Sunday, September 10, 2017

JE, YESU ALIMAANISHA NINI ALIPO SEMA MSIDHANI KUWA NIMEKUJA KUTENGUWA TORATI AU MANABII; LA, BALI KUTIMIZA?

Image may contain: text and nature
Hoja nyingine kutoka kwa wasabato hujengwa katika kitabu cha Mathayo 5:17-18 inayosema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, BALI KUTIMILIZA. Kwa maana, amini, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”
Hoja inayojengwa na wasabato katika andiko hili, ni kwamba, Bwana Yesu anakiri hajakuja kutangua torati wala manabii bali amekuja kuitimiliza, yaani wakimaanisha kuwa, naye amekuja kuishika sabato.
Watoto wa Mungu, hii hoja ni ya undanganyifu. Kuupata ukweli, ni vizuri turudi kwenye Biblia ya Kiingereza ya toleo la King James ili tupate tafsiri nzuri zaidi. Mathayo 5:17, “Do not think that I came to destroy the law or the prophets. I did not come to destroy but to FULFILL…..” Kadhalika na matoleo mengine ya Kiingereza, neno ‘Kutimiliza’ kwa Kiingereza limetumika ‘FULFILL’. Kulingana na kamusi ya Kiingereza, neno ‘fulfill’ lina maana zifuatazo; maana ya kwanza ya ‘fulfill’ ni ‘fill up’ yaani ‘jazia.’ Kwa hiyo inaleta maana ya kwamba, Bwana Yesu, hakuja kuitangua bali amekuja kuijazia (fill up), kwani kulikuwa kuna mapungufu katika lile agano. Na ndiyo maana katika kitabu cha Waebrania 8:7 tunasoma, “Maana kama lile la kwanza, lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.”
Maana ya pili ya ‘fulfill’ ni ‘an act of doing something to satisfaction’ ikiwa na maana kwamba ni kitendo cha kufanya kitu ili kifike kwenye utoshelevu. Kwa hiyo, Bwana Yesu hakuja kuitangua torati na manabii, bali amekuja kuboresha ili ifikie utoshelevu, maana bado torati na manabii, haikuleta utoshelevu wala kuleta matokeo mazuri kwa watu, kwani kila kukicha watu walikuwa wakiuawa kwa kushindwa kuiishi torati. Maana ya tatu ya ‘fulfill’ ni ‘an act of achieving goal’ kwa Kiswahili inamaanisha ni kitendo cha kufanya kitu kifike kwenye malengo.
Kwa hiyo kwa lugha nyingine tungeweza kusema kwamba, Bwana Yesu amekuja kuifanya torati na manabii iweze kufikia malengo aliyokusudia, kwa sababu bado ilikuwa na shida kulingana na uwezo wa mwanadamu. Sasa kwa lugha fasaha ni kwamba, Bwana Yesu, hakuja kuiondoa torati na manabii, bali alikuja kufanya maboresho, marekebisho, masahihisho; ikiwa na maana kwamba kilichotakiwa kuondoka kiliondoka, na kilichotakiwa kubaki, kilibaki; na hii ilifanya na chekecho la msalaba. Mfano, mambo ya kushika sabato yaliondolewa, kwa sababu sabato ilikuwa ni amri ya ishara, ilikuwa ni kivuli, ikimuashira Yeye Bwana Yesu mwenyewe kama pumziko la kweli la kiroho. Hivyo, kwa vile Yeye pumziko halisi amekuja, sabato haikuwa na kazi tena. Bwana Yesu anasema, “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao, na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” (Mathayo 11:28)
Upungufu wa Agano la lake unaozungumziwa katika Waebrania 8:7, haupo katika torati, kwani torati kwa asili, haina tatizo na ni njema maana ni maagizo ya Mungu mwenyewe. Tatizo lilikuwa kwenye uwezo wa wanadamu wenyewe katika kuifuata torati yote kwa nguvu zao; maana kipindi cha agano la kale, walipewa sheria na hukumu tu, lakini hawakuwa na neema ya kuwafanya washike hiyo sheria. Kwa hiyo, kimsingi wana wa Israeli waliipenda torati (sheria) na hukumu walizopewa na Mungu, na waliikubali hiyo torati (sheria) na hukumu, na ndiyo maana walikubali kufanya agano na Mungu, kwa kuwa kila agano ni lazima kuwepo kwa makubaliano katika pande mbili.
Mioyoni mwao waliikubali na kuipenda torati (sheria) na hukumu zake, lakini mwili uliwazuia kuitekeleza hiyo torati, kwa kuwa walipewa torati (sheria) na hukumu tu bila neema au kiwezesho cha kuiishi sheria. Sasa hapo ndipo tunapopata upungufu wa Agano la kale.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW