Saturday, July 2, 2016

YESU NI MWANA WA MUNGU MAANA YAKE NINI?Wanadhuoni wa Kiislam pamoja na waumini wa dini ya Kiislam huwa wanauliza na kusema kwa Wakristo yafuatayo:
1. Kivipi Yesu ni Mwana wa Mungu?
2. Mungu atakuwaje na Mwana bila ya Mke?
KIVIPI YESU NI MWANA WA MUNGU?
Yesu Kristo si Mwana wa Mungu kulingana na ubaba wa kawaida wa binadamu, nikimaanisha kuwa Mungu hakuoa na kupata mwana wa kiume. Nikiwa na maanisha kuwa, Mungu hakufanya tendo la ndoa na Mariamu, na pamoja naye kuzaa mtoto wa kiume ambaye anaitwa Yesu, la hasha.
1 YOHANA MLANGO 5 aya 1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
MUNGU ATAKUWAJE NA MWANA BILA YA MKE?
Yesu ni Mungu katika hali kwamba ni Mungu anajithirihisha kama mwili. (Yohana 1:1, 14) Yesu ni mwana wa Mungu kwa dhana kwamba Mariamu alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu. Luka 1:35 yasema, “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, MWANA WA MUNGU.”
Mariamu aliambiwa na Malaika kuwa, Mtoto atakaye zaliwa atakuwa Matakatifu na ataitwa MWANA WA MUNGU. Huu ushahidi upo kwenye Luka 1:35.
YESU AKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU MBELE YA KUHANI MKUU
Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, MWANA WA MUNGU” (Mathayo 26:63). [NOTE: YESU HAKUKATAA ALIPO ITWA MWANA WA MUNGU NA KUHANI MKUU, SOMA JIBU LAKE] “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia, wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64) viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66).
WAYAHUDI WANAKIRI KUWA YESU AMEKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU
Baadaye mbele ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) [KWENYE HIYO AYA YA YOHANA 19:7, WAYAHUDI WANAKIRI KUWA YESU AMEKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU] ni kwa nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili hukumu ya kifo?
Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu. Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”
Mfano mwingine unaweza patikana katika Yohana 17:12 mahali Yuda anaelezwa kama mwana wa “upotevu”? jina upotevu lamaanisha “uharibivu” Yuda hakuwa mwana wa uharibivu, lakini mambo hayo ndio ya kutambulisha maisha ya Yuda. Yuda anadhihirisha upotevu. Vile vile Yesu mwana wa Mungu. Ni Mungu anajidhihirisha (Yohana 1:1,14).
Hii mada iatufundisha maana ya Yesu ni Mwana wa Mungu, SWALI ambalo limekuwa likiulizwa na Waislam kila siku. Leo wamesha pata jibu thabiti tena lenye ushahidi wa aya za Biblia.
Hakika Yesu ni Mwana wa Mungu
Max Shimba Ministries

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW