Monday, July 11, 2016

JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?


Ndugu msomaji,
Mwezi huu nitaweka mada kadhaa zitakazo fundisha kuwa, Isa wa Quran na Yesu wa Biblia ni wawili na tofauti:
MAANA YA JINA ISA
Ni jambo la kawaida sana jina au majina kuwa na maana. Mfano majina haya ya kiarabu yana maana hizi: Muhammad, linamaanisha mwenye kushukuriwa, Abdalla ni Mtumwa wa Allah; Abu-Bakar maana yake ni Baba wa bikira; Abu Huraira ni baba wa Mapaka. Aidha majina ya Kiebrania nayo pie yana maana. Malaki ni mtumishi au Mjumbe wa Yehova, Isaya ni Wokovu wa Yehova; Ezekiel inamaanisha Mungu hutia nguvu, Daniel – Mungu ni hakimu wangu.
JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?
Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe "ZERUZERU". Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?
JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?
JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.
Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.
Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na Sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
Leo tumejifunza kwa kifupi tu kuwa, Jina la ISA lenye maana ya Wekundu unao zidiana na weupe ni TOFAUTI KABISA NA Jina la Yesu lenye maana ya MWOKOZI katika Biblia. Zaidi ya hapo, tafsir ya Jina la Yesu kwa Kiarabu ni Yasu na sio Isa kama ambavyo Waislam wanadai katika vitabu vyao.
Mungu awabariki sana na tuendele kujifunza Neno lake bila ya kuchoka.
Katika huduma Yake,
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 7, 2016

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW