Friday, April 14, 2017
KWANINI WASABATO NA WAISLAM HAWAITAMBUI PASAKA?

“Siku Hii Itakuwa Ukumbusho Kwenu”
TORATI INAITAMBUA PASAKA:
“Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaisherehekea ikiwa sherehe kwa Mungu Yehova.”—Kutoka 12:14.
“Kristo Pasaka yetu ametolewa dhabihu.” (1 Korintho 5:7)
Nisani 14 ndiyo iliyokuwa siku ya Pasaka, lakini siku zote nane za sherehe hiyo ziliitwa pia Pasaka. (Kutoka 12:14-17; Luka 22:1; Yohana 18:28; 19:14) Pasaka ilikuwa mojawapo ya sherehe rasmi (“sikukuu,” Union Version) ambazo Wayahudi walipaswa kusherehekea kila mwaka.—2 Nyakati 8:13.
YESU ALISHEREKEA PASAKA, LAKINI WASABATO NA WAISLAM WANAIPINGA PASAKA:
Yesu na mitume wake walisherehekea Pasaka kila mwaka kwa sababu walikuwa Wayahudi na hivyo walikuwa chini ya Sheria ya Musa. (Mt. 26:17-19) Mara ya mwisho waliposherehekea Pasaka, Yesu alianzisha mwadhimisho mpya ambao wafuasi wake wangekumbuka kila mwaka, yaani, Mlo wa Jioni wa Bwana. Lakini walipaswa kuuadhimisha siku gani?
Kwa kuwa Yesu alianzisha Mlo wa Jioni wa Bwana baada tu ya Pasaka hiyo ya mwisho, mwadhimisho huo mpya ulifanywa katika siku ambayo Pasaka ilikuwa ikisherehekewa.
Kristo aliwaambia hivi Petro na Yohana: “Nendeni mkatutayarishie pasaka ili tule.” (Luka 22:7, 8) ‘Mwishowe, saa ikafika’ ya mlo wa Pasaka, baada ya jua kutua mnamo Nisani 14, ilikuwa Alhamisi jioni. Yesu alikula mlo huo pamoja na mitume wake, kisha akaanzisha Mlo wa Jioni wa Bwana. (Luka 22:14, 15) Usiku huo, alikamatwa na kushtakiwa. Yesu alitundikwa mtini karibu saa sita mchana Nisani 14, naye akafa siku hiyohiyo alasiri. (Yohana 19:14)
Hivyo, ‘Kristo pasaka yetu akatolewa dhabihu’ siku ileile ambayo mwana-kondoo wa Pasaka alichinjwa. (1 Korintho 5:7; 11:23; Mt. 26:2) Yesu alizikwa mwishoni mwa siku hiyo ya Kiyahudi, kabla ya Nisani 15 kuanza. *—Lawi 23:5-7; Luka 23:54.
Baada ya kusoma aya zote hapo juu, kwanini Wasabato "SDA" na Waislam wanaikataa sikukuu hii ya Sabato iliyo kwenye Torati?
Kama kweli Wasabato na Waislam wanaitambua TORATI, Kwanini wanasema PASAKA ni sikukuu ya WAPAGANI?
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
JE, YESU ALISULUBIWA SIKU YA IJUMAA?

Kama ni hivyo, ni namna gani alimaliza siku tatu kaburini kama alifufuka Jumapili?"
Yesu alisema katika Mathayo Mtakatifu 12:40, “Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi” wale wanaoshikilia kuwa Ijumaa ndio ilikuwa siku ya kusulubiwa, wanasema kuna hali halisi amboyo Yesu anakisiwa kuwa kaburini siku tatu.
Katika fikira ya Kiyahudi katika karne ya kwanza, sehemu ya siku ilichukuliwa kuwa siku nzima. Jinsi Yesu alikuwa kaburini sehemu ya siku ya Ijumaa, Jumamosi nzima na sehemu ya siku ya Jumapili anachukuliwa kuwa kaburini siku tatu.
Mojawapo ya dhana kuu ya Ijumaa inapatikana katika Mariko Mtakatifu 15:42, ambayo inasema kuwa Yesu alisulubiwa “siku iliyo kabla ya sabato” Kama hiyo ilikuwa sabato ya kila juma, kwa mfano Jumamosi, kwa hivyo hiyo hoja huasiria Ijumaa kuwa siku halisi ya kusulubiwa.
Fundisho lingine kuhusu siku ya Ijumaa lasema kifungo kama Mathayo Mtakatifu 16:21 na Luka Mtakatifu 9:22, zatufundisha kwamba Yesu angefufuka siku ya tatu; kwa hivyo, hangehitaji kuwa kaburini siku tatu mchana na usiku. Tafsiri zingine zinapotafusiri “katika siku ya tatu” kwa hizi aya, si zote, na si kila mmoja anakubaliana kwamba “siku ya tatu” ndio njia nzuri ya kutafusiri aya hizi. Zaidi ya hayo, Mariko Mtakatifu 8:31 yasema kwamba Yesu atafufuliwa “baada” ya siku tatu.
Kwanini inatupasa kukumbuka kifo cha Yesu?
Yesu aliwaambia wafuasi wake wakumbuke kifo chake kwa kula mlo wa mfano, wakitumia mkate na divai. Mkate unawakilisha mwili wa Yesu nayo divai inawakilisha damu yake.—Soma Luka 22:19, 20.
Mkate ambao Yesu alitumia haukuwa na chachu. Katika Biblia, mara nyingi chachu hutumiwa kufananisha dhambi. Kwa hiyo, mkate ulikuwa mfano unaofaa wa mwili mkamilifu wa Yesu. Alitoa mwili wake uwe dhabihu, ambayo iliondolea mbali dhabihu za wanyama zilizotolewa kulingana na Sheria ya Musa. (Waebrania 10:5, 9, 10) Divai ilikuwa mfano wa damu ya Yesu yenye thamani iliyomwagwa ili kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu.—Soma 1 Petro 1:19; 2:24; 3:18.
Kukumbuka kifo cha Yesu kunafaida gani?
Kukumbuka kifo cha Yesu kila mwaka huimarisha uthamini wetu kwa upendo wa Mungu usio na kifani. Alimtuma Mwana wake ili afe kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa hiyo, tunapohudhuria Ukumbusho, tunapaswa kutafakari kifo cha Yesu kinamaanisha nini kwetu. Tunapaswa kufikiria jinsi tunavyoweza kuonyesha uthamini kwa yale ambayo Yehova na Yesu wametufanyia.—Soma Yohana 3:16; 2 Wakorintho 5:14, 15.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Vitabu vya Korani vyapatikana katika vyoo Dallas Marekani

Polisi wameanza uchunguzi baada ya nakala za korani kupatikana ndani ya vyoo katika jumba moja la chuo kikuu cha Texas huko Dallas.
Picha kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha vitabu hivyo vikiwa ndani ya vyoo.
Polisi wa chuo wanasema kesi hiyo ni ya "kushangaza sana" na "isiyo ya kawaida" kwani chuo hicho kina wanafunzi kutoka makabila na dini mbali mbali.
Polisi wanajaribu kumtambua mmoja kati ya watu sita walioonekana wakiingia chooni wakati wa tukio hilo la tarehe 28 mwezi wa Machi. Wachunguzi wamekuwa wakikagua video za CCTV wakiwatafuta waliohusika.
- Gavana aliyetusi Quran afunguliwa mashtaka
- Ibada ya Hajj yafika kilele chake mlima Arafat
- Uchunguzi wa ugaidi, kuanzishwa Ufaransa
Hakuna kitu kilichoguswa katika chumba kimoja ambacho huwa na vitabu vya dini tofauti, kulingana na wachunguzi.
Mkuu wa polisi Larry Zacharias aliiambia Dallas Morning News: "Hakuna anayemjua mmiliki wa vitabu hivyo."
Mohammad Syed ambaye ni rais wa chama cha wanafunzi wa Kiislamu chuoni aliambia vyombo vya habari tukio hilo ni la "kuhuzunisha kweli na pia linatatiza."
"Licha ya kuwa kuna sauti kidogo ya chuki, kuna sauti kubwa ya upendo na unaotuunga mkono na kweli tunashukuru," alisema.
Aliongeza kuwa "mazingira chuoni ni mazuri ."
Korani hizo ziligunduliwa na viongozi wa wanafunzi baada ya mkutano wao jioni hiyo.
"Nilishangaa sana," alisema Jonathan Schuler, aliyepata vitabu hivyo takatifu katika vyoo.
"Tukio hilo liliifanya maneno mengi ya chuki i niliyokuwa nikisikia na kuona kwenye taarifa za habari kuwa halisi, na karibu sana."
Maseneta wa wanafunzi wametoa taarifa wakisema hilo ni ni tukio la kipekee na haliwakilishi jamii ya chuo kikuu.
http://www.bbc.com/swahili/39601347?ocid=socialflow_facebook
AHADI ZAKE NI KWELI NA AMINA

POKEA BARAKA TELE KUTOKA KWA YESU KRISTO MUNGU WETU MKUU.
Ngoja nikupe siri hii nzuri, zipo baraka nyingi sana za kiulinzi kutoka kwa Bwana zinazoambatana na wewe kumtumikia Mungu kwa njia ya kuwaambia wengine habari za huyu Yesu.
Mungu hutimiza ahadi zake. Imeandikwa katika 2Wakorintho 1:19-20 "Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi yaani mimi na Silwano na Timotheo hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa sisi."
Kuwa na imani kwamba Mungu atatenda yale aliyoahidi katika neno lake (Waefeso 6:16)
Waefeso 6:16 inasema ‘zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu’.
Waebrania 11: 1 inatueleza kwamba ‘Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana’.
Ndani ya Biblia zipo ahadi nyingi za Mungu kwako ambazo zinagusa kila eneo la maisha yako kiulinzi, baraka, uponyaji, afya njema, uzima, uzao, mafanikio nk. Ni jukumu lako kuzisoma na kuifunga imani yako hapo. Maana mara nyingi Shetani huwawekea watu mashaka juu ya Mungu wao na ahadi zake kwamba hatazitimiza. Kwa hiyo kama huzijui hizo ahadi ni rahisi sana kutekwa na fikra za Shetani. Hivyo ni jukumu lako kuhakikisha unaweka imani thabiti kwenye ahadi za Mungu katika maisha yako.
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.
PASAKA YA KALE ILIKUWA KUVULI CHA YESU

Sehemu ya 3 na ya Mwisho:
PASAKA YA KALE ILIKUWA KUVULI CHA YESU
Mungu Mwenyezi alileta mapigo kumi juu ya Wamisri ili awaokoe Waisraeli kutoka utumwani. Pigo la mwisho lilikuwa mauti ya - ya wazaliwa wa kwanza wa Wamisri lilo wapa ushidi waisraeli kutoka nchini Misri (Kutoka 12:29-36); Wakristo nasi tunapata ushindi kwa kufufuka kwa Yesu na kuishinda mauti (Wakolosai 2:11-13)
Kusudi Waisraeli nao wasiuawe, Mungu aliwaamru wamchinje mwanakondoo na kutia damu yake penye miimo na miisho ya milango yao.(Kutoka 12:13); vivi hivyo Wakristo pia tunapo shiriki kula mkate na kukinywea kikombe cha mzao wa mzabibu kwa ukumbusho wa Yesu, tunakuwa na uzima ndani yetu. (Yohana 6:51-53)
• Baada ya kuwaokoa Waisraeli, Mungu aliwapa siku kuu ya kukumbuka walivyookolewa. Siku hii iliitwa "Pasaka" kwa sababu neno "pasaka" maana yake ni "kupita juu" (Kutoka 12:1-28, 43-48); Vivyo hivyo baada ya Yesu kutuokoa alitupa agizo la kumega mkate na kukinywea kikombe. (Mathayo 26:26-28; 1 Wakorintho 11:23-16; Matendo 20:7)
• Waisraeli walitumia mwana-kondoo kwa pasaka (Kutoka12:3-5); Bali Wakristo mwana-kondoo wetu ni Yesu (Yohana 1:29, 36), Yeye ndiye "Pasaka" wetu (1 Wakorintho 5:7).
• Waisreli waliamriwa kutwaa mwana-kondoo asiye na hila (Kutoka 12:5); kwetu sisi Wakristo Yesu ni mwana-kondoo asiye na hila (1 Petro 1:19)
• Waisraeli waliamriwa kutokuvunja mfupa wa Mwanakondoo wa Pasaka waliposhiriki kumla (Kutoka 12:46; Hesabu 9:12); Vivyo hivyo Yesu naye aliye Pasaka wetu hakuvunjwa mfupa.(Yohana 19:33, 36)
• Wayahudi walishiriki Pasaka pamoja na mikate isiyotiwa chachu wakikumbuka walivyokula jangwani (Kutoka 12:8, 15; Kumbukumbu 16:3); Wakristo pia tunashiri mikate isiyotiwa chachu tukikumbukwa mwili wa Kristo uliyoteswa kwa ajili yetu (Mathayo 26:26; 1 Wakorintho 11:23-24)
• Wayahudi waliokolewa kwa damu ya mnyama waliyoipaka milangoni, (Kutoka 12:7); Lakini Wakristo tunaokolewa na damu ya Yesu iliyomwagika kwa ajili yetu (Mathayo 26:28)
• Wayahudi walishiriki pasaka kila mwaka mara moja (Kutoka 12:2, 14); Bali Wakristo tunashiriki pasaka kila mara. (Matendo 20:7).
MUDA WA KUFA KWA MWANAKOONDOO WA PASAKA.
Katika Agano la Kale Mwanakondoo alitakiwa kuchinjwa jioni
Kut 12:6 “Tunzeni wanyama hao mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni..”
Katika Agano Jipya mwanakondoo aliuwawa jioni ili kutimiza taratibu za Pasaka
Mat 27: 45-50. 45 “Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, ``Eli, Eli lama sabakthani?'' Yaani, ``Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?'' 47Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, ``Anamwita Eliya!'' 48Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49Lakini wengine wakasema, ``Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.'' [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu]. 50Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho.”
Marko 15:33-37 33 “Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu ``Eloi, Eloi lama Sabaktani?'' Yaani, ``Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?'' 35Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, ``Mnamsikia? Anamwita
36Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, ``Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!''
37Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.”
Luk 23:44-47. 44 “Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46Yesu akapaza sauti akasema, ``Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.'' Baada ya kusema haya, akakata roho.
47Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, ``Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.''
Mat 1:21 Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.''
Ebr 9:11-14 “11Kristo alipokuja kama kuhani mkuu wa mambo mema ambayo tayari yamekwisha wasili, alipitia kwenye hema ya kuabudia ambayo ni kuu zaidi na bora zaidi na ambayo haikujengwa na binadamu, yaani ambayo si sehemu ya ulimwengu huu ulioumbwa. 12Yeye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa wakati wote, akichukua, si damu ya mbuzi na ndama, bali damu yake mwenyewe, na hivyo kutupatia ukombozi wa milele. 13Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama hunyunyizwa juu ya watu wachafu kidini ikawatakasa kwa kuwaondolea uchafu wao wa nje, 14 damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia Mungu aliye hai.”
Ebr 9:24-26 24 “Kwa maana Kristo hakuingia kwenye hema ya kuabudia iliyotengenezwa na bina damu kama mfano wa hema halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ambapo sasa anatuwakilisha mbele za Mungu. 25Wala hakuingia mbinguni kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama kuhani mkuu ain giavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka na damu ambayo si yake. 26Ingekuwa hivyo, ingalimpasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini ilivyo ni kwamba ametokea mara moja tu kwa wakati wote, katika siku hizi za mwisho, ili atokomeze dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu.
Ebr 10:8-10 8Kwanza alisema, ``Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi hukutaka, wala huku pendezwa nazo,'' ingawa hizi zilitolewa kwa mujibu wa sheria. 9Kisha akasema, ``Niko hapa, nimekuja kutimiza mapenzi yako.'' Anaweka kando ule utaratibu wa kwanza na kuanzisha utaratibu wa pili. 10Na kwa mapenzi hayo, sisi tumetakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu, kwa wakati wote”
Basi kama tulivyoona yakuwa Pasaka ya kale iliondolewa pamoja na taratibu zake na sasa Pasaka wa Wakristo ni Yesu .
Pasaka katika Agano Jipya, Yesu ndiye Mwanakondoo mwenyewe wa Pasaka asiye na ila wala waa.
Bwana wa Mbinguni akubariki. Nimatuimaini yangu kuwa utafikisha ujumbe huu kwa watu wa mataifa ili wamwamini Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo,ili waokolewe. Bwana akubariki sana.
Mwalimu Chaka wa Musa
SIFA ZA WATU WAENDAO JEHANNAM
Warumi 1: 26 Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile. 27 Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu.
28 Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya. 29 Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya, 30 na kusingiziana; ni watu wa kuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye kiburi na majivuno; hodari sana katika kutenda mabaya, na hawawatii wazazi wao; 31 hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine. 32 Wanajua kwamba Sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo hayohayo.
Angalia sana ndugu usiwe na hizo sifa hapo juu. Hizo ni sifa za watu waendao Jehannam. Endelea kumtafuta Yesu ambaye ni Mungu na akulinde kwa damu yake. Endelea kufunga na kuomba bila ya kuchoka. Maana Shetani anatafuta mtu wa kummeza.
HABARI NJEMA KWA WATU WABAYA
“Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.” (Warumi 5:6)
Pengini utastaajabu vile vile kujua kwamba kuna-yo maandiko mengine yanayothibitisha ya kuwa kuna habari njema kwa watu wabaya. Hapa ni baadhi ya maandiko hayo:
Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi (1 Timotheo 1:15).
Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi (Warumi 5:8).
Kwa manna jinsi hii Mungu aliupenda ulim- wengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16).
Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea (Luke 19:10).
Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako (Matendo 16:31).
Kila atakayeliita jina la Bwana ataokoka (Warumi 10:13).
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu (Warumi 5:1).
KUMBUKA KATIKA YESU KUNA ULINZI WA DAMU YAKE.
Yesu akasema, “Ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe!” (Yohana 6:37).
Shalom,
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
KULIA NA KUSAGA MENO MILELE YOTE

Je, jina lako lipo ndani ya kitabu cha uzima?
Siku za mwisho zimekaribia, wenye dhambi tubuni, na watakatifu jiandaeni kunyakuliwa na Bwana, maana atakuja muda wowote sasa, tutanyakuliwa na tutaenda mbinguni, wenye dhambi wote, watatupwa kwenye ziwa la moto.
Luka 13:28 Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje!
(Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na ziwa la moto, liwakalo na kiberiti ambapo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10).
Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (Mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.
Mpendwa, ni hatari kama nini ukikosekana kwenye Ufalme wa Mungu, hakuta kuwa na nafasi nyingine ya kutubu. Ndio maana tupo hapa kila siku kukumbushana kuwa, tuwe tayari na tuendelee kumfuata Yesu aliye kufa kwa ajili ya dhambi zetu.
HAKIKISHA JINA LAKO LIMEANDIKWA KWENYE KITABU CHA UZIMA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
WAPENDWA: FURAHINI KATIKA BWANA SIKU ZOTE

"Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.'' ( Wafilipi 4:4-7 )
NIFANYE NINI ILI NIWEZE KUSHINDA TAMAA NA FIKRA ZA NGONO KILA SAA?

Je, Unatatizo la kupiga Punyeto?
Nifanye nini ili niweze kudhibiti fikira chafu za ngono?
Nifanye nini ili niweze kudhibiti fikira chafu za ngono?
Mpendwa:
Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke wakiwa na uvutano wenye nguvu kati yao, na hakuna ubaya wa kutosheleza tamaa za ngono katika mpango wa ndoa. Kabla ya kufunga ndoa, huenda ukawa na tamaa kali za ngono. Hilo likitokea, usidhani kwamba wewe ni mtu mwovu au kwamba huwezi kuishi maisha safi. Unaweza kudumisha usafi wa kiadili ukiamua kufanya hivyo! Lakini ili ufanikiwe, utahitaji kudhibiti mawazo yako kuhusu watu wa jinsi tofauti. Unaweza kufanya hivyo jinsi gani?
Epuka kujifurahisha kwa mambo machafu. Bila shaka, haimaanishi kwamba sinema zote, au miziki yote ni mibaya. Hata hivyo, katika ulimwengu wa leo burudani nyingi zimekusudiwa kuamsha tamaa zisizofaa za ngono. Biblia inatoa shauri gani? “Acheni tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Epuka kabisa burudani zote zinazoweza kuchochea tamaa zisizofaa za ngono.
Je, unatatizo la kupiga Punyeto?
Vijana fulani hujaribu kupunguza tamaa ya ngono kwa kupiga punyeto. Lakini kufanya hivyo kunaweza kutokeza matatizo makubwa. Biblia inawahimiza Wakristo hivi: “Viueni viungo vya mwili wenu vilivyo duniani kwa habari ya uasherati, uchafu, hamu ya ngono, tamaa yenye madhara, na kutamani.” (Wakolosai 3:5) Kupiga punyeto ni kinyume kabisa cha ‘kuua hamu ya ngono.’ Kwa kweli, kupiga punyeto huchochea na kukuza hamu hiyo!
Kupiga punyeto kwaweza kukufanya kuwa mtumwa wa tamaa zako. (Tito 3:3) Hatua moja unayoweza kuchukua ili kushinda zoea hilo ni kuzungumza na mtu unayemtumaini. Mkristo aliyekuwa na tatizo la kupiga punyeto kwa miaka mingi anasema hivi: “Laiti ningeweza kupata ujasiri wa kuzungumza na mtu fulani kuhusu tatizo hilo nilipokuwa kijana! Kwa miaka mingi nilisumbuliwa na hisia za hatia, nazo ziliathiri sana uhusiano wangu na wengine, na zaidi ya yote, uhusiano wangu na Yehova.”
Ni nani unayeweza kuongea naye? Mara nyingi ingefaa kuzungumza na mzazi. Au huenda Mkristo mkomavu kutanikoni anaweza kukusaidia. Unaweza kuanza kwa kusema, “Ningependa kuzungumza nawe kuhusu tatizo linalonisumbua sana.”
Nifanye nini ili niweke kudhibiti fikira chafu za ngono?
Mtume Paulo alisema: “Naupigapiga mwili wangu na kuuongoza kama mtumwa.” (1 Wakorintho 9:27) Vivyo hivyo, huenda wewe pia ukahitaji kujitia nidhamu wakati mawazo yasiyofaa kuhusu watu wa jinsia tofauti yanapoingia katika akili yako. Mawazo hayo yakiendelea, jaribu kufanya mazoezi ya kimwili. Biblia inasema: “Mazoezi ya kimwili ni yenye faida kidogo.” (1 Timotheo 4:8) Kutembea kasi kwa muda au kufanya mazoezi ya kimwili kwa dakika chache kwaweza kukusaidia kuondolea mbali mawazo hayo yasiyofaa.
Zaidi ya yote, usipuuze msaada kutoka kwa Baba yako wa mbinguni. Mkristo mmoja anasema hivi: “Tamaa za ngono zinapoanza kuamka najilazimisha kusali.” Si kwamba Mungu atakufanya uache kupendezwa na watu wa jinsia tofauti. Lakini anaweza kukusaidia kuona kwamba kuna mambo mengine mengi unayoweza kukazia fikira zako.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Subscribe to:
Comments (Atom)
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...





