Monday, July 11, 2016

NA UZIMA WA MILELE NDIO HUU, WAKUJUE WEWE ULIYE MUNGU WA PEKEE, WA KWELI NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA

Ndugu wasomaji,
Leo nitaielezea aya ya Yohana 17: 3 ambayo Waislam wamekuwa wakiitumia mara nyingi sana kudai kuwa eti, Yesu amekana kuwa yeye ni Mungu. Waislam kwa kupitia mihadhara ya kidini na kwa kutumia vijarida mbali mbali wanatishia Umma wa Wakristo kuwa, Yesu ameukana Uungu. Je, hayo madai ya Waislam ni kweli? Je, hiyo aya ina la zaidi la kujifunza?
Ili uielewe Biblia vizuri, nilazima usome aya kadhaa ili upate kuelewa nini hasa Mungu anasema kupitia Neno lake. Hivyo basi, nimeweka aya ya 4 na ya 5 ili kufafanua nini hasa Yesu alikuwa anasema katika Yohana 17.
Ngoja niziweke aya zote hapa:
Yohana 17: 3 Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.4 Nimekutukuza Wewe duniani kwa kuitimizaile kazi uliyonipa niifanye. 5 Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
Yesu katika aya ya 5 [Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako] ==> YESU anasema kuwa
1. Yeye aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo! Hapo panaanza kukupa mwanga halisi, wa nini Yesu alikuwa anasema na Yesu ni nani. Imani zote zinakiri kuwa aliye kuwepo kabla ya vitu vyote ni Mungu. Lakini katika aya ya 5, Yesu nae anadai kuwepo kabla ya uumbaji.
2. Yesu anaendelea kusema katika aya hiyo hiyo kuwa, yeye alikuwa na adhama ya Mungu -"UTUKUFU". Yesu anamwambia Mungu Baba kuwa, AMTUKUZE YESU KWA UTUKUFU ALIOKUWA NAO KABLA YA ULIMWENGU HAUJAKUWAKO. Sasa, kama Yesu, sio Mungu na alikuwa Binadamu wa kawaida, kwanini basi amwambie BABA YAKE AMTUKUZE? Yesu anatumia mamlaka gani hayo kudai Utukufu ambao sio wake bali ni wa Mungu pekee?
3. Kama Yesu sio Mungu. Je, alipo dai atukuzwe na Mungu Baba, huoni kuwa alikuwa anakufuru? Lakini Hatusomi kuwa YESU aliwai tenda dhambi yeyote ile. Hata dini ya Waislam, inakiri kuwa, Katika Binadamu wote ambao waliishi Duniani, ni Yesu pekee aliweza kuishi bila ya kutenda dhambi na kuwa na dhambi.
Ndugu wasomaji, madai ya Waislam kuwa Yohana 17:3 INAPINGA UUNGU WA YESU ni Batili kabisa, maana, leo tumejifunza katika Yohana hiyo hiyo kuwa Yesu aliishi kabla ya Ulimwengu kuwepo na Yesu anautukufu wa Mungu.
Aya ya 5 NUKUU: Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako.
HOJA:
1. Yesu anadai kuwa aliishi kabla ya ulimwengu kuumbwa.
2. Yesu anadai kuwa anautukufu kama wa Baba yake.
SASA BASI:
1. Yesu ni nani mpaka adai utukufu kama wa Mungu tena kutoka kwa Mungu Baba?
2. Yesu ni nani mpaka aseme kuwa aliishi hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, tena namwambia Mungu Baba?
Ndugu zanguni,
Mada imekamilika na kujibu maswali ya Waislam kuwa Yesu aliukana uungu wake katika aya 3 ya Yohana 17.
Nawakaribisha wote Kwa Yesu Kristo aliye hai. Yeye ndie njia kweli na uziama. Njooni kwake ili mpate maisha ya milele na yenye uzima tele.
Katika Huduma yake,
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu.
Kwa Max Shimba Ministries Org.
April 28, 2015 @Max Shimba Ministries.

JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?


Ndugu msomaji,
Mwezi huu nitaweka mada kadhaa zitakazo fundisha kuwa, Isa wa Quran na Yesu wa Biblia ni wawili na tofauti:
MAANA YA JINA ISA
Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe "ZERUZERU". Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?
JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?
JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.
Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.
Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na Sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
Leo tumejifunza kwa kifupi tu kuwa, Jina la ISA lenye maana ya Wekundu unao zidiana na weupe ni TOFAUTI KABISA NA Jina la Yesu lenye maana ya MWOKOZI katika Biblia. Zaidi ya hapo, tafsir ya Jina la Yesu kwa Kiarabu ni Yasu na sio Isa kama ambavyo Waislam wanadai katika vitabu vyao.
Mungu awabariki sana na tuendele kujifunza Neno lake bila ya kuchoka.
Katika huduma Yake,
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 7, 2016

KWANINI ALLAH HAKUITAJA PALESTINA KWENYE QURAN?



1. Allah asema Israel ndio taifa la Mungu
2. Palestina yakatwa na haipo kwenye Quran
Ndugu wasomaji,
Huu ni Msiba kwa Waislam wanao pigia debe Wapalestina. Hivi kwanini Allah hakuitaja Palestina kwenye Quran yake? Lakini ameitaja Israel na Waisraeli?
ALLAH ANASEMA KWA WAYAHUDI:
Allah (s.w.t.) amesema: Enyi watu wangu! Ingieni katika hiyo ardhi iliyotakaswa ambayo Allah amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika.(5:21)
Katika aya hapo juu, Allah anawaita Waisrael kupitia Musa "WATU WANGU" zaidi ya hapo anawaambia kuwa Waende Israel kwenye ARDHI ILIYOTAKASWA. Ndugu msomaji, kwanini Allah anaiita ardhi ya Israel kuwa imetakaswa lakini hakuwai sema hivyo kwa Saudi Arabia/Makka?
Ardhi hii imebarikiwa kiroho na kirutba. Ni jambo hili ndilo lililowafanya watu na staarabu tofauti kuigombania. Agano la Kale inatuhadithia ya kuwa ardhi hii ilibubujika asali na maziwa.(Hesabu, 13:27) Na katika kitabu cha Hesabu Sura ya 13 inatueleza kuwa WAISRAEL walipo kuwa wakitoka Misri walipata humo matunda ya makudhumani, tini na zaituni ambayo yalikuwa makubwa na kila tunda kubebwa na watu wawili.
Swali lamsingi: KWANINI ALLAH HAKUITAJA PALESTINA KWENYE QURAN YAKE?
Waislam, Allah kasema kwa Waisrael kuwa, WAINGIE KATIKA ARDHI ILIYOTAKASWA, sasa, kwanini nyie mnataka Wapalestina ambao hata Allah hawajui, wavamie ardhi ya Israeli?
Waislam wana wivu mkubwa sana kwa Israel kwasababu Allah amesema kuwa Israel ni ardhi iliyotakasika na hakusema kuwa Uarabuni kumetakasika. Huu ni MSIBA kwa Waislam.
ALLAH ANASEMA:
SURAT AL BAQARA 40. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni, na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu.
Allah anaendelea kusema kuwa Israel wana neema ya Mwenyezi Mungu, lakini hatusomi Palestina ikitajwa hata sekunde moja.
ALLAH ANASEMA KUWA ISRAEL NI ZAIDI YA WAARABU WOTE
Surat Al Baqara 47. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizo kuneemesheni, na nikakuteuweni kuliko wote wengineo.
Kama ulivyo soma hapo juu, Israel ina neema na ni zaidi ya wengine wote, pamoja na Palestina na Waarabu wote. Kumbe ndio maana Waarabu hawana ubavu kwa Israel.
Leo ningependa muelewe kuwa, Israel ni nchi iliyo barikiwa na hata Waarabu wafanye nini hawata weza kitu, hata Allah wao amekiri kuwa Waarabu wataendelea kufuata mkia kwa Israel mpaka Kiyama.
ALLAH KAWAPA ISRAEL KITABU, HUKUMU NA UNABII
Surat Al Jaathiya 16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
Kumbe Israel wamepewa Unabii, Kitabu na Hukumu. Hii ndio sababu Waraabu wanaendelea kusaliti amri kwa Israel.
Kwanini Allah hakuitaja Palestina kwenye Quran?
Mungu awabariki sana,
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries

YESU KWA KIARABU NI YASU "YASUA" NA SIO ISA.



Ndugu msomaji
Katika somo letu hili tutajifunza kuhusu jina sahihi la Yesu/Yashua na tafsiri yake katika Kiarabu. Je, Isa ni jina la Yesu wa Biblia?
Jibu sahihi la kihistoria na la wataalam wa kutafsiri litatupa ukweli halisi wa Jina la Yesu na kwanini alipewa Jina hilo katika " sherehe ya kumtaja " (Luka 2:21). Jina ambalo aliitwa na Mama yake, Baba yake wa Kambo, Ndugu zake na jamaa wengine, majirani zake , marafiki zake na wanafunzi wake wakati wa maisha yake duniani. Hakuna kutokuelewana kuhusu ukweli kwamba jina la Yeshua halikuwa la Kiarabu bali la Kiyahudi na Yesu/Yeshua mwenyewe aliishi katika Israeli, na alizaliwa katika familia ya Wayahudi wacha Mungu.
Jina la Yesu bila ya shaka yeyote ile ni la Kiyahudi. (Maana yake ni “kweli”). Tafsir ya jina la Yeshua Kiebrania katika Kiingereza itakuwa ni Jesus. Jina la Yesu halikuchaguliwa kiholela na wazazi wake, lakini yeye alipata jina lake moja kwa moja kutoka kwa Mungu (Mathayo 1:21 , Luka 1:31) kwa sababu ya maana ya jina lake na nani alilileta, basi leo hii tunaelewa madhumuni ya Yesu kuzaliwa na kuja hapa duniani (Mathayo 1:21 ).
Katika utamaduni na jadi ya Kiarabu. Jina la Yesu ni Yasu na si Isa kama ilivyo andikwa kwenye Koran ya Kiislam. Na hata leo, jina la Yasu linatumiwa na zaidi ya 99.99% ya Wakristo wote wa Kiarabu. Tembea katika kanisa lolote la Kiarabu huto sikia wanatumia jina la Isa, Sikiliza matangazo ya Wakristo wa Kiarabu katika Radio na Televisheni (za Kiarabu) huto sikiwa Mkristo anatumia jina la Isa, bali wanatumia jina la Yasu. Matangazo yote ya Kikristo katika Uarabu wanatumia jina la Yasu. Kamwe huto ona jina la Isa kama lilivyo kwenye Koran ya Waislamu.
Katika jadi ya Kiarabu na utoaji wa tafsiri wa jina, jina sahihi la Kiebrania (Yeshua) ni Yasu katika Kiarabu. Kila uchaguzi wa tafsiri ya jina la kigeni katika lugha tofauti ni uvumbuzi wa binadamu.
Kiisimu ipo wazi jinsi jina la Yeshua Kiebrania lilivyo tafsiriwa na kuwa Yesu Kiswahili na Jesus Kiingereza:
Yeshua '(Kiebrania) -> Ιησους (Kiyunani) -> Yesu (Kilatini) -> Jesus (Kiingereza) -> Yesu (Kiswahili).
Mpito muhimu ni kutoka Kiyahudi kwenda Kigiriki. Hatua hii ilifanyika miaka 200 kabla ya Yesu kuzaliwa. Watafsiri wa Septuaginta (LXX), classical Kigiriki tafsiri ya maandiko ya Kiyahudi, kutokaa Yeshua Kiebrania jina kama Ιησους katika Kigiriki. Injili ziliandikwa katika lugha ya Kigiriki ilitumia utamaduni huu wa kutafsir kwa muda mrefu.
Kwasababu Kiyahudi na Kiarabu ni lugha mbili za Kisemiti, na zina uhusiano wa karibu, kuna baadhi ya sheria maalumu ambayo sauti/maneno/maandishi ya Kiebrania yanahusiana na ambayo sauti/maneno katika Kiarabu. Hasa, Neno la Kiebrania Shin mara kwa mara linatumika kama Dhambi katika Kiarabu, kwa mfano neno la Kiyahudi la amani, shalom ni sambamba na neno “salam” la Kiarabu. Kulingana na sheria za lugha na mahusiano kati ya Kiyahudi na Kiarabu, Yasu 'ni sahihi kwa Kiarabu na kwa Kiebrania ni Yeshua:
Yeshua '= Yod + + Shin Waw +' Ain
Yasu '= + Ya + Sin Waw +' Ain
Tena, katika lugha sahihi, jina la Yasu ni Kiarabu sawa na Yeshua Kiebrania. Hivyo, katika utamaduni na jadi ya Kiarabu jina la Yasu ndilo sahihi na pekee kutokana na kiisimu. Mpito kutoka Yeshua kwa Yasu inafuata sheria ya kawaida ya mabadiliko fonetiki kutoka Kiyahudi na Kiarabu. Yasu ni jina la Kiarabu la Yesu. Kinyume chake, Yasu ndio jina lenye asili ya Yeshua.
Early Hebrew (long form): Yehoshua' = Yod + He + Shin + Waw + 'Ain
Later Hebrew (short form): Yeshua' = Yod + Shin + Waw + 'Ain
Arabic (Christian): Yasu' = Ya + Sin + Waw + 'Ain
Arabic (Muslim): 'Isa = 'Ain + Ya + Sin + Ya
“Ya” na “Waw” ni maneno dhaifu, katika lugha ya Kiarabu, hufundisha kwamba mtu anaweza kurejea katika maneno mengine kama kuchukua juu ya aina mbalimbali (declension, inflection). Hivyo, mtu anaweza kuona kwamba fomula ya Kiislamu 'Isa kimsingi ni ya bandia/kutungwa na binadamu (inversion) (pamoja na mabadiliko ya Waw ili Ya) kwa Mkristo wa Kiarabu jina la Yesu ni Yasu na si Isa kama ilivyo andikwa kwenye Koran ya Kiislamu.
Nategemea leo umejifunza tofauti iliyopo kati ya Jina la Yesu-Kiswahili, Yasu-Kiarabu na Yeshua-Kiebrani.
Jina la Yesu Libarikiwe Sana
Katika Huduma yake
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

WAISLAM WENYE SIASA KALI WA BOKO HARAMU WAKAMATWA NDANI YA KANISA.



WATU sita kati ya 100 wanaoaminika kuwa ni memba wa kundi la kigaidi la Boko Haram waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Ulinzi la Nigeria wamekamatwa wakiwa wamejificha Kanisani huko Festac Jijini Lagos.
Zoezi hilo lilifanikiwa jana kutokana na ushirikiano wa raia wema wa maeneo ya karibu kutoa taarifa kwa jeshi hilo kuhusu kuwepo kwa watu waliyowatilia shaka wakiingia kwenye Kanisa hilo lililopo mjini Festac kwa lengo la kujificha ilihali muonekanao wao sio wa kusali.
Washukiwa hao waliripotiwa kutafutwa na jeshi hilo tangu wiki iliyopita baada ya kufanya shambulizi na kutokomea huko mjini Maiduguri Borno.
Watuhumiwa waliokamatwa jana wametamnbulika kwa majina ya Ali Ibrahim, Ahmed Abubakar, Kamsalem Goigoi, Adams Ibrahim, Mohammed Ibrahim na Ali Blam Babagana waliokuwa wakitoroka kutoka Borno walikotekeleza shambulio.

TOFAUTI KUMI (10) KATI YA ISA WA KWENYE QURAN NA YESU WA KWENYE BIBLIA.



ISA WA QURAN KAZALIWA CHINI YA MTENDE WAKATI YESU WA KWENYE BIBLIA KAZALIWA KWENYE ZIZI LA NG'OMBE
TOFAUTI KUMI (10) KATI YA ISA WA KWENYE QURAN NA YESU WA KWENYE BIBLIA.
Taarifa za Malaika kabla ya kuzaliwa kwao, kadiri ya Qurani na Biblia.
Jibrili alivyomtokea Mama wa Isa == Gabrieli alivyomtokea mama wa Yesu:
A. MARYAM ALIKUWA MSIKITINI vs. MARIAM ALIKUWA NYUMBANI KWAKE:
1. WAISLAM-JIBRIL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa Msikitini Qurani 19:16-17
2. WAKRISTO-GABRIEL Alienda kwa Mariamu aliyekuwa nyumbani kwake - Lk 1:26-28
B. MARYAM HAJULIKANI ANAISHI WAPI vs MARIAM ANAYE ISHI NAZARETI:
1. WAISLAM-Mariamu Mama wa Isa haijulikani aliishi kijiji kipi wala mji gani wala hata nchi haijulikani. Isitoshe Quran inasema kuwa Jibril ndiye aliyemletea utume Muhammad asiwapelekee Mayahudi (hana kosa) Sura 2:97
2. WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama yake Yesu alitokewa na Malaika Gabriel akiwa katika kijiji cha Nazareti mji wa Galilaya nchi ya Israeli (Lk 1:26) Mariamu Mama wa Yesu ni Myahudi.
C. JIBRIL HAKUMSALIMIA MARYAM vs GABRIEL ALIYE MSAMILIA MARIAM:
1. WAISLAM-Jibrili hakutoa salamu kwa Mariamu mama wa Isa ila alijimithilisha kwa umbo la binadamu aliye kamili - Sura 19-17
2. WAKRISTO-Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu Mama wa Yesu – Luka 1:28
D. JIBRIL ALISEMA YEYE NDIE ANATOA MTOTO vs . GABRIEL ALIYE SEMA KUWA MARIAM ATACHUKUA MIMBA:
1. WAISLAM-Jibril alimwambia Mariamu kwamba mimi ni mjumbe wa mola wako ili nikupe mwana mtakatifu - Sura 19-19
2. WAKRISTO-Lakini malaika Gabrieli alimwambia mama wa Yesu kuwa utachukua mimba – Luka1: 31
E. JIBRIL HAKULIJUA JINA LA MTOTO vs. GABRIEL ALIYE SEMA KUWA MTOTO ATAITWA YESU:
1. WAISLAM-Jibrili alisema kwa Mariamu kuwa ili tumfanye mtoto muujiza kwa wanadamu – Sura 19: 21. Isitoshe Jibrili hakutaja jina la mwana kwa Mariamu. Bali alisema ili nikupe mwana mtakatifu.
2. WAKRISTO-Malaika Gabrieli alisema kwa Mariamu mama ya Yesu kuwa mtoto jina lake utamwita Yesu (Luka 1:31; 2:21) Gabrieli hakusema kuwa atampa mwana Mariamu. Bali alisema, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, yaani motto atazaliwa kwa uwezo wa Mungu.
TOFAUTI YA KUZALIWA KWA ISA NA YESU
Isa bin Mariam vs. Yesu Kristo
F. ISA KAZALIWA CHINI YA MTENDE vs YESU KAZALIWA KWENYE HORI LA NG'OMBE:
1. WAISLAM-Isa alizaliwa katika shina la Mtende –Quran 19:23
2. WAKRISTO-Yesu kazaliwa katika hori la kulishia ng’ombe. Luka 2:7
G. MIMBA YA ISA HAIJULIKANI ILKUWA YA MUDA GANI vs. YESU ALIYE ZALIWA KWA SIKU ZAKE ZILIPO KAMILIKA:
1. WAISLAM-Kuzaliwa kwa Isa haijulikani mimba ya mama yake ilichukua muda gani maana malaika Jibrili alisema nikupe mwana mtakatifu mara akachukua mimba na kuzaa. (19: 22-23)
2. WAKRISTO-Lakini Mariamu Mama wa Yesu siku zake za kuzaa zilitimia. (Luka 2:6-7)
H. ISA HAKUTABIRIWA KWENYE QURAN vs. YESU ALITABIRIWA KWENYE BIBLIA:
1. WAISLAM-Qurani haionyeshi kama Isa alitabiriwa na manabii kuwa atazaliwa
2. WAKRISTO-Lakini Biblia inatuthibitishia kuwa Manabii walitabiri kuzaliwa kwa Yesu, (Isaya 7: 14; 9:6) utabiri huu ulitolewa na Nabii Isaya miaka 750 kabla ya Yesu kuja kuzaliwa nao ulitimia (Mathayo 1:18-23)
I. ISA HAJULIKANI ALIZALIWA WAPI AU KIJIJI KIPI vs. YESU ALIYE ZALIWA BETHLEHEM:
1. WAISLAM-Isa haijulikani alizaliwa katika kijiji gani wala mji, wala nchi aliyozaliwa Qurani haikueleza.
2. WAKRISTO-Biblia inatujulisha kuwa Yesu alizaliwa Bethelehemu ya Uyahudi katika Mji wa Daudi umbali wa maili 5 toka kusini mwa Yerusalemu nchi ya Israeli (Lk 2:8-16). Kuzaliwa kwake mahali hapo pia ni kutimiza unabii uliotolewa na nabii Mika miaka 750-686 kabla ya kristo kuja wakati wa wafalme hawa wakitawala – Jotham, Ahaz na Hezekia wafalme wa Yuda. Yesu mwenyewe alizaliwa kama mwaka wa 4 wakati wa Mfalme Herode.
J. ISA ALIONGEA AKIWA MTOTO MCHANGA vs. YESU HAKUONGEA AKIWA MTOTO MCHANGA:
1. WAISLAM-Isa aliongea na watu akiwa mototo mchanga, na kusema kuwa yeye ni mja wa Mungu amepewa kitabu na amefanywa Nabii (Sura 19:30-33)
2. WAKRISTO-Yesu hakuongea na mtu akiwa mtoto mchanga. Alianza kuwauliza maswali na kutoa majibu akiwa na wazee Hekaluni akiwa na miaka 12. (Luka 2: 42-49)
Hivyo tunaona kwamba tuna tofauti nyingi tu kati ya Bwana Yesu na Isa. Swali kwako mfuatiliaji je, Isa bin Maryamu ndiye Bwana Yesu Mwokozi? Tafakari.
Mungu awabariki sana na tuendelee kujifunza tofauti za Isa wa Quran na Yesu wa Biblia.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
Max Shimba Ministries Org.

Friday, July 8, 2016

WAISLAM WENGI AFRIKA WANAOKOKA KWA KASI




“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14).

INJILI KATIKA ULIMWENGU WA KIISLAMU

Bwana Yesu ndiye Muumba wa dunia hii na wanadamu wote – ikiwa ni pamoja na Waarabu ambao viongozi wao wamefanya kila waliloweza kuhakikisha kwamba Neno la uzima haliwafikii. Kwa karne nyingi walionekana kama wamefanikiwa. Lakini Neno la Bwana ni juu ya wanadamu wote. Bwana amesema katika Neno lake: Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. (Mathayo 24:14).
Na tena akasema: Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. (Mathayo 5:18).
Viongozi katika nchi za Kiislamu watafanya kila wawezalo ili kulinda imani yao na kuzuia watu kupokea uzima kutoka kwa Mwokozi wao, lakini Neno la Bwana ndilo litakaloshinda. Na hilo ndilo tunalolishuhudia hivi sasa.
*************
Ndugu uliye Muislamu, huu si wakati wa kuendelea kung’ang’ania mambo hata kama moyo wako unakushuhudia kabisa kwamba huna amani na wala hujafanikiwa kuyafanya mambo ya kumpendeza Mungu. Usishindane na hali halisi. Usikubali kuendelea kuishi katika maisha ambayo, mdomoni unasema hivi lakini moyoni unateketea kwa sababu hata wewe mwenyewe unajua kuwa kile unachokisema kwa kinywa chako, moyo unakikataa.
Njoo kwa Yesu, Mwokozi wako, ili akuweke huru leo. Yesu ni Mungu aliye hai. Nimekuwa nikitoa changamoto hii – nataka niitoe tena na kwako pia.
Iwapo Yesu ni mwanadamu tu na si Mungu kama dini yako ilivyokufunza, basi ongea naye, maana anasikia. Mwambie hivi, “Bwana Yesu, kama wewe ndiwe Mungu wa kweli, basi nionyeshe ukweli uliko.”
Naamini hili si tatizo kwako. Maana kama Yesu ni mwanadamu, bila shaka hutapata tatizo lolote. Lakini kwa kuwa Yesu ni Mungu aliyekuumba na kukuokoa msalabani, nina uhakika kwamba atakujibu.

WAISLAM WENGI WA IRAN KUMPOKEA YESU





Utafiti unaonyesha kuwa Waislam wengi wa Iran watampokea Yesu na kuwa WAKRISTO.
Hii ni habari njema sana maana sasa Waislam wamechoka kufuata dini isiyo na miujiza zaidi ya kufanya mambo ya ajabu ajabu kama ya ISIS.

WAISLAM MILIONI MBILI WANAINGIA UKRISTO KILA MWAKA NCHINI INDONESIA





Uchunguzi unaonyesha kuwa kila dakika 15, Muislam mmoja nchini Indonesia anaingia Ukristo. Hii ni sawa na Waislam Milioni 2 kila Mwaka. Mambo yakiendelea namna hii, basi ifikikapo Mwaka 2035, Uislam utafutika nchini Indonesia.
Soma hapa kwa habari kamili na ingia kwenye Video ujionee mwenyewe.
Muslims in Indonesia report losing one follower of Islam to Christianity every 15 minutes. That's 2 million a year. At that rate, by 2035 Indonesia will no longer be majority Muslim nation. What can Christians do to help advance Christ's cause there?

Jesus is good because He is God

 

TRENDING NOW