Thursday, June 18, 2015

KUMBE QURAN IMEJAA SHAKA NA HAIPO WAZIWAZI

  1. Je, madai ya kuwa Quran imekalika na ipo waziwazi ni ya kweli?
  2. Allah ateremsha aya na kudai kuwa, Quran haijakamilika na haipo waziwazi.
  3. Allah asema kuwa aya zingine ndani ya Quran hakuna ajua maana yake isipokuwa Allah.

Ndugu wasomaji;

Leo tutaangalia utata ulio jaa ndani ya Quran ambayo wanadhuoni wengi hudai kuwa imenyooka, huku Allah akiwapinga na kuteremsha aya ambayo inasema kuwa Quran haijanyooka na haipo waziwazi.

Kwanza tuanze kwa kuangalia aya ambayo inasema kuwa Quran ipo wazi na aya zake zimepambanuliwa ni uongofu kwa walio ongoka.

Surat HUD (11:1). Alif Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha zikapambanuliwa, kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari

Surat Al Anaam (6:114). Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka.
Surat An nah’k (16:89). Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu
Surah tulizo ziweka hapo juu, zinasema na kudai kuwa Quran  imepambanuliwa na ni kitabu kilizo elezwa waziwazi. Ikimaanisha kuwa, unapoisoma Quran, hautapata maswali au kusoma utata katika aya zilizo teremshwa na Allah.

SAA YA WOKOVU NI SASA!

NINI MAANA YA KUOKOKA?

KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani.Ambavyo jamii yetu maneno haya tunayatumia sana,

NINI MAANA YA WOKOVU?  

Watu wengi neno hili wamelitafsiri vile wa pendavyo au waonavyo  sasa Swali hili acha lijibiwe na maandiko matakatifu, na maneno haya yasibadilishwe kwamba ni wakati gani wa kuokoka kitendo kikishamalizika cha kukiri kifuatacho ni uwokovu kwa mjibu wa neno, fuatilia hapa chini,
Kwasababu ukimkiri Yesu  Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)

Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)

 

Lini unatakiwa ufanye uamuzi huu muhimu?

Hebu MUNGU na aseme nawe kupitia maneno yake ambayo ni amina na kweli anasema:
Warumi 13:11 
Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini

2Wakorintho 6:2 
"Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa"

Biblia inaonya kuwa "tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa" yaani wakati huu unaposoma hapa ndio wakati wako wa kutubu na kumgeukia Mungu kwa njia ya kristo kama bado haujafanya hivyo kwani huu ni uamuzi ambao kila mwanadamu lazima aufanye.Mungu ana kalenda yenye miaka mingi lakini kwenye swala la kuukiri wokovu wa kristo wakati ni sasa..Ninakuomba umpe kristo maisha yako,ili hata kama ukifa muda wowote akupokee na uishi naye milele.

WOKOVU SIO DINI

MAANA HALISI YA WOKOVU
Wokovu ni mpango wa Mungu mwenyewe wakumtafuta na kumkomboa Mwanadamu.

Baada ya Adam na Hawa wanadamu wa kwanza kutenda dhambi na kuvunja uhusiano wa Mungu na Mwanadamu , bado Mungu aliendelea kumpenda mwanadamu na kutafuta ni kwa namna gani na kwa njia ipi ya kurudisha uhusiano wake na mwanadamu aliyemuumba.

“kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele, Yohana 3:16”

Wednesday, June 17, 2015

WAISLAM WAMELAZIMISHWA KUFUNGA SWAUMU

Quran 2:183 Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga saumu kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu.

Aya hapo juu inatuambia kuwa, kumbe kufunga kwa ndugu zetu hawa ni kwa kulazimishwa na sio hiyari yao.

1. Wapi tunasoma katika Taurat kuwa Adam alifunga Ramadhani?
2. Wapi tunasoma katika Taurat kuwa Musa alifunga Ramadani?
3. Wapi tunasoma katika Taurat kuwa Ibrahim alifunga Ramadhani?

Ndugu zanguni, hii dini ni ya kujitungia na si kama wanavyo dai kuwa eti iliteremshwa na Allah. Kama kweli Allah ndie aliye iteremsha hii dini kwa Adam, sasa kwanini Adam hakufunga Ramadhani/Swaumu?

Zaidi ya hapo, kwanini katika mfungo hawa ndugu zetu wanakula Usiku kucha/daku? Wapi katika Taurat panasema kuwa watu wale Daku?

Waislam huwa wanatumia aya ambayo inasema kuwa Yesu alifunga, lakini hawasemi kuwa Yesu alifunga kwa siku ngapi na wala hakuna aya ambazo zinasema kuwa Yesu alikula Daku saa nane/kumi za usiku.

Zaidi ya hapo, hatusomi kuwa Yesu alianza kufunga pale alipo uona Mwezi umeandama, la hasha. Wala hatusomi kuwa Yesu alifungulia/maliza kufunga pale Mwezi ulipo andama, la hasha.

Hii tabia ya kuabudu Mwezi ipo kwenye Uislam peke yake.
Maswali kuhusu Mwezi:
1. Hivi kati ya Allah na Mwezi ni nani mwenye Mamlaka ya kuongoza Waislamu?
2. Hivi kwanini Waislam wafuate maamrisho ya Mwezi?

KUMBE MWEZI NDIYE MOLA MLEZI ANAYEABUDIWA NA WAISLAMU!
Q6:77 SURAT AL - AN-A'AM
Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua asema:Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea.
HII NDIYO SIRI YA ILE NYOTA NA MWEZI ILIYO JUU YA KILA MSIKITI!

KULA DAKU ASUBUHI:
Kula Daku saa alfajiri ni jibu tosha kuwa, Waislam wamebalisha masaa ya kula na kuamua kula usiku kucha na kukaa na njaa mchana kutwa.
Kumbe basi, hata Wakristo wanao lala usiku na kula asubuhi wao vile vile wanafuga.

Kumbe basi, ndio maana Wazungu wanaita chakula cha asubuhi "BREAKFAST"
Waislam kwanini kula usiku mnaita kufunga?

Wapi Yesu kasema kwenye Injir kuwa watu wafunge Ramadani?

Hakika Ukristo ndio Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni.

Max Shimba

Max Shimba Ministries Org @2015.

JE, IBADA ZA WAFU NI ZA KIBIBLIA?


Ukweli hakuna Andiko lolote lenye pumzi ya Mungu mahali popote linasomeka kuwakumbuka marehemu, iwe kwa dakika moja au kwa dakika mbili. Lakini lipo Andiko linasomeka, "wafu hawana Ijara tena katika nchi ya walio hai". Kwa hiyo kwa mujibu wa andiko hilo, hata misa za wafu HAZIRUHUSIWI, ikimaanisha arobaini za marehemu wote hazina nafasi ndani ya Neno la Mungu.

WAFU/MFU NI NANI?
Utangulizi:-Neno wafu ndani ya Biblia limetumika likiwa na Maana zaidi ya moja, Linaweza kutumika kama

i.                   Ni hali ya Roho kutengana na mwili yaani Kifo cha mwili.(Luka 8:55, Muhubiri 9:5)

ii.                 Ni hali ya Mtu kutengana na Mungu au kuvunja uhusiano mwema na Mungu (Kutenda dhambi) yaani Kifo cha Kiroho (Ayubu 21:25)

Kifo cha kiroho. Kuna aina tatu ya wafu katika eneo hili ambayo mtu anaweza kufa kiroho lakini bado anaendelea kuwa hai kimwili. Huyu anaweza akatubu na kufufuka katika wafu akawa hai tena .Pia mtu anaweza kufa kiroho na kimwili maana yake Roho imekufa na mwili umekufa hana nafasi ya kutubu tena. (Ufunuo 20:5). Kifo hiki ni kibaya zaidi na kinatisha. Ambacho Bwana Yesu alisema msiwaogope wawezao kuuwa mwili bali Mungu mwenye uwezo wa kuuwa mwili na Roho, (Soma Matayo 10:28). Kifo cha tatu ni Mtu kufa kimwili lakini bado anaendelea kuishi Kiroho. Hapa Yesu alisema mtu akiniamini mimi na kutimiza neno langu ataishi hata kama akifa.


MAOMBI KWA AJILI YA WAFU 

Viongozi wengi hufundisha kwamba hakuna kuokoka duniani na hao hao mtu akifa wanamwombea kwamba alazwe pema peponi kana kwamba kuna wokovu baada ya kufa. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu.(Waebrania 9:27).

Kanisa au Mchungaji au Padri, au Mtume haliwezi kuomba mfu kupumzika kwa amani pema peponi, Ndugu zangu wakati wa wokovu ni sasa hivyo baada ya kufa ni hukumu (Waebrania 9:27). Watakie kupumzika kwa amani wafu ila tambua kwamba huwezi kuwabadilishia makao yao ya milele, kama ni mbinguni ni mbinguni tu na kama ni motoni ni motoni tu.

Kuombea wafu huwafanya wenye dhambi kuendelea kutenda dhambi wakiamini kwamba baada ya kufa kanisa litaomba ili wao waingie mbinguni. Ndugu nakuambia tena WOKOVU NI SASA. Katika Luka 16:26…Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'' Biblia inatuonyesha watu waliokufa  wengine wako pema peponi na wengine wako kuzimu,’’  ’’ MUNGU humpokea mwenye dhambi ambaye hutubu kwa woyo na kujitakasa kwa msingi wa imani peke yake katika damu ya YESU KRISTO. Hivyo humpa uzima wa milele. 2 WaKorintho 6:2’’(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa)‘’ Wakati wa wokovu ni sasa Wakati wa kuokolewa/kuokoka ni sasa Wakati huu ndio unatakiwa kuokolewa sio baada ya kufa.

Ndugu zanguni, ningependa kuwakumbusha kuwa, wakati wa Wokovu ni sasa na sio utakapo kufa. Mafundisho ya kuombea wafu hayapo kwenye Biblia na hatuoni Yesu akiombea wafu bali akifufua wafu. (Yohana 11:43-44; Luka 7:11 -15; Marko 5:35).

Mungu awabariki sana


Max Shimba Ministries Org.

Friday, June 12, 2015

WAKRISTO JIEPUSHENI NA SALAAM MNAYOSALIMIWA NA WAISLAMU

Imekuwa ni desturi kuwasikia, au kumsikia Muislamu, akimsalimia Mkristo, Sam aleykum (سم عليكم) Kwa Mkristo ambae hajui kitu, huitikia kwa haraka, Wa'alaykum Ssalaam, matumaini yake yote ni kuwa, amepewa salamu, ambayo waislamu wote husalimiana,

Yaani السلام عليكم (ASsalaam aleykum) Wakimaanisha, Amani ya Allah iwe juu yenu...
Mkristo mwenzangu, tambua kuwa, Muislamu abadani akijua wewe ni Mkristo, hawezi kukusalimia السلام عليكم (ASsalaam Aleykum) yaani kukutakia amani ya mungu, muabudiwa na waislamu, bali yeye muislamu humsalimia Mkristo kwa kusema:-

Sam Aleykum (سم عليكم) yaani akiwa na maana kwa kiswahili, "Mauti iwe juu yenu" hiyo ni kwa wengi, kama ni Mkristo mmoja basi husalimiwa kwa kuambiwa:-

Sam Alaika (سم عليك) Maana yake, "Umauti uwe juu yako" Sasa hapo Mkristo pasina kujua anaitikia kwa uchangamfu, akidhani anapewa Salaa nzuri, kumbe anatakiwa mauti
(Hastahili kuishi)...

Kwa hivyo kuanzia Leo, unaposalimiwa na muislamu, Sam aleykum, basi mjibu tu kwa kumwambia:-
Wa alyekum Faqatu (عليكم فقة) Umauti huo umrudie yeye mwenyewe, na hata kama atakutakia Amani halisi ambayo wao hutakiana السلام عليكم Yaani amani ya Allah iwe juu yenu/yako, usimrudishie, maana amani watoayo waislamu (Ulimwengu) ni tofauti na Amani aliyoitoa Yesu kwa wanafunzi wake aliposema.
سلام لكم (Salaamu'n Lakum) Maana yake Amani iwe kwenu

Hapo kuna utofauti wa amani (سلام) hiyo ya Yesu na hiyo (سلام) amani waitoayo Waislamu... maana Yesu amesema.

"Amani yangu nawapeni, amani yangu nawaacheni, niwapavyo mimi, sivyo kama Ulimwengu utoavyo" (Yohana 14:27)

Kwa hivyo JIHADHARI sana na salaam zao.

MUHAMMAD NI NABII NA MTUME PEKEE ALIYE PATA UTUME KWA KUUGUA HOMA, NA ALIYEKUFA KWA KUUGUA HOMA


Abel Suleiman Shiriwa
Sijambo la kustaajabis kuwasikia Waislamu
waKIMNADI Muhammad kuwa ni mtume wa Mwenyezi Mungu, na tena mbaya zaidi
husema kuwa yeye ndiye kiongozi wa mitume na mwisho wa Manabii, NA MBORA WAO.
yaani wakiwa na maana kuwa,
Ibrahimu
Isaka
Musa
Yusufu
Yona
Haruni
Eliya
Daudi
Yohana
Yesu
Wapo chini ki ubora dhidi ya Muhammad, kwa hivyo Marehemu Muhammad, yeye ni mbora wao,
maana yeye ni kipenzi cha Mwenyezi Mungu, jambo hili kwa mtu mwenye akili timamu, haliwezi kumuingia kabisa, kwani Muhammad thamani yake inazidiwa na hata Yuda Isakariote (Aliyemsaliti YESU) seuze Manabii hao? Ukimzungumza Eliya tu pekee ambaye yeye kwa Yesu hafiki hata robo, bado Eliya yupo juu mara 100,0000. dhidi ya marehemu Muhammad, na pia ni Makosa makubwa sana kwa Mkristo kusema eti Muhammad siyo nabii wala siyo mtume, ukimkuta Mkristo anakataa utume wa Muhammad, basi tambua kuwa huyo Mkristo hasomi kabisa habari za Yesu Kristo, kwani kila Mkristo ni lazima atambue kuwan Muhammad ni Mtume na NABII, swali la msingi sasa ni hili

JE! NI MTUME NA NABII WA UKWELI?

QURAN YAMKIRI YESU KUWA NI MUNGU WA KWELI

Mwandishi Abel Suleiman Shiriwa

Katika vitu ambavyo waislamu huwasumbua vichwa na akili zao, ni kuhusu Uungu wa Yesu, sema vitu vyote lakini ukifika hapo kwenye Uungu wa Bwana Yesu basi mnapotezana, na kitu ambacho kinawafanya waislamu washindwe kukubali kuwa yeye ni Mungu, ni ukosefu wao wa ROHO MTAKATIFU, maana mtu hawezi kukiri kuwa Yesu ni Bwana (Mungu) kama hana ROHO MTAKATIFU, kama yasemavyo maandiko.
2 Korintho 12: 3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
Kwa hivyo Ndugu yangu Mkristo unapojadiliana na Muislamu kuhusu Habari za Uungu wa Yesu, kamwe hawezi kukubali mpaka ROHO MTAKATIFU auhusike, kinyume na hapao itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi Gitaa, kwa hivyo hoja zake zote zitaegemea katika hali ya Kuutazama mwili kama ambavyo Elisabeti, alimtazama Yesu kama mtu wa kawaida sana ambaye atazaliwa na Mariam, lakini mara baada ya kujazwa na Roho Matakatifu, ndipo alipokiri kuwa Yesu ni Bwana yaani Mungu wake.
Luka 1: 39 Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,
40 akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti.
41 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
43 Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
Hapo tumeona ni namna gani Umuhimu wa ROHO MATAKATIFU, katika kumjua Yesu kuwa ni Mungu, kwa kuwa Waislamu hawana Roho Mtakatifu, kazi yao hasa ni kumtaza Yesu alipoutwaa Mwili wa Kibinadamu, na kuwa na asili ya mtu, na kuuficha Uungu wake katika mwili, ndo maana akawa akiijita Mtume, Mwana, Kuhani, na hata Nabii, sasa leo sina lengo hasa la kuueleza Uungu hasa wa Yesu, kiundani kwa Biblia, bali nataka niitazame Quran namna ambavyo imemkiri Yesu kuwa ni Mungu, kwa kueleza Sifa za Mungu, ambazo Yesu anazo, kwa hivyo nitaeleza SIFA 5 NDANI YA QURAN ambazo zinakiri UUngu wa Yesu.
(1) Mungu ni mwenye kujua yaliyomo katika nyoyo za watu.
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ إِن تَكُونُواْ صَالِحِينَ فَإِنَّهُ كَانَ لِلأَوَّابِينَ غَفُورًا
Quran 17:25. Mola wenu anajua sana yaliyomo nyoyoni mwenu, kama mkiwa wema, basi hakika yeye ndiye Mwenye kusamehe wenye kurejea.

IBADA YA VIATU NA SHUTUMA ZA WAISLAMU KWA WAKRISTO

SOMO LA LEO:
“IBADA YA VIATU NA SHUTUMA ZA WAISLAMU KWA WAKRISTO”
Kumekuwepo na shutuma nyingi sana kutoka kwa jirani zenu walio kushoto (Waislamu) wakitushutumu sisi Wakristo kwa kuingia kwetu Ibadani hali ya kuwa tumevaa Viatu, wakati wao wanapoenda kuswali msikitini, huingia bila viatu, kuonesha kwamba wao ndiyo wenye kufanya Ibada sahihi kuliko watu wa imani zingine zote Ulimwenguni, shutuma hizo huambatanishwa na baadhi ya maandiko ndani ya Biblia, ambayo kwa sehemu kubwa sana yametumika kuwasilimisha Wakristo (Kuwaingiza kwenye uislamu) wakidhani kwamba, kuingia kwao huko wataenda kufanya Ibada sahihi inayodhaniwa na jamaa zetu waislamu, ibada ya kuvua Viatu, maandiko ambayo huyatumia ni haya:
Kutoka 3:4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Yoshua 5:15 Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.
Mandiko haya ndiyo ambayo huwafanya waislamu wavue viatu vyao msikitini, hata wengine kuzifunga YEBO YEBO, au Kandambili zao kwa kutumia kamba, au Kufuri, ili tu kuzuia wezi wasiwezi kuiba yebo yebo zao, hata kama zimetoboka, na maandiko hayo pia yametumika kuwasilimisha Wakristo wengi bila wao kujua kuwa walipotoshwa, sasa fuatana nami katika somo hili ili uweze kujifunza juu ya Ibada hii ya kusali na Viatu, au kusali bila viatu:
1. MUSA NA KUVUA VIATU KATIKA NCHI TAKATIFU

ATHARI YA MKRISTO KUOANA NA MUISLAMU

Abel Suleiman Shiriwa's photo.
Imeletwa kwenu na Abel Suleim Shiriwa
Imekuwa ni jambo la kawaida kushuhudia Wakristo na waislamu wakiishi pamoja kama mke na mume, na wengi wao huona ni jambo sahihi, kwa sababu Mungu wetu ni mmoja, kwa hivyo hata kama ataolewa na muislamu, hakuna tatizo kwake, tena kama ataoneshwa mapenzi ya dhati kwa kipindi fulani, basi hapo atajiona kuwa amefika sehemu salama, na wengine hujitetea kupitia andiko ambalo Paulo alitoa ushahuri kuhusiana na mtu aaminie kuishi na mtu ambae hana imani kama yake:
1 Korintho 7:12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika
Andiko hili Watu wengi hulitumia vibaya, wakidhani kwamba, limewapa ruhusa ya Mkristo kuolewa na mtu ambae si Mkristo, Kwanza hapo naomba ifahamke kwamba, katika maelezo hayo ya PAULO, hakuna ndoa baina ya mtu asie amini (Asiye Mkristo) na Mkristo ambae ameamini, ndiyo maana Paulo akasema:
1 Korintho 7:15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
Amesema huyo asie amini kama ataamua kundoka, basi ni ruksa kwake kuondoka, na hapo hapatakuwa na kizuizi cha Mkristo kuoa au kuolewa, ushauri huo hakumlenga Mkristo na Muislamu, bali ulilenga juu wa watu ambao Walipelekewa Injili huko Korintho, kuna baadhi ya watu ambao walilipokea neno, wakaamini, lakini wengine hawakukubali, na miongoni mwa wale ambao hawakukubali, walikuwa tayari wanaishi na kama mume na mke na wale ambao wamekwisha kuamini, kwa hivyo Paulo hakutaka kuwatenganisha, akawataka wale walioamini waendelee kuishi nao, kwa ushauri wake Paulo, na si agizo la Yesu, maana aliamini kwamba kupitia jambo hilo, huyo asie amini anaweza kuongoka kupitia mume au mke alie ongoka, ila kwa wale ambao walioana katika ndoa inayokubalika kwa Mungu, aliweka msimamo wa Yesu mwenyewe akasema:
1 Korintho 7:10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
Hapo aliposema kuwa waliokwisha kuoana, maana yake wale ambao ndoa zao zinatambulikana na Mungu, (Hawakuchukuana tu na kuanza kuishi pamoja) bali hao ni wale ambao tayari wameshaunganishwa na Mungu, kwa kufuata taratibu zote, akasema hakuna ruhusa ya kuachana, kama ilivyo kwa mtu asie amini na aaminie, hata kama mmefunga ndoa, ikatokea mmoja akakengeuka, hakuna ruhusa hiyo ya kuachana, mke akae bila kuolewa, na mume nae pia akae bila kuoa.
Mathayo 19:5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

ABEL SULEIMAN:KWA NINI NILIAMUA KUACHANA NA UISLAMU NA KUWA MKRISTO?

SEHEMU YA 1
UTANGULIZI:
Hii ni sehemu ya ushuhuda wangu, ambao nitaeleza ni sababu gani ambayo ilipelekea niachane na uislamu, na hatimae kuwa Mkristo, Katika DVD ya ushuhuda wangu, nilieleza kwa kifupi, na mengi sikuyasema, nilieze hasa harakati zangu katiks mihadhara, ila hapa nitachumbua mengi zaidi.
Nimezaliwa miaka 27 Iliyopita, katika JIJI LA MWANZA (Rock city) Jina langu ambalo nilikuwa nalitumia katika uislamu, ni Aboubakar, nimesoma Madrasa Pale THAQAAFATUL ISLAMIYA, Mwanza, karibu na Shule ya msingi Mirongo, shule hiyo imepakana na Lake Secondary School, pia na Ipo karibu na hospitali ya Seketule.
Miongoni mwa walimu wangu wa madrasa, ni:
Ramadhani Maganga
Ustadh Kikatani
Ustadh Hassan Lolo.
Ustadh Kaisy
Ustadh Shekue.
Pia nilisoma Madrasa iliyopo TAQWA, maeneo ya Ghana, chini ya Sheikh Abdallah Panya, pia Ghana mtaa wa kifua Wazi, kwa Ustadh, Thuqmal bin Hussein (Huyu ni ustadh aliyekuwa ana diri na Elimu za dua za kafara, kuchinja mbuzi, kuku na kisha kutuchukya kwenda kufanya zindiko ndani ya nyumba, kwa kutumia vitabu mbali mbali vya kiislamu) Nitaeleza habari zake katika mwendelezo wa ushuhuda wangu....

TRENDING NOW