Sunday, September 10, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TISA)

Image may contain: night and text
Vijana Huuliza . . .
Ninaweza kuepukaje Ponografia?
 Elewa ponografia ni nini? Ni mbinu ya kishetani ya kushushia heshima kitu ambacho Yehova aliumba ili kiheshimike. Kuelewa ponografia kwa njia hiyo kutakusaidia ‘kuchukia yaliyo mabaya.’—Zaburi 97:10.
 Fikiria madhara yake. Ponografia huharibu ndoa. Inawashushia heshima wanawake na wanaume. Inamshushia heshima mtu anayeitazama. Kwa sababu nzuri Biblia inasema: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha.” (Methali 22:3) Andika hapa chini mfano mmoja wa msiba unaoweza kukupata ukiwa na zoea la kutazama ponografia.
“Mvulana mmoja shuleni kwetu alikuwa amebandika picha ya msichana aliye uchi kwenye mlango wa kabati lake. Kabati hilo lilikuwa karibu na langu.”—Robert.*
“Nilikuwa nikifanya utafiti kwenye Intaneti kwa ajili ya ripoti ya shule nilipopata kituo cha ponografia.”—Annette.
WAZAZI wako walipokuwa na umri kama wako, mtu aliyetaka kutazama ponografia alihitaji kuitafuta sana. Siku hizi ni kana kwamba ponografia inakutafuta. Kama vile Robert, aliyenukuliwa hapo juu, huenda umejikuta ukitazama ponografia ya mwanafunzi mwenzako. Au kama Annette, huenda ukaipata bila kukusudia kwenye Intaneti. Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 anasema, “Nyakati nyingine ninapitia-pitia Intaneti tu au kununua vitu kwenye Intaneti au hata kuchunguza tu habari za akaunti yangu ya benki kisha ghafula ponografia inajitokeza!”*
Hilo si jambo la kushangaza. Katika uchunguzi mmoja, asilimia 90 ya vijana walio kati ya umri wa miaka 8 na 16 walisema kwamba walipata ponografia kwenye Intaneti bila kukusudia, mara nyingi walipokuwa wakifanya kazi za shuleni! Ukweli ni kwamba, kukiwa na mamilioni ya vituo vya Intaneti vilivyo na mamia ya mamilioni ya sehemu zenye habari za wazi kuhusu ngono, ponografia inapatikana kwa urahisi sana. Inaweza pia kupatikana kupitia simu ya mkononi. Denise mwenye umri wa miaka 16 anasema, “Shuleni kwetu ni jambo la kujisifu. Jumatatu mazungumzo huwa kuhusu, ‘Una picha gani kwenye simu yako ulizotoa kwenye Intaneti mwishoni mwa juma?’”
Kwa kuwa unajua watu wengi sana wanatazama ponografia, huenda ukajiuliza, ‘Je, ponografia ina madhara?’ Sababu kadhaa zinaonyesha kwamba jibu ni ndiyo. Fikiria sababu tatu tu:
 Ponografia huwashushia heshima wale wanaoitayarisha na wale wanaoitazama.—1 Wathesalonike 4:3-5.
 Kupendezwa na ponografia ni kama kuiga mapendezi ya ngono yasiyo ya asili ambayo roho waovu wa siku za Noa walikuwa nayo.—Mwanzo 6:2; Yuda 6, 7.
 Mara nyingi kutazama ponografia huwa hatua ya kwanza inayomwongoza mtu kufanya dhambi zinazohusu ngono.—Yakobo 1:14, 15.
Ponografia huwaathiri vibaya wale wanaonaswa nayo. Fikiria mifano miwili tu:
“Niliona ponografia kwa mara ya kwanza nilipokuwa mdogo, na imekuwa vigumu sana kuachana nayo. Miaka mingi sana imepita, lakini picha hizo zimebaki katika kumbukumbu langu. Ni kana kwamba mawazo hayo huwa tu katika akili, na hakuna wakati dhamiri inakuwa safi. Ponografia inakufanya usijiheshimu na inaweza kukufanya ujihisi mchafu na mtu asiyefaa. Nyakati zote unakuwa na mzigo wa siri ambao lazima ubebe.”—Erica.
“Nilikuwa mraibu wa ponografia kwa miaka 10, na sasa miaka 14 imepita tangu nilipoacha kuitazama. Lakini hata sasa, lazima nipambane kila siku. Ingawa tamaa imepungua sana, bado ipo. Udadisi bado upo. Picha bado zimo akilini. Ninajuta kwa nini nilianza kufanya jambo hilo. Mwanzoni ilionekana kama haina madhara. Lakini sasa ninaelewa ukweli wa mambo. Ponografia inadhuru, ni potovu, na inawashushia heshima watu wote wanaohusika. Hata wale wanaoitetea waseme nini, hakuna kitu chochote kizuri kuhusu ponografia.”—Jeff.
INAWEZEKANA NA MWAMBIE TATIZO LAKO YESU NA ATAKUKOMBOA.
BARIKIWA SANA NA TUENDELEE KUMTUMIKIA YESU MUNGU MKUU.
Tumefikia tamati ya somo letu, lakini endelea mwenyewe kumtafuta Yesu na atakufunulia mengi.
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW