kumkataa Shetani ambaye anawapenda Waislam.
Karibu kwa Yesu.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo.

OMBA KWA JINA LA YESU KRISTO SEHEMU YA PILI

Image may contain: one or more people, cloud, sky and text
Maombi ya mapatano kwa Jina la Yesu Kristo.
“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:19-20)
Maombi ya mapatano kwa Jina la Yesu Kristo yana uwezo wa ajabu. Yesu Kristo alisema watu waliokusanyika kwa jina lake wakipatana kuomba JAMBO LOLOTE watafanyiwa na baba yetu aliye mbinguni.
Kwa nini iwe hivyo? Yesu Kristo alisema, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Kwa maneno mengine tunaweza kusema jina la yesu Kristo limebeba uwepo wa Yesu Kristo. Palipo na Jina la Yesu Kristo, Yeye mwenyewe Yesu Kristo yupo – na atahakikisha mnaloliomba linapatikana. Unapoliitia jina la Bwana mahali popote ulipo, Yesu Kristo anatokea hatakama humuono kwa macho ya kimwili.
Kuna wakati Fulani mwaka 1986, watu Fulani walifika nyumbani kuambia kuwa matokeo ya mitihani waliyofanya mwishoni mwa mwaka wa kwanza katika chuo walichokuwa wanasoma yametoka, na kwamba mwenzao mmoja ameshindwa masomo matatu kwa hataendelea na masomo tena. Kwa hiyo kwa kufika nyumbani kwangu, walikuwa wamemsindikiza mwenzao kuniaga.
Habari hizo nilipozisikia sikuzipenda kwa kuwa nilifahamu kuwa watu hao walikuwa wacha Mungu, wameokoka na wanampenda Yesu Kristo sana. Na biblia imesema wazi kabisa kuwa Bwana atawafanya watu wake, “kuwa kichwa, wala si mkia” (kumb. La torati 28:13). Bwana atawafanya kuwa juu tu, wala siyo chini.
Kwa hiyo nilijua hakika haukuwa mpango wa Munguhuyo mmojawao ashindwe mitihani. Ndipo nilipoanza kumwuliza maswali huyu kijana; “je umefeli mtihani au umefelishwa”?
Yeye akajibu kwa mshangao akasema; “matokeo ya mitihani yametoka na yanaonyesha kuwa nimeshindwa mitihani mitatu – ambayo kwa utaratibu wa chuo huwezi ukaendelea na masomo”.
Kwa jibu hili nilielewa kuwa alikuwa haaelewa kwa nini nilimuuliza swali hilo. Kwa hiyo nilimwuliza swali jingine, nikasema; “Je uliwahi, kushuhudiwa rohoni juu ya matatizo utakayokuwa nayo kimasomo?” Yule msichana akajibu, “ndiyo”, na niliomba sana hata kwa kufunga”.
“Je uliomba tu pamoja na kuomba ulofanya bidii ya kusoma? Mimi nilimuuliza. Nilimuuliza swali hili kwa kuwa kuna wanafunzi wengine wakiokoka wanadhani watafaulu mitihani kwa maombi tu bila kufanya bidii katika kusoma. Wamesahau Biblia imesema “…..ufanye bidii katika KUSOMA…” (Timotheo 4:13)
Yule msichana akasema nilipokuwa naomba niliweka bidii pia katika kusoma masomo. Je ulipomaliza kufanya mitihani ya masomo yote, ni masomo mangapi ambayo ulikuwa huna uhakika wa kufaulu?” nilimuuliza tena.
“Masomo mawili tu – ambazo kufuatana na taratibu za chuo nisingefukuzwa bali ningerudia mwaka mmoja tena” alieleza yule msichana. Baada ya mazungumzo hayo nilifahamu moyoni mwangu ya kuwa Ibilisi alikuwa alikuwa amenuia kuharibu masomo ya kijana huyo. Ghafla wazo lilinijia moyoni mwangu, halafu nikamwuliza swali Yule msichana; “Je unataka kurudi nyumbani au unataka kuendelea na masomo?”
Yule msichana alishangaa nilipomwuliza swali hilo, lakini akanijivbu akasema; “napenda kuendelea na masomo, lakini wamekwisha sema nimeshindwa na matokeo yamekwisha kupelekwa makao makuu ya wizara.
Ndipo nikamkumbusha nikasema; “Mungu tunayemtumikia na kumwabudu katika Kristo Yesu, ni Mungu yule yule wa Joshua aliyesimamisha jua na mwezi visisogee mpaka wana wa Israeli walipomaliza vita kwa ushindi”.
Nikaendelea kusema kuwa; “zaidi ya hayo tunalo jina la Yesu Kristo ambalo linapita majina yote na lina mamlaka mbinguni, duniani, na chini ya nchi. Yesu Kristo alisema tukipatana lolote duniani na kuomba kwa Jina lake tutafanyiwa na Baba Mungu. Kwa hiyo tunakwenda kupatana na kuomba kwa Mungu kuwa matokeo ya mitihani yabadilishwe na urudi chuoni uendelee na masomo. Je! Wote tunakubaliana na patano hili?”
“ndiyo!” walijibu wale vijana kwa pamoja.
Halafu nikasema hivi ndivyo mtakavyofanya; “mtarudi chuoni na kuanza kumtafakari Mungu, uku wake na matendo yake yaliyoandikwa katika Biblia. Pia, mtafakarimambo ambayo amekwisha watendea ninyi binafsi. Baada ya muda mtaona ndani ya mioyo yenu uzito wa mawazo ya kushindwa mtihani yanatoweka; na badala yake mioyoni mwenu mtajaa imani ya kujua hakuna lisilowezekana kwa Mungu”
“kwa maneno mengine nataka mumtafakari Mungu na ukuu wake, kiasi ambacho mfikie ndani yenu anakuwa mkubwa kuliko tatizo mlilonalo”.
“Mkiifikia hali hiyo, ingieni katika maombi kama tulivyokubaliana, bila kusahau kutubu kwa ajili ya kushindwa mitihani. Na mimi nitashirikiana nanyi katika maombi nikiwa hapa nyumbani. Halafu kesho asubuhi uende (nikimtazama yule msichana aliyeshindwa mtihani) kwa mwalimu wako umwombe uone alama za matokeo ya mitihani ya masomo wanayosema umeshindwa – mwambie ya kuwa wewe unaamini kuwa umefaulu.
Kwa jinsi ya kibinadamu lilionekana kama ni jambo lisilowezekana – lakini wale vijana walilikubali na wakaondoka. Kesho yake jioni walirudi nyumbani kwangu kwa furaha, na yule kijana akanieleza yafuatayo:- “tulifanya kama ulivyotuambia, tukaomba na asubuhi leo nilikwenda kumwona mwalimu. Akanionyesha alama za mitihani yangu, na wakagundua kuwa kulikuwa na makosa kwa upande wao katika kuandika alama katika somo moja – badala ya kuandika maksi 19 waliandika 9. Wakaniambia nandike barua kwa mkuu wa chuo, na nikafanya hivyo, na mkuu wa chuo akasema niendelee na masomo.
Yule kijana aliendelea na masomo vizuri, sasa amemaliza na anafanya kazi! Jina la Bwana libarikiwe!
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

TRENDING NOW