Sunday, September 10, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TISA)

Image may contain: night and text
Vijana Huuliza . . .
Ninaweza kuepukaje Ponografia?
 Elewa ponografia ni nini? Ni mbinu ya kishetani ya kushushia heshima kitu ambacho Yehova aliumba ili kiheshimike. Kuelewa ponografia kwa njia hiyo kutakusaidia ‘kuchukia yaliyo mabaya.’—Zaburi 97:10.
 Fikiria madhara yake. Ponografia huharibu ndoa. Inawashushia heshima wanawake na wanaume. Inamshushia heshima mtu anayeitazama. Kwa sababu nzuri Biblia inasema: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha.” (Methali 22:3) Andika hapa chini mfano mmoja wa msiba unaoweza kukupata ukiwa na zoea la kutazama ponografia.
“Mvulana mmoja shuleni kwetu alikuwa amebandika picha ya msichana aliye uchi kwenye mlango wa kabati lake. Kabati hilo lilikuwa karibu na langu.”—Robert.*
“Nilikuwa nikifanya utafiti kwenye Intaneti kwa ajili ya ripoti ya shule nilipopata kituo cha ponografia.”—Annette.
WAZAZI wako walipokuwa na umri kama wako, mtu aliyetaka kutazama ponografia alihitaji kuitafuta sana. Siku hizi ni kana kwamba ponografia inakutafuta. Kama vile Robert, aliyenukuliwa hapo juu, huenda umejikuta ukitazama ponografia ya mwanafunzi mwenzako. Au kama Annette, huenda ukaipata bila kukusudia kwenye Intaneti. Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 anasema, “Nyakati nyingine ninapitia-pitia Intaneti tu au kununua vitu kwenye Intaneti au hata kuchunguza tu habari za akaunti yangu ya benki kisha ghafula ponografia inajitokeza!”*
Hilo si jambo la kushangaza. Katika uchunguzi mmoja, asilimia 90 ya vijana walio kati ya umri wa miaka 8 na 16 walisema kwamba walipata ponografia kwenye Intaneti bila kukusudia, mara nyingi walipokuwa wakifanya kazi za shuleni! Ukweli ni kwamba, kukiwa na mamilioni ya vituo vya Intaneti vilivyo na mamia ya mamilioni ya sehemu zenye habari za wazi kuhusu ngono, ponografia inapatikana kwa urahisi sana. Inaweza pia kupatikana kupitia simu ya mkononi. Denise mwenye umri wa miaka 16 anasema, “Shuleni kwetu ni jambo la kujisifu. Jumatatu mazungumzo huwa kuhusu, ‘Una picha gani kwenye simu yako ulizotoa kwenye Intaneti mwishoni mwa juma?’”
Kwa kuwa unajua watu wengi sana wanatazama ponografia, huenda ukajiuliza, ‘Je, ponografia ina madhara?’ Sababu kadhaa zinaonyesha kwamba jibu ni ndiyo. Fikiria sababu tatu tu:
 Ponografia huwashushia heshima wale wanaoitayarisha na wale wanaoitazama.—1 Wathesalonike 4:3-5.
 Kupendezwa na ponografia ni kama kuiga mapendezi ya ngono yasiyo ya asili ambayo roho waovu wa siku za Noa walikuwa nayo.—Mwanzo 6:2; Yuda 6, 7.
 Mara nyingi kutazama ponografia huwa hatua ya kwanza inayomwongoza mtu kufanya dhambi zinazohusu ngono.—Yakobo 1:14, 15.
Ponografia huwaathiri vibaya wale wanaonaswa nayo. Fikiria mifano miwili tu:
“Niliona ponografia kwa mara ya kwanza nilipokuwa mdogo, na imekuwa vigumu sana kuachana nayo. Miaka mingi sana imepita, lakini picha hizo zimebaki katika kumbukumbu langu. Ni kana kwamba mawazo hayo huwa tu katika akili, na hakuna wakati dhamiri inakuwa safi. Ponografia inakufanya usijiheshimu na inaweza kukufanya ujihisi mchafu na mtu asiyefaa. Nyakati zote unakuwa na mzigo wa siri ambao lazima ubebe.”—Erica.
“Nilikuwa mraibu wa ponografia kwa miaka 10, na sasa miaka 14 imepita tangu nilipoacha kuitazama. Lakini hata sasa, lazima nipambane kila siku. Ingawa tamaa imepungua sana, bado ipo. Udadisi bado upo. Picha bado zimo akilini. Ninajuta kwa nini nilianza kufanya jambo hilo. Mwanzoni ilionekana kama haina madhara. Lakini sasa ninaelewa ukweli wa mambo. Ponografia inadhuru, ni potovu, na inawashushia heshima watu wote wanaohusika. Hata wale wanaoitetea waseme nini, hakuna kitu chochote kizuri kuhusu ponografia.”—Jeff.
INAWEZEKANA NA MWAMBIE TATIZO LAKO YESU NA ATAKUKOMBOA.
BARIKIWA SANA NA TUENDELEE KUMTUMIKIA YESU MUNGU MKUU.
Tumefikia tamati ya somo letu, lakini endelea mwenyewe kumtafuta Yesu na atakufunulia mengi.
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO

Image may contain: one or more people and text
Baada ya kuokolewa, tunahitaji pia kutakaswa. Bila utakaso, tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi za ndani katika mawazo, na moyoni, ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda. Dhambi za ndani , ni kama hasira, wivu ,chuki, masengenyo, kugombania ukubwa, kiburi, majivuno, kutokusamehe, kinyongo, kupenda udunia n.k.
Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa: Mawazo yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23), kugombania ukubwa (Luka 22:24-26; Mathayo 20:20-22,25-28; Marko 9:30-37), hasira (Mathayo 20:24) wivu, fitina, ugomvi (Marko 9:38-39; Luka 9:49-50; 1Wakorintho 3:3-5), faraka na matengano (1Wakorintho1:10-13), umimi (Mathayo 28:6-13), kutokusamehe (Mathayo 18:21-35), chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani (Luka 9:51-56; 1Wakorintho 6:1-8); Warumi 7:15 n.k . Mambo haya huondolewa kwa utakaso.
Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka (Yohana 17:14-19).
Roho mtakatifu ndiye atupaye Utakaso (1Wakorintho 6:11; 1Petro1:2)
Je, hujatakaswa, mwambie Roho Mtakatifu akutakase, yeye ni waminifu, atafanya (1Thesalonike 5:23-24)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

Image may contain: fruit, text and food
Katika Wagalatia 5:22-23, tunajifunza juu ya tunda la Roho. Katika lugha ya asili, yote katika mistari hii yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu, Upendo. Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu katika tabia na matendo kama furaha, amani, uvumilivu, utu wema,f adhili, imani, upole, na kiasi. Ni pale tu tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo, ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Pasipo upendo, tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao, tunakuwa si kitu. Lolote jingine tunalolifanya linakuwa halina faida (1Wakorintho 13:3). Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8) Sasa basi , ni muhimu kufahamu kwamba upendo ni tunda la Roho, tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.
Tukilipokea tunda hili, na kukua kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12), Kama matunda yanavyokua, ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli. Tukiwa na tunda la Roho la upendo, tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili (Yakobo1:2). Tutakuwa na amani ipitayo fahamu zote (Wafilipi 4:7) inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.
Tutakuwa na lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote (Waebrania 12:14) Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso, makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka (Marko 10:17). Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.
Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29; Wafilipi2:5-8) Na pili tutakuwa na kiasi (self-control) yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki, kwa gharama yoyote.
Je, unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu, naye atafanya.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: one or more people and text
Hili ni somo linalo tatanisha na kuwewesesha watu wengi, na labda naweza hata kuhukumiwa kuwa natumia lugha chafu, la hasha. Nilazima tujifunze kila kitu, maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
KUJICHUA NI NINI HASA?
Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘masturbation’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.
Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!
Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha
Unapoanza kubalehe, tamaa za ngono zinaweza kuwa zenye nguvu sana. Kwa sababu hiyo, huenda ukaangukia mazoea ya kupiga punyeto. Wengi husema kwamba si neno kufanya hivyo. “Hakuna mtu anayeumia,” wanasema. Hata hivyo, kuna sababu nzuri ya kuepuka mazoea hayo. Mtume Paulo aliandika: “Kwa hiyo, viueni viungo vya mwili wenu . . . kwa habari ya . . . hamu ya ngono.” (Wakolosai 3:5-Toleo la Ulimwengu Mpya) Kupiga punyeto hakuui hamu ya ngono bali kunaichochea. Isitoshe, fikiria yafuatayo:
Kupiga punyeto humfanya mtu kuwa mwenye ubinafsi. Kwa mfano, mtu anapopiga punyeto, anakazia fikira hisia zake mwenyewe za kimwili.
Kupiga punyeto humfanya mtu kuwaona watu wa jinsia tofauti kuwa vitu au vifaa vya kujitosheleza tu.
Badala ya kuamua kupiga punyeto ili kuzima tamaa za ngono, jitahidi kukuza sifa ya kujizuia. (1 Wathesalonike 4:4, 5) Ili ufaulu, kwanza kabisa Biblia inapendekeza ujiepushe na hali zinazoweza kuamsha tamaa ya ngono. (Methali 5:8, 9) Namna gani ikiwa umekuwa mtumwa wa zoea la kupiga punyeto?
Labda umejaribu kuacha lakini hujafanikiwa. Ni rahisi kukata kauli kwamba huwezi kubadilika, na kwamba huwezi kuishi kulingana na viwango vya Mungu. Hivyo ndivyo mvulana anayeitwa Pedro alivyojiona. “Niliporudia zoea hilo, nilihisi vibaya sana,” anasema. “Nilifikiri kwamba siwezi kamwe kusamehewa. Nilishindwa kusali.”
Ikiwa hivyo ndivyo unavyohisi, jipe moyo. Kuna tumaini. Vijana wengi, na watu wazima pia, wamefaulu kushinda mazoea hayo ya kupiga punyeto. Wewe pia unaweza kufaulu!
INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni
kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika. Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha.
Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo. Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.
Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA.

Image may contain: cloud, sky, bird and text
Kila Mkristo au mtu aliyeokoka, hana budi kuwa na lengo la kufikia kimo na cheo cha utimilifu wa Kristo katika tabia na Utumishi wa Mungu (Waefeso 4:11-15 ). Kufikia kiwango cha Yesu Kristo katika tabia ni jambo linalowezekana, Kama siyo, tusingetakiwa kuwa wakamilifu na watakatifu kama Baba wa mbinguni alivyo Mtakatifu (Mathayo 5:48;1`Petro 1:15-16) Neno la Mungu pia, linatufundisha uwezekano wa kuwa na viwango vya utumishi vya Yesu alipokuwa duniani, na hata kuzidi (Yohana 14:12).
Hata hivyo haya yote hayawezekani kama sisi siyo waombaji kama Yesu alikuwa mwombaji namba moja. Alifanya maombi alfajiri na mapema (Marko 1:35). Alijitenga na shughuli mchana na kufanya maombi (Luka 5:15-16) Aliomba jioni (Mathayo 14:23) Wakati mwingine alifanya maombi usiku kucha (Luka 6:12).
Je,sisi tunaweza kuwa waombaji kiasi hiki? Kwa nguvu na jitihada zetu hatuwezi.
Tunaweza tu, tukisaidiwa na Roho Mtakatifu. Ndiyo maana tunajifunza somo hili muhimu leo katika mfululizo wa masomo haya ya Roho Mtakatifu, na kichwa cha somo la sasa ni
”ROHO MTAKATIFU, ATUSAIDIAYE KUOMBA”, NA TUTAJIFUNZA SOMO HILI KATIKA VIPENGERE VINNE:-
A. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
B. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
C. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
D. ROHO MTAKATIFU,MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
A. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
Shetani ndiye adui yetu mkuu. Kazi yake ni kuiba chochote kizuri cha kiroho tulicho nacho, na tena kuchinja au kuua na kuharibu yote mema kwetu kiroho na kimwili.Tukiwa peke yetu, kamwe hatuwezi kupambana na shetani na kumshinda. Hatuna budi kuwa na Mungu katika maisha yetu ili tumshinde ibilisi. Daudi alimshinda Goliathi kwa Jina la Bwana.
Hakumshinda kwa nguvu zake. Kwa maana nyingine hatuwezi kuzaa matunda yoyote mema ya kiroho kama hatuko ndani ya Yesu. Usalama wetu na ushindi wetu wa kiroho, unategemeana sana na sisis kukaa ndani yake Yesu, yaani sisi kuwa na uhusiano au ushirika na Kristo. Pasipo yeye, sisi hatuwezi kufanya neno lolote. (Yohana 15:4-5). Kukaa ndani ya Yesu, kunafananishwa na tawi lililounganishwa na shina.
Kuunganishwa huko ndiyo uhai wa tawi.
Tawi likijitenga na shina, linanyauka na kufa. Sasa basi, tunaunganisha na Mungu na Mungu tunapokuwa tunawasiliana naye katika maombi. Tukiwa hatuna maisha ya maombi, kimsingi ni kwamba tunakuwa ni tawi lililojenga na shina, na hivyo tunanyauka na hatimaye kufa kiroho. Hatuwezi kuwa na kitu tusipoomba (Yakobo 4:2)
Tutaingia majaribuni tusipoomba (Mathayo 26:41).
Tutapepetwa kama ngano na ibilisi na mazuri yote ya kiroho yataondoshwa, na imani yetu itatoweka (Luka 22:31-32).
Shetani atatumeza na kuturudisha katika ufalme wake (1Petro 5:8).
Hatuwezi kuwaleta watu kwa Yesu, tusipokuwa waombaji, maana Shetani hatawaachia (Zaburi 2:8).
Hatuwezi kuona watu wakifunguliwa katika vifungo vya shetani vya kimwili (Luka 13:16) na vile vinavyotokana na mambo ya rohoni (Matendo 12:5-17). Kwa ufupi tutachukuliwa na mafuriko ya Shetani (Zaburi 32:6).
B. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
Maandiko yanatufahamisha kwamba makao ya Mungu mbinguni, ni Mahali palipoinuka, na Mlimani kwenye kiti cha enzi cha Mungu (Isaya 57:15; Kutoka 24:12-13 ; Ufunuo 7:9-10). Ingawa Mungu wetu yuko mlimani, maandiko yanasema tukimwomba, yeye husikia huko mbinguni na kutujibu maombi yetu kwa kuyatenda tunayoyataka (1Wafalme 8:32; Zaburi 76:8;1 02:19).
Hata hivyo, hatuna budi kufahamu pia kwamba katika mazingira fulani Mungu hushuka kutoka mlimani na kuja duniani katika hali isiyo ya kawaida. Mungu anaposhuka kwa jinsi hii, hutenda mambo ya kutisha, na ya kushangaza, yasiyo ya kawaida na hivyo kuwavuta wengi mno kwake (Waamuzi 4:12-16,5:13; Isaya 31:4; Hesabu 11:23-25,31-32).
Uamsho hutokea Mungu anaposhuka, na watu wagumu wa mioyo huvutwa kwa Yesu, walio vuguvugu huwa moto, mambo mengine makubwa ya kuitikisa jamii kama mamia ya wenye ukimwi kupona kwa mpigo, hutokea, Mungu akishuka.
Hata hivyo kushuka kwa Mungu hutokea baada ya maombi ya kuugua na kulia kwa uchungu mkubwa (Kutoka 2:23-24;3:7-8;
Matendo 7:32-34). Wakati wote Yesu Kristo alimfanya Mungu kushuka katika huduma yake kwa kuwa aliomba kwa kulia sana
na machozi (Waebrania 5:7), na wengine walimuombolezea kwa kilio na uchungu mkubwa (Luka 23:27).
Kulia kwa kuugua katika maombi hushusha majibu ya maombi namna ya kipekee (2Nyakati 34:27; Zaburi 34:17;39:12;51:1-2,17;72:12;12;88:1-2; Isaya 58:9; Yeremia 31:9; Luka 18:7).
Sasa basi ni rahisi kuomba maombi kwa kulia na kuugua?
Jibu ni la ,bila msaada wa Roho Mtakatifu, itakuwa kama tunaigiza tu.
C. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU.
Tunajifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na maombi kwa kuyaangalia maisha ya maombi ya Yesu, na mafundisho yake kuhusu maombi:-
§ Yesu Kristo alikuwa na wakati wa kuomba pamoja na wanafunzi wake (Luka 9:18), Lakini pia alikuwa na muda mrefu wa maombi ya peke yake (Luka 5:16; Marko 6:45-46). Ni muhimu kujiunga na kikosi cha maombi cha Kanisa na kushiriki maombi ya pamoja na wengine, lakini ni lazima kila mmoja kuwa na muda wa kuomba mwenyewe.
§ Yesu hakukubali kuchukuliwa na huduma za kushauri watu, kuwaombea watu n.k na kuziruhusu zimkoseshe kuomba.
Alijua bila maombi, huduma hizo zitakuwa hazina nguvu. Aliziacha huduma, akafanya maombi (Luka 5:15-16). Kabla ya kuzungumza na watu, alizungumza na Mungu KWANZA. Alifanya maombi ya alfajiri na mapema sana na baadaye alipokutana na watu ilikuwa rahisi mno kwake kuponya ukoma na kutoa pepo. (Marko 1:35-42).
§ Kabla ya Yesu kutembea juu ya maji, na kukomesha upepo, alikuwa na kipindi kirefu cha maombi (Marko 6:46-51). Vipindi virefu vya maombi vinaweza kutupa uwezo wa kuona yasiyowezekana yakiwezekana!
§ Utukufu wa Yesu ulitokana na maombi! (Luka 9:28-29) Hatuna utukufu wa Mungu kwa kuwa siyo waombaji! Mwombaji, utukufu wake humwogopesha shetani
§ Alipokuwa na huzuni aliomba hakunung'unika tu na kulalamika, na ghafla alipata ujasiri wa kukabili lolote lile (Mathayo 26:36-39; 47-49). Hatuna ujasiri na tumejaa woga kwa kuwa hatuombi
§ Maombi yake yalikuwa ni vita hasa. Alipokuwa akiomba, alitoka jasho (hari) kama matone ya damu (Luka 22:44).
Maombi ni mapambano dhidi ya shetani anayezuia majibu yetu (Danieli 10:12-13). Ni lazima iwe ni vita. Mwili ni lazima tuushughulishe kama wapiganaji hasa, tukiwa katika roho Maombi yenye matokeo makubwa, ni yale ya kutoka jasho! Ni lazima tumkabili shetani katika vita ya maombi kabla hata hajatushambulia.Katika vita ya siku sita kati ya waisraeli na wamisri, miaka kadha iliyopita; Waisraeli walishinda Wamisri ingawa walikuwa na ndege nyingi zaidi za kivita kuliko wao,kwa kuwa walizipiga KABLA hazijaondoka katika vituo vyao.
Tusingoje matatizo ndio tuombe!
§ Imani yetu na ya ndugu zetu,inaweza kutokutindika,ikiwa tu tutakuwa waombaji;kinyume cha hapo ni rahisi kumezwa na
shetani (Luka 22:31-32;1Petro 5:8-9)
§ Maombi ndiyo yanafanya tuutunze utakatifu wetu,na kuwa mbali na dunia. Bila maombi ni rahisi kuvutwa na masumbufu
ya dunia (Luka 21:34-36).
§ Yesu aliliombea Kanisa (Yohana 17:14-15). Ni muhimu kuliombea kanisa na siyo kujiombea wenyewe tu wakati wote.
Je tunaweza kuyatendea kazi yote haya kwa nguvu zetu? Jibu ni la kwa nguvu zetu hatuwezi ,bila msaada wa Roho Mtakatifu.
D. ROHO MTAKATIFU MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
Shetani anafahamu sana umuhimu wa maombi, na hivyo atatuzuia sana kufanya maombi kuliko yote mengine, ili tubaki kama matawi ambayo hayajaunganishwa na shina. Anajua pasipo Mungu, sisi hatuwezi neon lolote. Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi. Tunaweza kuomba sisi hatuwezi neno lolote. Kwa kujifunza tu juu ya maombi, bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi. Tunaweza kuomba siku mbili, tatu, halafu basi. Pamoja na wanafunzi wa Yesu kuhimizwa kuomba na Yesu mwenyewe, bado walishindwa kuwa waombaji (Mathayo 26:37-43).
Ndipo hatimaye akawaambia atakuja Msaidizi ambaye kazi yake mojawapo, ni kutusaidia kuomba (Yohana 16:7; Warumi 8:26-28). Yeye Roho, kwa kuwa hutuombea kwa kuugua, na tena ni Roho ya neema na kuomba, huweza kutupa msaada wa kutuwezesha kuomba kwa kuugua na kulia (Zakaria 12:10) Baada ya Roho Mtakatifu kuja na kuwasaidia wanafunzi wa
Yesu, maisha yao ya maombi yalibadilika (Matendo 10:9). Siri ni hii, usitumie nguvu zako kuomba. Kabla ya kuingia katika maombi, mwombe Msaidizi akusaidie kuomba.
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: 1 person, text


CHANZO NI NINI HASA?
Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii mbaya hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta ayari!
Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo
mwanzo wa kutopea huko.
Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.
Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.
Kama ilivyotajwa mapema, wale walio na mazoea ya kupiga punyeto mara nyingi hujiona kuwa wenye hatia. Bila shaka, ‘kuhuzunishwa kwa njia ya kimungu’ kunaweza kukuchochea ushinde mazoea hayo. (2 Wakorintho 7:11) Lakini kujiona kuwa mwenye hatia kupita kiasi kunaweza kuwa na matokeo mabaya. Kunaweza kukuvunja moyo sana mpaka utake kukata tamaa.—Methali 24:10.
Kwa hiyo, jaribu kuwa na usawaziko. Kupiga punyeto ni uchafu. Mazoea hayo yanaweza kukufanya uwe ‘mtumwa wa tamaa na raha za namna mbalimbali’ na kukufanya uwe na maoni yasiyofaa. (Tito 3:3) Hata hivyo, kupiga punyeto si upotovu wa kingono, kama vile uasherati. (Yuda 7) Ikiwa una tatizo la kupiga punyeto, usikate kauli kwamba umefanya dhambi isiyoweza kusamehewa. Siri ni kupinga tamaa ya kufanya hivyo na kutokubali kamwe kushindwa!
Ni rahisi kuvunjika moyo baada ya kurudia zoea hilo. Ukirudia, kumbuka maneno ya Methali 24:16: “Huenda mwadilifu akaanguka hata mara saba, naye hakika atasimama; lakini waovu watakwazwa na msiba.” Kujikwaa hakumaanishi kwamba wewe ni mwovu. Kwa hiyo, usikate tamaa. Badala yake, chunguza jambo lililofanya urudie zoea hilo, kisha ujaribu kuliepuka.
Tafakari kuhusu upendo na rehema za Mungu. Mtunga-zaburi Daudi, ambaye pia nyakati fulani alifanya dhambi kwa sababu ya udhaifu wake, alisema: “Kama vile baba anavyowaonyesha wanawe rehema, ndivyo ambavyo Mungu amewaonyesha rehema wale wanaomwogopa. Kwa maana yeye mwenyewe analijua vema umbo letu, akikumbuka kwamba sisi ni mavumbi.” (Zaburi 103:13, 14) Ndiyo, Mungu hukumbuka hali yetu ya kutokamilika na ‘yuko tayari kusamehe.’ (Zaburi 86:5) Kwa upande mwingine, anataka tujitahidi na kufanya marekebisho. Hivyo basi, unaweza kuchukua hatua gani ili kushinda zoea hilo?
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU








Ili tuweze kuwa mashahidi wa Mungu,tunahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka na kutakaswa. Ili tumtendee Mungu kazi kikamilifu, ni lazima tupokee nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8;Luka 24:49). Kwa sababu hili, somo hili, ni la muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mtendakazi mzuri wa Mungu. Tutaligawa somo hili katika vipengere vinne:-
A. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
B. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
C. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
D. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
E. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
F. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
A. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Baada ya mtu kuokolewa,inambidi kubatizwa kwa maji kwa jina la baba,Mwana na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19). Hata hivyo,huo siyo ubatizo wa mwisho.Baada ya mtu kutakaswa,anahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu (Mathayo 3:11) Ubatizo wa maji, unamfanya mtu azamishwe ndani ya maji na kuzungukwa na maji pande zote. Vivyo hivyo, Ubatizo wa Roho Mtakatifu unamfanya mtu aliyeokoka,kuzamishwa ndani ya Roho Mtakatifu na kuzungukwa na Roho Mtakatifu pande zake zote.Roho Mtakatifu,anakuwa msaidizi wake (Yohana 15:26). Ubatizo wa maji,tunabatizwa na wanadamu waliopewa Agizo la Mungu lakini Ubatizo wa Roho Mtakatifu, tunabatizwa na Yesu mwenyewe (Mathayo 3:11).
B. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU, UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
Neno “mashahidi” katika (Matendo 1:8), linatokana na neno la lugha ya Kiyunani “Martus” ambalo linatafsiriwa katika Kiingereza" Martyr” ambalo maana yake ni “Mtu anayekuwa tayari kuteswa sana au hata kuuawa kwa sababu ya imani yake,pamoja na hayo, hawezi kuiacha imani yake”.Bila ubatizo wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kuwa mashahidi kama walivyokuwa Stefano na Antipa (Matendo 22:20; Ufunuo 2:13). Kabla ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu,Petro alisema asingemkana Yesu hata ikibidi kuuawa, lakini kinyume chake alimkana mara tatu,na yeye pamoja na wanafunzi wenzake walipoyaona mateso yanakuja,walimwacha na
kumkimbia Yesu (Mathayo 26:31-35,56) Lakini baada ya ubatizo walikuwa na ujasiri mkubwa. Matendo 4:13
C. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
§ Maji (Yohana 7:37-39)Hakuna maisha bila ya maji.Mwanadamu ni asilimia 60%maji.Kuharisha na kutapika sana humfanya mtu kupoteza maji mengi na huweza kusababisha mtu kupoteza uhai. Vilevile sisi tunaosema tumeokoka, hatuwezi kabisakuwa na maisha ya kiroho yaliyo hai yenye nguvu, bila Ubatizo wa Roho Mtakatifu.Ni lazima tunyweshwe Roho (1Wakorintho 12:13).
Jambo jingine, maji ni muhimu katika usafi wa miili yetu hutuondolea kunuka n.k Roho Mtakatifu hutumulikia dhambi au uchafu wowote.
§ Moto (Mathayo 3:11).Kuwepo kwa moto ni alama ya uwepo wa Mungu (Kutoka 3:1-5; Matendo 2:2-3). Moto vilevile,unangarisha madini kama dhahabu na fedha (Malaki 3:2-3). Ubatizo wa Roho Mtakatifu hufanya uwepo wa Mungu uwe dhahiri kwa mtu na pia humng’arisha mtu na kuwa mtumishi wa Mungu anayeng’aa . Siyo hayo tu, moto huleta mwanga.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa mwanga mkubwa wa maandiko yaani Biblia na kutupa mwanga wa uzuri wa mbinguni na ubaya wa Jehenam.Ukiwa na mwanga huo hakutakuwa na gharama kubwa yoyote ya kukufanya ushindwe kufanya mapenzi ya Mungu. Moto pia huleta nguvu ya kuendesha, magari, treni, Ndege n.k vifaa vyote hivyo huendeshwa kutokana na moto unaotokea baada ya cheche za umeme kuunguza mafuta.
Kazi ya Mungu inaendeshwa kwa nguvu ya moto, ubatizo wa Roho Mtakatifu na kwa moto. Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu, moto unawake ndani yake na hawezi kuacha kushuhudia au kuhubiri na kufundisha (Yeremia 20:9; Isaya 62:1; Matendo4:20). Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu,maneno yake huwa moto unaoteketeza kila ugumu wa mioyo ya watu kwa kuwa Roho Mtakatifu hushuhudia pamoja naye na hivyo matokeo yake ya utumishi wake huwa makubwa. Ni nguvu kwa ajili ya Utumishi (Yeremia 5:14; Yohana 15:26-27;16:6-8;Mika 3:8).
§ Upepo (Yohana 3:8) Upepo wakati wote unatembea, na uko mahali pote. Roho Mtakatifu hakufanya kazi wakati wa mitume tu, hata sasa anatembea na yuko kwetu tayari, ni wajibu wetu kumpokea tu. Upepo huvuma upendako.
Ni vigumu kuubadilisha mkondo wa upepo tunavyotaka sisi,jahazi hufuata mkondo wa upepo. Ni muhimu kutakaswa kwanza kabla ya Ubatizo huu.
Utakaso humfanya mtu kuwa mtii mno katika yote na Roho Mtakatifu ni mshirika wa wale wamtiio(Matendo 5:32) Upepo pia hutuletea hewa safi inayotuburudisha wakati wa joto, moshi n.k Mazingira yoyote magumu tukiyakabili katika utumishi wa Mungu, Roho Mtakatifu huwa hewa safi kwetu inayorekebisha mazingira.
§ Mafuta (Luka 4:16-21) Roho Mtakatifu hututia mafuta au kutuweka katika utumishi wa Mungu (1Samweli 16:13; Kutoka 30:30; 1Wafalme 19:16;Yohana 2:27) Rais kabla hajaapishwa huitwa Rais mteule na hana mamlaka sana wakati huo kisheria.
Kuapishwa kwa leo ndiyo kutiwa mafuta kwa zamani.Bila ubatizo huu,mamlaka yetu huwa hafifu. Mafuta yanalainisha na kuzuia msuguano.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa hekima ya kuvuta roho za watu(Mithali 11:30) mafuta huufanya mwili uwe laini.
Ubatizo wa Roho Mtakatifu hulainisha ukavu wa maombi yetu (Warumi 8:26).
§ Mvua (Zaburi 72:6;Hosea 6:3) Nchi haiwezi kutoa matunda bila mvua.Mtu aliyeokoka hawezi kuwa na matunda mengi bila mvua yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu (Yohana 15:16).
§ Mvinyo (Waefeso 5:18;Matendo 2:12-13) mvinyo kwa walevi unasahaulisha shida. Ubatizo wa Roho Mtakatifu, humwezesha mtu kudharau majaribu na kuondoa wasiwasi na kubabaishwa na mambo madogo madogo tu. Mvinyo kwa walevi, pia unawapa ujasiri wa kufanya lolote lile, aibu, woga vinatoweka. Ubatizo wa Roho Mtakatifu humfanya mtu kuwa jasiri kama simba na mtu aliye kuwa mwoga kama Petro, kuwa jasiri (Mithali 28:1; Mathayo 26:31-35,56; Matendo 4:13).
§ Hua (njiwa)- (Yohana 1:32) Ubatizo wa Roho Mtakatifu haufanyiki kwa mtu wa ulimwengu huu yaani ambaye
hajaokoka. Njiwa hakutua kwenye ulimwengu,alirudi safinani kwa waliookoka (Mwanzo 8:8-9)Roho Mtakatifu ni mweupe, kama hua.Ni Mtakatifu,huja kwa watakatifu waliotakaswa.
§ Muhuri (Waefeso 1:13) Muhuri ni alama ya mamlaka.Bila muhuri barua hupungua mamlaka yake. Ubatizo wa Roho Mtakatifu humfanya mtu kuwa na mamlaka ya Yesu kwake na shetani husema “ Yesu namjua na Paulo namfahamu (Matendo 19:15) Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni mamlaka au uwezo kutoka juu wa kuzifanya kazi za Yesu.
§ Arabuni (2Wakorintho 1:21-22)Neno arabuni maana yake- Uhakikisho au uthibitisho wa Uimara.Ubatizo wa Roho Mtakatifu, hutufanya kuwa na uthibitisho wa uimara wa Neno la Mungu, hutuongezea imani ya kufanya maajabu.Shetani hawezi kumpeperusha huku na kule mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu.
D. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
Kuokoka au kuzaliwa mara ya pili.Mafuta haya hayatiwi kwa mtu mgeni ambaye jina lake haliko katika kitabu cha Uzima mbinguni (Kutoka 30:31-33)
Kutakaswa (Yohana 17:17;1Wathesalonike 5:23) Wanafunzi 120 orofani,walitakaswa kabla ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Kuwa na Imani kama Roho Mtakatifu yuko kwetu tayari na kwamba ni ahadi ya Mungu kwetu(Matendo 2:38-39); Luka 11:10-13)
Kuwa na kiu ya kumtumikia Mungu (Isaya 44:3)
Kuomba kwa kufumbua sana kinywa na kutokuruhusu kutumia akili,wala kuwaza kwambatutasema lugha ya mapepo. (Luka 11:10-13; Zaburi 81:10).
E. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
Mtu akibatizwa kwa Roho Mtakatifu,kutakuwa na mambo ya kusikia kwake na ya kuyaona kwake(Mathayo 3:16-17).
Ishara ya kwanza ni kusikia kutoka kwake kabla ya kuona mengine. Atasema au ananena kwa lugha mpya asiyoifahamu
ambayo siyo ya dunia hii (Matendo 2:4;10:44-46;19:6). Ni muhimu mno kwa mtu aliyeokoka kuomba kwa kunena kwa lugha hii (1Wakorintho 14:2,4-5,15). Hata hivyo hatupaswi kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasioelewa kitu. Watadhani sisi ni wendawazimu (1Wakorintho14:18-25)
Kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasiojua kitu nikuwapa mbwa kilicho kitakatifu na kutupa lulu zetu mbele ya nguruwe matokeo yake watatudhihaki kwa kuwa hawajui maana (Mathayo 7:6).
F. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
Moto bila kuchochewa huzimika (Mithali 26:20). Hatuna budi kuwa waombaji na kuomba kwa Roho, yaani kunena kwa lugha katika maombi mara kwa mara katika maombi yetu binafsi (1Wakorintho 14:14-15; Yuda 1:20) Vile vile hatuna budi kudumu katika usafi kwa Neno (Zaburi 51:4,11;119:11; Yohana 15:3).
Hatuna budi pia kujihusisha katika kushuhudia na kuwaleta watu kwa Yesu (Mika 3:8).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: one or more people and text
Chunguza burudani yako. Je, wewe hutazama sinema au programu za televisheni au hutembelea vituo vya Intaneti vyenye kusisimua kingono? Kwa hekima, mtunga-zaburi alisali kwa Mungu: “Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.”*—Zaburi 119:37.
Sali kuhusu jambo hilo. Mtunga-zaburi alisali hivi kwa Yehova: “Uyafanye macho yangu yapite ili yasione jambo lisilofaa.” (Zaburi 119:37) Yehova Mungu anataka ufaulu, naye anaweza kukupa nguvu za kufanya yaliyo sawa!—Wafilipi 4:13.
Zungumza na mtu. Mara nyingi kuchagua mtu unayeweza kumfunulia moyo wako husaidia sana kushinda zoea hilo. (Methali 17:17) Andika hapa chini jina la mtu mkomavu ambaye unaona ni rahisi kumweleza jambo hilo.
ATHARI ZA KUJICHUA "PUNYETO"
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.
Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.
Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa
kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.
Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.
Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!
Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.
“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.
USIKOSE SEHEMU TA NNE
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

JE, KUJICHUA SEHEMU ZAKO ZA SIRI (PUNYETO) NI DHAMBI? (SEHEMU YA NNE)

Image may contain: food
Mpendwa:
Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke wakiwa na uvutano wenye nguvu kati yao, na hakuna ubaya wa kutosheleza tamaa za ngono katika mpango wa ndoa. Kabla ya kufunga ndoa, huenda ukawa na tamaa kali za ngono. Hilo likitokea, usidhani kwamba wewe ni mtu mwovu au kwamba huwezi kuishi maisha safi. Unaweza kudumisha usafi wa kiadili ukiamua kufanya hivyo! Lakini ili ufanikiwe, utahitaji kudhibiti mawazo yako kuhusu watu wa jinsi tofauti. Unaweza kufanya hivyo jinsi gani?
Epuka kujifurahisha kwa mambo machafu. Bila shaka, haimaanishi kwamba sinema zote, au miziki yote ni mibaya. Hata hivyo, katika ulimwengu wa leo burudani nyingi zimekusudiwa kuamsha tamaa zisizofaa za ngono. Biblia inatoa shauri gani? “Acheni tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Epuka kabisa burudani zote zinazoweza kuchochea tamaa zisizofaa za ngono.
UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.
MFADHAIKO:
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili.
KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza.
Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe.
Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.
Baadhi yao, hubaki wakiwa baada ya wahusika wao kuwagomea katikati ya safari. Zipo athari nyingi zaidi ya hizo,
kutegemea na namna tatizo lilivyokomaa na aina ya jinsia.
Baadhi ya madhara ya Waathirika wa Upigaji Punyeto na Kujichuwa.
• Kupiga Punyeto Kunapelekea kufika mshindo kabla na bila kujijua na husababu matatizo ya Nguvu za Kiume.
• Kutokwa na manii usingizini bila kujijuwa.
• Maumivu ya mgongo.
• Punyeto usababisha udhaifu wa mwili.
• Kuwa na sura ya ujuvi.
• Udhaifu wa Macho, kutoona vizuri.
• Nywele Kutokuwa na Afya.
• Kupungua uzito chini ya kiwango.
• Uchovu na udhaifu wa mwili, wa mara kwa mara
• Kupata maumivi kwenye kinena.
• Maumivu kwenye mapumbu.
• Mbegu za uzazi kuwa dhaifu.
• Kutosikia raha ya mapenzi/jimai.
• Kupungua kwa hamu ya kula.
• Matatizo ya kusimamisha.
• Kupotea/kutosikia njege.
• Kufikia mshindo mapema, dakika moja hoi.
TUMEFIKIA TAMATI YA MADA YETU KUHUSU KUJICHUA SEHEMU YA SIRI.
JE, UPO TAYARI KUACHA MCHEZO HUU BAADA YA KUSOMA HII MADA?
INAWEZEKANA NA NJIA RAHISI NI KUOMBA KWA MUNGU AKUSAMEHE DHAMBI HII NA KUTOA HILI PEPO LA KUJICHUA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

BIBLIA INARUHUSU KULA NYAMA YA NGURUWE

Image may contain: grass, outdoor and nature
JE, KULA NYAMA YA NGURUWE NI DHAMBI?
1. Je, kuna aya yeyote ile katika Agano Jipya inayo mkataza Mkristo kula nyama ya Nguruwe?
2. Je, kuna sheria yeyote ile kwenye Agano Jipya inayo kataza kula nyama ya Nguruwe?
3. Je, Yesu alisema au waamrisha Wafuasi wake wasile Nyama ya Nguruwe?
4. Je, Yesu alipo vitakasa vyakula vyote [Marko 7 :15-19] kunapingana na sheria ya hapo mwanzo kwenye Mambo ya Walawi?
Ndugu msomaji,
Katika hili somo, tutajifunza kuhusu ulaji wa Nyama ya Nguruwe na kwanini Wakristo wanakula Nyama ya Nguruwe.
Tuanze moja kwa moja kwa kusoma aya za Biblia:
"Bwana Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawambia Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, kila mnyama wa katika nchi watawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani pamoja na viti vyote vilivyojaa katika ardhi,na samaki wote wa baharini vimetiwa mikononi mwenu, kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani ,kadhalika hivi vyote ,balo nyama pamoja na uhai ,yaani damu yake msile" {Mwanzo 9:1-4}
Ndugu msomaji wangu maandiko yamefunua wazi kwamba Mungu alitoa wanyama wote kuliwa baada ya mboga za majani walakini hatuoni Mungu akitoa sheria ama akiwabagulia wanyama wa kuliwa yaani walio safi na wasio safi, bali maandiko yametuonyesha kuwa Mungu alitoa wanyama wote kuwa chakula kwa wanadamu kama ilivyo shuhudiwa katika Mwanzo Mlango wa 9 aya ya 1-4.
Je sheria inayohusiana na wanyama safi na wasio safi ilitolewa wapi?
Ndugu msomaji kama ambavyo nilivyokwisha kutangulia kusema kuwa sheria hii inayohusiana na vyakula haikutolewa tangu mwanzo kwa ushaidi wa andiko ambalo nimekupa limeonyesha hivyo, swali la lini sheria hii ambayo ilihusiana na vyakula ilitolewa maandiko yapo wazi kabisa eneo ilo ni baada ya wana Israel kutolewa utumwani Misri ndipo tunaona katika biblia sheria inayohusiana na wanyama walio safi na wasio safi kwaiyo kabla ya hapo wanyama wote walikuwa chakula {Mambo ya Walawi 11 :1-7} kupitia fungu ili la biblia tunaona kuwa Mungu anatoa sheria inayohusiana na wanyama wanaopaswa kuliwa na wasiopaswa kuliwa?
Ni kweli kabisa Mungu alitoa hiyo kuwa ni sheria kwao wana wa Israel walakini tusiishie tu hapo katika kuangalia sheria kuwa ni sheria tusafiri pamoja kifikra,utakumbuka kuwa watu ambao kiasili sio wayahudi walikuwa hawana desturi za usomaji wa torati?
Je hii sheria iliyohusiana na wanyama safi na wasio safi ilifahamika kwao?
Bila shaka jibu ni hapana labda utajiuliza kwanini?
Napenda tujifunze ili jambo na kutokuacha historia ya vizazi pia na chanzo cha kusambaa kwa wanadamu duniani kote
Theolojia inatueleza kwamba vizazi vya ulimwengu huu vimetokana na wana watatu wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu, na Yafethi sasa katika historia ya chanzo cha mataifa mbalimbali kama inavyoelezwa kwamba wanadamu yaani mataifa yote yaliotokana na watoto wa Nuhu walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na waliishi pamoja, wanadamu hawa ikumbukwe kwamba hawakupewa sheria yoyote inayohusiana na wanyama wapasao kuliwa na wasiopaswa hawakupewa na hapa tunaelezwa ndio chanzo cha mataifa mbalimbali maana baada ya Mungu kuwachafulia lugha walisambaa kila mmoja mahali pake (Mwanzo 11:1-9}
Sasa swali la kujiuliza je wanadamu hawa waliondoka na ufahamu upi kuhusiana na vyakula, kwamba Nguruwe haramu ama?
Maana ifahamike kuwa kwao walipewa wanyama wote kuwa chakula kwa sababu hawakuwa na sheria inayohusiana na vyakula safi na visivyo safi kwao wanyama wote ni safi tu waliondoka na imani hiyo kama walivyopokea huu ndio ukawa mwanzo wa mpishano wa vyakula baina ya watu walioitwa wa mataifa na wayahudi baada ya wao kupewa sheria iliyohusiana na wanyama walio safi na waschakula.
Wayahudi walipata tabu sana kushiriki katika kalamu za watu ambao kiasili hawakuwa wasomaji wa torati na kuishi katika nchi zao, kwa sababu walipishana katika desturi za vyakula ,wayahudi hata wale ambao walikuja kuwa wafuasi wa Kristo walipata ugumu mno katika eneo ilo,sababu wao wayahudi walipewa sheria kuhusiana na wanyama safi na wasio safi ila mataifa kwao wanyama wote walikuwa safi sasa mtume Paulo hali akiwa na ufunuo wa Kimungu aliwaeleza wale wayahudi waliokuwa wakristo zama zile na walikuwa wakiambatana na mitume katika uinjilisti alisema maneno haya
" Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila ya kuuliza uliza kwa ajiri ya dhamiri ,maana ,dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo, mtu asiyeamini akiwaalika ninyi mnataka kwenda ,kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila ya kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri" {1 Wakorintho 10:25-28}
Kwanini mtume Paulo awaagize wale kila kitu ikiwa wapo wanyama waliozuiliwa je alikuwa anapingana na Mungu? Lah hasha! hakuwa akipingana na Mungu, bali Mtume Paulo alifahamu kesi kuhusiana na vyakula, Yesu aliye kielelezo cha imani yetu aliitatua kupitia Marko 7 :15-19 pale alivyovitakasa vyakula vyote, akamaliza utata huo, hivyo baada ya hapo kila chakula kilikuwa halali kuliwa rejea tena kusoma Mwanzo 9:1-4
" Akawaambia hivi hata ninyi hamna akili ?
Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia mtu unajisi , kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni kisha chatoka kwenda chooni?
Kwa kusema hivi ali itakasa vyakula vyote ,akasema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho mtu unajisi ,kwa maaana ndani ya mioyo watu hutoka mawazo mabaya ,uasherati,wivi uuaji,uzinzi, tamaa mbaya"
Kwa sababu Yesu alivitakasa vyakula vyote ndio maana tunaona agizo lake kwa Wayahudi aliokuwa akiambatana nao kwa ajili ya kueneza ujumbe wa Mungu kuwa wakialikwa katika majumba ya wasio amini na wakawapikia nyama ambazo mmezuiliwa msile na torati kuleni kwa sababu unajisi haupo ndani ya nguruwe wala ngamia ila unajisi upo mioyoni mwa watu
Ndugu pamekuwa na hoja juu ya nguruwe kuwa na madhara jamani kwani ni nguruwe tu ana madhara?
Je Ng'ombe hawa wa leo nyama zao hazina madhara?
Je Kuku wa kizungu na mayai yake hawa madhara kiafya?
Je chumvi za viwandani na mafuta pamoja na mavinywaji havina madhara?
Watu wa Mungu kimsingi kupitia Agano Jipya, Wakristo, hatuna sheria yoyote inayotuagiza kutokula Nguruwe hivyo basi sio dhambi kula Nguruwe ,dhambi katika tasfiri ya Biblia ya Union Version kupitia 1 Yohana 3:4 imetafsiriwa kuwa " dhambi ni uhasi wa sheria" kwaiyo ili dhambi iwepo lazima pawepo na uvunjifu wa sheria je katika agano jipya Wakristo tumepewa sheria inayotutaka kutokula Nguruwe ama ngamia kwa wanaokula?
Kama hakuna basi kula Nguruwe ama Ngamia sio dhambi?
Mungu tangia mwanzo alipotoa agizo la wanadamu kula nyama, alitoa wanyama wote kuwa chakula itakuwaje dhambi kwao?
Maana hakuwapa sheria iliyowabagulia wanyama wa kuliwa na wasio paswa kuliwa kwao wanyama wote walikuwa chakula sawa kama ambavyo Mungu ametoa wanyama wote kuwa chakula kwao, kama kweli alitaka wasiliwe nguruwe angewataza wasiliwe kabla hakuwapa wanadamu wanyama wote
Biblia inasema kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna kiumbe cha kukataliwa ,kama kitapokelewa kwa shukrani ,kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba {1Timotheo 4:4-5}
Kama hakuna kiumbe cha kukataliwa maana viumbe wote ni vizuri sasa ubaya wa Nguruwe ni nini?
Kama hacheuwi hii ndio sababu ndio Mungu ametaka awe hivyo!!!!!!! Ukianzia mistari ya juu utaona anaonya watu ambao wanawazuia wengine na baadhi ya vyakula kwa kisingizio cha wanyama wazuri na wabaya, sasa hawa leo ambao wanawataka watu kujitenga na baadhi ya vyakula tunawaweka kundi gani?
Biblia inasema viumbe vyote ni safi unganisha na Mwanzo 9:1-4 upate maana halisi, hivyo kula nguruwe sio dhambi ni halali kabisa
Sio vyakula ambavyo vinatuudhurisha mbele za Mungu tunakula kwa ajili ya miili yetu sio kwa ajili ya Mungu (Warumi 15:17 na Marko 7:15-19)
Hakuna kosa kula Nguruwe kwa mujibu wa Agano Jipya asanteni mbarikiwe nyote.
Mungu awabariki sana.
By permission: Pastor Samuel J. M, Christ Nations Org, Max Shimba Ministries Org, NKJV, Gideon Bible 1960, Green Island Tabernacle Inc., Rev. Dr. J. E. Grant
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 25, 2016

TRENDING NOW