Thursday, December 14, 2017

MMILIKI WA YERUSALEM NI ISRAEL NA SIO PALESTINA

Image may contain: one or more people and text
Israeli ni jina la watu au taifa walioitwa taifa teule katika Tanakh au Biblia ya Kiebrania (kwa hiyo pia katika Agano la Kale lililo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.
Kihistoria waliishi katika nchi iliyoitwa Kanaani, halafu Israeli kuanzia mnamo 1200 KK hadi mnamo mwaka 70 BK Waroma wa Kale walipovamia na kuharibu Yerusalemu, ambao tena mwaka 135 waliwafukuza wote kutoka nchi yao.
Wenyeji walijiita mwanzoni Wanaisraeli na baadaye pia Wayahudi.
Historia ya Israeli ya Kale inaanza tangu kupatikana kwa taifa hilo katika nchi yake inayoitwa Israeli. Kufuatana na Torat kwenye Agano la Kale taifa la Israeli lilianzishwa na Wanaisraeli waliotoka Misri chini ya uongozi wa Musa na kuvamia Kanaani mnamo mwaka 1200 KK chini ya Yoshua.
Muungano huo wa vikundi na makabila ukawa taifa na kuunda ufalme wa kwanza wa Israeli wakati wa mfalme Sauli aliyefuatwa na Daudi na mwanae Suleimani.
Baada ya kifo cha Suleimani likatokea farakano na jina la "Israeli" likatumiwa na ufalme wa kaskazini, wakati mji mkuu wa kale Yerusalemu ukaendelea kama mji mkuu wa ufalme wa Yuda.
Wakati wa Agano Jipya, mji wa Yerusalemu, pamoja na nchi ya Israeli, vilikuwa chini ya Dola la Roma, ambalo lilitawala maeneo yote yanayozunguka bahari ya Mediteranea. Mkuu wa Dola alikuwa na cheo cha "Kaisari" akikaa mjini Roma (Italia).
Waroma walidai utiifu na kodi za mataifa na makabila yote yaliyokuwa chini yao. Lakini hawakuwa na neno juu ya utamaduni na dini za nchi hizo.
Utawala wa Kiroma ulirahisisha biashara na uchumi pamoja na mawasiliano katika maeneo haya yote. Waroma hawakuwa na mitambo ya injini lakini walikuwa wataalamu wa uhandisi. Walikuwa hodari sana kujenga barabara na nyumba za ghorofa. Majengo kadhaa waliyoyajenga husimama mpaka leo. Magofu ya miji yao yanaonekana leo hii kuanzia Misri na Algeria hadi Ujerumani na Asia. Wasanii wao walichonga sanamu za mawe za kudumu.
Israeli ilikuwa na serikali yake ya Kiyahudi lakini pia na liwali au gavana wa Kiroma. Waroma walizima kwa ukali majaribio yote ya kupindua utawala wao. Wayahudi katika Israeli walijaribu mara mbili kuwafukuza Waroma nchini: miaka 66-73 na 135 BK. Kila safari Waroma walilipiza kisasi, wakichoma moto miji na vijiji na kuwafanya wananchi kuwa watumwa au kuwaua kabisa.
ALLAH ANASEMA KWA WAYAHUDI KUWA ARDHI YA ISRAEL IMETAKASWA NA IMEANDALIWA KWA AJILI YAO:
Allah (s.w.t.) amesema: Enyi watu wangu! Ingieni katika hiyo ardhi iliyotakaswa ambayo Allah amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika.(5:21)
Katika aya hapo juu, Allah anawaita Wayahudi kupitia Musa "WATU WANGU" zaidi ya hapo anawaambia kuwa Waende Israel kwenye ARDHI ILIYOTAKASWA, kumbe ata Allah anafahamu kuwa ardhi ya Israeli si ya Wapalestina.
Sources:
Biblical History The Jewish History Resource Center - Project of the Dinur Center for Research in Jewish History, The Hebrew University of Jerusalem
Catholic Encyclopedia: Jerusalem (Before A.D. 71)
Holy land Maps
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW