Saturday, July 2, 2016

JE, YESU ALITUMWA KWA ISRAEL PEKE YAKE?


Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi), ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.
Imeandikwa:
Akajibu akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).
Mungu ni Mungu wa utaratibu na ratiba kamili. Ndiyo maana hakuumba kila mtu kwa mara moja. Alianza na mtu mmoja tu, kisha wengine wote tukatokea kwa huyo mtu. Vivyo hivyo, alianza kwa kujifunua kwa taifamoja tu duniani kote. Kisha kutokea hapo ndipo wokovu unasambaa kwenye mataifa yote. Ni ukweli ulio wazi kwamba, ukiacha Israeli, jamii zote zilizobakia duniani, kwa asili zilikuwa zikiabudu miungu (yaani mashetani). Ni Israeli peke yao ndio ambao kwa asili walianza na Mungu wa kweli.
Ndiyo maana Bwana Yesu alipoongea na mwanamke Msamaria pale kisimani alimwambia hivi:
Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. (Yohana 2:22).
Wokovu unatoka kwa Wayahudi kwa sababu hakuna taifa jingine lolote duniani ambalo lilimjua Mungu wa kweli – yote yalikuwa na dini za kipagani – iwe ni wazungu, Waafrika, Wahindi, Waarabu, n.k. Huo ndio ukweli.
Kusema kwamba Yesu hakuja kwa ajili ya mataifa yote hakuna tofauti na kusema kuwa, kwa vile Mungu alimuumba Adamu na Hawa peke yake, basi Yeye si wa familia yangu maana hakuniumba na mimi kama alivyomuumba Adamu.
Yesu aliongea na wanafunzi wake siku moja na akawaambia kuwa:
Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanzia tangu Yerusalemu. (Luka 24:46-47).
Je, unaona kwamba Injili inatakiwa kuanzia Yerusalemu? Na je, unaona pia kwamba anasema kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake? Je, mataifa yote ni Israeli peke yake?
Mwanamke Mkananayo alikuja wakati usio wake. Huo ulikuwa ni wakati wa kuhubiri Injili kwa Israeli kwanza ndipo iende ulimwenguni kote.
Ufuatao ni ushahidi zaidi wa maneno ya Bwana Yesu mwenyewe kuthibitisha kwamba alitumwa kwa mataifa yote ulimwenguni na kwamba Yeye ndiye Masihi wa Mungu, yaani aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu wote.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katikaYerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. (Matendo 1:8).
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19).
Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. (Yohana 3:17).
Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. (Yohana 12:47).
Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. (Yohana 10:15-16).
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. (Mat 24:14).
Nihitimishe kwa kurejea tena mambo machache niliyoyasema. Mungu amekuwa na kawaida ya kuanza jambo na mtu mmoja.
Aliumba mwanadamu mmoja, kisha tukatokea humo wote.
Alijifunua kwa taifa moja, kisha tukamjua wote.
Alianza na Mwana mmoja (Yesu), kisha tunazaliwa wote kwa imani katika huyo.
Vivyo hivyo, alileta wokovu kwa taifa moja la Israeli, kisha unasambaa kote – ndiyo maana anasema na mwanamke Msamaria pale kisimani – “Wokovu watoka kwa Wayahudi.” (Yohana 4:22).
Hali hii ya kuanza na mtu au sehemu moja, ni ushahidi kuwa wale wote wanaojifariji kwa maneno eti “dini mbalimbali ni njia tofauti ambazo zote zinaishia kwa Mungu”, wanajidanganya na kupoteza muda wao na uzima wao wa milele! “Wokovu watoka kwa Wayahudi” – yaani KWA YESU PEKEE!
Sasa, kwa kuwa muda wa kusambaa kwa wokovu huo ulikuwa haujatimia (maana Mungu anakwenda kwa ratiba ya majira na nyakati), ndiyo maana akamwambia yule mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi) kuwa hakutumwa ila kwa Israeli.
Lakini utimilifu wa majira ulipofika, yaani alipokufa na kufufuka, tunaona akiwaagiza sasa mitume wake waende ulimwenguni kote.
Na Biblia inasema wazi: Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwambazamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. (Waefeso 2:11-16).
Tafakari
Hoji mambo
Jiulize
Chukua hatua

YESU NI MWANA WA MUNGU MAANA YAKE NINI?



Wanadhuoni wa Kiislam pamoja na waumini wa dini ya Kiislam huwa wanauliza na kusema kwa Wakristo yafuatayo:
1. Kivipi Yesu ni Mwana wa Mungu?
2. Mungu atakuwaje na Mwana bila ya Mke?
KIVIPI YESU NI MWANA WA MUNGU?
Yesu Kristo si Mwana wa Mungu kulingana na ubaba wa kawaida wa binadamu, nikimaanisha kuwa Mungu hakuoa na kupata mwana wa kiume. Nikiwa na maanisha kuwa, Mungu hakufanya tendo la ndoa na Mariamu, na pamoja naye kuzaa mtoto wa kiume ambaye anaitwa Yesu, la hasha.
1 YOHANA MLANGO 5 aya 1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
MUNGU ATAKUWAJE NA MWANA BILA YA MKE?
Yesu ni Mungu katika hali kwamba ni Mungu anajithirihisha kama mwili. (Yohana 1:1, 14) Yesu ni mwana wa Mungu kwa dhana kwamba Mariamu alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu. Luka 1:35 yasema, “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, MWANA WA MUNGU.”
Mariamu aliambiwa na Malaika kuwa, Mtoto atakaye zaliwa atakuwa Matakatifu na ataitwa MWANA WA MUNGU. Huu ushahidi upo kwenye Luka 1:35.
YESU AKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU MBELE YA KUHANI MKUU
Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, MWANA WA MUNGU” (Mathayo 26:63). [NOTE: YESU HAKUKATAA ALIPO ITWA MWANA WA MUNGU NA KUHANI MKUU, SOMA JIBU LAKE] “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia, wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64) viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66).
WAYAHUDI WANAKIRI KUWA YESU AMEKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU
Baadaye mbele ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) [KWENYE HIYO AYA YA YOHANA 19:7, WAYAHUDI WANAKIRI KUWA YESU AMEKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU] ni kwa nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili hukumu ya kifo?
Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu. Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”
Mfano mwingine unaweza patikana katika Yohana 17:12 mahali Yuda anaelezwa kama mwana wa “upotevu”? jina upotevu lamaanisha “uharibivu” Yuda hakuwa mwana wa uharibivu, lakini mambo hayo ndio ya kutambulisha maisha ya Yuda. Yuda anadhihirisha upotevu. Vile vile Yesu mwana wa Mungu. Ni Mungu anajidhihirisha (Yohana 1:1,14).
Hii mada iatufundisha maana ya Yesu ni Mwana wa Mungu, SWALI ambalo limekuwa likiulizwa na Waislam kila siku. Leo wamesha pata jibu thabiti tena lenye ushahidi wa aya za Biblia.
Hakika Yesu ni Mwana wa Mungu
Max Shimba Ministries

SHETANI ATEREMSHA AYA ZAKE KWENYE QURAN NA KUKIRI KUWA ALLAH NDIE MOLA WAKE MLEZI


1. Shetani akiri kuwa Allah ni Mola wake Mlezi.
2. Asema Allah ndie aliye mfundisha kutenda dhambi.
3. Asema na yeye atafanya maovu aliyofundishwa na Allah kwa Binadamu
4. Tabia za Shetani na Allah zafanana
SOMA:
Surah Al Hijr 39. Shetani akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
[Sûrah al-A`râf: 16-17], [Sûrah al-Isrâ’: 62] ,
Ndugu zanguni, huu ni MSIBA mwingine Mkubwa sana kwa Dini ya Jibril. Leo tunajifunza kutoka aya ambayo Jibril aliiteremsha kwa Muhammad. Aya hii katika Surat Al Hijir inakiri kuwa ALLAH NI MOLA MLEZI WA SHETANI.
Sasa Kama Allah ndie Mlezi wa Shetani, na sie wote tunafahamu kuwa Shetani kazi yake ni kufanya Maovu, Kuua watu, na kuendeleza ubaya hapa dunia, JE, inamaanisha hayo yote Shetani kajifunza kwa Allah?
Shetani anaendelea kusema kuwa, NI ALLAH ndie aliye mtia makosani, Je, inamaana kuwa MALEZI ya Allah ndio yaliyo mfunza ubaya na dhambi Shetani?
Shetani anaendelea kusema na kukiri kwa Allah kuwa, NUKUU "basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote" ATAWAPOTEZA WATU WOTE, Swali: Kwanini Allah alikaa kimya wakati Shetani anajitamba kufanya mabaya kwa viumbe visivyo na hatia? Au ni kwasababu yeye Allah ndie aliye mfuza ubaya Shetani, ndio maana alishindwa kumkanya au mwonya Shetani?
Ndugu zanguni, sidhani kuna Muislam atakaye weza bisha na au ipinga hii aya amabayo ipo wazi kabisa kuwa, ALLAH NI MOLA MLEZI WA SHETANI na ALLAH NDIE ALIYE MFUZA UBAYA SHETANI. Huu ni MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAM.
Waislam, ningependa mtujibu sio kwa jazba bali kwa aya, KWANINI ALLAH HAKUKATAA KUITWA MOLA MLEZI WA SHETANI?
Max Shimba Ministries Org

MUHAMMAD ALIKUWA ANAVAA VIATU MSIKITINI



Ndugu msomaji,
Leo ningependa tujikumbushe na kujifunza kuhusu kusali na viatu katika nyumba za ibada. Hususan Msikitini.
Waislam mara nyingi wamekuwa wakiwashutumu Wakristo na kuwakejeli kuwa, eti wanasali na viatu Kanisani.
Je, Mtume wa Allah aitwaye Muhammad alivaa viatu alipo kuwa anaswali Msikitini?
Hebu tuangalie ushahidi huu hapa:
Ukisoma kitabu cha Al-u-lu wal-marjan Uk. 179
14. Mlango:
Ruhusa ya kusali na Viatu.
325. Hadithi ya Anas Bin Malik (R.a) kutoka kwa Said Bin Yazid Al-Azid (r.a) amesema, Nilimuuliza Anas Bin Malik (r.a) “Hivi Mtume (s.a.w) alisali huku amevaa viatu vyake?” Akanijibu, “Ndiyo” (Bukhari, Hadithi N. 383, Juzuu ya 1)
Hapo tunamuona Muhammad akisali na Viatu, na mlango hapo umesema, Ruhusa ya kusali na Viatu, maana yake waislamu hapo wameruhusiwa kusali na Viatu, pia haikuishia hapo, Muhammad akasema tena kuwaambia Waislamu.
Ukisoma kitabu kinachoitwa “TAFSIRI YA BULUGH AL-MARAM MIN JAM’I ADILLATIL AHKAM
Ukurasa wa 101 Hadithi Na. 171
Abu Said (r.a) amesimulia: Mtume (S.a.w) amesema: “Ye yote miongoni mwenu atakapoenda msikitini kusali, basi atizame, akiona uchafu au najisi katika viatu vyake aondoe kisha aswali navyo”. Abu Dawud Ibnu Khuzaimah ameipa daraja ya Sahih.
*Murad wa kutwaharisha viatu:
Iwapo mtu amekanyaga najisi kwa kiatu, atakitwaharisha kwa kusugua chini mchangani*
Hapo kwa mtu mwenye akili zake timilifu, hawezi kukomaa na kuanza kuwalaumu Wakristo, eti kwa nini wana Sali na viatu? Wakati Muhammad mwenyewe, alisali huku amevaa viatu, na pia akawaambia waislamu wanapoenda kusali, basi watazame viatu vyao kama kuna najisi, basi wavisugue chini mchangani, labda waislamu watuambie wao kusali na viatu, ni Uviviu wa kusugua viatu mchangani? Au mazingira yao wanayoishi hayana mchanga?
Tena Muhammad akakazia zaidi kuhusu Viatu, aliponukuliwa katika Hadithi hii.
Kasema Mtume (S.a.w) “Atakaepata (ona) nge nae anasali, basi amuue kwa kiatu cha kushoto” (Mkweli Mwaminifu, Juzuu ya 1-2, Hadithi Na. 188, Uk, 88)
Muhammad anawataka Waislamu wakimuona Nge basi wamuue kwa kiatu cha kushoto, sasa jiulize, wewe umevua viatu, unaswali peku peku (kama bata) Halafu amekatiza nge, unaweza kweli kumkanyaga kwa mguu? Nachoweza kusema ni uvivu tu wa waislamu katika kusugua mchangani viatu vyao vilivyo na najisi, kwani wameshapewa ruhusa ya kusali navyo.
Kumbe Mtume Muhammad alikuwa anavaa viatu alipo kuwa ndani ya Msikiti.
Kumbe Mtume Muhammad alisali na viatu Msikitini.
Hakika Uislam ni dini bandia.
Max Shimba Ministries Org

IMAM KUTOKA YEMEN AKAMATWA NA NYAMA YA NGURUWE AIRPORT AKIWA AMEIFICHA KWENYE SEHEMU ZAKE ZA SIRI NCHINI QATAR



Maofisa wa Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Hamad International Airport, Nchini Qatari, wamemkamata raia wa Yemen aliye kuwa akijaribu kuiingiza nyama ya Nguruwe nchini humo.
Abd Al Rahman Smoun mwenye umri wa miaka 53 aliificha nyama hiyo kwenye sehemu zake za aja kubwa ikiwa ndani ya Kondom kubwa nne. Nyama hiyo yenye uzito wa Kilo 12 iligundulika baada ya Mbwa maalum ambao wamefungwa kuchunguza watu wenye Nyama ya Nguruwe na Madawa ya Kulevya.
SWALI LA KUJIULIZA:
KWANINI WAMEWEKA MBWA WA KUCHUNGUZA NYAMA YA NGURUWE UWANJA WA NDEGE?
HAKIKA HAWA NI WALAJI WAKUBWA WA HII NYAMA YA NGURUWE KIASI CHA KUWEKEWA MBWA WA KUWACHUNGUZA KILA WANAPO INGIA NCHINI QATAR.
NDIO MAANA NASEMA YANINI KUWA MUUMINI WA HII DINI YA KULAZIMISHANA HUKU NYOYONI MWAKO UNATAMANI KULA NYAMA YA NGURUWE?
Kwa habari zaidi soma hapa

UTHIBITISHO: ADAM NA HAWA WALITUMIA LUGHA YA KIEBRANIA NA SIO KIARABU


Ndugu msomaji,
Katika somo letu hili, tutajifunza na kujibu swali kuhusu; ni lugha ipi Adam na Hawa walitumia wakati wakiwa katika Bustani ya Edeni?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Adam na Hawa walitumia Kiebrania kwasababu ya majina mawili ambayo Adam alimpa Hawa ambayo yanaweza kuwa yakinifu pekee katika lugha ya Kiebrania. Adam alimuita Hawa jina la “ISHA” ikiwa na maana ya MWANAMKE kwasabau ya kuwa alitoka kwa “ISH” ikiwa na maana ya MWANAUME , zaidi ya hapo, Adam alimuita mkewe “CHAVA” [HAWA] ikiwa na maana ya mama wa watu wote “CHAI” [UHAI].
Zaidi ya hapo, jina la ADAM linatokana na neno la Kiebrania “ADAMAH” likimaanisha “udongo”, hili jina linathibitisha kuwa Mungu alimuumba Adam kutoka kwenye udongo, kama ambavyo Biblia inasema katika Kitabu cha Mwanzo Mlango 2 na aya ya 7. Hivyo basi, tokea wakati wa Adam na Hawa mpaka wakati wa Mnara wa Babeli, watu wote walitumia lugha ya Kiebrania. Bereshet 2:23, 3:20, Midrash Bereshet Rabbah 38
Wasomi wa Kiyahudi na wa Kikristo wanaendelea kuthibitsiha kuwa Lugha ya Kiebrania ndio ilikuwa lugha ya kwanza, na majadiliano makali yalifanywa zamani na watafiti kama Dante Alighierl (1265-3121), Guillaume Postel (1510-1581) Claude Duret (1570-1611), Etienne Guichard (wakati huo huo wa ATHANASIUS Kircher (1602-1680) na Franciscus Mercurius van Helmont (1614-1698) wana sema kuwa, lugha ya Kiebrania ndio ilitumika na Adam na Hawa. Kwa mfano Mtaalam Guichard alisema kuwa neno la Kilatini “divider” likimaanisha tenganisha au kutenganisha limetokana na neno la Kiebrania la “batar” likimaanisha kukata katika sehemu mbili, hili neno lilifanana na la “tarab” ambalo lilikuja neno la Kilatini la “tribus” likimaanisha “kabila “tribe”
Hebu tuangalie ushahid mchache kutoka Biblia:
Matendo ya Mitume 26:14 Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya KIEBRANIA, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.
Yohana 19: 17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa KIEBRANIA, Golgotha.
Matendo ya Mitume 22: 2 Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema,
Kutoka 2:6 Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.
Katika kitabu cha Kutoka hapo juu, tunajifunza kuwa MUSA ANAITWA MTOTO WA KIEBRANIA “Eevriym in Hebrew” na katika kipindi chote watoto wa Kiisraeli waliitwa kama WAEBRANIA ambao ni watoto au wajukuu wa Ibrahim na Musa. Soma Mwanzo 10:24. Zaidi ya hapo, katika kitabu cha Mwanzo 14:13 tunasoma kuwa Ibrahim anaitwa Muebrania (Eevriy in Hebrew).
Huu ni ushahid tosha kuwa Lugha ya Mungu kwa Adam na Hawa ilikuwa ni Kiebrania na sio Kiarabu au lugha nyengine.
Je, Kwanini Mungu alitumia Kiebrani alipo zungumza na Adm na Hawa?
Kwanini Adam na Hawa walitumia Kiebrania walipo kuwa katika Bustani ya Edeni?
Hapa pana hitaji ufunuo wa hali ya kuu kufahamu kwanini Mungu alitumia lugha ya Kiebrania ambayo ni tofauti kabisa na Allah anaye tumia Kiarabu tu.
Kumbe sababu za Allah kutumia Kiarabu ni kupinga Mungu wa Biblia ambaye alitumia Kiebrani na kuwapinga Waisraeli ambao waliitwa wana wa KIEBRANIA.
References:
1. Merrill F. Unger, "Tower of Babel," Unger's Bible Dictionary, 1977 ed.: 115. (BCE - Before the Common Era, equivalent to BC)
2. J.I. Packer, Merril C. Tenney, William White, Jr., Nelson's Illustrated Encyclopedia of Bible Facts (Nashville: Thomas Nelson, 1995) 337.
3. Madelene S. Miller and J. Lane Miller, "Sumer," Harper's Bible Dictionary, 1973 ed.: 710.
4. Unger, "Scythian," 987.
5. Unger, "Egypt," 288.
6. William Smith, "Hebrew Language," Smith's Bible Dictionary, 1948 ed.: 238.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 12, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA UISLAMU NI DINI YA WAARABU NA SIO WAAFRIKA




Katika hii mada ninawaletea ushaidi kuwa Uislam ni dini ya Waarabu peke yao.
Waislamu bila kuchoka wamekuwa wakidai kuwa Uislamu utatawala dunia nzima. Katika kufanya hivyo, wao watakuwa wamekwenda kinyume na maneno ya Allaha kama yarivyo teremshwa kwenye Qur'an. Kwa hiyo, ni haki kwa kusema wao ni Makafiri.
Quran 10: 47. Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Angalia hii aya pia
Quran 14: 4. Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Allah humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Kama aya hizi ni kweli, basi Uislamu si kwa mashirika/mataifa/ummah yasiyo ya Waarabu. Quran inasema kwamba kila watu wamepokea ujumbe wao kutoka kwa Mungu katika lugha yao wenyewe ili waweze kuelewa na Qur'ani akaishuka kwa Waarabu ili Waarabu waweze kulewa nini Allah anasema.
Dhana hii ya Allah kushusha Kitabu kwa kila lugha ni muhimu sana kwasababu imejirudia mara nyingi na ndio msingi wa hili somo.
Quran 16: 36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
Quran 5: 48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Quran 36: 5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.
Hizi aya zimekamilka na kueleza kiuwazi kuhusu kuja kwake kwa Waarabu pekee. Allah katika Koran anasema kwamba kila watu wamekuwa na Mtume wao wenyewe ambao aliwaonya katika lugha zao wenyewe, na kwamba amemtuma Muhammad kwa wale ambao bado hawajaanza mwongozo wowote, na ambao baba zao hawakuonywa, yaani Waarabu. Kwa njia hii watakuwa hawana udhuru wowote na hawezi kusema, lakini hatukuwai kupokea ujumbe wowote.
Endelea kusoma Koran hapa chini:
Quran 6: 156. Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma.
157. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Quran ni wazi ilitumwa kwa Waarabu. Wale ambao si Waarabu hawawezi kuielewa Koran, hayo ni maneno ya Allah. Waislamu wanasisitiza kuwa hakuna tafsiri ya Qur'ani inaweza kuwa sahihi. Hivyo, haiwezi kamwe kuwa wazi kwa mashirika yasiyo ya Waarabu na haikutumwa kwa mashirika/ummah yasiyo ya Waarabu.
Uthibitisho mwingine kuwa Qur'ani ilitumwa tu kwa ajili ya Waarabu ni katika mistari ifuatayo hapo chini:
Quran 26: 198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, 199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
Kama ambavyo Waarabu wana haki ya kuto amini kitabu chechote kile kilichotumwa kwa lugha ambayo si yakwao, ikimaanisha Kiarabu, vivyo hivyo, mashirika yasiyo ya Waarabu nao wana haki ya kuto iamini Koran, kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Ndio kwasababu Koran inasema Allah atatuma mjumbe kwa kila lugha ili wao wenyewe kwa wenyewe waweze kuelewa.
Kuhakikisha hakuta kuwa na kutokuelewana, Allah anashusha hii aya 05:19 Quran: Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu.
Kwa mujibu wa Qur'an watu wote wamepokea ufunuo. Aya ya hapo juu inasema Qur'ani ni kwa wale ambao kamwe hawakupokea ufunuo, iliwasije kusema, `kuwa sisi hatuja wai kutumiwa mbashiri na hakuna mjuonyaji aliye tumwa kwetu'.
Jambo hili ni wazi, lakini Allah anataka liwe wazi hata na kwa asiye na ufahamu wowote ule aelewe kuwa Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee kwa kuzitaja sehemu halisi za kijiografia ambazo Muhammad alitumwa kama Mtume wa Allah.
Quran 6:92. Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao.
Leo, tumejifunza kuwa, Koran ilitumwa kwa Waarabu pekee na si kwa Mataifa yote. Sasa, nina uhakika baadhi ya Waislamu wanaweza kuleta aya nyingine zinazosema kwamba Uislamu ni kwa wanadamu wote. Kama Waislam watafanya hivyo, basi waelekuwa kwa kufanya hivyo ni kuthibitisha kwamba aya hapo juu ni za uongo.
Ama Quran ni pakiti ya uongo na utata au ni tu kwa Waarabu wa Makkah na jirani yake kama alivyo sema Allah ambaye ni mungu wa Waislamu.
Katika huduma yake,
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

VIOJA VYA UISLAM KUHUSU KIFO NA KUFUFUKA WAKATI WA KIYAMA


1. Eti Binadamu asili yake ni MBEGU YA "Ajabu Dhanab"
2. Eti Siku ya Kiyama Allah atanyeshea Mvua Ajab Dhanad na wewe ndio utafufuka tena.
3. Huu ni msiba mkubwa sana kwa Waislam.
Ndugu Msomaji, ebu jiunge nami leo na jifunze kuhusu Sayansi dhaif ya Allah na Muhammad.
MTU ANAPOKUFA, ZILE ASILI TATU KILA MOJA INARUDI MAHALA PAKE PA ASILI
Kwa kifo, udongo ambao kwao ndio mwili ulijengeka, unarudi mahala pake pa asili napo ni ardhini.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Kwa hakika tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi katika miili yao (wakati wanapooza huko makaburini) Na kwetu kiko kitabu kinachohifadhi (kila kitu)".
Qaf -4
AJABU DHANAB- ETI BINADAMU NDIO KATOKEA HAPO
Kinachobaki katika mwili wa mwanadamu ni kitu kidogo kinachoitwa "Ajabu dhanab" (kilichoingia pamoja na mbegu). Hii ni sehemu ambayo ndani yake mtu aliumbiwa, na kitu hiki asili yake kilikuwa katika uti wa mgongo wa Baba yetu Adamu(AS), kwa vile kitu hiki ni kidogo sana (Hakiwezi kuonekana ila kwa kutumia microscope zenye nguvu sana), ndiyo maana uti wa mgongo wa Baba yetu Adamu(AS) uliweza kuzibeba asili hizi zote za wanawe.
Na sehemu hii iitwayo "Ajabu dhanab" haiozi wala haivurugiki.
Mtume(SAW) amesema:-
<<Mwili wote wa mwanaadamu unaoza isipokuwa "Ajabu dhanab", kutokana nayo ameumbwa na kutokana nayo atakusanywa tena >>.
Bukhari – Muslim – An Nasai, Malik katika Muwata a na Abu Daud.
Ama Roho itarudi mahali anapopataka Mwenyezi Mungu (katika Barzakh) mpaka Siku ya Kiama.
SIKU YA KUFUFULIWA ZILE SEHEMU TATU ZINAKUSANYIKA TENA
Unapofika wakati wa kufufuliwa, Mwenyezi Mungu atateremsha mvua na kuifanya ile mbegu isiyooza "AJABU DHANAB”, imee tena.
Mtume (SAW) amesema:-
<<Kisha inateremshwa mvua na watamea kama imeavyo mboga, na hapana katika mwili wa mwanadamu kisicholiwa na ardhi isipokuwa fupa moja nalo ni "Ajabu dhanab" ndani yake humo watakusanywa viumbe Siku ya Kiama>>.
(Bukhari, Muslim, Imam Malik, Abu Daud na AnNasaiy)
Yaliyofanana na haya yanatokea duniani kila siku. Panapotokea ukame, tunaona miti ikianguka na kufa (na kutoweka). Hauonekani mti wowote wala mmea. Lakini Mwenyezi Mungu amejaalia ndani ya ardhi au ndani ya mawe kuwemo mbegu, na mbegu hizo hazionekani kwa macho, isipokuwa mvua inaponyesha ndipo hupasuka na kuchipua miti na mimea mbali mbali.
Mwenyezi Mungu anasema:-
"Hukitoa kilicho hai katika kilichokufa na hukitoa kilicho kufa katika kilicho hai na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake na hivyo ndivyo mtakavyofufuliwa".
(Al - Rum - 19).
Mtu mmoja alimuuliza Mtume (SAW):-
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, namna gani MwenyeziMungu atawarudisha tena viumbe, na nini dalili yake?”
Mtume (SAW) akamjibu;
"Uliwahi kupita bondeni kijijini kwenu wakati wa ukame (miti yote ikiwa imekufa), kisha ukapita tena wakati miti (imeota tena na) imejaa na ardhi ikageuka (na kuwa) rangi ya kijani?
Akasema:- "Naam".
Mtume(SAW) akamjibu:
"Basi hiyo ndiyo dalili ya Mwenyezi Mungu katika kuumba kwake na hivyo ndivyo atakavyowafufuwa wafu".
(Imam Ahmad )
(Siku ya Kiama), Pale Ajab dhanab itakapochipua na kutoka ndani ya ardhi na mwili ukarudi tena, ndipo zitakapokuja roho na kuingia kila moja katika mwili wake.
Ndio sababu Mwenyezi Mungu akasema:
"Na nafsi zitakapounganishwa (na viwiliwili vyake)."
(At - Takwiyr - 7)
Na hivi ndivyo watakavyorudi viumbe mara ya pili kama walivyoanzishwa hapo mwanzo.
Mwenyezi Mungu anasema:-
"Kama tulivyoanza umbo la awali tutalirudisha tena, ni ahadi ilio juu yetu, bila shaka sisi ni wenye kufanya (tusemavyo).”
(Al - Anbiyaa -104).
Ndugu msomaji, hivi ni kweli Allah wa hii dini ya Kiislam aliumba? Mbona hii imani imejaa shaka na utata kila kona?
Leo Allah kesha jisahau na kusema kuwa eti wewe umetoka katika Ajabu Dhanab na sio tena vumbi.
Je, Adam aliumbwa kwa tone la Damu?
Quran 96 1-2
1. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, ***2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, ***
Allah anasema kuwa, Binadamu aliumbwa kwa tone la damu. Endela kupa ilmu ya Koran.
Je, Adam aliumbwa kutokana na Maji?
Quran 25:54. Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji na Mola wako Mlezi. ***
Allah anachanganya madawa. Sasa anaumba Mwanadamu kupitia MAJI. Tuendelee kusoma usanii wa Allah.
Je, Binadamu aliumbwa kutoka kwa Udongo?
Quran 15:26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. ***
Allah amebadilika tena, sasa anaumba Mwanadamu kupitia Udongo, tena unao toa Sauti. Jamani huu si Msiba?
Endelea kupata Elimu.
Je, Binadamu aliumbwa kutoka VUMBI?
Quran 30:20. Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kutoka Vumbi. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote. ***
Sasa Allah anaumba mtu kutoka vumbi. Mimi ningependa Waislam watuambie, hivi Allah wenu ana kigeugeu au ni msahalifu wa anacho sema au ni yule yule Ibilisi ambey sifa yake kubwa ni Muongo?!!!
Ndugu zanguni, hivi kweli Koran ilishushwa kutoka kwa Mungu? Mbona kuna UTATA kila sehemu?
Binadamu aliumbwa kutoka nini? Tone la Damu? Maji? Udongo? Vumbi?
Kweli Allah anafahamu yote, ingawa hajui alimuumbaje Adam.
Katika Huduma yake.
UHAKIKA WA UFUFUO WA WAFU KWA WAKRISTO
Ufufuo wa wafu, ni moja kati ya masomo ya msingi sana katika Ukristo na ni mafundisho ya kwanza ambayo kila Mkristo inampasa kuyafahamu ( WAEBRANIA 6:1-2 ). Kiyama ya wafu au Ufufuo wa wafu, umetabiriwa mapema katika Neno la Mungu ( LUKA 14:13-14; YOHANA 5:28-29; WAFILIPI 3:10-11; 1 WATHESALONIKE 4:16 ). Yesu Kristo ndiye kielelezo cha wafu na uhakika wa ufufuo wa wafu kwa watu wote ( 1WAKORINTHO 15:21, 20-23). Yesu kristo alitabiri mapema juu ya kufufuka kwake kabla hata hajafa (MATHAYO 16:21; 17:22-23; 20:17-19; MARKO 8:31-32; 10:32-34; LUKA 9:20-22; 18:31-34). Yesu Kristo huyuhuyu alitabiri juu ya kufufuka kwake na ikawa hivyo, ndiye pia aliyetabiri juu ya ufufuo wa watu wote ( YOHANA 5:25-29 ). Ni muhimu kufahamu kwamba walikuwepo watu wenye mashaka, ambao hawakuamini kwamba Yesu angefufuka kama alivyosema ( LUKA 18:31-34 );lakini kutokuamini kwao hakukuzuia kufufuka kwa Yesu. Vivyo hivyo leo, pamoja na kuwapo watu wasioamini kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kutokuaminii kwao hakutaweza kuzuia jambo hilo kutokea ( WARUMI 3:3-4 ). Uongo wa askari Walinzi wa kaburi la Yesu, waliutawanya baada ya kupokea rushwa na kufundishwa kusema uongo, kwa kuabiwa “ semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala “, ni uongo ulio dhahiri ( MATHAYO 28:11-15 ). Ikiwa walinzi walikuwa wamelala usingizi, waliwaona namna gani watu waliokuja kuuiba mwili wa Yesu na kufahamu kwa hakika ni wanafunzi wake? Na kama waliwaona kwa nini waliwaacha wakauiba mwili huo na wasiwazuie kufanya hivyo? Ni uongo ulio wazi. Ni jambo lililo dhahiri kwamba Yesu alifufuka! Kwa jinsi hiyohiyo, ufufuo wa wafu wote ni jambo lililo dhahiri kabisa kutokea.
Max Shimba Ministries Org.

BIBI KHADIJA AMPA UTUME MUHAMMAD ILI KUMFARIJI BAADA YA KUPIGWA NA MALAIKA JIBRIL



Ndugu zanguni,
YALIYOMKUTA MTUME BAADA YA KUTOKA PANGONI!
Basi Mtume akafanya khofu, akarejea kwa mkewe, akamhadithia, na pale pale homa kubwa kabisa, ikampanda, akataka afunikwe maguo, akawa anatetemeka kwa ngerema, na kuweweseka, na kusema, "Najikhofia nafsi yangu, kuchezewa na mashetani, na kuniharibu akili yangu na kunizuga"(Kitabu cha maisha ya Nabii Muhamaad s.a,uk.17 kilichoandikwa na Sheiky A.Farsy).
MASWALI:
(i). Kama Jibril ndie alitumwa na Allah, na huyo Allah ni Mungu, kwanini Muhammad alisema kuwa nafsi yake imechezewa na MASHETANI baada ya kukutana na Jibril?
(ii). Kama Jibril alitoka kwa Allah, kwanini Muhammad alipo toka pangoni alisema kuwa Jibril AMEMZUGA AKILI YAKE?
Vipi kwa Hadidja?
Mjane aliyefiwa na waume wake 2 kisha akajichukulia Muhammad kama mume wake wa tatu, Huyu ndiye aliyeingia wa kwanza katika imani potofu ya uislamu. Lakini natujiulize hili swali:
Je, inakuwaje mtu ambaye bado ni mkafiri kutowa utume kwa mwingine kabla yeye hajajuwa ujumbe wa mtume huyo nakuuamini?
Bila shaka jibu laweza kuwa ni upumbavu wakupindukia.
Hebu tuone Qura’n inavyosema kuhusu kupewa utume, kupewa wahyi au ujumbe,
Qr.7:144 au surat Al-A’raaf 144
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukuwa niliyikupa na uwe katika wale wanaoshukuru.
Kwanini Allah Subhanau Watahallah hakufanya hivihivi kwa Muhammad s.a.w katika pango la Jabal Hira?
Swala la Muhammad kuwa ni mtume katika maandishi ya Qura’n na hadithi zote siyo hoja lakini hoja yetu ni «Kapewa na nani huo utume?
MKEWE AMPA UTUME ILI KUMFARIJI!
Pale pale bibi Khadija akamdakiza, akamwambia, "Wacha hayo siyo yatakayokuwa hayo, wewe huwezi kuchezewa na mashetani, shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako, wewe unatazama vema Jamaa zako, unawadhihirisha watu sifa nzuri, ambazo hukuwa mwenye nazo, unachukua mizigo ya watu wasiokuwa wako, unafanya hivi, unafanyi hivi, furahi ndugu yangu, pumua moyo wako, Wallahi mimi mkeo naona umekwisha kuwa mtume."
(Kitabu cha wakeze Mtume wakubwa na wanawe, uk. 12)
KHAJIDA ANASEMA HIVI "Nukuu" WALAHI MIMI MKEO NAONA UMESHAKWISHA KUWA MTUME.
Huu ni uhakikisho kwamba Muhammad hakupewa utume na Mungu wa Israeli, sababu ukisoma pia kitabu chawakeze wakubwa na wanaweukurasa wa 12 kuna maneno yanayorudilia haya ambayo tumeyasoma hapo juu yakisema hivi:
Nanukuu,
Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe, akamwadithia na palepale homa kubwa kabisa ikampanda, akataka afunikwe na maguo mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema: «Najihofia nafsi yangu kuchezewa na mashetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga!
Hapo katika pango la Jabal Hira ndipo Waislamu na Qura’n hudai kwamba ndipo alipopokea Wahyi wa Qura’n, utume na unabii.
Lakini twaona na kusikia maneno ya Mtume mwenyewe yanashuhudia alichokutana nacho pangoni ambacho ni Shetani sababu hata Biblia Takatifu hushuhudia hivi:
1 Yohana 1:3
Hilo tuliloliona nakulisikia, twalihubiri na nyinyi: ili na nyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.»
Ukweli ni kwamba huyu Shetani aliyekutana na maskini Muhammad pangoni hakumpa hata utume wala unabii isipokuwa mkewe Hadidja na Bwana Waraqa bin Naufal ndio waliomshauri Muhammad kujibashiria kuwa yeye ni Mtume wa Umma kama tulivyo soma katika kurasa ambazo tumekuwekea picha zake hapo juu.
Huu ndio mwanzo wa utume wa Muhammad alio pewa na Mkewe Khadija. Muhammad baada ya kupigwa na Jibril na kukiri kwake kuwa amezugwa na kuchezewa akili, ni sifa tosha kuwa huyu Muhammad ni BANDIA zaidi ya kupewa utume na Mkewe Khadija.
Huu ni msiba mkubwa sana na hii juisi ya Pilipili Waislam kamwe hawawezi kuinywa.

YESU NDIE NJIA NA KWELI NA UZIMA



1. ALLAH AMBAYE SIO YEHOVA SIO NJIA.
2. MAREHEMU MUHAMMAD SIO NJIA.
3. QURAN SIO NJIA.
4. UISLAM SIO NJIA.
5. DINI SIO NJIA.
Kumbe Dini sio Njia
Katika Biblia tunasoma kuwa Yesu anasema yeye ndie "NJIA", "KWELI" na UZIMA, na anaendelea kusema kuwa KWELI ndiyo itakuweka HURU miaka 680 kabla ya Uislam kuanxoshwa. Hebu rejea kwenye hii aya:
Yohana 14:6 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.
Kufuatana na aya hapo juu iliyo kuja miaka 680 kabla ya Uislam, Mtu yeyote yule hawezi kwenda kwa Baba na/au Mbiguni bila ya kupitia "NJIA" ambayo ni YESU. Kumbe basi dini haiwezi kukupeleka popote pale. Kumbe, NJIA PEKEE ya Uzima wa Milele ni YESU na SI DINI.
Kumfahamu Yesu ambaye ni KWELI kutakufanya umwelewe Mungu wa UKWELI!! Kumbe basi, Yesu ndie mwenye uwezo wa kukufanya uelewe KWELI ya Mungu.
Yohana 8:31-32 Kwa hiyo Yesu akawaambia wale waliomwamini, “Kama mkiendelea kutii maneno yangu mtakuwa wanafunzi wangu halisi. 32 Mtaelewa yaliyo kweli kumhusu Mungu na ukweli huu utawafanya muwe watu huru.
Kufuatana na aya hapo juu, inatuhakikishia kuwa mafundisho ya YESU PEKEE ndiyo yatakufanya uelewe KWELI na kumfahamu Mungu wa KWELI. Zaidi ya hapo, kuwa Mwanafunzi wa Yesu (Ukristo) ndio njia pekee ya kufahamu kweli.
Yesu Ndie Njia ya Kweli na Uzima.
Mwamini leo ili upate uzima wa milele.
1. Allah sio Njia.
2. Marehemu Muhammad sio Njia.
3. Uislam sio Njia.
4. Quran sio Njia.
5. Dini sio Njia.
Bali Yesu ndie Njia pekee ya kweli na uzima wa milele.
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

TRENDING NOW